BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BANANA ZORRO KUPATA JIKO MWEZI HUU December, 6, 2007

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Developing News,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 11:50 AM

 

Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya,Banana Zorro, anatarajia kufunga ndoa na mchumba wake, Suzy Walele tarehe 30 mwezi huu jijini Dar-es-salaam ndani ya Msasani Beach Club(kwa waalikwa tu)

Pichani kutoka kushoto ni mwanamuziki Richard Mangustino (zamani aliwahi kutamba na Diamond Sound na Beta Musica na hivi sasa anapika vipaji ndani ya Tanzania Talent House), mke mtarajiwa wa Banana,Suzy Walele, Banana Zorro pamoja na Hafsa(aliyeimba naye kibao Presha).

Katika mazungumzo mafupi tuliyofanya na Banana hivi karibuni alitudokezea kwamba mara tu baada ya ndoa atarejea studio kukamilisha albamu yake ya tatu ambayo ameipa jina Sultan.Inatarajiwa kutoka mwakani. Banana pia ni mmiliki wa B-Band.BC inamtakia Banana Zorro na mchumba wake Suzy Walele,maandalizi mema ya harusi na baadaye maisha mema ya ndoa.

Picha kwa hisani ya MichuziJR.

Advertisements
 

33 Responses to “BANANA ZORRO KUPATA JIKO MWEZI HUU”

 1. Bob Sankofa Says:

  Kila la heri kaka Banana Zoro. Tuko pamoja!

 2. […] Suzy anamchukua Banana Zorro jumla, unaweza ukasema sentensi hiyo kinyumenyume. Kwa habari zaidi cheki Bongo Celebrity. […]

 3. Dinah Says:

  Banana dogo ufunge ndoa na utulie humo ndoani….tumechoka na Talaka. Kila la kheri na Mungu awajaalie maisha mema na marefu ya ndoa…..mkue na kuzeeka pamoja inshallah!

 4. mesa Says:

  hongera banana mie jirani yako pale miko kwa kina gabi, naomba kuuliza hivi suzy walele ni yule mdogo wake shafii walele na baba yao aliwahi kuwa RPC kigoma? ok kama ni wewe big up sana

 5. Edwin Ndaki Says:

  Suzy kila la kheri hapa Edo

 6. any Says:

  huyu jamaa mwenye rasta hiyo ni jasho au rangi ya shati, mi sirudi bongo, mambo ya wavuja jasho siyawezi.

 7. Majita Says:

  Ndoa njema na mzae mapacha tena msome fungu hili..”Zaeni muongezeke muijaze nchi”.Mambo ya uzazi wa mpango tutakosana mchana kweupeeeee.

  Banana wewe baba yako si alikutosa??Sasa na wewe uwatose wanao uone tutakavyokutungia Mashairi.Sijui kuimba Hip hop ila ntajifunzia kwako.naamini sauti yangu kama ya chura wakati wa masika itafikisha sauti.

  Kikwetu bila kumpiga mkeo japo mara 6 kwa mwezi atasema humpendi.Sasa bwana Banana nakushauri uwe unamkung’uta mkeo ki-sawasawa.Nikiwakuta Polisi mnachukua PF3 ili akatibiwe ntafurahi sana.
  UWE UNARIPIGA NA KURIGARAGASA CHINI KWA MATEKE.Ndo mapensi ya kikwetu.Ambao hamujaorewa karibuni musoma kwa wanamume

 8. some Says:

  Kila la heri katika ndoa yenu.Mwenyezi Mungu awatangulie katika kila jambo lenye heri. Hongera Suzy kwa kumpata mume mtafutaji mhangaikaji siyo kula kulala.MUngu awajalie mzae watoto wema.

 9. Lizzie Says:

  MAJITA UMENI MALIZA KWI KWIIII! AZIKUTOSHI WEWE UJATULIA

 10. Hellen Says:

  Hongera kwa uwamuzi uliofikia kaka,Ila utulie sasa maana magonjwa mengi sana.Mtoto wako usimsahau kwa mkeo mlioachana.Ni hayo tu.

 11. Jasmine Says:

  Big up, ni wa uamuzi wa busara kwa kijana maarufu kama wewe, kila la kheri ktk ndoa yako!!

 12. maya65 Says:

  Aisee majita kama ulikuwepo, mimi mke wangu ni mjapan kama sijampiga mwezi mzima huwa hana raha!!!!
  wakati mwingine huwa ananiuliza eti ” mbona siku nyingi zimepita hujanipiga”….haahaahaaa hii ni kweli wala si utani, naona pengine angefaa kuishi musoma!!!!!
  hongera Ndizi Zorro

 13. Edwin Ndaki Says:

  Wamai…MAJITA…yaani banana akikagecha ka Suzzy ndio malovee yataende vema….lol…

  Teeeeeeeeeeee teeeeeeeeeeeee…. B&S naombeni ka tenda ka kuwa MC wenu…

  Ila banana piga ua usimsahau mtoto wetu(mwanao)…

 14. Mzawa Says:

  Wee unayesema kuwa BONGO JOTO kaoshe matako ya vizee huko ulikoo #$^&&*(*()_ weeee!!!!

 15. any Says:

  bora kuosha matako ya wabibi kuliko kuvuja jasho. wee umenyimwa VISA nini, mbona mkali? rudi shule kanyooshe kingereza then go back to the embassy they will give u.

 16. Subira Says:

  Ka jamani watu wengine wakiwa nje kwa madharau na majidai? Sijui ndio nini hapo huyo Banana pengine alikuwa anaperfom, au amemwagikiwa na kinywaji jasho hilo mbona wenziwe hawajaloa kama Bongo ni joto hivyo?

  Mhu! yetu macho wale wenye neema ya kweli walobarikiwa na Mungu ni wanyenyekevu sie mungu aliyetuona jioni usiseme. Kwani kujua kiingereza ndio kupata Visa na kutokujua kiingereza ndio kukosa visa!

  Hali kadhalika wenye shule ya nguvu hutawasikia wakiwadharau wenzao lakini sie shule zetu ambazo bado tunasoma au ndio tuna digirii ya kwanza au ya pili basi tena watu wote wajinga hawajui kitu. Tuache dharau jamani aliyekupa wewe ndiye aliyemnyima yule!

  Hongera Banana kwa kutarajia kupata mke hivi karibuni.

 17. any Says:

  acha kulia.

 18. John. Says:

  Ni kweli subi mara nyingi watu wanojiona ni wale ambao “Kipofu kaona Mwezi”Watu wenye Elimu zao kama akina Prof.Lipumba hawajidai hata siku moja wanatembea na walala hoi kwenye maandamao wanapigwa virungu na polisi,Profesa anakwenda Ulaya kwa kadri anavyotaka sio kama yeye yupo hapo Uk.ndio ataishia hapo hapo mwisho wa siku baada ya kupata Pesa zake za Kubeba Maboksi atarudi nyumbani.Acha maringo kaka.
  John.

 19. any Says:

  Siko UK wala US wala India, ni huyo jamaa apo juu alipoanza matusi anaonesha ana chuki binafsi ndo namuuliza visa amenyimwa au?

 20. gnasha Says:

  Mesa Suzy huyo ndiye yule yule mdogo wake na shafii. Ameamua kuachana na ukapera. Hongereni sana.

 21. Alhaj meddie Says:

  A.alleykum kaka,
  ukisikia ukubwa maanake sio ukishindwa ya nyumbani basi we talaka,hutomaliza dunia na mwisho wa siku hata sisi wa nje tutajiuliza una nini kijana wewe?haya tuache hayo… me nakuatakia kila la kheri na Inshaallah Mola awafunge macho usione mwingine nae asione mwingine pembeni….

 22. Banana vipi?
  Inakuwaje mtu wangu?
  Japo nitakutafuta kwenye 4n lakini nimeona pia nitoe pongezi zangu hapa mtandaoni baada ya kupitia kutaka kujua mawili ma3 yanayo jiri nyumbani. Mzee nakupeni kwanza hongera na pongezi kwa uamuzi mliochukua! Angalia sasa mbele msikwazane na Shem, kuheshimiana, kujali kila mmoja, kuvumiliana na kusikilizana ndizo silaha ya wawili wanaotaka kufika mbali. Kwasasa nipo Nairobi sijajua kama nitarudi kabla ya weddo! Please take care of ma shem and the child! Tuko pamoja tunawaunga mkono,
  Ahsanteni,
  Kasambula Jr.

 23. ANNA ULOMI Says:

  HONGERA BANANA,ALL DA BEST

 24. maya65 Says:

  Acheni kutukanana humu…..

 25. anoni Says:

  kwani mtu akiingia humu na kusoma vitu vipya na kutoka bila ku comment anapungukiwa na nini? Mbona watu mnatoa comments zisizo na kichwa wala miguu? We umezaliwa bongo ukatoka jasho ndo ukapata kwenda huko uliko, sijui Iraq ama kenya au DRC? lakini nyodo nyingi? mamako mwenyewe alitoka jasho ndo akakuzaa wewe, sasa unajifanya kuona jasho kitu cha ajabu!!!!! halafu unamwambia mwenzio arudi shule akanyooshe kiingereza. acha dharau na matusi kaka elewa mpanda ngazi hushuka

 26. any Says:

  kurudi shule umeona tusi, yeye kusema wenzie wanashika matako ya wazee apo hamkuona tusi.
  Niko tz tena mikoa ya baridi Mbeya, Bongo wengine tunajua ni dar, ndo maana sirudi huko bongo, bora nikae mbeya.
  Mpanda ngazi hushuka, hiyo ni dua la kuku. haya, ngoja nikashike matako ya bibi yangu anaenipa kula yangu huku mbeya.

 27. any Says:

  thats ur assumption, sio watz wote wamezaliwa tz, wengine ni watz wa kuomba uraia kama babake na Richa wenu miss tz. wengine wanazaliwa drc wazee wake walikuwa huko kikazi tnen wanarudi home. na wengine wanazaliwa huko huko mamtoni na wanaamua kubaki huko na kubaki na utz wao, so dont assume all tz were born there.

 28. Phina M Says:

  Banana nakupa big up mwana, pia nakupa fagio suzy kwa uamuzi wako wa busara ulioamua, 2ko pamoja shoshti kwa hali na mali ili ufanikishe shughuli yako nafikiri utaifurahia sherehe yako kuanzia k’party, sendoff pamoja na harusi yenyewe mtu mzima, ila tuzidi kumuombea baba yako mzee walele apone haraka ili asherehekee kwa furaha harusi yako.

 29. KIMWAGA Says:

  Yaani huwa nakufagilia Banana sana!!!!!!!!!!!! napenda kuchangia hii harusi nisiikose nimpe nani mchango wangu?????

 30. moureen Says:

  what you have decided to do is a big step in life.
  we dont expect to hear any bad news from you.you are a father to be so behave nicely.
  all the best in your new life and always do remember to thank GOD

 31. felista Says:

  Unajua ndgu zangu hata mkimpinga Any, kuhusu hali ya BONGO ni ujinga tu.Kweli ukienda mahali ukaanza kuongelea eti BONGO hamna joto,vumbi na matope kweli watu wata kushangaa.Mkitembela kwa wenzetu ndo mtaona jinsi tulivyo nyuma na ndio maana wabongo wanaoenda nje wanaona kuliko kurudi kwenye vumbi,matope,joto naongezea Trafick jam bora kubaki mamtoni ubebe mabox.Sababu hutayabeba wewe utadirect machine ifanye.Sasa kweli huyo mtu utamlinganisha na sisi wauza maji, jamani tukubali ukweli ili tuendelee.

  Halafu fikra za mpanda ngazi hushuka zimepitwa an wakati kama umeandikiwa YES always ni YES. Halafu wewe unayesema eti kupata visa ni kujua Kingereza au la.Jamani naona hujawahi kwenda Embassy labda. kama hujui Kingereza ni muhimu sana. jamani kama hujui ukipata visa ni bahati sababu kwanza application forms zipo kwa Kingereza sijui utajibu ni nini halafu ukafanyiwe interview yakingereza

 32. hater Says:

  We Any ungekuwa umesoma basi usingeogopa kurudi bongo kwa sababu ungekuwa n kazi nzuri, pesa, gari yenye A.C na nyumba na ofisi vyote A.C..usijidai chochote, tupo bongo na misha super, Ulaya tumekaa tumesoma na dgree zetu..Utabaki huko kuwa mtuma..
  Na kuhusu kujua lugha huna chochote…nimendika kiswahili il wananch wote waelewe..
  Una dharau, huna utu na kama umesoma usingekuwa unafuta vibibi vizee.shwaiiiiiniiiiiiiiiiiiiiiii weye!!!!!!!!!!! mxzymxzy!

 33. hater Says:

  si lazima kujua kingereza unapoenda kuomba VISA unless unaenda kama mwanafunzi..niulize, Watalii wa Uingereza, Japan na nchi zote za ulaya wanajua kiswahili?
  Nimeenda balozi za Tanzania nchini humo na interview zake si za kiswahili..Nimeshuhudia, siandiki pumba!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s