BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MEET THE COACH. December, 17, 2007

Filed under: Kabumbu/Soka,Michezo,Soka,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Ingawa watanzania wengi wanaendelea kuwa washabiki wa kutupwa wa timu mbalimbali zilizoko kwenye ligi kuu ya Uingereza(Premier League), nchini Tanzania msisimko fulani kwenye medani ya soka unarejea kwa kasi.

Siku hizi “utaifa” unaanza kurudi.Ukisikia Timu ya Taifa inacheza,basi kila mtanzania husubiria matokeo kwa hamu.Wapo wanaoenda viwanjani kuiunga mkono timu ya taifa na wapo wanaoishia mitaani kule vijiweni kwenye ule ubishi wa kufa mtu.

Msisimko huo mpya ndio unaomfanya Kocha wa Timu ya Soka ya Taifa,Taifa Stars,Mbrazili Marcio Maximo Barcellos(pichani) kuwa mmojawapo kati ya watu mashuhuri nchini Tanzania hivi sasa. Maximo ambaye aliwahi kuwa mmoja wa wakufunzi wa timu ya taifa ya Brazili kwa vijana chini ya miaka 17 na pia chini ya miaka 20, aliwahi pia kufundisha timu ya Livingston Football Club ya nchini Scotland (daraja la kwanza) katika msimu wa 2003/2004. Akiwa na timu hizo za vijana za Brazili aliwahi kuwafundisha wachezaji nyota wa Brazili wanaotamba hivi sasa kama Ronaldo (AC Milan) na Ronaldinho(Barcelona). Aliwahi pia kuwa mkufunzi huko Cayman Islands.

Kuhusu wapi atalipeleka soka la bongo ni suala la kusubiri na kuona. Pamoja na hayo wapo wanaosema,dalili njema zimeanza kuonekana na hivyo wanawasihi watanzania wampe muda.Unaweza pia kuitembelea tovuti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kujua mengi kuhusu soka la bongo kwa kubonyeza hapa.

Picha kwa hisani ya Mroki.

Advertisements
 

8 Responses to “MEET THE COACH.”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Samahani kwa kwenda nje ya mtundiko.

  Hivi huyo kocha wa stazi mshahara wake na marupurupu ni kiasi gani?

  Natanguliza shukrani.

 2. Dave Says:

  Analipwa hela ya kibongo milioni 30 kwa mwezi (30,000 US $), kapewa gari mbili za kutembelea kila moja ina thamani ya milioni 40, kapewa mjengo baab kubwa na unalindwa na mapolisi kama ilivyo nyumba ya waziri mkuu kule masaki. Marupurupu sijui anapewa kiasi gani lakini ana neema ya kutosha nina uhakika hatamani kurudi brazil kwa sasa.

  Ila unajua nini?Asipoifanya team icheze soka la kuvutia nna uhakika watanganyika watam-mourinho sababu hata muajiri wake braza JK anataka soka la kitabuni sio lile la sasa hivi la butua.

  Ila kajitahidi aise, tumepanda kwenye rank ya FIFA.

 3. Dave Says:

  alaf hicho kidole hicho!!!

  aangalie asije akakinyoosha mitaa ya uswahilini hawachewi kumkata-funua.

 4. yani akinyoosha hicho kinachofuatia na kupunguza smile lake hata Brazil tutaifunga

 5. Edwin Ndaki Says:

  asante Dave kwa kunisaidia ilo jibu

 6. timethief Says:

  Test comment due to your forum post.

 7. Matty Says:

  Bora yake anapata mshko heavy sasa sijui anasaidia masikini huyu??au ndo anabanwa na muda kwenda tiz kila siku.

 8. Dullah Says:

  Jamaa hata hafai mara kumi angekua Julio ndo kocha wa taifa, mfanao ni ile siku ya Msumbiji jamaa walitufundisha soka. Kina nizar sidhani hata kama wana kitu walichoelewa baada ya mafunzo ya kocha, kiungo hawezi hata kukaa na mpira! kocha na wachezaji wote wa sasa hawatufai!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s