BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

FIRST LADY December, 10, 2007

Filed under: Fashion,Mahusiano/Jamii,Mambo Mseto,Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 11:37 AM

 

Pamoja na kuwa mstari wa mbele katika shughuli za kijamii,Mama Salma Kikwete (First Lady) anasifika kwa kupendeza au kuvaa mavazi yakampendeza…vyovyote utakavyotaka kusema.Pichani ni hivi majuzi mjini Dodoma ndani ya uwanja wa Jamhuri wakati wa sherehe za Uhuru.Unaonaje?

Advertisements
 

99 Responses to “FIRST LADY”

 1. mesa Says:

  amependeza sana ila diet plz

 2. salaam salim Says:

  salma kikwete anakula hela ya nchi wabongo mnakaa kusifia,anakula haki zenu nyinyi mnalala na njaa
  na kusifia badala ya kujadili pesa anazotumia zinatoka kwenye mfuko gani!wabongo mmelala!

 3. Joseph Says:

  this is a show-off!

 4. Loly Says:

  Salaam Salim,

  Kwani ulitaka Huyo Mama Salma Kikwete aje kuwapatia ugali majumbani mwenu? Kwamba yeye aache kuvaa na atembee mtupu kwa uvivu wenu? nA AACHE KUVAA KUONYESHA KUWA DHIKI ZETU ZINAMGUSA SANA? NDIO NYIE NYIE MKIFIWA MNAJIPAKA VUMBI NA MATOPE ILI KUONYESHA KWAMBA MMEGUSWA SANA. hIZO NI FIKRA POTOFU. Na wasi wasi sana na uwezo wako wa ubongo katika kuchanganua mambo ya muhimu.

  Hivi hata wewe ungekuwa ndio uko kwenye nafasi yake ungeacha kuvaa? au jamani huwa mnajisemea tu kwakuwa ni SIZITAKI MBICHI HIZI- HATA SUNGURA ALISEMA. Acha wivu wewe utakufa na kijiba cha roho.

  Panapostahili kusifia sifia, pakija pa kukosoa kosoa. Hapa tunazungumzia mambo ya ametoka vipi? kwani swala uchumi wenu wa Kitanzania mama Salma ndio AJIKATE KATE VIPANDE ILI MTOKE NDANI YA UMASKINI WETU?

  Kwanza mama wa watu anajivalia matenge yake mwenyewe wala hana makuu na masuti yenu ya ma hundreds OF Dollars.

  Any way and any how, Amependeza sana sanaaaaaaaaaa

  SHE IS REAL AFRICAN WOMAN!

 5. Matemu Says:

  Loly,
  Kula tano!Umenena ukweli kabisa.Watu kama hawa kina Salaam Salim ni wivu tu unawasumbua au frustration zao.Mama kapendeza,mama anawaka..hilo ndio la msingi.First Lady tunae bwana,tuache matani.Go Salma.We love you.Watanzania tuache chuki.

 6. Leyla Says:

  Loly
  Yaani sijui nikubebe!!Nimependa ulivyomkomesha huyo mjinga mjinga Salaam Salim,anaboer kwa hoja zake sizizo na msingi.

 7. sibah Says:

  hongera endelea kudumisha upendo na amani tanzania, women power.

 8. Majita Says:

  Wewe Loly!

  Mbona unapenda kukurupuka na kuvamia meli kwa mbele????Acha maneno ya ushankupuna. Inaonyesha wewe ni hodari sana na msema Ovyo.Si pahala pake hapa.Utagongwa.

  Umeanza kwa kumshambulia Salaam Salm nikafikiri utakuwa na hoja yoyote ya busara.Ukafikia hadi kuhoji uwezo wa mwenzako wa ubongo kuchambua mambo muhimu.Ajabu wewe unatuletea mambo ya wauza vitumbua mtaani kwetu.Acha kidomodomo mtoto.HOJA YA SALAAM SALM Ni nzito na ya busara sana.Anahoji matumizi ya hela ya sisi wavuja jasho.Nina wasiwasi kama hata kodi umeanza kulipa wewe kwa jinsi ilivyo na mdomo mchafu.

  Unasema mama wa watu kavaa MATENGE.Una akili kweli wewe???Hayo matenge umewahi kuyaona wapi yakiuzwa ili na sisi tukanunue???Unajua gharama za matenge hayo na mashono yake pia yameshonwa nchi gani???Nina hakika akili zako na za mzoga havitifautiani kuwaza.Hilo vazi alilovaa mama Kikwete huwezi kulinganisha na suti unazofikiri wewe ni za bei kubwa.Hilo tenge kwanza limeagizwa (Special order) pia fundi ni fundi maalumu acha aliyebuni maua na mshono wake.Wewe unakurupuka na kusema kavaa matenge.Wewe mjita nini wa majita kisiwani irugwa????

  Nimesikitika sana na unavyohoji eti kama ungekuwa wewe katika nafasi hiyo ungevaaje.Kwa hiyo unataka kutwambia kuwa hiyo nafasi ya mama Kikwete yeye ndo wa kwanza kuwa nayo.Kwa Ma-first lady wengine waliopita walikuwaje?????Au first lady ni mama Kikwete na hajakuwepo mwingine???

  Suala la msingi hapa ni matumizi ya hela (kodi) ya walala hoi.Kaa ukijua kuwa Tanzania hakuna cheo cha U-first lady. Lakini utashangaa kuwa imefikia sasa hadi first lady anapewa majukumu ya kiserikali. Nani kasema???Sisi watanzania hatukumpigia kura Salma Kikwete sasa kwa nini awe bize na mambo ya serikali na aigharimu kiasi hicho????Mara leo yuko mtwara,leo musoma leo kule wakati mmewe yuko safari zingine,na kote anakuwa na wapambe na gharama kibao za serikali pamoja na night kibao.Tusemeje sasa????

  Salma kikwete yeye ni Mwalimu,alikuwa mwanachuo pale kigurunyembe chuo cha ualimu MOTCO siku si nyingi.Ni hivi karibuni tu amekuwa mjumbe wa CCM mkoa fulani.Sasa leo tu nae aanze kutupeleka kisa kawa mke wa Kikwete.Araaaa.
  Jana nashangaa eti katumwa kuongea na mahujaji waliokosa usafiri Dar.Araaaaa. Kama nani???Msaidizi wa Rais,kwa lipi??? Katika cheo kipi ATC???Kwa gharama zipi kumpeleka huko Airport na wapambe wake. Ina maana Mama Salma Kikwete ni msemaji wa Rais anayeshughulikia wenye matatizo na ATC???Kuna Waziri wa wizara hiyo,manaibu,wakurugenzi,mameneja na watu kibao serikalini kushughulika hilo.Sasa yeye cha mno hadi kumwacha mmewe Dododma ili achukue usafiri mwingine na walinzi juu hadi Dar na kurudi.

  Kwa hiyo itabidi tufanye hivi.Ukiwa
  Rais—Mkeo msaidizi.
  RPC—Mkeo??????
  Jaji Mkuu–Mkeo???????
  Hakimu—mkeo????
  OCD–Mkeo ?????
  Mkuu wa majeshi–mkeo????
  Mganga—Mkeo??????

  acheni hizo nyie,tuna uchungu eti.Mbona Nyerere hakuwahi kumtuma Maria akamfanyie kazi za Serikali.Unafikiri yeye hakuwa first lady??Mbona na yeye alikuwa mwalimu kama mama Kikwete tuuuuu.
  Majita hapa

 9. Kalumanzila Says:

  Nakupa tano Majita. Umemaliza kila kitu… kwa kweli umetoa mchango ulioenda shule hasa….. IMO.

 10. Wapiwapi Says:

  Ha,ha,hahaa! I like the heat.
  Salma kapendeza ingawaje,du, kajirundikia sana miguo!
  However, swala la ATC na mahujaji limenigusa… Kwani viko wapi vyombo na watu wanaohusika? Tanzania tunaendesha mambo kienyeji (kisiasa) sana ndiyo maana tunaua mashirika yote!

 11. Manka Says:

  Majita unapatikana wapi, kichwa kinafanya kazi kuliko naniii.. nini tena nimesahau!!!

 12. lily Says:

  jamani mbona tunakwenda nje ya hoja? hoja ni kwamba kapendeza.sasa kapendeza hajapendeza? nafikiri kila mtu anyejua nguo na kuvaa anaona.ila ningependa nipate picha ya mbele hii imepigwa kwa pembeni.pia tunaomba picha zake nyingine kama itawezekana

 13. Hujaji Says:

  Kwa taarifa yenu Baba yake au Mama yake na ndugu zao kibao ni miongoni mwa waliokwama uwanja wa ndege…

 14. Hellen Says:

  Kupendeza kwa Mama kimekuuma sana mjita?yaani mpaka unasema Kwa hiyo itabidi tufanye hivi.Ukiwa
  Rais—Mkeo msaidizi.
  RPC—Mkeo??????
  Jaji Mkuu–Mkeo???????
  Hakimu—mkeo????
  OCD–Mkeo ?????
  Mkuu wa majeshi–mkeo????
  Mganga—Mkeo??????
  Anyway ndio binadamu tulivyo,kila mtu na riziki yake apa duniani.Tuombe mungu na tufanye kazi sana.

 15. ANNA GABRIEL Says:

  YEAH SHE LOOK NICE.BUT DIET PLEASE

 16. salama lema Says:

  habari ya wote huko dar, mimi nimeona mama kikwete kapendeza sema badala ya kusahidia watu ambao awana pesa ya nguo au kula wanapenda kujionyesa sana hao wake wa raisi na kikwete mwenyewe, nchi yetu ni chafu sana balabla zimealibika,maji hakuna hapo dar sema wao wanajinunulia nguo na magari tanzania yetu haita endelea na watu wataendelea kufa na magonjwa mbalimbali asanteni sana

 17. Nerra Says:

  Yaani sielewi, kuvaa inakua issue! mama kikwete anajipenda kabla ya kua first lady yaani ni smart changieni mada zingine lakini sio nguo zinamaliza hela za wavuja jasho.

 18. Kimori Says:

  Those who understand a snippet in the realm of economics…it is quite clear that it’s damn expensive to prepare that single piece of cloth for a single person…and to make it worse to be worn on a single independence day!

  We have a lot of first ladies around the world, but ours is very peculiar…I would be much happier to see her in a classroom teaching and bodyguards surrounding the school!

 19. trii Says:

  hadi raha anavyopendeza,lazima awe kioo cha jamii,hata akiwa kwenye mikutano na wenzake she looks presentable,thats how 1st lady should look like.

  endeleaaaaa mama kikwete.

 20. Jennas Says:

  Majita kula tano kijana wangu

  Hivi fikirieni sisi watanzania na wafanyakazi wa kima cha chini unakuta mtu wapokea 60elfu unakatwa kodi cjui madubwasha gani unaenda na 20thousand home hapo majukumu kibao ambapo hiyo ela umeisotea mwezi uzima.

  Kodi zinaenda wapi wajameni(Nimetoka nje ya mada ila inastaili kujua hilo tena baada ya majita kunikumbusha)

  Hivi huyu mama kwanini asingeendeleza hata kusoma ama akasaidia watoto yatima hizo gharama anazotumia na wapambe wake akajenga jumba moja kubwa sana aweke jina lake kwajili ya watoto yatima.

  Mmmmh kupendeza kapendeza lakini haituhusu na kama she’s beuty hiyo ni nounsese kabisa.

  Embu mie niwatumikie wadosi nipate kufaidisha wengine

 21. Matty Says:

  Jamani Kapendeza mpeni sifa yake, masuala mengine hata tukisema hapa hayatabadilika, nadhani ndo kwanza atazidi kubadilisha viwalo.
  Whatever anatumia hela za serikali kuvaa muacheni mbona anaomfano mzuri tu analea mtoto yatima aliyetupwa na mamayake au hamkuona picha za Birthday ya Jk?si tu kama lazima yatima wote na wenye shida awasaidie yeye coz she is first lady hata sisi pia kama tunachokidogo tutoe fungu la 10 kwa moyo mmoja tutaongezewa.
  Wanaomponda jamani kuweni wastarabu hapo kapendeza full stop!!

 22. Panjee Says:

  well, hw do you expect a first lady to look like?? she has a very important position in this society, yule aliyepita yeye hakuvaa, kanunua ma flat ya mamilioni pale Ilala kama si mabilioni mbona hamkusema akatoe misaada??

 23. asaki Says:

  we mjita mpiga domo usituletee siasa zako apa. nyie ndio walewale mkiwa nje domooooooooo mkipata madaraka kidogo ndani ya wiki tumbo ka pakacha.kwanza mwenyewe cajabu hata kodi yenyewe hulipi mpiga domo.
  MAMA KAPENDEZA HILO NDIO SWALA ZIMA.

 24. Mpoli Says:

  Majita,
  Kimsingi unazo point katika mada unayoiongelea.Tatizo lako ni kwamba umekuwa kama wale wanafunzi wanaoingia kwenye chumba cha mtihani kisha badala ya kujibu maswali yaliyopo kwenye karatasi ya mtihani wao wanatunga maswali yao wenyewe na kujipa majibu yao wanaoyajua.Mara nyingi huwa wanakuwa sahihi kabisa ingawa kwa sababu yalikuwa sio maswali ya mwalimu(yaani ya mtihani) basi wanafeli.Kwa ufupi uko nje ya mada ya msingi.Ulichotakiwa ni kusema kapendeza au hajapendeza?Otherwise hayo mengine yooote unaonekana mtu mwenye wivu tu.JK anatunza mkewe,na wewe tunza wako.Mvalishe vizuri,sisi tupo wa kusifia.Kama unataka kumjua fundi wa nguo za Mama Salma sema tu watu watakusaidia.Made in Tanzania hizo.Shangaa shangaa tu.

  Halafu kwa nyongeza tu,Mama Salma hajaanza kuvaa leo.Anajipenda tangu enzi na enzi.Uliza wanaomfahamu.

 25. Anne Says:

  yahh the wome look very nice and good, but it too much have that alote of nguo, please mama punguza kujikoki katika matatizo ya nchi tuliyo nayo

 26. ako Says:

  labda huyo first lady yuko kwenye commpetition na mtu, maana sizani kama kuna kitu cha maana anachofikilia zaidi ya kufikilia kesho watanzania watanionaje,maana kama mtu kama mama Anna mkapa alikua very smart fist lady; hana muda na hujinga kama huo anafikilia atafanyaje kumsadia mume kuinua nchi, ata akitaka sasa hivi kugombea urais anweza kwasababu ni hardworker; sasa huyu kila akilala anafikilia kesho nivaa lemba gani nitoke bomba;

 27. Nay Says:

  Mama Anna gani alikuwa very smart lady? Kwa sababbu alikuwa anafikiria maslahi yake na jamaa zake?

  Kweli watu wanadouble standard, hebu usingumzie mambo ya watu waliofanya biashara wakiwa ikulu, walio nunua majumba na maghorofa ya serikali wakiwa Ikulu, walioweka jamaa zao (Net group solutions partners na Simu limited) mahali nyeti ili waweza kufaidi. Tuachane na hayo.

  Huyo mama kapendeza na vitenge vinatengenezwa hapo hapo bongo, Hatters acheni wivu, alivyokuwa ana vaa masuti ya nje mama Anna hamkusema, alivyojilimbikizia majumba ya maghorofa kimya? Leo Salma kuvaa tu imekuwa mwao? Je na yeye aanze kununua kama mama Anna ndio mtamuona smart sio! Acheni acheni kabisa kulete chuki kwa mambo yasiyo maana. Hata kwa mshahara wako hicho kitenge unanua hakikushonwa kwa nyuzi za gold.

  Huyo mama kapendeza mwenye wivu ajinyonge. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. La waswahili, hivi wakeni zenu hawavai nguo kwa sababu Tanzania kuna shida? Au kwa kuwa mumewe ni Raisi basi anapewa tu pesa bila mpangilio maalumu au anatumia mshahara na allowance za mumewe. Kaazi kweli kweli.

  Zungumzieni mambo ya kufanya ili kuondoa umaskini na huo umaskini hauwezi kuondolewa kwa kuacha kuvaa nguo. Watu wavae kaniki, shuka na madurufu kwa kuwa wanashida? Nenda Tandika na Manzese uone wanawake wanavyovaa pamoja na shida zilizopo. Hukuti watu wanatembea uchi hata kijijini!

 28. neutral Says:

  WACHANGIAJI WOTE HAPO JUU,MMEGUSA KILA KITU.NAFURAHI KUONA WATANZANIA TUNAVYOAMKA NA KUJUA HAKI ZETU ZA MSINGI,BINAFSI NILIKUWA SIJAFUATALIA SANA KATIBA YA NCHI KIPENGELE CHA MAMLAKA YA RAISI NA WATENDAJI WAKE ,BAADA YA KUPITIA COMMMENTS ILIBIDI NITAFUTE VIFUNGU/MISTARI HASA YA MAMLAKA YA RAISI NA SERIKALI KWA UJUMLA.FIRST LADY ALIKUWA HANA NAFASI YOYOTE YA KUMUWAKILISHA RAISI ,SWALA LA HIJA LILIKUWA NI LA KIJAMII (KIDINI) ILA KWA KUWA SHIRIKA LA NDEGE NI LA SERIKALI,NI WAJIBU WA WATENDAJI WA SERIKALI KUINGILIA KATI,MAY BE ANGEENDA KUTOA POLE TU KAMA MAMA WA KWANZA ,LAKINI SIO KUMUWAKILISHA RAISI (RAISI NI SERIKALI) HANA MAMLAKA HAYO,OTHERWISE INAONEKANA KULIKUWA NA WANAFAMILIA WA KUWAPA POLE.KUNA KIPINDI TONY BLAIR ALIENDA NEWYORK WEEKEND (SUNDAY)KUCHEZA GOLF NA RAFIKI ZAKE
  AKATUMIA NDEGE YA SERIKALI ,WATU WALIMHOJI KUTUMIA VIBAYA KODI ZA WANANCHI KWA MAMBO BINAFSI,WAKATI TICKET YA BUSINESS CLASS NI CHINI YA PAUNI 200.KUHUSU VAZI NAONA NI LA KAWAIDA TU SIJAONA MICHIRIZI YA GOLD AU PLATINUM KWENYE NGUO,HATA MAI WIFE WANGU WA SISI KIPATO CHA CHINI ANAWEZA KUAFFORD

  WAKILISHA

 29. priska Says:

  salaam sijui una mambo!Loly niko pamoja nawe!!!
  wabongo ovyo ukipendeza ooooh anakula pesa zetu!!!
  mama mkapa alikuwa yuko yuko tuuuuu oooh first lady gani!!!
  mnataka nini???????????
  kapendeza hata me nikiwa na pesa lazima nipige pamba alaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!
  kama first lady kula pamba muhimu!!!
  Marehemu Amina Chifupa kala pamba wabunge wenzie majungu inaonekana wabongo tuwe na pesa tuwe maskini majungu hatuachiiiiiiiiiiiiiiii!!!ovyo kabisa!!!
  mtakalia hivyo hivyo!!!majungu tuuuuuuu!!!
  kula pamba mama Kikwete!

 30. rehani Says:

  wewe mama mkapa kichwa kile ndio mnasemea uzuri sijui lakini kichwani sio kama wewe DR yule

 31. salaam salim Says:

  Loly wewe naona hujui maana ya Demokrasi! wakufundishe
  kwanza maana yake halafu zungumza point! watu duniani wanataka maendeleo sio kuvaa nchi zenye Demokrasi makingi wanapanda town treni na raiya wao ili nchi iyendelee sasa wewe unamwambia mtanzania hajakula siku tatu na ana VVu na umwambia kuhusu mama kikwete ambae anafikiria kila masaa matatu avae nini! haileti maana kwa nchi kama Tanzania!

 32. punani Says:

  Watu mna matatizo sana angevaa kaniki awe mchafu mchafu pia mngemsema. na ndio maana hatuendelei tutaishia kusemana tuuu kwa mambo yasiyo na msingi. picha imetolewa kuwa mama kaepndeza. hayo ya mahujaji n.k yana mahala pake. Kwanza anajitahidi kutoa ajira kwa watanzania. Fundi wake ni mtanzania na anatumia rasilimali za Tanzania. Kamuulizeni aliye pita alivyo multi milionea mpaka ukoo wake wote wacheni kabisa msiyoyajua. mlitaka aishi kimaskini ndio muone yuko sawa na ninyi. Mke wa rais ni mke wa rais hata unge kuwa wewe ungevaa vizuri pia.

 33. Nay Says:

  Nakuunga mkono Punani, kwa uliyosema sina la zaidi la kuongeza, labda niwaambie tembeleeni mitaa ya Kariakoo! Muone watu wanavyojazana madukani kununua vitenge na batiki na lesi lesi kibao. Na maduka yanandelea kufanya biashara na watu wanasafiri kwenda kuleta lesi. Kungekuwa hakuna wanunuzi maduka yangefungwa zamani!! Mwanamke kuvaa hata ukiwa masikini!

 34. Edwin Ndaki Says:

  Samahani naomba break.Muhudumu .wasikilize wote…bill lete kwangu.

  Usisahau mimi niletee kama kawaida.

 35. mkereketwa Says:

  Watanzania wenzangu, mimi naona nimepitwa na wakati, First Ladies wa Tanzania walioiwakilisha Tanzania kwa kusaidia jamii na bila ya kuvaa VITO VYENYE THAMANI NA DESIGNER CLOTHS NI MAMA MARIA NYERERE NA MAMA SITTI MWINYI. Nakumbuka miaka hiyo nikiwa nakwenda kwenye magwaride ya sherehe mbali mbali ya Uhuru, muungano na kupata nafasi ya kuwaona Viongozi mbali mbali na First lady sikumbuku kuwaona wakiwa wamevaa Vibakuli au madunguli ya dhahabu au diamonds sana sana utaona kitenge cha urafiki kilichosjonwa kwa ustadi na shanga za kiafrika. Na walifanya kazi na sio biashara wakiwa IKULU. Nadhani inabidi miiko ya Viongozi Baba wetu wa Taifa alikuwa akiisema wakati wote inabidi iangaliwe kwa ukaribu kabisa. Hatukatai mama yetu lazima apendeze lakini anaweza kupendeza bila kuvaa nguo too expensive na dhahabu zinazoonekana kuwa zimegharimu FORTUNE, wanawake twaijua thamani ya dhahabu ile ya manjano!

 36. Nay Says:

  Hama ama kweli mmeshasahau mara hii? Mama Siti gani leo wamsifu hapa kwenye blogu? Mama wa watu alivyokuwa Ikulu hakupumua hata kidogo, kila siku mlikuwa mnamsakama kwenye magazeti, mara hivi mara vile ooh Ikulu inaendeshwa na mwanamke, mara anafanya biashara Ikulu. Hivi mnafikiri tumesahau au wote ni vijana wa leo? Yaani hakuna first lady aliyesakamwa na kusingiziwa kashfa kibao kama Mama wa watu Mama Siti Mwinyi. Lakini alinyamaza kimya yeye na mumewe. Soma gazeti la Raia Mwema kuna mtu ameandika makala ya kumuomba msamaha Mzee Mwinyi. Tena mwandishi wa habari.

  Looh Double Standard, alivyoingia Mama Anna wala sikusikia maneno na kashfa kama alivyokuwa anatupiwa Mama Siti hivi mlienda likizo? Sasa mmerudi tena?

  Huwa mnatumia vigezo gani? Kama ni kuvaa dhahabu hata Mama Siti anavaa ni jadi ya wanawake wa kiswahili halafu kuna nyingine zinaitwa rusha roho usirukwe na roho bure!

  Haapa sio mahala pake lakini mtu ukishafikia ngazi ya juu ya uongozi, una uhakika wa kula na kulala pazuri mpaka unaingia kaburini kinachowafanya watu na usomi wao kujilimbikizia mimali tena kwa njia isiyo ya halali ni nini? Wakati una uhakika wa maisha yako tambarare? Faida ya kisomo chako ni nini?

 37. kano Says:

  mwenye wivu ajinyonge, huyu firts lady ni kiboko, na ametulia kabisa. Hana papara za hapa na pale, ni mtu wa ajabu sana sana. Endelea ivyo ivyo salma, Tanzania is behind you. Ni mwanamke muwazi kwa watanzania wote kwa ujumla, hana ubaguzi big up salma. You are truly a star in Tanzania and Africa.

 38. bano Says:

  huyo mwenye jicho baya na alie. Salma umependeza tena sana, mafundi kazaneni na ongezeni bidii ya kazi. Mvalisheni mama yenu jamani. Mtu wa watu huyo. Na ana akili sana anajali mtu yoyote, kwa roho moja na nyeupe.

 39. jano Says:

  amependeza kweli, mwenye jicho baya alifumbe, akifumbua anamuona salma kapendeza. Big up

 40. Edwin Ndaki Says:

  wazima wazalendo…duu hapa inabidi tupaite TRAVENTINE magomeni.maana naona sasa ni rusha roho na uswazi…

  Tunataka no or yes with the reason sio ubishi bila point.Anayehusika sms delivery..hatutaki habari za kwenye kahawa…au za saloon…lol..msikasirike sana jamani..nawatania tu

 41. kalili Says:

  Jamani watanzania hamna dogo, wakati ule wa Mkapa watu eeh mbona mke wa mkapa hapendezi, sasa Salma anapendeza oooh mbona watu wanakufa na umaskini. Salma Mwaego umependezaaaaa weeeeh. Kalagabaho vimtimanyongo wengiiiii

 42. banso Says:

  nakubaliana na kalili, kalagabaho wengi sana jamani wasemeni ili tuendelee kudumisha amani, huyo mama kapendeza 100%, vimtimanyongo wengiiii, tena wana hatari kabisa kwa taifa letu. i love you salma.

 43. schola Says:

  JAMANI MIMI NIMEKUA NIKIFUATILIA HOJA ZOTE ZA WACHANGIAJI HAPO JUU UNAJUA HAPA KINACHOONGELEWA ZAIDI NA HOJA ZINAZOTOLEWA KWA MTAZAMO WANGU NI WENGI NI WIVU HUYU MAMA ANA MWILI MZURI HATA MKIMPA GUNIA KULIVAA ATAPENDEZA NA WATU WATASEMA KALITOA WAPI HICHO KIVAZINI JINSI ALIVYO KUNA WATU KILA ANACHOWEKA MWILINI KINAONEKANA KIZURI NENDA KAVAE WEWE KAMA HUKUONEKANA KITUKO,NI UMBILE LAKE TU NA KUJUA KUJIPANGILIA MBONA ANAVAA NGUO ZA KAWAIDA SANA VITENGE VYAKE HATA WAKE ZENU WANAVYO MBONA HAMSEMI JAMANI NI UMBILE LAKE,MIMI NAOMBA TUACHANE NA HOJA ZA KIPUUZI HIZI NI ROHO ZA KWANINI NA WATU KAMA HAWA WENYE ROHO HIZI HUWA HAWAFANIKIWI MAISHANI.

 44. Dida Says:

  MH JAMANI HEBU TUWE NA AKILI ZA KUREASON SOMETIMES! KAMA HOJA NI KUVAA DHAHABU WANAWAKE WANGAPI TANZANIA WANAVAA DHAHABU? UTAKUTA WAMEPANGILIA MACHENI, MAPETE; NA MAHERENI, MFANO MZURI NI KHADIJA KOPA NA WAIMBA TAARABU WENGINE, JE NA WAO WANAWAIBIA WALIPA KODI? HILO NI VAZI LA KAWAIDA MTU YOYOTE AKITAKA ANAWEZA KUVAA. MSIMSAKAME KWAKUWA YUPO IKULU AU MKE WA RAISI,
  NAOMBA NIWAULIZE NYIE MLITAKA AVAEJE? KWA NINAVYOELEWA MIMI CHOCHOTE ATAKACHOVAA LAZIMA KINA GHARAMA AU KUNA MAVAZI YA BURE?

 45. lola Says:

  na kweli watanzania nakubaliana na maelezo yote hapo juu. Watu wenye roho za wivu ni hatari sana kwa maisha yetu, jamani. Acheni wivu binadamu, mnaumiza wenzenu vichwa, na huyo mwenye jicho aache kabisa, kwani wengi tunalionaga.

 46. Emma K Says:

  Hivi Majita akili zake zimo kweli jamani ha ha ha ha ha , dizain alizungusha. Huyu mtu jamani naona ni wale Vichwa vya Panzi, anasafiri kwenda Tanga, anapanda gari la kwenda Songea.

  mimi naona huyo loly hajakosea hata kidogo. kwani huo uchumi anaozungumzia huyo majita unatokea wapi kwenye mavazi ya mama Salma kikwete? ili hali tunazungumzia mama wa watu ametoka vipi na hizo pamba. Wewe kama una maelezo kuhusu uchumi, subiri hoja za uchumi, halafu utoe reference za hizo nguo labda.. pengine kama zina mantiki

  Mimi nadhani swala la kupendeza na nguo ni mwili wa mtu, mwingine hata akivaa nguo za mamilioni hapendezi, na mwingine ka mtumba tu ka mia anatoka bomba.

  Wewe majita, kama umeoa au hujaoa na una demu, basi demu wako ni mbaya kupita kiasi.

  Mama wa watu kapendeza jamani, kwanini roho zinawauma?

  Huyu majita ni mpuuzi na mjinga sana, kama loly alivyosema, naona yeye pia ubongo wake una ka MOSHKELI

  Tulia wewe na usituletee upuuzi wako, ovyoooooo

  BIG UP LOLY

 47. Abdallah Says:

  Hakyanani tena kaazi kweli kweli humu ndani, nimecheka sana.nimesoma hizo hoja hapo juu duu!! kweli watanzania tuna safari ndefu ya kujikomboa kifikira. Kwani mtu akivaa vizuri kuna tabu gani? Huyo mama Salma kikwete kuvaa vema kumbe kuna watu zinawakera sana.

  Huyu majita anasema ana hasira sana, best ulikimbia umande? nini fujo wewe kwani kuvaa vizuri ni ajabu? ina maana wewe huwa huvai ukapendeza? nadhani wewe watisha ka jina lako.

  kwani huko Airport ulitaka wewe uende kuwatembelea wahujaji? kama mama Salma amekwenda, ameenda pengine kivyake tu, kuwapa moyo na kwakuwa yeye pia ni mwislamu anaelewa hayo mambo zaidi ya yote ni mama. Kwani mpaka kuwe na sheria ya kwenda mahali. Kwani hao mawaziri wahusika hawakupata hizo taarifa kwanini hawajaenda?

  Mimi nadhani kwenda pale kuwapa moyo mahujaji,lilikuwa swala huru, na kila mwanajamii mwenye uwezo wa kwenda angeenda,hata wewe MAJITA nadhani ingekuwa vema ungepita pale kuwapa moyo na matumaini, hata kama usingetolewa kwenye gazeti au TV, awe waziri,naibu waziri, katibu,mkurugenzi, kila mmoja alikuwa huru kwenda. Lakini yeye pale binafsi naona amekwenda tu kama First lady ndiyo, na pia kama mama mzazi yeyote. Kwahiyo kuhusu hilo Majita naona halina maana na hujatumia akili yoyote ila ndugu yangu.

  Pia kuhusu kumsifia mama Salma, nadhani amependeza sana tuu, kama mama yeyote ambaye anajipenda. Wewe nadhani kwa hilo una tatizo.naweza sema ni wivu usio wa maendeleo. Huo ni ule wivu wa ukiona mwenzio amejenga nyumba unakwenda ipiga moto, watu kama hawa ni hatari kwa maendeleo yao wenyewe na Taifa pia. Maana hakuna jema mbele ya macho yao

  Na pia, Tunaomba usiwe unatuchanganyia habari, hapa wameuliza je mama kapendeza au la, jibu lako lilitakiwa ndiyo au hapana, sio unatuletea propaganda zako kama za Lyatonga mrema, zisizo na data zozote.

  Kweli Majita acha kutuletea habari ya kuchanganya BIA na CHAI.

 48. Mary Says:

  Ushamba kazi.

  Hivi kwani ni wamama wangapi bongo wana shughulizao, tena biashara zao za kawaida wanavaa matenge ya nguvu na wanapendeza?

  Kwahiyo watu walitaka mama wa watu avae NINI? mama wa wazamani alivaa suti wakasemaa oohhh kazi kuvaa masuti, maskini huyu kaja na matenge, oohhh kazi kuvaa matenge ya ghali.

  Hivi mm nadhani swala la nguo ni dogo sana, isitoshe hata mm napenda kuvaa tu vizuri,na naimani hakuna asiyependa kuvaa bwana wala msitudanganye.

  Acheni wivu, ni first lady, lazima avae, mbona hayo matenge ni ya kiwanda cha hapa bongo, hasira za nini, si mshone halafu mtuletee picha zenu hapa kama mwataka?

  Loly kweli wewe nadhani upo civilized, maana matenge ya mama salma hayawezi kutupunguzia umaskini.

  Pia nadhani hali zetu ngumu kimaisha, zinatufanya tuwe na wivu na chuki za kijinga, kiasi kwamba mtu akimuona mwenzie kapendeza au ana mafanikio kidogo na ya kawaida anatamani kumtafuna, lakini pia tukumbuke hatuwezi kulingana kamwe, mbali na matatizo yetu ya kiuchumi, hata kama rushwa ikiisha, bado hatutaweza lingana kamwe!!

 49. lola Says:

  abdalah, emma, mary wote mnaongea points kali sana, huyo mama kapendeza kalagabaho, vitimamnyongo, wafundisheni adabu, amewaka waka tena sana, huyo mwenye wivu aliye machozi yamtoke.

 50. Matty Says:

  Mhhhhhh!hii nchi sijui itaendelea lini ili kila mtu atake time yake kuliko kuona wivu watu waliosema amevaa mavazi ya gharama sasa wakaangalie picha kule kwa michuzi waone alivyokuwa anfungua branch ya CRDB alivaa nini….jamani mavazi yake ni ya kawaida tu ila yamepangiliwa hebu cheki kavaa kanga ya urafiki begani na nyingine kichwani na katoka bomba tu.
  Wengine kazi kuona wivu na chuki zao binafsi tu Majita mimi nayajua hayo matenge hata kariakoo yamejaa tele kama mkeo hapajui panapouzwa nitafute nimpeleke ashindwe mwenyewe na akitaka nitamsaidia kuchagua rangi nzuri na atapendeza tu, kuliko kung’ang’ania masuti na manguo ya spesho kila siku mwanamke tenge hata mimi huwa najipigilia kisawasawa upo?

 51. hano Says:

  matty nakubaliana na wewe roho moja 100%, mwenye jicho jamani, litawapa wengine ugonjwa wa moyo, semeni tu, huyu mwanamke hana visa na mtu yoyote. Ametulia hata kwenye misafara yake yote, i love you salma, endelea kuwa na roho nzuri my dear, mungu akuzidishie mema duniani, wala huumizi roho za watu, una moyo mmoja kabisa.

 52. Matty Says:

  Hano si unajua waswahili walivyo asingevaa wangesema first lady gani hata hajui kuvaa, sasa anavaa wanachonga juu yake jamani muache roho za kwanini wapendwa hapo ubaguzi ndo unapoanzia miongoni mwetu siye wenyewe tena swahili/black people du kaziiiiii kweli kweli.

 53. Kekue Says:

  Let me tell u 1 thin ee, unajua unaweza ukavaa nguo ya bei rahisi ila ukapendeza balaaa, na utavyopendeza wa2 wanadhani ile nguo ni bei ghali, pale ni vile umependeza tuuu!! sasa huyu mama ni vile amependeza lakini hizi nguo sio za bei kubwa mpaka muanze habari ya kodi, anakula hela ya nchi mara nini sijui he!!! Hata m2 kama wewe ni nini maana ya kuwa mke wa Rais?? mwacheni avae hata akivaa dhahabu tupu ni wakati wake!!! lazima kuwe na tofauti kati ya mtu wa kawaida na mke wa rais alaa!! Msinipe hasira mimi.

 54. Matty Says:

  Safi sana Kekuu waambie maana wamezoea mtu asivae kisa eti anaogopa watasema, du waswahili hawana dogo.
  Mbona hivyo vitenge ni vya kawaida sana kila mtu anaweza kuvaa jamani wapendwa tuache hizo za kidomodomo.

 55. salaam salim Says:

  Majita tungekuwa na watu kama nyinyi nchi ingeendelea
  lakini Bwana loly ndio serikali ya Tanzania ndio inawataka! wakati wa uchaguzi akipewa doti ta kanga anafunua paja! Point ni kuikomboa Tanzania! watu wapate kazi! Bakteria ambao wanatengenezwa nchi za ulaya na marekani wasijaribiwe Tanzania! mzungu sio analosema unaitika Yes kwa sababu ya msaada wake! Raisi atumie mshahara wake kama waajiriwa wengine na mama kikwete aombe kazi kama watanzania wengine na asipewa kazi akiangaliwa kama mke wa raisi. Mungu ibariki Tanzani(Amin) Majita your the Bom!!

 56. any Says:

  HUYU MAMA AENDE MWANAMBOKA AKASAIDIANE NA YULE MWANAMITINDO WA PALE, HUKU ANATUONYESHA MABAZEE TU, ANASAIDIAJE JAMII, ZAIDI YA KUPENDEZA MAVAZI.

 57. sibah Says:

  watanzania ni vuzuri mnapotoa maoni yenu. Salma atujibu basi, kusema anaonaje haya, ili tuone kama anapata ujumbe, wa watanzania mtandaoni, jamani mwenye website, mfikishie ujumbe.

 58. salaam salim Says:

  Sibah you get the point! we need u (Viver TAnzania)

 59. Kekue Says:

  Tehe tehe!! salam unasema rais atumie mshahara wake kama waaajiri wengine, ni hicho kitenge tu mama salma alichokivaa hapo ndo mnataka apangiwe mshahara he!! Makubwa!!! kwani ndo mkewe hata vaa? Mshahara unakuja unapangiwa, mama anapewa hela yake ya matumizi anaipangia vilivyo!! au wewe hutoagi hela ya matumizi??

 60. Matty Says:

  Salaam Salim, unataka kusema nini hapa ni Fist lady gani aliyepita ambaye aliwahi kuomba kazi akawa sawa na sisi wenzangu na mie? na hata nchi zilizoendelea ni yupi tupe vivid example pls don’t cheat us.
  Kekuu watu wananongwa nimeamini kitenge tu ndo kitafanya maendeleo??????kama hajaajiriwa you never know kama dingi anampa mshiko wa kutakata asivae??kwani wanawake wangapi ni mother house lakini waume zao wanawapa mshiko wa mboga heavy na kinachobaki mama anajipigilia mwilini upo???nadhani unanipata na kama wewe mkeo unambania kiasi hicho ni ujinga tu tena unachekwa wewe.

  Maendeleo si tu kama lazima first lady avae vibaya ndo yatakuja wewe umemuona huyo sababu kawekwa hapa wakiletwa na wake za vigogo wengine wa serikali wanaoting pamba za gharama sijui utakuwa na la kusema jamani kila aliyenacho basi achangie asiye nacho ili tuendelee full stop!!!!!!kazana kuvaa mama.

 61. sibah Says:

  sasa salma, mbona hajibu jamani, kwani maoni yenu ni muhimu sana, we mwenye website umewasiliana nae, maana watanzania wengine wana maoni ya maana, ajibu basi. Tusibaki kuandika tu, amepata ujumbe.

 62. lim Says:

  Matty,loly,Mary,Emma k,Abdallah, jamani nawapa Big up,
  I like that people. Simply, hata mm huwa napenda kuvaa vizuri nipendeze, japo sio tajiri, na maisha yangu ya kawaida.

  Hivi huyu salama salim na Majita sijui wametokea wapi? nadhani ni watu wanaotisha, maana kama mtu hapendi mwenzio apendeze, huyo ni hatari.

  Mara uchumi mara democrasia, mkoje nyie si mkaongelee hizo issue kwa wataalamu wa uchumi, nguo tu zinawapa homa na amevaa vitenge vya urafiki, vya hapa bongo.kAMA HALI NGUMU KWENU CHAPENI KAZI ACHENI UVIVU, NA MVAE VIZURI. daima mwenye wivu wa dizaini hiyo kufanikiwa ni ngumu.

  Hivi kumbe kuna watu wana akili kama soli za viatu, hata umwambie hichi kitu kizuri hakubali kamwe, hii ni hatari kweli kweli.

  MAJITA NA SALAMA SALIM ACHENI WIVU, MAMA SALMA KAPENDEZA.

 63. Neema Says:

  Duhh Jamani mama salma kapendeza kweli. hivi vitenge vipo tu mbona madukani, si mvinunue mshone. Naona mna complicate life watu. Is not a big deal kuvaa vizuri.

  I like mama Salma, keep it real

 64. Majita Says:

  KWAKO ABDALLAH NA MATTY NA WENZENU.

  Nashindwa kabisa kuwaelewa na napata kigugumizi jinsi ya kuwasaidia ili japo mpate kuelewa nusu ya ninayofahamu.Wewe unaehoji mtu kuvaa tu kama kunaweza kuathiri uchumi,UNA AKILI KWELI???Unaujua huo uchumi au tunaongea na mbumbumbu. Umewahi kusoma principles za uchumi???kwa mwanauchumi hata shilingi moja kwake inamaanisha kitu.Ije kuwa kuvaa!!!!Hivi wewe unajua mvao mmoja wa mtu extravagant ukoje?Wewe kalia tu na kufikiri gharama za kuvaa kwako hiyo mitumba yako ndo wote wanavaa hivyo.Labda kwa kukusaidia tu siku moja fanya utafiti wa hao mafisadi gharama zao za kuvaa kuanzia kiatu hadi kichwani halafu ujue kuwa hiyo ni siku moja tu na fuatilia hiyo nguo atairudia baada ya siku ngapi,utapata anatumia kiasi gani kwa mavazi tu kisha ujue kama kuvaa tu ni hivyo what about the other stuffs.

  Namshangaa sana eti anajiita ABDALLAH kumbe mla nguruwe tu huyu.Yani wewe jina lako lina-sound like mwislam kumbe hamna chochote.Mwislam gani atakae sema huyo mke wa Kikwete kapendeza???Kwa mwislam hapo atasema yuko uchi.Sasa sijui mnasema kapendeza kwa vigezo vipi.Huyo mama ni mwislam na kum-judge kama kapendeza tungemwona kafunika mwili wake.Wewe Abdalla jina hili ni la cheti tuu nini.

  Nimependa ulivyosema nimekwepa umande. Hujakosea ndg yangu kwani familia yangu kule majita ilishindwa kunisomesha na sasa nasoma Elimu ya ukubwani(ngumbalu) baada ya kufeli sehemu zifutazo:-Mukigo s/msingi-Kigoma,Mpwapwa sec(Kwa Mwasamila), Eckernforde Adv Sec(Kwa Kimathi),MOTCO kwa Watu wanaopaswa kufahamu,Mzumbe(Kwa wakata Kiu)na sasa najaribu tena kusoma hii MEMKWA huku majita kwenye mapori ambayo nyie mnayaita Bush.Nafikiri si vibaya kutwambia wewe ndg ambae hukukwepa umande uliukanyaga wapi.

  Matty!!!acha kuvamia mambo yanayokushinda umri.Utavunjwa bi**ra yako.Kariakoo unakaa wewe.Mie nilishasema kwetu ni majita-Bugunda kata ya bwasi tarafa ya nyanja ‘W’ musoma VIJIJINI.Basi la kwenda huko ni Bukwaya au United zilizochoka kabisa na unakula vumbi barabara nzima. Tunategemea uvuvi wa kokoro na kilimo cha mhogo na viazi kama zao la biashara,Sasa huko Kariakoo si mke wangu atapotea???Ungenambia huku majita hayo matenge yanapatikana wapi.HIVI WEWE UNAFIKIRI DAR NI TANZANIA NZIMA????Wakati huyo mwanamke (Salma kiwete)anavaa hivyo kisa sherehe ya siku moja mama na baba zangu kule majita hata sabuni ya kuogea ziwani hawana,chumvi ya kuunga mboga wanaenda kuomba kwa jirani.Hivi una akili kweli??? Nambie kijijini kwenu ni wapi??Je kuna maisha yapi???Dar,Dar.Dar kitu gani bwana.mbona baada ya kuuza samaki nikaja hapa Dar maisha kama ya majita tuu.Nakaa Yombo Dovya ni juzi tu nimehama toka Tandika kwa Abiola.Utasema nini.Hapa jirani zangu hata uwezo wa kununua kandambili hawana,ijekuwa matenge ya urafiki.

  Tena nahisi wewe Matty maisha yamekukamata sana ila ukifika majita utasema kweli hawa Ma first”RED” wanakufuru kwani wewe na umasikini wako ndo utakuwa tajiri wa Majita.Nawashauri mjaribu kuwa mna-read between the lines.
  Ndimi
  Majita mtoto wa mzee Bugunda.
  Mtoto wa Mvuvi wa kokoro.
  Utotoni nilikuwa na kwashakoo.
  Nilivaa viatu aina ya Bora za kijani kwa mara ya kwanza nikiwa form I.
  Sikuwahi kunywa maji ya Bomba hadi Fm I.
  Nilizima umeme kwa shuka nikiwa form I.
  Nilikuwa najipakaa sabuni aina ya kwanga baada ya kuoga.

  Utanambia nini bwana???Sasa hivi nia uwezo wa kuchambua mambo kwa kiwango cha juu kabisa.Nina uzoefu wa hali zote.FUKARA na tajiri.

  So mama Kikwete apunguze matumizi.
  Anavyofanya hayo mashindano ya mavazi ajue kuna watu ambao mmewe anawaongoza hawana hata uwezo wa nusu mlo.Ijekuwa kuvaa!!!!Kikwete haongozi kariakoo tu. Hadi Kipumbuiko huko Singida wanamtegemea.
  Majita

 65. amina Says:

  Jama mbona mna hila?cha muhimu ni jibu moja tu!Kapendeza au hajapendeza,kukosoana au complains hazina mana,mana hata mchone mama ataendelea kung`ara tu,na istoshe hata haya tunayopigizana kelele hana hata time ya kuyasoma,tufanye kazi kwa bidii kivyetu tujenge maisha yetu,ila kushindana na mwenye nacho ni ujinga tu,,,Mama matenge ya haja hayo,yani kama ungeloose kilo kidogo ningekuita model,,ila according to ur age,madaam bado uko kwenye line!!!!

 66. Neema Says:

  majita it seems you have nothing to do, binafsi siwezi kusoma hiyo msg, its soo long, na mtu mwenye kazi na mambo ya maana ya kufanya hawezi andika that much. may be you have some points, jaribu kufupisha.

  I think you better take time to work on u r business, instead of wasting time with people you even dont know them.

  Otherwise, I still support mama kapendeza

 67. Mary Says:

  Thanks soo much neema, huyo Majita anaonekana ni mwanamke, maana nimejaribu kusoma mistari michache, nikaona ni PUMBA ZA NAFAKA ZOTE. na basi kama si mwanamke, basi ni mtoto si ……! GOD FOR BIT!

  WOOOOWWW. TOTALLY NONSENSE!!

  SALMA KIKWETE AMEPENDEZA MWENYE WIVU AJITUNDIKEEEEEEEEE
  AU AJIMALIZEEEEEEEEE

 68. carlos Says:

  Hee wacha niwahi kubeba mabox yangu, nadhani watu wa bongo sasa wameanza kudata mazima.

  Mbona mwamsakama mama Kikwete!amewakosea nini mwalimu wangu? she is still beautifull, kweli kikwete anajua kuchagua, hongera kikwete kwa kuwa na mke bomba.Ulijua utakuwa rais siyo, sawa bwana

  ila mashallah, ametoka bomba mbaya. du kweli bongo kutamu, karibia ntarudi huko, acha nikusanye visenti kidogo!!

 69. zena Says:

  mama salma kapendeza sana, duu.

  MATTY HIVI WEWE ULISHAKAAGA ARUSHA? KWA FATHER BABU HOSTEL KAMA NDIO NADHANI TWAFAHAMIANI

 70. salaam salim Says:

  lim!mimi napigania tu hakiza watanzania hata siko bongo lakini jinsi ninavyoona demokrasi kwa wenzetu nasikia wivu kuona mjomba wako ilula anakosa hata dawa
  hospitali kwa ajili ya uzembe wa watu fulani! Go majita your like julius kambarage nyerere!

 71. sibah Says:

  halafu salma hana papara kama bibi fulani, ametulia kabisa. Na ni muwazi, kabisa kwa watanzania ana roho moja na ya upendo kwa watu.

 72. Mkereketwa Says:

  Mh jamani hembu nyie wenyewe fikirieni kama ndio mngekuwa mama Salma mngefanyaje?Tena mama Salma ni bora kuliko mama flani ambaye kila kitu alikuwa ana-order kutoka nje.Pia mama Salma mimi nimeanza kumuona tangu zamani sana alikuwa ni mvaaji hivyohivyo. Mama wa watu anajua kuvipangilia viwalo hata akienda ugenini bila hata kutambulishwa, anaonekana tu kuwa ni first lady.Sura mvuto “A”, pia ana point za kuongea hadharani na akaeleweka.HAo wanaolalamika kuwa anakula hela za serikali naona mmekosa tu la kusema na ni wivu. Vyovyote vile hata kama nchi ingekuwa maskini namna gani, still ni first lady na angetakiwa kuvaa vizuri tu no mater what. Mimi siwezi kuwa raisi then mke wangu awe anavaa kanini…no way. kwani mnadhani anavyosafiri kila mahali kwenda kuwawakilisha sijui kuwatetea, mnadhani yeye ndio hachoki? Na kokote aendako inabidi saa zingine ajishushe kwa ajili ya wa-Tz wote. Tena ingekuwa ndio mimi, ningevaa ma-gold ili muongee vizuri nyie msioona mazuri ya wenzenu.

 73. kaloi Says:

  mkereketwa nakubaliana na wewe, huyu mama yuko simple, hana za hapa na pale. Leo huku, leo kule, ametulia kabisa, na ni muwazi hata kusaidia maskini, kwani vitu vya duniani vinapita.

 74. maso Says:

  ni kweli ana msimamo kabisa, sio mwingine leo unamuona hapa, kesHo unasikia yuko ughaibuni, walau salma tunajuaga safari zake, maana zinasemwa wazi wazi kwa watanzania wote. Wengine tumeshindwa kuwaelewa kabisa, sijui wana agenda gani kichwani, hetu watuambie. Shukrani kwa wanaokutendea mema, pia sio kusahau, maana na wewe ni binadamu eti, leo kwako kesho kwangu. Salma hongera mwaya.

 75. lanoi Says:

  watanzania wenzangu nakubaliana na maoni yenu kabisa. mwenye wivu anaumiza roho za wengi, ishini kwa amani, cheo ni dhamana, leo kwako kesho kwangu jamani. Tupunguze chuki watanzania kwani ni hatari sana.

 76. Pusi-ndaya Ole Kidongói... Says:

  Kaaanyo kidingita doi Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa Amependesaa

 77. siba Says:

  ndaya ole kidongoi, you are right kabisa. Huyo kalagabaho, anapenda kufanya watu wawe chini kwake, hana hata shukrani, huyo salma wakati wote, ana roho moja, hana majidai majidai.

 78. Matty Says:

  WEWE MAJITA,
  Unaonyesha jinsi gani ulivyo naroho ya kwanini tena hata hujui kujieleza unajitahidi lakini nakudharau sana, unahasira ya Mama Salma kupendeza halooooo!!!!!!umemaliza page na kutaka kupigana na computer yako kisa????????mtu mstaarabu hakai akaandika kama ulioandika wewe Majita.
  Hiyo historia yako nani anataka kuijua hapa???kama unataka kuwa Cerebrity basi weka picha yako tukupe maksi kama umependeza au la!! na i’m sure huwa hupendezi hata ukivaa ndo maana unawashwa mama wa awtu kapendeza, kama unaguswa na wanaovaa kazi kwako!!!!!

 79. kibo Says:

  watanzania mnaongea point kwlei hapa. huyo mwenye jicho aache mara moja, kwani ni wengi sana limewadhuru basi tu wengine tunanyamaza kimya. Ila mwaka ukianza, itabidi apewe lesson na salma, atulie, la sivyo tanzania itamwajibisha.

 80. Fredrick Says:

  MAJITA you have a strength that is struggling to come out. Kuwa mtaratibu mzee ukali ukali kama wa vijana wa getto za Kimarekani hapa Bongo huwa haulipi. Utatulizwa tu.

 81. Kamanzi Says:

  Sina uhakika kama Majita ni mwanamke ila kama ni mwanamke ningependa kumuoa wakati wowote maana kichwani amejaza akili. Ninyi wengine ni matope msiweza kusoma between the lines. Swala sio kapendeza au la, swala ni kwamba huyu mama ni miongoni mwa watanzania wachache wanaopata MAISHA BORA ambayo MUMEWE aliyaahidi kwa KILA MTANZANIA. Nchi imeyumba na itaishia kubaya.

  Mkapa kaiba sio siri hata mkewe pia ila kusema ukweli wakati wa Mkapa tulikua na MCROECONOMIC STABILITY. Heshima ilianza kurudi TAnzania. Ila nawahakikishia mpaka Kikwete anaondoka tutakuwa tumerudi kwenye zama za SERIKALI KUSHINDWA KULIPA WAFANYAKAZI MISHAHARA. Enzi za mtukufu ruksa. WAlau mzee ruksa hakua mjuaji kama huyu chekibobu.

  Watanzania acheni kuongelea wanja na angel face ya Salma Kikwete, hebu amkeni na kusoma alama za wakati, tunakokwenda hakufai.

  NAOMBA KUWASILISHA!!!

 82. salaam salim Says:

  Kamanzi unaongea vitu kama wewe ndio ungepaswa kuwa Raisi wabongo wengine wanaandika tu ilimradi andike wanatupotezea muda! hawajui sisi huku tunawalipia tex ya misaada wanayoipata kwahiyo ukilishwa tafuna!

 83. Mie Says:

  Duh! wote hapo juu mmeandika points lakini walionikuna ni hawa wanne Saalam Salim( mwanzilishi), Kimori mara moja ukapotea), kidoogo kamanzi sijui ni owa mwaitu!, funga kazi MAJITA, Go MAJITA i real like ur comments! kweli umeenda shule, unajua uchungu wa nchi yako. Your words show that there´s something in you, JITOKEZE MAJITA tunakuhitaji, yaani unafaa kuwa mbunge wetu au mpiganaji wa haki za watu, we check wakina Zitto Kabwe mwanzoni hawakueleweka lakini sasa tunatambua nini wanataka katika nchi yetu.

 84. lani Says:

  watanzania ni vizuri, mkiongelea mambo ambayo hamyapendi jamani. Maana, huyo mwenye jicho, hana hata shukrani jamani, madai yuko on top of the world, mbona salma wa kawaida tu. Huyo mwenye jicho aombe msamaha kwa wanachi please.

 85. kijiwe Says:

  UNAJUA UNAWEZA KWENDA SHULE UKAPATA MPAKA DEGREE LAKINI USIWE NA BUSARA MAANA WAKATI UKO SHULE BADALA YA KU KEEP IN MIND KUWA NIPO KATIKA MOJAWAPO YA STAGE ZA LIFE UPO BUSSY KUFIKIRIA MAMBO MENGINE AMBAYO HAYAHUSIANI NA SHULE.HALAFU PIA HATA KAMA HUJAENDA SHULE KAMA HUNA BUSARA BADO UTAKUA KILAZA.NA NDIYO TATIZO LETU WATANZANIA WENGI TU.
  1.HUYO MAMA AVAE ASIVAE MTU WA KUMBANA NI MUMEWE ANAYESAFIRI SAFIRI KA VASCO DA GAMA HAPO MNAWEZA KUONGEA KUHUSU FEDHA ZA UMMA.
  MAMA WA WATU ALIKUWA ANAPIGA PAMBA TANGU ENZI ZILE ALIPOKUWA MWALIMU SHULE YA MSINGI MBUYUNI.
  2.ILE YA KWENDA KUWAONA MAHUJAJI WAMECHEMKA KIDOGO SABABU RAIS ALITAKIWA A-MAKE SURE WAZIRI WA MIUNDO MBINU NA MA BOSS WA ATC WAPO PIA WAKATI MAMA SALMA KAENDA PALE.NI STRATEGY YA KUJENGA LOYALTY KWA WANANCHI (SABABU WATAKUMBUKA ULIFANYA NINI WAKATI WANAPIGA KURA)KAMA KULIKUWA NA NDUGU ZAKE HILO SIO TATIZO LETU.
  3.KAMA KUNA MTU ANA UCHUNGU NA TANZANIA(MAJITA(mpiga mbio za sakafuni) AENDE AKAGOMBANIE UBUNGE ILI AWE NA POSITION YA KUSIKIKA NA JAMII NA ATOE MADUKUDUKU YAKE.
  ACHENI UNAFIKI NYIE WATU MNATAKA KUMBADILISHA PROFILE MAMA WA WATU SABABU MUME WAKE KAWA RAIS.ALAAAAAA

 86. nano Says:

  he, kalagabaho mwingine, ametuzungusha mpaka katuumiza kichwa, sijui tufanyeje, mbona salma katulia jamani. Huyo mwingine, presha juu salma avae nyekundu, njano, matenge anapendeza.

 87. Matty Says:

  Safi sana Kijiwe huyo Majita labda ni mwanamke asiyependa maendeleo ya mtu, mwenye wivu, chuki na ubinafsi.
  Majita nakuuliza kinachokuuma ni nini hasa??????labda lipo jambo si bure Kienge cha mama Salma haliuzwi Milions of tshs upo???utabaki na labda kwa kushupalia mavazi ya watu ndo nyie mtu akipendeza mnanunu…UNALO!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Development is not a dream!! work hard for yours!!!

 88. Tina Says:

  Majita huna nguo ya thikukuu nini??????

 89. Mutoto wa mujini Dar Says:

  Inasemekana huyo salaam salim alikuwa bibi ya …….., sasa tangu mzee ashike hatamu, AMEMWAGWA JUMLA.Anamsikia kwenye PIPE. Kwa kifupi mama Salma ndio anayepeta. Hizi nyumba ndogo kazi kweli kweli jamani
  Humu ndani jamani kumbe watu wana visa vyao wanajifanya wana mauchungu na nchi.

  Dataz aliimba, Mume wa mwenzio si wako, kalagabahoooo
  Usijali salaam, tafuta wako.

 90. Ney Says:

  BIG UP MAMA SALMA KIKWETE U LOOK GREAT, AFRICAN LADY!

 91. kijiwe Says:

  LOL mi nahisi salaam salim na majita ni mademu wanye chuki binafsi!LOL

 92. Nerra Says:

  Jamani naomba nijaribu ku conclude hii issue ya mama Salma, mie kwa jinsi nilivyosoma comments za watu wote ni hivi :- walio wengi wamesema kweli amependeza na wachache wame compalign juu ya matumizi mabaya ya fedha sio hajapendeza hivyo MAMA AMEPENDEZA na si vinginevyo kwani swali lilikua KAPENDEZA au HAJAPENDEZA? sijaona comments ya hajapendeza au wadau mmeliona hilo jibu nisadieni labda nime overlook mahali.

 93. Mama wa Kichagga Says:

  Ukisoma hoja zote 1 hadi 92 hapo juu utapata picha ya mfano halisi wa akili, tabia, na hoja za mtanzania.

  Kwa kifupi:
  1. Wivu ni sehemu ya maisha yao ya kila siku
  2. Kauli chafu za kukatisha wenzao tamaa wamezipa kipaumbele
  3. Chuki binafsi zisizo na kichwa wala miguu ni sehemu ya maisha
  4. Wanapenda kusema maneno ya chinichini wakijipa moyo wao ndio kiboko ya wachangiaji
  5. Wanapenda kuumiza nafsi za wenzao na kuhukumu wakijidai wanamsaidia Mungu majukumu (OLE WAO MAANA ADHABU YAO NI KUBWA)

  MAMA SALMA KAPENDEZA SANA (Kitenge KINAUZWA ELFU 6 TU URAFIKI NA MASHONI ELFU 12 vimejaa Kariakoo na kila mahali au tembelea duka la urafiki).

  Mtu mwenye matusi, chuki, wivu, ukabila, udini na tabia ya kuhukumu mwenzie kamwe Mungu hawezi kumpa baraka katika maisha yake. Atabakia kupiga kelele na kupoteza muda wake siku zote hadi atakapoihama dunia hii. Ukisoma hoja 1-92 unaweza kuwaona wale wote wenye tabia hizi chafu nilizozitaja katika aya hii.

  Ni jambo la kusikitisha sana tena la kukatisha tamaa na kutia aibu mtu anapoanza kumponda mke wa Rais wa nchi yake! Tena kana kwamba haitoshi anawaponda hata maFirst Lady waliokwisha kumaliza muda wao bila aibu! Inakusaidianini ndugu yangu? Ungelalamika angalau kwa mhusika mojakwamoja hapo ningesema angalau ujumbe umefika.

  Rais kashatoka madarakani, mwingine kaingia katoka kaja mwingine ndio unatoa hoja? Huu ni ujinga mtupu na nauchukulia kama chuki na uchochezi kama si wa kikabila basi ni wa kidini ambavyo vyote havina nafasi.

  TUTOFAUTISHE KATI YA KUTOA HOJA/KUCHANGIA HOJA NA KUJENGA UCHOCHEZI MAANA HAPA SIO MAHALA PAKE NA TAMBUA FIKA WEWE UNAYEHUSIKA TANZANIA TAMBARARE UTAKAPOANZISHA VITA YAKO YA UKABILA AU UDINI HUTAUNGWA MKONO MAANA TUMEOANA NCHI NZIMA NA MAHUSIANO YETU NI MAKUBWA SANA LABDA WEWE NA JAMAA ZAKO MNAOISHI KAMA KISIWA!

  Tuwe macho na baadhi ya wachangiaji wa hoja maana wanaweza kutupotosha. Tusiwaunge mkono wasiokuwa wenye hoja za kutungenga na mitazamo ya machafuko hata siku moja! Inawezekana mtu anaugonjwa wa akili na anaandika linalimjia kwa siku hiyo (Chizi Fresh). Tuwatambue watu kama hao kwa kutizama hoja zao.

 94. Mama wa Kichagga Says:

  Mmoja wa wachangiaji ametoa hoja kuwa tuko mbali sana na tunahitaji ukombozi wa KIFIKRA. Namuunga mkono kwa asilimia 100 kwani iwapo fikra zako ni finyu na potofu maendeleo yetu yatakuwa kama ndoto za Abunuwasi!

  – Tubadilike namna ya kufikiri kwanza kama kweli tunataka maendeleo! Swala la mavazi kwa jamii yeyote ni la lazima na muhimu wachilia mbali Mke wa Rais.

  – Wivu, chuki, kisasi ni sumu ya maendeleo

  – Prob ya kuwa ikulu ni ndogo sana, moja ya milioni tisa (1/9,000,000 sawa na ~~ 0.0000001 hivyo sio wote wanaoweza kuwa marais au maFirst lady!

  – Kamwe tusishabikie kushindwa kwa mtu/watu maana haitusaidii

  – Tuwape heshima viongozi wetu waliotutangulia na wake zao. Sana sana tukitaka kuwahoji basi sisi tuwaombee waishi maisha marefu halafu tulete mafanikio makubwa kupita yao ili yaone fundisho ili kama hawakutimiza wajibu wao ipasavyo waweze kupata mwanga wa kutubu ili waingie mbinguni.

  – Tupelekane taratibu jamani maana hakuna mtu asiyekuwa na dhambi na pia tusihukumu maana na sisi tutahukumiwa vilevile

  – Tujifunze kuchangia hoja tajwa bila kuchanganya matatizo tulionayo kichwani ili yuweze kueleweka. Mfano Mama JK kupendeza ama kutopendezo kuna mahusiano gani na Mrema! na mambo mengine yanayofanana kama hayo.

  Asante, ngoja niwajibije

 95. siko Says:

  huyo kalagabaho, kazi kujiona vip, wakati hamna kitu, atulie kama salma. anatuletea nuksi tu wengine.

 96. sino Says:

  huyo mwingine, hapo muangalieni sana, jichi hilo. salma mfundishe huyo kalagabaho.

 97. nilo Says:

  huyo mwingine ana roho ya shukrani kweli, nilitaka tu kujua, naona anaonekana kua na raha kweli.

 98. King 17th Says:

  this is a realy afr women, she remindes me sometimes ago i used to see a lot of womens dress like this when i was in Tanzania;
  but now i’ve been in USA for a long time and i have never see any women dress that way except my mom.
  she look so cool…

 99. watubwana Says:

  siri ya mtungi aijuaye ngata,watu bwana mh!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s