BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

CLOUDS FM YAMPOTEZA MENEJA MKUU. December, 10, 2007

Filed under: Uncategorized — bongocelebrity @ 8:00 AM

 

Meneja Mkuu wa Clouds 88.4 fm Godfrey Odhiambo (pichani) ametutoka (hatunaye tena).Kwa mujibu taarifa zilizotolewa na moja ya wakurugenzi wa kituo cha redio hiyo Ruge Mutahaba,Marehemu amefariki jana saa kumi jioni hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar-es-salaam.

Hayati Odhiambo ambaye ni raia wa Kenya,anatarajiwa kuagwa rasmi kesho kuanzia majira ya saa sita mchana kwenye kanisa la Pentekoste kinondoni linalotazamana na soko la TX,kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Kenya kesho (jumatano).

BC inatoa pole kwa ndugu,jamaa na marafiki na pia watangazaji na wafanyakazi wote wa Clouds FM .Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi-AMEN

Advertisements
 

6 Responses to “CLOUDS FM YAMPOTEZA MENEJA MKUU.”

 1. Karim Says:

  Poleni wafiwa wote.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

 2. david mngara Says:

  Poleni sana Clouds Fm lakini ni mipango ya Mungu.Bwana ametoa na Bwana ametwaa.Tulimpenda sana ila Mungu kampenda zaidi.

 3. Habiba Says:

  Poleni sana ndugu zetu kwa kumpoteza mchapakazi mwenzenu,hata kambi yenu haitakuwa na raha tena ila mjipe moyo mana hili liko kwa kila mmmoja wetu,na mola siku zote huchagua amtakaye na si tumtakae.Na kama tungekuwa na uwezo wa kuchagua nadhani dunia ingekuwa bado imejaa mana nani angechagua ampendae ili aiage dunia? Bwana alitoa na ametwaa kiumbe chake cha kufanya ni kumuombea Mungu ampumzishe panapoishi wema na watakatifu

 4. Langu jicho Says:

  Natumaini hajaacha misiba EA RADIO na hapo CLOUDS…. maana….

 5. Kimori Says:

  I remember him when he was still in the marketing department of IPP media…It is always so sad when a person dies, especially a young man like Mr Odhiambo!

  May the Almighty God be the greatest Comforter of his family at this particular moment of sorrow…Amen!

 6. Edwin Ndaki Says:

  Binafsi nilikuwa simfahamu.Ila ninaloweza kusema baada ya kusoma wasifu wake.Hakika bado ni miongoni mwa watu tulikuwa tunawahitaji katika TASNIA yetu ya habari.

  Mwenyezi mungu awafariji ndugu,jamaa,mjane na marafiki katika kipindi hiki kigumu.

  Roho ya marehemu ipumzike kwa amani.AMINA

  Bwana alitoa na bwana ametwaa,jina la bwana libarikiwe.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s