BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

UMEWAHI KUMSIKIA IRENE SANGA? December, 8, 2007

Filed under: Burudani,Sanaa/Maonyesho,Utamaduni,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 11:21 AM

 

Jana usiku katika ukumbi wa Utamaduni wa Watu wa Ufaransa jijini Dar-es-salaam, mtunzi na mghani mashairi wa Kitanzania, Irene Sanga, alifanya onyesho lake la kwanza labisa la jukwaani hapa nchini Tanzania. Alizikongoa vilivyo roho za washabiki wake kwa mashairi yake ya PANGISHENI pamoja na uchezaji wake mahiri wa ngoma za asili zinazoambatana na ushairi wake. Dada Irene tayari anayo DVD pamoja na CD ambazo atazizindua katika tarehe itakayotangazwa muda si mrefu.

Pichani ni Irene Sanga(kulia) akiwa na mshirika wake mkubwa katika masuala ya muziki na mtayarishaji wake wa sauti, Elidadi Msangi wakiwapa washabiki burudani hiyo jana.

Picha na habari kwa hisani ya Bob Sankofa.Kwa picha na habari zaidi juu ya onyesho la Irene Sanga tembelea www.mwenyemacho.com.

Advertisements
 

8 Responses to “UMEWAHI KUMSIKIA IRENE SANGA?”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Hakika huyu dada anastahili pongezi sana.

  Nakumbuka nimemwona kwenye wimbo mmoja wa kuhusu watoto yatima..HODI TUFUNGULIENI pia alisimama vyema kwenye wimbo wa SALAMU MJOMBA aliomshirikisha MRISHO MPOTO.

  Kila la kheri

 2. J4 Says:

  Safi sana IRINE SANA, yaani unaimba ile mbaya mtu wangu! leo nimeusikia kwenye TVT wimbo wako mmoja unaitwa NDOTO, oooh bomba ile mbaya! Nimekukubali hata kwenye wimbo wako SALAMU KWA MJOMBA kweli unastahili pongezi, unaimba nyimbo zenye asili ya kiafrica!
  Ushauri wangu mmoja hebu kwenye nyimbo zako unazotoa kwenye TV yapite maandishi yanayotafsiri lugha ya kiingereza i know utapata soko ile mbaya! Kwani nyimbo zako zina maudhui mazuri ile mbaya hivyo hata wasiojua kiswahili wakizisikiliza kwa njia ya maandishi wataenjoy na ujumbe uliomo ndani yake! Pongezi sana Irene kwa kazi nzuri yenye madhari na maudhia bomba ile mbaya ndani yake.

 3. trii Says:

  dada kazi zako nzuri sana.

 4. any Says:

  huyu dada hali bange kweli?

 5. any Says:

  tukucha anakula na meno badala ya kukata na nail clip

 6. lameck bonaventure Says:

  yaaaaaaaaap, namkubali mwanadada huyu. nimeziona kazi zake. jitahidi zaidi na zaidi kuwa mtamaduni na mzalendo halisi.
  keep it up lady, all the best

 7. hans Says:

  uliwaza nini dadaangu mpaka kutunga salaam kwa mjomba???? kila mtu wimbo ameukubali. ninachokuomba ni kuongeza juhudi tu

 8. alzira Says:

  Hi, how are you doing?
  I need some help about the meaning the word “mahiri”. I’ll appreciate very much your help. Tanks,
  Alzira Aymoré, from Brasil.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s