BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“ELIMU NDIO NGAO THABITI”-JOKATE MWEGELO December, 18, 2007

Filed under: Fashion,Mahusiano/Jamii,Miss Tanzania,Urembo — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Jina Jokate Mwegelo (pichani) linazidi kutokuwa geni vinywani na vichwani mwa watanzania siku baada ya siku. Kama ambavyo tuliwahi kusema siku za nyuma, Jokate ni miongoni mwa vijana wa kitanzania wenye vipaji mbalimbali ambavyo wanavitumia ipasavyo. Mbali ya kujulikana zaidi kama mshindi namba mbili (2) wa shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania mwaka 2006 na Balozi wa kinywaji cha Redds, Jokate pia ni mwanamitindo na msimamizi wa shughuli mbalimbali (MC). Isitoshe mwaka huu ameingia pia kwenye ulimwengu wa uigizaji filamu kama alivyoonekana katika filamu ya Fake Pastors iliyoingia sokoni miezi michache iliyopita.

Kama hiyo haitoshi, Jokate pia ni mtengenezaji mzuri wa matangazo ya radio kwa kutumia sauti yake. Hivi karibuni tulipata nafasi ya kufanya naye mahojiano kuhusu mambo mbalimbali yakiwemo historia ya maisha yake, kazi zake, ushauri alionao kwa vijana wenzake nk.

Ungependa kujua role model wake ni nani? Kama angepewa nafasi ya kuwaalika watu watano kwa chakula cha jioni angewaalika kina nani? Kwa hayo na mengineyo, fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Karibu sana ndani ya BongoCelebrity

JM: Asante sana,nashukuru.

BC: Ni wazi kwamba watu wengi wangependa kujua historia ya maisha yako.Kwa ufupi tu unaweza kutueleza ulizaliwa wapi,lini na mpaka hivi sasa umesomea katika shule gani?

JM: Nimezawaliwa Washington DC nchini Marekani mwaka 1987 ambako wazazi wangu walikuwa wakifanyia kazi.Primary nimesoma Olympio Primary School,Dsm. Secondary nimesoma St.Anthony’s Secondary School na High school nimesomea Loyola High School. Kwa sasa nipo katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam nasomea Political Science.

 

BC: Unakumbuka ulipokuwa mtoto ulitaka kuwa nani? Kama ndoto yako imetimia au inaelekea kutimia, nini kimechangia mafanikio yako?

JM: Kusema ukweli sikumbuki nilikuwa na matarajio gani nilivyokuwa mdogo ila ninachojua ni kwamba ninachokifanya hivi sasa kinaendana kabisa na purpose au dhumuni langu la maisha. Pia napenda kusema kwamba ndoto yangu haijatimia kwani bado najijenga kuwa a global personnel in either the political or social development field or as a serious TV show host.

BC: Ilikuwaje ukajiingiza kwenye fani ya urembo?Nini kilikuvutia? Na je wazazi wako walisemaje ulipowadokeza juu ya nia yako ya kushiriki mashindano ambayo mpaka hivi sasa bado yanapata upinzani kutoka kwa makundi fulani fulani ndani ya jamii?

JM: Kilichonivutia ni jinsi walimbwende walivyojituma katika kazi mbalimbali za kijamii zenye high profile na vile vile kupata exposure ya kutembea sehemu mbali mbali duniani, kukutana na watu na kujitambua zaidi nini ningependa kufanya katika maisha yangu.But above all it’s a year full of fun and entertainment with lot of public appearances and interviews…..its a chance to inspire others!!

Wazazi wangu walikubali wakijua ni sanaa tu kama zilivyo zingine na hawakuniacha na kila siku waliendelea kunisisitizia kwamba nifanye yote lakini nikumbuke kwamba elimu ndio ngao thabiti ya maisha yangu. Mengine yote yanapita.

BC: Nani ni role model wako kwenye masuala ya urembo hapa nchini? Na kimataifa ni mrembo au warembo gani wanaokuvutia zaidi?Kwanini?

JM: Kwa hapa nchini role model wangu ni Irene Kiwia kwani ana degree yake.Alikuwa Miss Temeke mwaka 2000. Pamoja na hayo ana kampuni yake ambayo inasimamia events na models. Anajituma kwa kweli na si mtu wa kukata tama, ana upendo na ni mwenye kutia moyo.

Kimataifa nampenda Tyra Banks. Kikubwa ni TV show yake ambayo naamini si kitu kirahisi kufanya ila yeye anaonyesha ujasiri na kuweza kubadili fikra za wengi kuwa hata yeye anaweza. Kama unavyoona, napenda wanawake wa substance na ninaamini she is one of them.

BC: Wengi tunajua kwamba mwaka 2006 ulishika nafasi ya pili katika mashindano ya Miss Tanzania.Sasa kwa sababu hukushika namba moja,namba ambayo wote huwa ndio mnayoiwania katika mashindano kama yale,unadhani kama ingekuwa inawezekana siku ile au kipindi kile kikarudishwa nyuma, ungebadili kitu gani ili kuibuka mshindi?

JM: Nisingebadili jambo lolote.Naomba ieleweke I gave it my all and did my best to the best of my abilities at the time. Mengine hayo ni matokeo tu.

 

Jokate Mwegelo(kushoto) akiwa na Miss Tanzania 2006,Wema Sepetu(katikati) na Lisa Jensen(kulia). Jokate alikuwa mshindi wa pili na Lisa mshindi wa tatu.Hii ilikuwa muda mfupi baada ya matokeo kutangazwa mwaka jana. Picha kwa hisani ya Mroki.

BC: Baada ya kushika nafasi ya pili katika mashindano ya Miss Tanzania 2006 ulivikwa taji la Balozi wa Redds kwa muda wa mwaka mmoja. Unakumbuka nini zaidi katika “ubalozi” wako wa kinywaji hicho? Nini hasa maana ya kuwa “balozi” wa Redds?

JM: Naomba ieleweke kwanza kwamba sikuvishwa taji la balozi wa Redds baada ya kuwa mshindi wa pili.Redds Fashion Ambassador linajitegemea. Finalists wote wa Miss Tanzania wako liable kushiriki. Ndio maana kama mtakumbuka nilitangulia kutajwa kama balozi kabla ya kutangazwa mshindi wa pili.

Nikirudi kwenye swali lako. Kuwa balozi wa mitindo wa Redds inakupa jukumu la kuwa msemaji mkuu wa kinywaji hicho cha Redds katika maswala ya mitindo hapa nchini Tanzania.Redds Premium Cold imekuwa iki dhamini na kuwapatia wanamitindo na wabunifu wa mitindo kwa lugha ya kigeni platform ama jukwaa la kukuza zaidi vipaji vyao.Redds ni kinywaji cha kike na wanawake wengi wanapenda mitindo na kwenda kwa wakati hivyo Redds reflects exactly that.

Nitakachokumbuka zaidi ni jinsi nilivyoweza kupata uzoefu wa kufanya kazi katika idara ya masoko nikiongozwa na kiongezi wetu Mpeli Nsekela, Brand Manager wa Redds,Marketing Team ya Tanzania breweries Ltd na vile vile niliweza kuhost show zote za mitindo iliyofanyika kama Director of Ceremonies na hivyo kuniongezea uzoefu wa kuongea mbele za watu na kujiamini zaidi.

BC: Mbali na kujishughulisha na mambo ya urembo, mitindo na wewe pia ni msimamizi wa shughuli (MC).Unamudu vipi ratiba yako ya siku ili kufanikisha shughuli zote hizo na je vyote hivi ni vipaji ambavyo umezaliwa navyo au vingine umejifunza tu ukubwani?

JM: Ni kupangilia mambo yako tu. Nadiriki kusema inakuwa ngumu nyakati zingine kwani kazi zinaweza ingiliana au nakuwa na mambo binafsi nk. Ila namshukuru Mungu nimefanikiwa kwa hilo.Vile vile namshukuru Mungu kwani nafanya vyote kwa kutumia vipaji vyangu nikiongezea ushauri na fursa mbalimbali za kazi ninazozipata kujengea uzoefu ila sijawai kufanya any formal training.

 

Jokate(kulia) akiwa na MC mwenzake, Bobby siku walipokuwa wasimamizi wa Kili Music Awards 2007 mapema mwaka huu.Picha kwa hisani ya Issa Michuzi.

BC: Hivi karibuni umejiingiza katika uigizaji wa filamu. Nini kimekuvutia kuingia katika fani hiyo na kwa mtazamo wako unadhani kuna uhusiano gani kati ya urembo na uigizaji wa filamu? Mpaka sasa umeshashiriki kwenye filamu ngapi? Nini mipango yako ya mbeleni katika sanaa hii ya uigizaji?

JM: Nitajibu kwa kutoa mfano. Mfano ni hii movie ya Fake Pastors kwa mfano nimeicheza mwanzoni wa mwaka huu na kilichonivutia hasa ni ujumbe wa filamu yenyewe na pia kufanya kazi na watu tofauti kidogo ambao sikutegemea ingetokea siku tungefanya kitu pamoja. Pia ni just a means of socializing and familiarizing oneself with different scenerials and persons.

Hakuna coherent relationship kati ya urembo na filamu pengine itakuwa tu kwamba zote ni sanaa ambazo zinakuweka kwenye limelight na una uwezo mkubwa wa kuinfluence fikra za watu. Mpaka sasa nimeshashiriki filamu mbili ambapo moja iko sokoni na kuhusu mpango wangu hapo mbeleni,let’s just wait and see.

BC: Jokate, ungepewa nafasi ya kuwaalika watu watano kwenye chakula cha jioni(walio hai au hata waliokwisha fariki) ungewaalika watu gani?Kwanini?

JM: Condoleeza Rice-US Secretary of State, Hillary Clinton, New York Senator and democratic front-runner for the 2008 elections presidential nomination. Dr.Asha Rose Migiro, Deputy Secretary-General of UN, Christina Fernandes-President of Argentina na Oprah Winfrey- tv host and producer also CEO of Harpo Studios.Simply cause they are the best women and I am inspired by strong, intelligent inborn natural forces such as theirs.

 

Jokate akiwa ndani ya studio akitengeneza matangazo ya radioni.Picha kwa hisani ya Bob Sankofa.

BC: Unatoa ushauri gani kwa vijana wanaotaka kujiingiza kwenye mashindano ya urembo, uigizaji na uana-mitindo?

JM: Be yourselves, be inspired by the best, take your own stand and be ready to lead by example and maximize in every opportunity you get, make the most of your talents. Stay fresh and beautiful inside, out.

Picha zilizobakia kwa hisani ya Global Publishers.

Advertisements
 

54 Responses to ““ELIMU NDIO NGAO THABITI”-JOKATE MWEGELO”

 1. KABEWA Says:

  Big up! your cute and always you will be

 2. the one Says:

  Wawawa mtoto!!1 nakukubali sana. Mungu akulinde na azidi kukuongoza.

 3. Kekue Says:

  Mtoto Mashalaah mwenyenzi mungu kamjalia, nampenda sana she is beuty na ana akili si unaona anavyopangilia mambo yake? I lyke it. Keep it up! Isipokuwa kwenye filamu ya Fake pastor wewe na Lisa nilipoona kava la ile cd nikajua mle ndani mtakuwa mpeparticipate sehemu kubwa lkn ilikuwa tofauti na nilipo nunua cd na kuangalia yani mmeonekana sehemu chache sana, it cmc waliweka ile picha kuuza cd na sio kwamba nyie mlikuwa waigizaji wakuu mle ndani!! Inabidi awape pesa ya kuuza sura na kuigiza!!! Take care toto nzuli eeee!!!!

 4. ANNA GABRIEL Says:

  Ur cute and i admire u.Well done,Keep it up.
  TAKE CARE

 5. Mkata Issue Says:

  1.Msichana/Mwanamke ni mrembo – Libarikiwe tumbo la mama aliyekuzaa na baba aliyedondosha mbegu.

  2. Ama ni kasumba au ulimbukeni au muwasho wa shule ndogo mnapochanganya lugha pindi mnajibu maswali. Kutamka kisawe kimoja au viwili vya kiingereza wakati unatafuta neno linalofaa la Kiswahili inakubalika lakini unapoanza kujibu swali zima (mfano la mwisho) kwa Kiingereza kama kasuku hivi kwa kushusha mistari uliyokariri wakati swali limeulizwa kwa kiswahili nimekushusha kama shetani toka mbinguni fwaa!

  3. Kekue naheshimu sana mchango wako lakini kwa kusema yafuatayo,
  “..nilipoona kava la ile cd nikajua mle ndani mtakuwa mpeparticipate sehemu kubwa… ” sikuelewi kabisa.

  Usihukumu kazi yeyote ya kisanii kwa kigezo kimoja tu cha muonekano wa juu au utambulisho wake tu!
  Pili kwa nini wa ‘participate’ sehemu kubwa wakati wao si wachezaji wakuu (main characters)? wala dhamira kuu ya picha haikukusudiwa kubebwa na vitendo vya hao mabinti bali wale vijana waliokoswa kuajiriwa baadaye wakajiajiri katika nyanja ambayo hawakufuata maadili ya kazi ile!
  Tatu huna haja ya kuwakumbusha kuwa wanahitaji kuuza sura yao kwa ushiriki wao maana utakuwa unatukumbusha nasi WATEJA KUWA KUMBE TULIKUWA TUNANUNUA SURA NA SIO UJUMBE NA MAFUNDISHO YANAYOBEBWA KATIKA HIYO SINEMA. HIVYO NA MIMI NADAI PUNGUZO LA BEI KWA NAKALA NILIYONUNUA NA WENYE SINEMA WADAI ‘CHENJI’ KUTOKA KWA JOKATE NA MWENZAKE KUPITIA KWAKO MAANA MTAKUWA MMEINGIZA NIA NA SABABU TOFAUTI YA KUSHIRIKISHWA KINYUME NA MASHARTI YA MKATABA WA KUSHIRIKISWA.

 6. Reen Says:

  Umejieleza vizuri ila kwenye Fake Pastors nilivyokuwa ninahisi na nikaenda kununua dvd tofauti kabisa yaani ni uozo sijawahi kuona,Matangazo makubwa mnavutia lakini mmmmh.Soma mama elimi ndio nguzo yoko twalijua hilo ndio maana tunasoma sana.

 7. Sinzia Says:

  BC-Asante kwa mahojiano mazuri
  Naomba kama itawezekana utuletee CELEBRITY wapya wapya na sio kurudia rudia waliokwisha pata nafasi kwenye web yako kama huyu….mwanzoni na mwishoni mwa miaka ya 90 kulikuwa na watangazaji celebrity pale RADIO ONE kama Mike Mhagama…Rankeem Ramadhani…Vicky Msina, Dj Deo Mshigheni,wakina Sunday Shomari na wengineo wengi…kama utaweza kuwapata na kuwaweka hapa itakuwa poa…tujuwe wako wapi…na wanafanya nini kwa sasa kwani ni zaidi ya mwongo mmoja umepita bila ya kuwasikia.
  Naomba kuwakilisha

 8. Bertha Says:

  Sinzia,nadhani umechanganya majina hapo.Jokate hajawahi kuhojiwa na BC..au mimi tu ndio nimepitwa??Ila katoto kazuri haka tuacheni utani.

 9. Kyiteyi-teyi Says:

  Sinzia!! umelonga!!! Ni kweli kabisa kuna Ma-celebrity wengine wengi tu hawaja-appear humu.
  Mfano MISANYA BINGI,JOYCE MHAVILE,JOSEPH KUSSAGA etc…

 10. Mkware Says:

  Hivi jamani kaolewa huyo au ana boifrend?
  Anapatikanaje huyo?

 11. lily Says:

  Mimi namfagilia sana huyu,nahsngaa kamati ya miss tanzani inacha watu wanaokubalika inapeleka watu wa ajabu kwenye miss world .tuwe tuapiga kura kama zile za jumanne Iddi jamani.ama sivyo tutaishia aibu kila mwaka

 12. Matilda Says:

  Yes namkubali kiasi chake ingawaje some tym anajishebedua sana uyu dogo,Kama mtu humjui utaweza kusema ni kastaarabu ila akianza ubishi wake na kujishau mmmhh nilishakutanaga sehemu kibao,Na kuna siku nilikuwa nao sehemu wakawa wanabishana na wema yaani anataka awe juu wakati yy ni wachini tena wa Tmk ahahahah,Ila fresh maelezo yako yako fresh.Soma sana kama wazazi wako walivyokuambia.Ni hayo tu.Matilda

 13. ma'reen Says:

  Binti mzuri sana na anashiriki shughuli za kikanisa,anaimba kwaya st. peter.Kwa mtazamo wangu hupendeza zaidi akiwa hajapaka ma-make up, anavutia zaidi akiwa natural, she looks angelic,Mungu amlinde na midume yenye kiu na njaa ya kuharibu watoto wa watu.

 14. Sinzia Says:

  Bertha…ni kweli mahojiano na binti huyu hayajawahi wekwa hapa…lakini last three or four weeks ago BC aliweka pic yake humu na watu walitoa comments zao…nadhani ilikuwa enough na wengine wapate nafasi pia ya kuonekana hapa.

 15. James Says:

  Huyu dada nimesoma mahojiano yake na nimeona ni minongoni mwa warembo wachache ambao kama wanapata nafasi ya kutuwakilisha wanaweza kututoa kimamasomaso..you go girl…you smart,hard workin and i really like work…..jms_206@yahoo.com

 16. TanzanianDream Says:

  Duuh naona hapa kuna gender issue…Haiwezekani huyu awe inspired na wanawake tu…….nway kila mtu na mtazamo wake….Usiweke chuki

 17. TanzanianDream Says:

  Nway Speaking of 5 people you would invite for a meal,Who would make your list?????

  Mine is:
  1.Osama Bin Laden.
  2.George W. Bush.
  3.Steven Gerrard.
  4.Eddie Murphy.
  5.William Buffett.

 18. Nay Says:

  Jamani hivi kutoka Temeke ndio kuwa chini? Anaweza kuwa anatoka Temeke na akawa matawi ya juu vile vile na inategemea ametoka katika familia gani. Na huyo Wema kutoka kwake Sinza au kuwa mtoto wa Balozi sio kigezo cha kila neno analosema watu wasimbishie. Hii desturi ya hewala bwana mkubwa ndio imetufikisha hapa tulipo lazima tuwafunze watoto wetu kuhoji na sio kukubali kila jambo jinsi linavyokuja. Pengine ndivyo wazazi wake walivyomlea, kuhoji ni njia mojawapo ya kujionyesha kuwa unajiamini.
  Ni msichana mzuri kwa kweli, na siku hao majaji na kamati yao ya miss Tanzania walivyomchagua Wema kuwa miss Tanzania nilisikitika sana na nilijua tu asingefika kokote. Huyu ndiye angefaa kuwa miss Tanzania, basi kama waliona hafai wangemchagua hata huyo Lisa Jensen. Jokate, follow your dreams na uendelee hivyo hivyo kujiamini, utafika mbali!

 19. bano Says:

  nilidhani ni yule, bunuzi mchecheto. kumbe ni kisura huyu.

 20. Yeah mtoto mzuri, je unakwenda kwa mtandao upi??
  i mean namba yako ya simu au e mail address……..
  Thanx in advance

 21. timethief Says:

  Test comment due to your forum post.

 22. hugo Says:

  Mtoto namjua kwa ukaribu sana toka tukiwa wadogo alikuwa na kipaji cha tofauti katika rika letu.
  Uzuri alionao Jokate ni “natural beaut” na wala sio wa kununua dukani, pamoja na kujitunza na maadili ya wazazi wake.
  Wengi wanameza mimate ehhhhh……

 23. Luseshelo Says:

  — nanukuu —

  JM: Naomba ieleweke kwanza kwamba sikuvishwa taji la balozi wa Redds baada ya kuwa mshindi wa pili.Redds Fashion Ambassador linajitegemea. Finalists wote wa Miss Tanzania wako liable kushiriki. Ndio maana kama mtakumbuka nilitangulia kutajwa kama balozi kabla ya kutangazwa mshindi wa pili.

  — mwisho wa kunukuu —

  Maskini Jokate bado akili yako ndogo. Ukishapewa taji la Redds ujue U-miss Tanzania ndio kwa heri tena. Au umeshawahi kuona Miss mwenye mataji yote mawili – la Redds na la Tanzania? Mi sijaona, na kiutendaji itakuwa ngumu kubeba mataji yote.

  Somo hapa kwetu wasomaji ni kwamba Miss Tanzania ni utapeli. Mshindi huwa anaamuliwa kabla ya shindano. Kinachoendelea jukwaani siku ya shindano ni kiinimacho tu. Walijaribu kuficha hilo miaka yote lakini soo la Richa limewaumbua.

  Lundenga tumekushtukia tafuta staili mpya banange.

 24. siba Says:

  bano kweli, kuna binti anaitwa bunuzi anafanana na huyu, ila yule ni hatari, wa kuogopwa na rafiki ake janet. Wana hila za chini chini, mi mkereketwa nahofia watu ambao, wanawafwata fwata. Dada jokate, keep on being you.

 25. Jasmine Says:

  Go baibe, sky is the limit!!

  your so cute,intelligent and young woman with pleasing personality,really i have never seen a celebrity (TZ particular) who is down to earth like Jokate.

  God bless you!!

 26. Matty Says:

  All the best Jokate, mahojiano mazuri anajua kujieleza jamani mkimleta Richa au Wema hapa hawatamfikia, ila kuhusu hilo la kumualika nani msosi nadhani tumuachie yeye huo ndio mtazamo wake hata mimi ningealika watu wangu wa karibu hasa ndugu zangu te te te!!!!!!!
  Matilda acha zako kwani kama anatoka TMK ndo asiongee?????hujui nyumbani ni nyumbani???mbona warembo kibao wanakaa mbagala usafiri wa daladala si wa tabu mbona wanapoint nzuri tu kuliko hao watoto wa mathaki thijui thinza mhhhhhhhmuacheni jamani she is cute.
  Merry x-mas, Id al-haji(sorry kama nimekothea) na happy new year to all!!!!!!!

 27. Edwin Ndaki Says:

  Nilitumaini kuwa ndiye angekuwa misi tanzania kwenye kile kinyang\anyiro lakini ndio hivyo tena..wakampatia Mr blue..no imean TID noo…i mean WEMA

 28. Matty Says:

  Tanzania dream trupu yako ambayo ungeialika mbona inatisha du!!!!!!sasa Bush akikaa one table with Osama patatosha kweli???

 29. Nyaucho Says:

  jamani mimi sasa hivi ntakua nawaangalia then nalipua mabomu mwishoni naona wote mnaona aibu,,,,

  1) Naomba Admin mtafute aliyeshiriki Miss Tanzania na akatoa rushwa ya ngono na hela but hakuambulia chochote ukikosa nicheki ntaongea na mmoja then tutafute ufadhili aje aanike mambo hadharani maana sidhani kama atakubali kutoa habari hii nyeti bila posho ushahidi anao .

  2) Biashara ya u-miss ni utumbo na utapeli mkubwa hakuna lolote la maana huyu Lundega anatuharibia dadazetu kwa kufanya hicho ni kijiwe cha kuwakutanisha wasichana wazuri na mapedejee (matajiri wapenda ngono)-ushahidi upo

  3) Kuhusu huyo dada (Mwegelo) kweli anashape nzuri japo kwetu sisi waTanazania halisi tunaopenda Mwanamke halisi (Twangapepeta) kweli hanivutii sana. Ila niwaombe watanzania tusipende kuwapaka watu mafuta kwa mgongo wa chupa,,,muulizeni vizuri alishiriki vipi swala la “Rushwa” ktk kinyang’anyiro. maana kuna ushahidi si wa-maneno bali wa vionyeshwa kwamba hata yeye alishiriki kutoa Rushwa

  4) Najua wengine watakua wananishangaa lakini hawa watakua ni watu ambao hawaelewi nini hutokea ktk mashindano hayo-Ushahi upo

 30. any Says:

  wakikaa pamoja ndo watasawazisha mambo, huenda hawajawa na formal meeting, thats why they fight, heheh

 31. Matty usiwe na wasiwasi.
  Mtaani kwetu temeke kwa azizi ali yupo Osama na Bush.Wote ni wapangaji wa kwa mzee Malugujo (Shekhe Mbuzi) ambako huwa huwa tunachota maji.Kwa hiyo ndo naanisha nitakao waarika kwa lanchi ya mchana.
  Simaanishi Bush rais wala osama mwenyewe.

 32. maggie Says:

  your cute gal,but kwanini umekata nywele umekua mbaya

 33. samora Says:

  ukweli rushwa ya kungonoana kwenye hii fani ya kutafuta mlimbwende bora kuliko wote tanzania ipo,tatizo ni kwamba hawa wadada washiriki wengi wamekua kwenye mazingira ya kuficha siri.wana ule mtazamo wa kwamba ukilopoka mambo ya uani mbele ya watu shaurilo,sasa hapa nakuapia hakuna hata mmoja atakayejitokeza kuja kutoa ushahidi mbele ya jamii.hii ni siri yao na washika dau

 34. dcmayor Says:

  kuna utata kuhusu mambo ya bongo flava ilivyoanza na nani alipa jina hilo kati yaDOGO steve B namtangazaji mike mwagama .tunaomba bc ututafutie seba maganga na mwagama tuwasike maoni yao.
  huyo lundenga na mademu wake wazinguzi tu.

 35. Pierre! Says:

  Da mtoto kweli umeumbika but take care uzuri wako usije ukakupoteza coz wabongo mnaongoza kwa kulewa sifa,,,alafu mtoto jicho hilo ”yaani ni full mtego…”

 36. Dorice Says:

  kwa kweli Jokate ni beauty, big up Jokate kaza buti.

 37. Dorice Says:

  nilifikiri huyu binti ndie angeshika Taji la Miss Tanzania 2006, na muunga mkono mchangiaji aliyenitangulia kuwa tungekuwa tunapiga kura sisi watazamaji kama tulivyokuwa tuna mtafuta mwakilishi wa BBS.. hii itachangia kuwapata warembo ambao wako bomba, kama mimi ningepewa nafasi ya kushiriki kumchagua Miss Tanzania mwaka 2006 ningemchagua Jokate Mwelego. huyo wema sura imempalama utafikiri nini??? pale alikuwa ni Jokate na Lisa, Huyo wema wao angekuwa ni mshindi wa TATU na wala sio wa kwanza.

 38. glory Says:

  u ‘re beautiful. ila actress si fani u need more practice

 39. Dullah Says:

  Mh we Matilda acha wivu, inaonekana ulipoona sura ya Jokate tu ukajua kakufunika mbaya yaani kakuacha Dar na Tunduma ndo maana unaanzo ooh anajishaua ooh, acha hizo unakula cement nini? All in all Jokate is cute jamani mh!

 40. zawad haji Says:

  Namfagilia kwa saaaaaaaaaaaana Jocate ni mrembo usipime, awe makini na wadaku wasije wakamchafulia jina

 41. defy H M. Says:

  Big up!!mis Jokate- a friend you need are those who can provide you with the subject of confidence, all you have to hate are those brings you to the blunder world..welcome tomy world and see your modeling future, you are Hot star[tanzanian]Jokess!! alowed right? takecare.

 42. A Says:

  I think it’s time for people to go looking for things to do

  and stop gossiping, Jokate, you did well

  and like you said you did your best, you are very talented,

  beautiful and young, you have everything it takes to build up

  your career you got it all.

  Dont mind all the crap people are talking about you, they

  haven’t a clue, you’ll always get that no matter where in the

  world you go.

  people are jealous all they care about is to bring intelligent,

  beautiful, ambitious, talented and hard working people like

  you, down.

  I wish you all the best in your career, keep it up and dont

  let anyone bring you down.

  Much love
  A.

  Take care.

 43. samora m chipeta Says:

  Its really amazing to see you do a lot of stuff Jo,I dont see any difference between you and Tyra,Oprah,keep it going girl.Honestly, I have admired you one you are intelligent,talented and most importantly very and i mean very beautiful

 44. Simon Siwango Says:

  umependeza

 45. annette Says:

  its good that you have tried to accomplish some of the things tht you have always wished to accomplish that is very good and chall
  ellinging to other girls with same dreams..congrats girl

 46. polisi Says:

  Go babes!! you are hot.let no 1 tell you otherwise.You deserved kushinda last time and not runners up.nway show them you good in all ways.Stay beautifull and Take care.Usiache kusoma,its the key for life and life itself.

  Chiao.

 47. neema Says:

  jamani namfahamu Jokate hakuna mrembo mwenye mashauzi na kujisikia kama yeye,hawezi kuntroll temper yaani anaoverreact hata mbele ya kadamnasi akiwa anahost show na ana tabasamu la kinafiki
  ,ila kwa sura aaah msshalaaa

 48. Matty Says:

  Neema, mashauzu hivi ni nini???how? kwangu ni tungo tata kidogo!

 49. naa Says:

  jamani huyu dada ni mrembo! ni makini na mabmbo yake. Ila shost usisahau sana elimu.

 50. underwood Says:

  I give you 5 mics.
  God bless u.

 51. Eyemark Says:

  you look beautiful such that tunakutumia kama SI unit.

 52. watubwana Says:

  siri ya mtungi aijuaye ngata.mama kama kunabaya ambalo unaliona limetamkwa kwako,jifunze na ujirekebishe.na kama kunazuri liendeleze.ila usije jaribu kuutumia uzuri wako vibaya.maisha ni kitabu

 53. u r so cute zat i could ever imaji in ma laifu. keep it up in ur bisness.

 54. A2kii Says:

  ebwana sina zaidi ila mko juuu!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s