BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MTAFUTE,ANAISHI MSIMBAZI KOTA December, 7, 2007

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Wikiendi imewadia…au niseme Ijumaa kwa sababu siku yangu ya mwisho ya wiki kwa wengine inaweza kuwa ya kwanza.Mambo ya dunia yetu haya.Tumeshindwa hata kukubaliana siku gani ya wiki ndio ya mwanzo na ipi ni ya mwisho!

 

Piga picha hii.Umepata ajali mbaya ambayo huenda ikakupa ulemavu wa maisha.Umelazwa hospitalini kwa muda mrefu sasa lakini mpenzi wako (actually mchumba) hajatokea kukuona na kukujulia hali! Umetingwa na mawazo tele kila siku huku ukiuguza majeraha.Mara wazo linakujia,mgonjwa mwenzako mliyelazwa wodi moja,kitanda cha pembeni,yu karibu kutoka hospitalini.Kwanini usimtume akitoka aende kumtafuta mchumba wako,ampe habari za ugonjwa wako?Si inawezekana hajasikia?Au?Unampa na anuani kabisa ya anapoishi mpenzi wako.Bado mawazo yamekutinga.Zile feni za hospitali hata hazikusaidii kupunguza kijasho kitokanacho na mawazo.Itakuwaje mpenzi akisikia kwamba ndio ushapata ulemavu wa kudumu?Dunia yenyewe hii ya mkono mtupu usiolambwa…mawazo tele.

 

Ujumbe huu upo ndani ya mdundo wa leo kutoka kwa DDC Mlimani Park Orchestra(Wana Sikinde).Wimbo unaitwa CLARA.Pata burudani na ujumbe.Ijumaa Njema.

 

Kibwagizo cha leo hiki hapa kwa wale watumiaji wa lugha ya malikia.

A young man went to his father one day to tell him that he wants to
get married. His father was happy for him. Cheerfully, asked his son who
the girl is, and the young man told him that it’s a girl from the
neighbourhood. With a sad face the old man said to his son, “I’m sorry to
say this son but I have to. The girl u want to marry is your sister, but
please don’t tell your mother.”
The young man again brought three more names to his old man, but ended
up more frustrated cause the response was still the same.
So he decided to go to his mother. “Mama I want to get married but all
the girls that I love, dad said they are my sisters and I mustn’t tell
u.”
His mother smiling said to him,”Aagh! Don’t worry my son, u can marry
any of those girls you’re not his son anyway, but please don’t tell your
father.”

Advertisements
 

10 Responses to “MTAFUTE,ANAISHI MSIMBAZI KOTA”

 1. Edwin Ndaki Says:

  IJUMAAAAAAAAAAA IPO PALEEEEEEEE PALEEEEEEEEEE….

  Yaaani mwendo huo huo BC yaani hizi ndio nyimbo…

  Hapo nakumbuka nimejituliza kwenye meza jirai na pooltable pale CBE dsm nakula mchemsho pembeni maji ya kana…

  Navuta muda baadaye nijivute TGI au B bar sinza nikaa AGIZE KILO MOJA LOST na NDIZI…(nini?)

  Kama sipo hapo nipo SAUT malimbe CELTEL POINT navuta muda niende kwa komba BWIRU…

  Nikiwa TANGA hapo navuta muda nipo Tanga hotel baada ya muda najivuta nguvumali kwa mzee mguto..kula nyama..

  Au nimetulia zangu Mburahati kwa Mzee Robert…hapo ni ya kuokwa..nini?

  Kama ni musoma…taaratibu nipo zangu MKENDO kati KEMONDO….

  Yaaani piga ua wiki endi ipo tz bwana…

  Wamai MAJITA ijumaa hiyo upo wapi…

  Ijumaa njema…..

  HAO NDIO NDIGE..ukipenda SIKINDE…

  Ukimwona mpe salaaam nyingi sanaaaa..mueleze mchumba wakeee Edooo ninamsalimuuu….

 2. sinzia Says:

  kaka Edwin Ndaki,
  Umenikumbusha Kitimoto ya mzee Robert Mburahati…..kaka ile ni ya kuchomwa…ndizi 2/3 za kuchemsha, chachandu kwenye kisosi na kabia kako baridi pembeni…ahhhh utatamani mtu uhishi milele…..asante sana…mimi nipo mbali na home kwa mda mrefu…lkn at least umenipa kionjo ambacho kimenikumbusha Home….East or West…home is BEST.

 3. DarRu Says:

  Nyimbo kama hizi zinanikumbusha kipindi cha “OMBI LAKO” cha Redio Tanzania Dar Es Salaam enzi hizoooooo.
  Kazi nzuri BC.

 4. Edwin Ndaki Says:

  Sinzia yaani hapo ndiyo kwenye hata mimi namiss sana tz m2 wangu.Haya maminofu ya huku tatizo frozen..

  Nilikuwa mshirika mzuri wa mzee Robert Sinzia.ukifika pale jmosi magari unaweza fikiri kuna msiba maana ni makazi ya watu.

  DARRU umenikumbusha mbali sana RTD….yaaani kipindi kilichokuwa kinaniboa ni MALENGA wetu..yaaani mida hiyo ya mchana ka sa saba njaa inaumaa alafu mjamaa kwenye redio kakomaa naa vina tu…

  RTD baaaaaaaaaaaaaaab kubwa ..walitusaidia sisi watoto wawafugaji na wakulima japo kusikiliza hadithi za mama na mwana maana wengine Rininga tulikuwa tunaisikia kwenye magazeti ya MZALENDO,UHURU na MFANYAKAZI……

  Ngoja nipege fundo then tutaendelea….

 5. Majita Says:

  Edwin Ndaki Eeeeeh,
  Taratiiiiiiiiibu navutika JJ kwa ajili ya hiyo ya kuchoma.ni baada ya mchana kupiga lost ndizi kimara mwisho iliyopokelewa na ugali kamongo wa saa nne pale break point.Chai au supu niliikwepa pale Basihaya camp site kwa Mkumbi.Hiyo ni wakati natoka Dar kwenda Arusha ili niwahi mizunguko na ya J2 hapo TCC.

  Arusha nafika tuu napokelewa Bar mpya hapo Sanawari na machalii wangu.Matongee hatukwenda kwani tulikuwa na ahadi na washikaji tukutane jioni Sakina bar kwa ajili ya kuku wa kienyeji.Hata hivyo Wana Apolo wangu walikuwa makamanda kwani kidogo njaa ituue ndo lunch ya mchana tukakamata hapo Tripple A.Utanitaka???

  Nikasema Nooo.Lazima nile vumbi kidogo.Nikachukua Mtei baada ya Born City kuniacha hadi Singida.Mtumeeeee!!!Ile nakata Rwezaura tu,kona hii hapa.Tukapiga Serengeti boys kidogo kabla ya kwenda Cheyo hata hivyo tukaogopa majambazi hapo Stanley.

  Huyoo Mwanza.Du Bhageshi.Nakwambiaga achaga tu.Nilianza kukifata hicho cha moto kule Nyegezi Tema pale hostel ya SAUT.Jioni nikalichezaga pale kapirikabana.Bwiru sikuzifataga zile mishikaki za buku buku.

  Musoma sikwenda wikiendi hii.
  Bukoba nikaenda Hamugembe.

  Tanga nikakaa tu kidogo Raskazone kwa ajili ya upepo.

  Morogoro nikaenda kaumba usiku sana,ila sikupata naniii.Upo Ndaki wa Mai.
  Dodoma sikwenda NK.

  Nikachoka sana kwani nilikuwa nawahi BOX langu hapa kwa kaka Pori.Hata hivyo nikaishia tu Prudential baada ya kupokelewa na washkaji na sijui kama J3 box litapigika vizuri
  Ijumaa hii vipi wewe mwenzanguuuuu

 6. Edwin Ndaki Says:

  Duuu..Nimeikubali ratiba…hasa NYEGEZI tema..

  Ila moro jirani na kaumba kama palikuboa kwanini usingeenda pale CHIPUKIZI?maana mara nyingi hata mimi nikiwa dom kam sio NK maana DH siendi naogopa naweza kukutana na kiranja wa wa nchi akanipa majukumu.

  Sasa kama ulikuwa unaenda Raskazone natumaini ukitoka hapo badaye tutaonana RAKASA CHIKA…maana meridiani vibaka kibao…

  Ila Mi kesho sina boksi maana kesho jmosi NAVUTA PUMZI.

  Wa manai MAJITA usiku mwema

 7. Bob Sankofa Says:

  Jeff na timu yako ya BC itabidi mnilipe mbavu zangu kutokana na maelezo yenu hapo juu. KWa jinsi JEff anaelezea jinsi vile ujumbe unatakiwa ufike kwa huyo mpenzi toka kwa mhanga wa ajali inakuwa ni kazi ya kulipwa mshahara kabisa. Mambo ya kupeana anuani, kumtumia jirani aliye karibu na kitanda chako, kweli tumetoka mbali.

  Wimbo unatukumbusha kuwa simu za mkononi zimeokoa mengi. Zamani ilikuwa kuwasiliana na mwenzi wako lazima uso kwa uso au barua. Uzuri wa zamani ilikuwa huwezi kusema uko BAgamoyo wakati bado uko katikati ya Jiji kama ilivyo leo watu wanvyodanganyana kwenye simu za mikononi. Teknolojia hiyo.

  Jeff hizi nyimbo huwa ni zaidi ya nyimbo ukizichambua kwa undani. Ni historia yetu na BC inazitunza. Hongera kwa kazi nzuri.

 8. Upendo Furaha Says:

  Wimbo wenyewe mzuri; Lakini maudhui yake yanatia uchungu sana. Yaani mchumba anayekupenda wakati ukiwa mzima na mwenye pesa tu, huyo sio mtu wa kuishi naye maisha yako yote.
  duh!!!!! inauma sana.

 9. DUNDA GALDEN Says:

  BC hiki kisa kinachoeleweka sijui kkama kilitokea enzi hizo lakin kwangu kiliwahi kumtokea rafiki yangu hali haikuwa nzuri kwa huyo mwanamke alikutwa akiwa na bwana mwengine uzuni kubwa wacha niishie hapo uchungu sana
  Chafosa chai goda


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s