BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MCHUNGAJI RWAKATARE AMRITHI SALOME MBATIA December, 18, 2007

Filed under: Bunge,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 7:20 AM

 

Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokutana chini ya Mwenyekiti wake,Rais Jakaya Kikwete,imemthibitisha Mchungaji Dr.Getrude Rwakatare kuwa mbunge wa viti maalumu,kurithi nafasi ilioachwa wazi na marehemu Salome Mbatia aliyefariki Octoba mwaka huu kwa ajali ya gari.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar jana mara baada ya kikao cha kamati kuu,katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM Itikadi na Uenezi,Bw.John Chiligati,alisema kufuatia uamuzi huo, mchungaji Rwakatare sasa ni Mbunge mteule akisubiri kuapishwa wakati wa mkutano ujao wa Bunge utakaofanyika januari mwakani.

Picha na habari hii kwa hisani ya MichuziJR.

Advertisements
 

50 Responses to “MCHUNGAJI RWAKATARE AMRITHI SALOME MBATIA”

 1. Kekue Says:

  Aliyekuwa nacho huongezewa ila asiyekuwa nacho hunyang’anywa hata kile alicho nacho!!

 2. Dave Says:

  I doubt kama dini na siasa vinakwenda pamoja!

  Lets wait and see.

 3. Kichwele Says:

  Hongera sana mama.Kila la kheri.Sasa sijui atawezaje kuzihudumia hizi kofia mbili kubwa ambazo anazo;uchungaji na ubunge.

 4. Kimori Says:

  A truly religious person never participate in politics, because you can not serve two masters!

 5. Desert Eagle Says:

  Mama Rwakatare umemkana Mungu wako kwa kufanya biashara haram (Siasa) hasa ya Tanzania

  Mama Rwakatare step down from that position, kama ukikubali kula kiapo mbele ya Samwel Sita maana yake ni;
  (a) Rushwa kwako ni halali
  (b) Utabiga kura ya ndio kubariki ufisadi
  (c) Ushirikina ni njia yako mbadala ya kupanda vyeo na kumantain nafasi yako bungeni
  (d)Utasema uongo ili kutetea chama chako na watu wacheche kwa manufaa yako binafsi na wachache

  Usimkane bwana mungu wako kwa tamaa za madaraka na vijisenti vya posho

 6. any Says:

  uchungaji, st mary’s, ubunge, uwaziri? na kote anapata mishahara, ile sera ya asiwe na mishahara miwili iliishaga na Nyerere au bado iko. nauliza tu.

 7. any Says:

  ivi hawa ni watz au waangaza/warundi? hizi kazi wapewe wasio na kazi, mgawanyo wa kazi sijui ukoje huko bungeni.

 8. Ed (USA) Says:

  Nchi zetu zinazoendelea zinacopy kwa walioendelea mfano USA. Nakumbuka huko nyuma bongo alikuwepo balozi wa marekani anayeitwa mchungaji Smith. Kama iliwezekana kwa Smith why not kwa huyu mama? Historia inaonyesha huko nyuma alikuwepo Martin Luther King ambaye aliuwawa katika harakati za kisiasa. Bila kumsahau mtanganyika Mtikila huko nyumbani.

  Kilichotokea kwa huyu mama mchapakazi ni kawaida kwa wenzetu huku marekani. Suala la kulipwa zaidi nafikiri ni halali yake tuache masuala ya wivu.

  Kwa maoni yangu iwapo huyu mama kapata kibali kwa Mungu wake kuingizana kwenye serikali, basi Mungu wake atampa nguvu ya kukabiliana na yote. Huko nyuma kulikuwepo wacha Mungu kama Yusufu ambaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwenye utawala wa Farao wa Misri.

  Nafikiri ipo siri na sifa ya uchapakazi kwa huyu mama na iwapo tutakuwa makini tunaweza kujifunza na sisi kujiletea maendeleo katika taifa letu changa.

 9. Dave Says:

  any waangaza sio warundi,futa kauri yako.

 10. Nay Says:

  Mhu huko bungeni kutawaka moto kwa mitindo ya mavazi huyu mama anajipenda hasa, na hasa linapofika suala la mavazi. Halafu ni mtetezi mzuri wa masuala ya wanawake.

  Hilo la kuhusu uchungaji mbona watu mnakuwa na double standard, Mchungaji Mtikila yupo na anashiriki siasa na kila siku mnamsifia au kwa kuwa yeye ni mwanaume?

  Mie kwa mtazamo wangu ni kwamba asiende kuyumbushwa na kubadilisha msimamo wake, wazungu wanasema kama huwezi kuwashinda jiunge nao labda unaweza kujaribu kubadili mitazamo yao. Na sie kama kweli tunataka mabadiliko kukaa nje na kulalamika hakutusaidii kuleta mabadiliko yoyote, cha msingi ni kuingia kwenye mgoma na kuucheza.

 11. Desert Eagle Says:

  we mdogo wangu Ed wa USA kwanza nikushutum kwamba wewe ni mtoto wa wachache wanaotafuna Nchi yetu, na ndio maana huna uchungu na hauna hasara yoyote na yanayotokea huku nyumbani,,, Hoja iliyopo hapa ni kwamba anaenda kumuwakilisha nani huko bungeni??

  Tena nikuombe ufute upuuzi wako wa kumfananisha Mama Rwakatare na kina Luther king au Mtikila, huyu mama mlinganishe kwa kutoa mifano ya kina Bill Gates au Mabepari (matajiri) wote duniani

  wala usithubutu kumtaja mungu kwamba kamuongoza kwenda bungeni sehem iliyojaa waganga wa kienyeji (Washirikina), mafisadi, awongo, malaya n.k

  Ndugu yangu tunachotaka bunge la Tanzania liwe sehem ya watanzania wengi (masikini) na isiwe sehem ya wachache (matajiri.

  Kwa mfano, nitajie mbunge hata mmoja ambae ni ndugu yangu (hali ya kati).

  Kwa ushahidi nilionao, bunge la Tanzania limejaa mabepari (wafanyabiashara+matajiri)hakuna choka mbaya, mule bungeni wanaenda kutafuta Tender mbalimbali ili waendelee kuitafuna nchi yetu.

  TAFADHARI SANA BWANA ed(USA) tuhurumie tunaoumia huku nyumbani wakati wewe unaishi vizuri japo inawezekana unasafisha vyoo na kubeba mabox viwandani.

 12. Mkereketwa Says:

  Lakini jamani tukiangalia ukweli, kwanini wasiwape hata wale wabunge ambao walikosa hicho kiti mwanzoni kabla hata marehemu hajateuliwa?Hii nchi bwana!!!!Basi hapo watadaioooh, hao hwana ujuzi. Sasa ujuzi huwa unakuja kwa miujiza??

 13. mesa Says:

  poa mjanja wewe

 14. Edwin Ndaki Says:

  Ndugu yangu ANY nakupongeza sana kwa jinsi kila siku unavyotoa maoni yako mazuri.

  Hivi suala la UKABILA na UTAIFA hapo limetoka wapi?

  Naamini wewe ni muungwana,naommba ufute kauli yako kwa kuwaita WAANGAZA warundi.Na hata kama wangekuwa warundi hapa kwenye issue ya mama Rwakatare inakujaje?

  Ulishasikia muangaza au mrundi anaitwa Rwakatare?na hata kama angekuwepo hapa tunangalia kwa marefu ya mapama uteuzi wake.

  Naomba ufute kauli yako.

 15. any Says:

  I know waangaza sio warundi ila Warundi wengi wamekuwa wakidanganya wao ni waangaza na wakaja chuo kikuu dar wakasoma kwa hela ya serikali ya tz walipomaliza wakarudi kwao kufanya kazi na degrees zao.

 16. timethief Says:

  Test comment due to your forum post.

 17. Edwin Ndaki Says:

  Kuteuliwa kwa mama Rwaka.. kumenikumbusha wimbo mmoja.

  Embe dodo…kuna sehemu huo wimbo unasema…

  Umekwishaaa poteeeaaaaa ..umekwishaa poteaaaaa wapotea mchangaji mzuriiii kwa kufataaa siasaaaaa…..

  Ingekuwa enzi zangu nipo kwa bibi shule ya msingi kigomaaa…huyu mama angenikumbusha ZE FOLOZI OFU SAMU EMPAYAZI.

  Yaani huyu mama naona kachemka,maana ninavyo jua mimi sasa naye ameamua kuwa FISADI.Maana atapiga kura za ndio kuhararisha uharamia wa kuteka mali za masikini.

  Ze Comedy wanasema LAITI KAMAA…..malizia laiti kama mama RWAKA angekuwa na uwezo wa kusoma alama za nyakati,angekimbia hizo politiki.

  Ni mtazamo wangu.

  Ene wei tutafika tu

 18. Edwin Ndaki Says:

  kwa maana hiyo huyu mama alikuwa kwenye siasa tangu longi taimu eeehee.

  jamani jamani tanzania.Ila huyu mama anapesa hivyo unaweza kukuta alitumia pesa zake wenye kampeni sasa wanamlipa ze TAKRIMA.

  Kweli mwenye nacho ataongezewa ….

 19. Dave Says:

  Mama Rwakatare nakubali ni mtetezi mkubwa haki za wanawake na watoto na amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia watoto yatima kwa kuwapa elimu ya bure kwenye shule zake za St Marys na Kenton na kina mama wenye matatizo ya ndoa amekuwa akiwapa msaada wa kisheria.

  Upande mwingine ni mhubiri mzuri tu, anafanya kazi ya Mungu kukemea maovu kama rushwa, uchawi wizi, ubadhirifu n.k.

  Wasiwasi wangu ni kwamba imekuaje yeye akakubali kwenda kujichanganya na wala rushwa ,wachawi na wabadhirifu wa mali za umma? najua atasema hata Yesu alikula meza moja na Zakayo mtoza ushuru, lakini kumbuka hajatokea binadam kama Yesu.

  Nahisi anaweza kuwa ameingia kujimaliza sehem moja, kama sio dini basi kisiasa…hata siku moja dini na siasa haviendani, si mnakumbuka Kakobe alivyopoteza waumini baada ya kumfanyia campaign Mrema mwaka 2000?as matter of fact tunajua kabisa wanasiasa wengi wa tanzania wanaingia serikalini kwa ushirikina na rushwa, na wanaendekeza ushirikina sasa sijui mama yetu atafanyaje ili aweze kurudi bungeni 2010 manake bila kwenda bagamoyo mlingotini kutengenezwa plus kutoa rushwa hujashinda uchaguzi bongo… msiniambie Mungu anawasaidia wanasiasa!

  Nadhani braza JK angemtafutia nafasi kwenye wizara inayohusika na mambo ya wanawake na watoto, kumuweka bungeni ni sawa na kuiweka imani yake katika majaribu. I can bet mama Rwakatare lazima atashindwa sehem moja.

  BTW,hivi mnajua mama Rwakatare ni kati ya wanawake wachache mamilionea bongo? ana vitega uchumi sio mchezo,inawezekana wajomba wa CCM wamemvuta ili wapate fungu la 10 linapokuja suala la michango ya chama maana yule mama sio mgumu kuchangia harambee.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA!

 20. ANNA GABRIEL Says:

  Mmmmhhhhhh sasa hii serikali ya JK iko kazi kweli.Mnasema ujuzi i believe ujuzi mtu hufundishwa.Politics and religion are two things different especialy for the gvt of Tz which is full of corruption.
  Nway lets wait and see.

 21. pm Says:

  kimori kuserve two masters ni kuabudu huyu mama anaabudu mungu na kumtumikia ni siasa kazi tu kama nyingine kwahiyo huyu mama is not serving two masters at all,na kwani ukiwa mchungaji au mlokole safi au mwislam mzuri hufanyi kazi zingine? kuhubiri aka kutoa huduma za kiroho nafasi yake ipo tena inaweza kufanywa na kila mtu,na kufanya kazi zingine ambazo hazihusiani na kuhubiri dini zina nafasi yake.na aliyesema ukiwa mchungaji huwezi kuwa mwanasiasa safi nani,tena ndio vizuri kwa sababu anatumia ujuzi na uwezo mwingine mzuri wa kichungaji ili kurekebisha mabaya yaliyopo kwenye siasa.mwisho huyu mama hakusimama madhabahuni,au jukwaani kuomba kura kateuliwa. period

 22. maya65 Says:

  Naungana na wadau hapo juu, hilo bunge la tanzania sasa linaelekea kuwa ni bunge la mabepari na si chombo cha kutetea wazawa walalahoi tena….yaani kweli mtu akifa anakuwa na sera zake zote….mwalimu nyerere alipinga na kukemea mambo haya yanayofanyika leo hii Tanzania…hivi kweli alieshiba anamkumbuka mweye njaa?
  huyu mama Rwakatare ni bepari wa kutupwa!!!!!!

 23. Matty Says:

  Jamani waliowengi wanaenda bungeni kutafuta mali sio kutuwakilisha how?wanapitia ubunge wao kupata wafadhili, mikopo na hata kula fedha za barabara,madaraja,shule,hospitali nk.
  Sasa suala la mama huyu ni sawa nampongeza, ila nawasiwasi kama atakuwa bilionea maana haya mast.marry’s yamekuwa mengi na achilia mbali miradi aliyonayo tusiyoijua.
  Sasa hapa mimi naomba huyu mama ndo apunguze viwalo pale bungeni ili asaidie watoto/wazee na wasiojiweza maana mavazi yake yeye ni kweli ya gharama kuliko yale ya mama Salma.
  Swali linakuja je huko Ddm wabunge wote hasa wanawake wangekuwa wanaulamba kama yeye ingekuwaje??nadhani ni mashindano ya miss bantu kwa kwenda mbele.
  Namshauri Mama huyu uwapo Bungeni asijetekwa kifikra na ile Big brother ya Ddm maana watu wamedata pale (namaanisha asisahau Kuwaombea wabunge wetu waache dhambi walizonazo hasa za ufisadi nk.)

 24. trii Says:

  mbayaaaa?

 25. Loyce Says:

  Kweli Trii…….Mbayaaaaaaaaaaaaaaa

 26. John. Says:

  If you are engage in politics especially in our country Tanzania you must be associate your self in one of the following things
  Politics in Tanzania means to be greedy,supertitious,prostitute,
  graft, Character assasination,loyal to your political party even at the expenses of Wananchi etc.It’s not a secret if you do in depth analysis you will find out that our politicains esp.M.P have engeged themselves in dirty game thus why they can not fight corruption and other mess in our society becaause they are part and parcel of it.Even when they meet for the first time they started to discuss about their Salaries and allowance it should be toped up.As if Majority of Wananchi are Living Luxurious Life while in fact they are living Horrible Life.

  Shame on You.Umejiunga na Mafisadi.
  John.

 27. Kimori Says:

  Dear pm,

  you are missing the point here….unfortunately, you couldn’t read between the lines. In a very superstitious parliament with rampant irresponsibility like ours, a genuine christian can not take a seat….it is either you wear the robe of hypocrisy and join them by relinquishing your faith or you stand firm in your faith.

  In a contemporary Tanzanian politics, especially in the house of representatives (parliament) everybody is there for a spcial interest and not to bring about the necessary changes for the sake of majority in the country.

  Let us not think that, to be appointed or elected to join the house is a blessing from the Lord…the devil is also too strong to be undermined…rememner he got away with one third of all the angels!

  If you are accepted by the world and its worldiness then you are rejected by the Lord…you can’t have it both ways!…Please read carefully the rest of the comments!

 28. any Says:

  Kaka Edwin, ni kwamba kuna watu sio watz wako bungeni, ivo nilikuwa nakumbusha je wana uhakika na hizo post wanazotoa ni kwa watz au hata kwa wahamiaji? tuna wahindi bungeni, sasa tutaanza kuwa na warudi, na waganda. mimi sio mkabila lakini kazi nyeti wapewe watz, na business waingie walio watz na wasio watz. I was just curious kuhusu uraia wake, nilikuwa nauliza, sijamalizia/conclude.

 29. Desert Eagle Says:

  Ndugu wajumbe n imerudi tena, safari hii nataka niwaombe kitu kimoja muhimu,

  Kwanza tukubali kwamba, “Dua la kuku halimfiki Mwewe” hata tukipiga kelele huyo mama hawezi kustep down. ulizeni walioshiriki wakati wa uchaguzi wa kuteua viti maalum jinsi huyu mama alivyotembeza Fedha, ushahidi upo,

  Cha kufanya ni hivi, “makosa yalishafanyika kwa hiyo tujipange 2010, cha msingi tujielimishe wenyewe nini umuhimu wa kuongeza viti vya wabunge wa upinzani bungeni.

  naongea haya kwa moyo m1 wala mimi siko upinzani lakini nshaona umuhimu wake. Huyu mama alipitishwa jina lake na mafisadi wenzake so tumuache aendelee tu hawezi kustep down hata kama tutafunga kula siku 40 kama bwana Yesu.

  Cha msingi tutambue kwamba, the majority (vijana na masikini wa Tanzania) hatuna wawakilishi mule bungeni, bali kuna wawakilishi wa kina Bakhresa (matajiri+wafanyabiashara)

  Chachage alisema “Vijana ni wakati umefika tuamke maana uongozi wetu umejaa madalali (mabepari) wa soko huria na hivyo itauzwa muda wowote”

  Ni hayo tu kwa sasa

 30. Fukara Says:

  Kwa maana jinsi hii Mungu aliipenda TZ. Hata akamtoa mchungaji wake wa pekee ,ili kila fisadi aaminie asipotee.
  Bali waen delee kuitafuna Tz milele

 31. Fukara Says:

  Kachape injili huko Dom mama waambie wabunge wote waokoke,
  Hizi ni dakika za mwisho
  Waache ufisadi
  Lkn namshauri kwakuwa ni milionea ktk shule zake aweke nafasi za kuwasomesha watoto wa maskini byre maana anapata faida sana.
  Hapo hata aliye rohoni atabariki.
  kila la kheri mama

 32. any Says:

  Kwako editor, i dont know where to put this, but let me write here, sijaona sehemu ya maoni kwenye hii site. Sorry to hurt your feelings, wasnt my intention. I wrote some stuff here which to u wasnt acceptable due to the fact that different people of different ages view this website. I wrote Mb, ku etc. Different people define matusi differently, to me those are just parts of human bodies. Na kwamba watoto wanaingia humu, nadhani mtoto wa umri wa kujua kuna bongocelebrity site watakuwa aware kuwa kuna vitu kama hivo (vikojoleo). I saw kids wa secondary schools mambo wanayoangalia Cafe are more than kuandika neno kama k au M! sorry and happy holiday to u all.

 33. Tatu Says:

  Tumuombeeni tu huyu mama.Anahitaji maombi.Mkenge keshauvagaa.

 34. punani Says:

  Wote mmeongea sanaaa mkasahau labda ni mpango wa Mungu Mama lwakatare aingie bungeni. Kama yeye anatoa mapepo kanisani kwake basi bungeni ndio mahala pake akavunje tunguli za kishirikina kwa jina la yesu.Huwezi jua mpango wa Mungu ni wa kufanya mafisadi wakawa watu wema, wenye ushirikina wakapunguza ama wakaacha ila nina uhakika atapambana na nguvu za giza sio mchezo watamjaribu kuona kama kweli yuko fiti ki imani.Kwa hiyo mwacheni mama wawatu akaliokoe Bunge letu tukufu

 35. Pale kuna wazee wa Bagamoyo.Sasa sijui Yesu atawasambaratisha wote au vipi.

 36. Dave Says:

  Happy Holiday any.

 37. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  Dhamira yangu na pengine sehemu ya historia inanieleza kuwa dhana ya kuwepo uongozi wa kidunia na uongozi tukufu (secular and sacred) ni pazia bandia lililoshonwa na wenzetu wa Magharibi.

  Wala haniingii mimi akilini kwamba baada ya uumbaji Mungu alikwenda akakaa katika kona fulani iitwayo ‘sacred’ na akaitelekeza sehemu nyingine kwa jina la ‘secular’ ambayo hatupaswi kwenda!.

  REKEBISHO:

  TUNGO ISEMAYO ‘HUWEZI KUWATUMIKIA MABWANA WAWILI’ INAONGELEA KUWATUMIKIA MUNGU NA SHETANI WAKATI MMOJA NA NA SIO KATI YA MUNGU NA WANANCHI!

  Hivyo upendo, haki, uwajibikaji, usawa na moyo wa kuhudumia wananchi kwa moyo na uadilifu vinatakiwa kuwa na uzito ule ule popote; haijalishi uko hekaluni, msikitini, kiwandani, uwanja wa mpira, ukumbi wa mkutano wa kisiasa, au katika kikundi cha kinamama cha kufa kufaana n.k

  Hili suala la kutenga eti kuna mahala pa Mungu na mahala pasipo pa Mungu ndio limetufikisha sehemu tunaishi maisha ya kifarisayo yenye utambulisho wa kuwa na namna ya uraia wa aina mbili tofauti. Yaani unakuta mimi Nyakatakule najiita Mkristo siku ya Jumapili tu au pindi tukionana na Mchungaji wangu na siku sita zilizobaki hapo eti ndo naitwa Mwafrika au Mtanzania. Huu ni upuuzi na ni maisha ya ufisi.
  Mimi napenda mniite Mtanzania Mkristo au Mkristo Mtanzania na siyo mara kuitwa Mkristo mchana na halafu usiku ndio najiita Mtanzania.
  Mama Rwakatale hongera na tutakutakia uwajibikaji na uwakili mwemwa kwa mujibu wa dhamana uliyopewa.

  Zaidi ya mifano mingi ya Watu tuliotajiwa wanaohudumu katika asasi za kidini k.m akina King Jnr na wakati huo huo ni wanasiasa, napenda kueleza kuwa Manabii walifanya kazi zote hizo mbili bila taabu yeyote.
  Rejea Amos, Hagai, Nehemia na Yesu Mwenyewe walivyorekebisha jamii dhidi ya dhuruma na ufisadi na wakati huo huo walitema cheche za injili kwa ajili ya Wokovu.

 38. queen Says:

  mwacheni huyu mama akaokoe wabunge maana wamejisahau hadi wamemsahau hata muumba wao.Kila jambo lina sababu zake,tuzidi kumwombea aende na imani yake akafanye kazi ya Mungu huko.sehemu kama bungeni ndio hasa panatakiwa watu kama huyu mama mwenye moyo wa kazi ,upendo,huruma na ucha Mungu.Kuhusu kuwa na mali ni matokeo ya uchapa kazi wake.Nenda mama kapambane na pepo wachafu huko bungeni hiyo ni nafasi umepewa na Mungu ukakemee nguvu zote za giza zishindwe bungeni katika jina la Yesu.

 39. any Says:

  Ulaji tu ndo sababu KUBWA. Akaokoe wabunge na zile guests za Dodoma mnataka ziende out of business. na machangu watakula wapi wabunge wakiokoka?

 40. Mie Says:

  NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO unayosema ni kweli, nadhani wote ni wahebrew! Shalom! napenda kusema kweli huyu mama ni mchapakazi nafasi zote alizonazo anazimudu vyema.
  1. Ni mchungaji kiongozi wa kanisa kubwa Mikocheni
  2. Mkurugenzi wa St.Maryz schools
  3. Ameteulikuwa kuwa mbunge
  4. Pia kuhusu praise power radio anahusika
  Sio ajabu anaweza kumtumikia Mingu wake siasa isiingilie mbona Yusufu aliweza? Daudi? amewasaidia watoto yatima wengi kuwasomesha bure katika shule zake, wenye shida za kufanya biashara pia amewasaidia kupitia PPRm na kanisa lake.

  Watu kazi yao kuhukumu, kusema negative things, lakini anajua yeye na Mungu wake, kama ametoa rushwa au ameenda kinyume na imani yake, Mungu atamuumbua, kama sivyo atazidi kusitawi

  Unahitajika mchango wako NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO blogu ya http://www.strictlygospel.wordpress.com karibu

 41. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  Mie.
  heshima yako na asante kwa kunikaribisha ktk blogu ambayo nilikuwa sijaijua. Nikakutembelea huko. Unajua ni vizuri Watanzania (na binadamu wote) tukengwa katika msingi wa kuwa critical lakini pia tuwe constructive na siyo kulaumu tuuuuuuu bila kutoa mawazo ya kujenga.

 42. Matty Says:

  Merry x-mas and happy new year all of you!!!!!!!bora mama ukawaokoe ma mp wetu pale dom labda ufisadi, uzinzi, uchawi nk. vitapungua.
  Any huyo mama ni mtu wa morogoro sio mrundi wala mrwanda.

 43. chikala Says:

  Jamani mama huyu naye ni fisadi tu anakula nao kwani mwizi lazima amtambue mwizi mwenziye mimali yote hiyo kajilimbikizia bado tu hachoki amekubali kuwafaata mafisadi wenzie mjengo ndo hapo tunatambua huyu mama hata uchungaji anazuga tu pale anajisafisha mbona tunaambiwa anachukua mshiko kwa wahisani huko nje ili kusomesha YATIMA angalia kama kuna chance za YATIMA pale kama zinatolewa nyingi zaidi zaidi watoto wa MATAJILI ndo wamelundikana pale..
  Huyu mama anamasrahi yake binafsi na anampango aweke shule zake mikoa yote ya TZ na alivyo kubali kuingia MJENGO mtaaona sasa watoto watakuwa wanapewa BORA ELIMU pale na ss si tupo kama hata pewa uwaziri wa ELIMU sijui!!! kwani hata MUNGAI alikuwa hivi hivi na shule zake.
  Powa wadau ndo serikali zetu za kulindana tu.

 44. anoni Says:

  jamani tuache utani! Unaweza kuwa mchungaji na ukawa na kazi nyingine km part tym lakini sio siasa jamani!!! Unajua haya mambo mawili yanakinzana kabisa! Kuna mtu aliwahi kusema kuwa siasa ni mchezo mchafu, unadhan aliropoka! hapana.

  Ataweza kweli kuwa mwadilifu ndani ya bunge chini ya mwavuli wa “chukua chako mapema”? Kuna mambo itabidi akubaliane na kupigia kura ya “NDIO” hata km si sahihi.
  Mi nadhan aachie uchungaji ili atakapochemka bungeni tusiseme “Mbunge Mchungaji lwakatare amechemka”
  Alternatively, aachie hicho kiti hakimfai km mchungaji.

  By the way, yeye si wa kumfananisha na akina mtikila na Martin luther.

  Jamani, ametoa mchango mkubwa sana ktk kuokoa jamii inayoangamia kwa madhambi siamini ndo tunampoteza!!!! hii iiiiiiii !!!!!!!

 45. Desert Eagle Says:

  Naona kuna watu wanajidai watumishi wa bwana wazuri na kumtetea huyo mama,, nadhani ni wakati nanyie mtuambie historia ya utajiri wa huyu mama maana kila utajiri unahadith yake,, hata Bakhressa ana historia alipotokea..

  Huyu mama historia imegubikwa na utata hakuna anaejua ipi ni kweli mimi ninavyokumbuka kabla sijaanza kuhangaika na maisha nilimuacha mgodini mwadui mume wake alikua mfanyakazi pale,,,after there sijui katoka vipi

  Haya nyie mashahidi wa yehova tunaomba mtufumbue macho,,

  Tatizo jingine ambalo hamuelewi nyie mashahid wa Yehova, ni kwamba watu wanajiuliza maswali mengi kwa sababu hawajui anaenda kumuwakilisha nani??

  “”Yesu alisema, ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano, na ni vigum saaaaaana tajiri kuuona ufalme wa mbingu””

  Kwa maana nyingine huyo mjumbe anaesema kwamba mama Rwakatare anaenda kuwaokoa wazee bungeni asahau kwa sababu,, bunge letu ndo kijiwe cha matajiri wa Tanzania na kwa mujibu wa bwana Yesu kwao itakua ngumu sana kuuona ufalme wa mbingu,,,,

  Sasa kama yesu alishasema sijui wewe unajaribu kupingana nae au lah….

  “”Sauti ya watu ni sauti ya Mungu””

 46. Msee Says:

  Kazi mnayo

 47. Mwandishi Huru Mwafrika Mtanzania Says:

  NI JAMBO JEMA KUWA KUTHIBITISHWA KWA MCHUNGAJI DR. GETRUDE RWEKATARE NA KAMATI KUU YA C.C.M KUMEHITIMISHA ULE ULAGHAI WA KISIASA WA ” KUTOCHANGANYA DINI NA SIASA”. KILIO CHA WAISLAMU KUWA DINI NA SIASA INACHANGANYWA NCHINI TANZANIA KISAYANSI SASA KIMETHIBITI. POA! SAFI SANA! NAWAOMBA WAISLAMU WASILALAMIKE MLANGO UMEFUNGULIWA KAZI MOJA!
  NI DHAHIRI KUWA HON. MP. DR. RWEKATARE ATAKUWA AT THE SAME TIME “MWANASIASA NA KIONGOZI WA KANISA”.

  HONGERA MAMA! KARATA ZAKO ZIMESAIDIA KUIBAINISHA HAKI NA UKWELI ULIOKUWA UMEFICHWA.

 48. martildal Says:

  dini na sias ni vitu viwili tofauti mchungaji ili asionyeshe unafki inatakiwa aachie utuzi huo aongoze kondoo wa mungu na asipokubali basi yeye si mchungaji bali ni mtu wa kutafuta maslahi binafsi,jamani dini hizi tuwe makini wengine wanatafuta utajili kupitia jina la mungu,dini na sias ni sawa na kuchanganya oil na maji!!!!!!!!!!!!!!

 49. mirry Says:

  mama aongeze mabazeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
  na allowance za ubunge.

 50. Joseph Says:

  kwa kweli mimi nafagilia mabazeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee yake yaani anatoka bomba kichizi.

  damu na maji mwanangu wapi na wapi

  kazi kwenu watakao husika

  me simo


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s