BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MIAKA MIWILI,UNASEMAJE? XMAS NJEMA. December, 24, 2007

Filed under: Mahusiano/Jamii,Mawazo/Tafakuri,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 9:42 AM

 

Tumeshawahi kusema siku za nyuma kwamba,katika nchi,hususani zetu za kiafrika,Raisi ndio celebrity mkubwa kushinda wengine wote. Kinachomfanya raisi awe celebrity kushinda wengine ni ukweli kwamba umaarufu wake unadumu kwa kipindi chote anachokuwa madarakani wakati umaarufu wa watu wengine unapanda na kushuka hata ndani ya wiki moja au mbili tu.Leo yupo juu,kesho hatumsikii hata jina lake. Lakini Raisi naye akishamaliza muda wake, umaarufu nao huanza kupungua.Akitokea sehemu sio ajabu watu wengine wakamuulizia;hivi yule jamaa alikuwaga nani vile?!!Ndio hali halisi.

Wakati tunaelekea kuupa kisogo mwaka 2007,Raisi wetu wa sasa,Jakaya Mrisho Kikwete(pichani) naye huwa anazidi kuandika historia kwenye vitabu vya kumbukumbu.Hivi majuzi ametimiza miaka miwili tangu aingie madarakani.Aliapishwa rasmi kuiongoza nchi tarehe 21 Desemba mwaka 2005. Kwa hiyo mwaka unapoisha na yeye huketi chini na kutafakari.Wewe je,unasemaje kuhusu miaka miwili chini ya Jakaya Mrisho Kikwete?

BC inamtakia kila la kheri katika kuendelea kuiongoza Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Pia tunawatakieni nyote Kheri ya Xmas.

Advertisements
 

53 Responses to “MIAKA MIWILI,UNASEMAJE? XMAS NJEMA.”

 1. Desert Eagle Says:

  Yes The real “DESERT EAGLE” pia nawatakia kheri ya x-mass na mwaka mpya wadau hasa BC hakuna kulala hadi kitakapoelekea.

  Kuhusu Kikwete wala sina la kusema maana kila mtu anaona mambo yameendaje mwaka huu na miaka miwili kwa ujumla ya uongozi wa Bw. Da Gama.

  Pia namtakia safari njema rais wangu niliempaatia ticket za kukwea mapipa (kura). Najua mwaka unaokuja atatembelea nchi nyingi za Asia na Africa.

  Any way kila la kheri wa-Tanzania na rais wangu na watoto wake pia nawatakia masomo mema huko ulaya mungu awajaalie Mie Desert Eagle naendeleza kilimo ili nilipe kodi na nyie msome kwa raha maana ni haki yenu.

  “”One””

 2. mkata issue Says:

  Bila hiyana wala unafiki wa kutoa sifa sizizoenda shule wala pasipo kupinga tu kwa sababu ya kuonekana mpinzani mie naandika balance sheet ya miaka miwili ya Kikwete:

  Assets:
  1. wanawake wengi wamepewa nafasi za uongozi wa juu serikalini kuliko ilivyowahi tokea. Mfumo dume lazima uendelee kupigwa vita!

  2. Rais amekuwa karibu na kusisitiza umuhimu wa wachezaji na wasanii. Tuendeleze vipawa vya wachezaji toka utotoni. Tusiendekeze malumbano ya Yanga na Simba na malalamiko dhidi ya Lundenga yashughulikiwe. Tz isishiriki katika Big Brother mpaka hapo itakapobadili mwelekeo wake.

  3. Alipounda tume ya uchunguzi kuhusu mauaji yaliyofanywa na Polisi isivyo halali na hatimaye sheria ikachukuwa mkondo chati yake ilipanda toka 80% hadi 100%. Na nadhani Mola alimfungulia Kikwete milango ya neema isiyo na makufuri!.

  Liabilities:
  1. Ameunda Wizara na baraza la Mawaziri kubwa kuliko yote yaliyowahi kutokea na hivyo kuongeza gharama kubwa sana kwa serikali na kwa walala hoi.

  2. Ametamka (ahidi) mambo mazito yanayogusa hisia za wengi lakini wananchi hatujaona kama yuko serious kuyatekeleza mfano. kupambana na wahusika wa madawa ya kulevya, kurekebisha mikataba ya madini na tatizo la rushwa na ufisadi hususani katika ngazi za juu za utumishi wa umma. Gavana wa BOT ni lazima afikishwe mbele ya haki akiwa kwenye drip, machine, wheelchair etc (usimwangalie nyani usoni!!- vinginevyo watu wanakugeuzia kibao)

  3. kutokuwa makini katika kuhakikisha kuwa kuna haki na uhuru wa kushiriki vyama vingine vya vya siasa bila bughudha wala dhuluma. mfano. Kuachilia Bunge kumsimamisha Kabwe eti tu kwa sababu katoka upinzani) wakati yeye anaomba tume iundwe na baadaye akaunda tume na kumshirikisha aliyeadhibiwa bila kwanza kumwomba msamaha. Rais kumbuka kuwa kuomba msamaha sio dalili za kushindwa bali kushinda na ni ukomavu katika kuongoza. Mfano mwingine ni katika chaguzi za Madiwani na wabunge. kuna kesi kibao za ubinywaji wa haki, mimi nakupa hapa moja tu ya nguvu.
  Katika jimbo la uchaguzi Musoma mjini. Fanya uchunguzi wako wote kupitia CCM, Vyama vingine, Usalama na hata katika Misikiti na Makanisa watu Musoma walipigwa mabomu ya machozi bila sababu, wakanyimwa uhuru wa kukutana wakati wa kampeni sawa na kwa wagombea wa CCM. Huko Nyamatare mama Rhobi kuyenga hakustahili kuwa Diwani (eti alishinda kwa kura sijui moja) maana kura zilipigwa wakati mpinzani wake akiwa ndani yeye na ndugu zake wakazi wa kata hiyo. Hiyo ni dhuluma kubwa sana maana hata mgombea angepelekwa kupiga kura akiwa ndani ya pingu kama angeoneka kuwa tishio la amani. Igeni demokrasia na haki kwa wenzetu S/Afrika Leo hii Zuma ni rais wa ANC wakati anaendelea kuwa mtuhumiwa.
  zaidi ya hapo, nakueleza kuwa juzi ilipohukumiwa kuwa ndg. Mathayo anaendelea kuwa mbunge, Musoma yote ilionekana kuwa kama imemwagiwa maji baridi. Huyo mtu HAFAI KABISA si kwa sababu ya kisomo chake cha std 7 maana hakuna cha form four bila cheti bali ni ka ajili ya MATABAKA ANAYOYAJENGA , NA PIA KUTOMKUBALI MTU YEYOTE ANAYEPIGANIA AU SIMAMIA HAKI KWA GHARAMA ZOZOTE. Kama hulijui hili muulize EX – Mbuge Marwa maana hata wewe mwenyewe ulimwamini hadi ukampa u-DC. Tena ni kweli kuwa Mathayo alichaguliwa kwa rushwa ya wazi. Mimi sijali kama upinzani nao walikuwa wanahonga maana kama ni hivyo wote walitakiwa kuwa disqualified!! Kitendo cha kushindwa kukemea na kuwaondoa viongozi wabovu Musoma na Mara kwa ujumla kutatufanya tuwe na CCM – Chipolopolo kama ile ya Zuma na kipindi kijacho cha uchaguzi na moto utatuwakia!

  4. Mawaziri wake na watendaji wengi wa ngazi za juu ama hawajawajibika ipaswavyo au ni waoga katika kutekeleza wajibu wao. Mfano. Suala la kuchelewesha mahujaji kwa utapeli liko wazi, Mwenyekiti wa Bodi ATC angesimamishwa mara moja na siyo kuombwa ajiuzuru. Ndg. Ditopole asingepewa dhamana na kwa vile kesi yake na uchunguzi uko wazi angehukumiwa maisha liwe fundisho. (Najua inauma sana rafiki yako anapofanya jambo mabaya ikabidi aadhibiwe kikali lakini huo ndio msalaba wa kuwa Kiongozi). Majaji hawajiamini ndio maana hata mtuhumiwa hiyu alikuwa anapelekwa kupitia milango ya nyuma na si ajabu akahukumiwa kifungo cha nje. Ikitokea hivyo nakwambia kuwa Mola ataweka makufuri katika milango ya baraka na tutaona majibu yake.

 3. any Says:

  anauza sura tu, hakuna kinachofanyika, after ten yrs mtalia kwa uchungu wote mliompa kura, kazi yake ni ziara , na kupiga picha boyz two men. hehe, mwakani watatoa album mpya na boyz 2men.

 4. majita Says:

  Majita ninasema INYAMUWANGA ICHISAKILE.

  JF nashukuru sana kututakia Xmass njema na kutupa jambo la kutafakari tusherehekeapo xmass huku tukitafakari miaka 2 ya serikali ya mr Vasco Dagama.Nimefurahi binafsi kwa wazo hili.Na kama ilivyo ada,lazima tuangalie miaka 2 ya Vasco Dagama kwa kuhusianisha na wenzake waliomtangulia.Watu huwa wanasema kuwa huwezi kusema rangi fulani ni nzuri bila kufananisha na rangi zingine,kwa lugha nyingine naweza kusema kungekuwa na rangi 1 tu duniani tusingesema rangi fulani ni mbaya.sasa mimi nitachambua miaka 2 miwili ya Vasco kwa kulinganisha na awamu iliyomtangulia ya Mh.Ben Wiliam Mkapa.

  Nitachanganya mambo kutokana na ufinyu wa page na kuogopa kuchosha wanakijiji ila nita-base katika maendeleo ya uchumi,siasa na jamii aidha nitagusa kila eneo.

  Naanza kwa kusema kuwa Rais Kikwete aka Vasco Dagama AMESHINDWA kabisa kuleta maendeleo kwa taifa na hivyo kusababisha kuporomoka kwa maendeleo ya Taifa.Nikianza na:-

  UCHUMI:-Hapa Vasco kashindwa kabisa kiasi cha yeye mwenyewe kukiri akiwa Uingereza kuwa kamwe hajui kwa nini watanzania wanazidi kuwa masikini kiasi hiki.So hana mikakati kabisa.DENI la taifa kwa mwaka huu peke yake limekuwa Dola 440.5 milioni ambazo ni mabilioni ya shilingi ya kitanzania.Sidhani kama tunaelewa takwimu hizi sawasawa.Kibaya zaidi thamani ya shilingi yetu inazidi kushuka.MFUMKO wa bei hapo ndo usiseme.Kwa sisi wanakijiji wa chini hatutumii asilimia.Tunaangalia bei za vitu kwa miaka iliyopita.Wakati wa Mh.Mkapa kwa mfano kilo ya sukari ilikuwa tsh.800.Uliza sasa ni tsh 1800/=angalia bei ya mafuta(gas),sementi,na gharama za maisha kwa ujumla,hapo ndo utajua hali halisi.

  ELIMU:-Wakati wa mh.Mkapa tuliona maendeleo ya program ya MMEM/PEDP na MMES/SEDP.Hii ni sera ya CCM na ilani ya uchaguzi ya CCM.Mkapa alifanya vizuri kabisa hadi malengo ya MMEM yakafikiwa.Tuliona madarasa na wanafunzi wengi wakiwa enrolled huku walimu wa primary wakiongezeka.Hope tunakumbuka ule mwaka mmoja mmoja wa kusomea cheti cha ualimu grade A.Mwaka 2005/2006 MMEM ikaisha na tukategemea MMES kuunganisha.Mmmmm Uliza sasa kwa huyu mr Vasco Misafari,yani sijui anafikiria wapi.Ok anasisitiza kujenga madarasa huku hiyo shule haina walimu.Yani mimi siku zote nahoji uwezo wa akili na maamzi ya huyu mr.Misifa aka boys II men.Kwa nini ashindwe kuhusianisha mambo????

  SIASA:-Wapinzani wanazidi kuonewa tu.Sikuona umuhimu wa kumsimamisha Zito ubunge kwa hoja zake bungeni.Ona kichekesho sasa,Zito alisimamishwa ubunge,alichokuwa anadai ni pamoja na kuundwa tume huru kuchunguza mambo ya buzwangi.Huku alisimamishwa sasa kuna kamati iliyoandaliwa ya kuchunguza alichokuwa analilia ZITO.Kuna uongozi hapo???Serikali hii imeshindwa kupitia upya mikataba ya madini kama ilivyoahidi aidha bado inajikanyaga kanyaga tu.

  Tuhuma za UFISADI zimeongezeka sana kulinganisha na serikali iliyopita,so hapa suala la Utawala Bora ni ZIRO.Mnamkumbuka bwana Masilingi enzi zake na cheche zake???Hili baraza la mr.Vasco ndilo la kwanza kuongoza kwa tuhuma za ufisadi kuliko yaliyowahi kuwepo.
  TAKURU Sijui TAKUKURU nayo imezidi kuwa corrupt. akumbuka TAKURU waliwahi kuitetea kama sikosei RICHMOND kumbe huko ndo kumeoza kabisa.Sasa unabaki unahoji,hawa TAKURU wanapambana na nini na kwa uzoefu gani kama hata ya RICHMOND hawakuyaona.

  Ujenzi wa BARABARA.Laaah hapa sisemi.I wish Mkapa angeendelea tu kuwa Rais kwani am sure hadi sasa majita tungekuwa na lami.Mnamkumbuka Magufuri???Huyu mkubwa yani namuogopa sana kwa akili zake.Alikuwa na uwezo wa kukariri kilometers za mabarabara yote nchini bila kusoma sehemu.Yeye ugomvi wake ulikuwa kwa hao makandaras.Unakumbuka utamu huo???sasa ni kucheka cheka tu na kutuongezea misemo na nahau tu.

  Nina mengi.Naomba kuishia hapo.Ntaongeza tena badae.

  LAWAMA:-
  Waandishi wa habari wamezidi kupotosha wananchi kwa kuandika habari hasa za kuipendelea serikali.Ni juzi juzi tu ndo angalau baadhi ya magazeti yameanza kuandika ukweli kuhusu Vasco Dagama.Hii inatokana na ukweli kuwa Mh.Mkapa alikuwa IMARA kwa waandishi na alikuwa anajua longolongo zao hivyo waandishi wakatokea kumchukia.Sasa Mr.Vasco Misifa yeye baada ya kuliona hilo akawakumbatia waandishi kiasi cha Waandishi kumwona Vaso Dagama kama Mungu wao.Utaandika kinyume na mungu wako kweli???

  WITO:-Wananchi Mwaka 2010 tusifanye makosa.Rais Kikwete miaka yake 5 ya kutuangamiza inatosha sana.Tafadhali tusimchague tena.Hana jipya huyu.Ni kuchekacheka tu.Alisema I have a smilling face but strong in action.Tukaamini.Kumbe hakuna lolote.So its a right time now kuwaondoa mafisadi na mtandao wao wote.2010 usipoteze kura yako.Vote against Jakaya Mrisho kikwete.
  Wasalaamu

 5. baho Says:

  tanzania inakupenda, usisahau maoni ya wananchi ni muhimu sana.

 6. kiho Says:

  likizo njema jk, all the best pumzisha kichwa na kutafakari ya mwaka ujao, merry x-mas.

 7. Desert Eagle Says:

  Ndugu zangu,, hii kuna mahala nimeiweka ila naona kimya..

  Naomba kuwajulisha kwamba Mr. Vasco Dagama ataingia mwaka 2008 na mtihani wa kumteua mrithi wa Daud Balali (Dalali). Majina yafuatayo ni ya baadhi tu ya waajiriwa wa BOT naomba tupige kura nani anafaa kuiongoza BOT maana naona CV zao zinalingana so kilichobaki ni kuwapigia kura..

  Hii itatoa democrasia ya hali ya juu kwa wananchi wote kumchagua Governor wa benk kuu ili kuondoa Ufisadi

  Jamani katika pekua pekua nimekutana na baadhi ya waajiriwa wa BOT naomba tupige kura yupi anafaa kumrithi Dalali. Tafadhari Admn naomba uiache watu waitambue orodha hii usiitoe tafadhari.

  1. Pamella Lowassa,
  2. Filbert Frederick Sumaye,
  3. Zalia Kawawa,
  4. Harieth Lumbanga,
  5. Salama Ally Mwinyi,
  6. Rachael Muganda,
  7. Sylvia Omari Mahita,
  8. Justina James Mungai,
  9. Kenneth John Nchimbi,
  10. Blassia Blassius William Mkapa,
  11. Violeth Phillemon Luhanjo,
  12. Liku Irene Katte Kamba,
  13. Thomas Mongella,
  14. Jabir Abdallah Kigoda etc.

  Je nani anafaa????

  “”Am dersert Eagle and I dont deserve to serve any political party in Tanzania”” (Socrates)

  One blood (Its ok……..)

 8. MpandaNjia Says:

  WATANZANIA INABIDI TUONDOKANE NA UNAFIKI. UMEFIKA WAKATI INABIDI TUWE WAKWELI ILI TUWEZE KUENDELEA. PAMOJA NA MATARAJIO MAKUBWA TULIOKUWA NAYO SISI WATANZANIA BWANA JK AMETUANGUSHA SO FAR. AND IF HE IS NOT CAREFULL HE WILL GO INTO THE BOOKS AS THE MOST DISSAPOINTING PRESIDENT OF OUR TIME. TUMECHOSHWA NA POROJO SASA NI WAKATI WA VITENDO. MAMBO YA CHUKI VISASI KWA BAADHI YA WATU WALIOKUWA KARIBU NA UONGOZI ULIOPITA HAYANA NAFASI KATIKA JAMII YA WATANZANIA. MWL NYERERE ALIFANYA KAZI KUBWA YA KUTUUNGANISHA SASA SIONI SABABU YA JK KUTAKA KUWAGAWANYA WATANZANIA. CCM IMEFIKA WAKATI AMBAPO INABIDI TUSIONEANE HAYA. YALIYOMFIKA THABO MBEKI KIKWETE ASIYAEPUKE. JIANDAENI KUCHEZA MDUNDIKO IKULU

 9. Msafiri Says:

  Kwa kweli mimi nadhani kuna tatizo somewhere kwenye uongozi wake. Uongozi huu si kama ulivyokuwa wa MPAKA. Wakati wa Mpaka amambo yalikuwa moto mara moja! Hakuna ubabaishaji na lugha ndefu!

  Raisi huwezi kusema uchumi wa nchi unakuwa wakati hali halisi haionyeshi hivyo. Kwa mfano, mwezi wa saba mishahara ya wafanyakazi imepandishwa, japo kiduchu, lakini, mpaka leo baadhi ya idara za serikali, kwa mfano Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na maeneo mengi hawajaanza kulipwa hiyo mishahara. Miezi sita baada ya kupandishwa! Sasa huo uchumi na reserve ya dolla billion mbili za nini na zinafanya nini huko ziliko iwapo wahusika haziwagusi?!!

  Pili, hali halisi ya maisha kwa watu vijijini inazidi kuwa mbaya na ya kutisha siku hadi siku. Juzi juzi nilisafiri kwenda kijiji kwetu huko. Kuna maeneo watu hawajawahi kuona shilling 5000 kwa mwaka mzima huu tokea uanze! Sasa hii nini kitu gani kuweza dolla billion mbili reserve wakati watu wako hata 5000 hawaijui mwaka mzima!

  Tatu, nayo foleni ya magari Dar es Salaam inahitaji uchum kukua kuweza kutatua? Mbona wenzetu huko nje wana magari sawa na idadi yao lakini hatuoni foleni kama zetu hapo bongo? Ni uzembe tu, ambao kwa kweli unatokana na system nzima ya juu. Sioni kwa vipi Chenge aone uchungu mahujaji kukosa ndege ya kwenda Jeddah wakati pale Kibaha ukipiata usiku ni dhahama kubwa sana ya foleni! Hivi keli tunahitaji uchumi kukua kuweza kutatua tatizo la foleni poale mzani?! Wenztu wanasema time is money sisi tunaipotezea kwenye mzani? NI jambo la ajabu sana kupima gari ya tani tano na ukaifanisha na gari ya tani kumi! Hakuna kitu kama hii DUniani, ni Tanzania tu!

  Barabara ya Mikumi – Ruaha Mbuyuni. Hivi kweli mpaka waziri apate ajali sehem kama hizo ndo serikali itakumbuka kukarabati!? Barabara mbaya sana lami imetobokatoboka hovyo, ili mradi kero tupu! Sasa hiyo reserve ya dolla billiona mbili inafnya nini badala ya kukarabati hizi barabara? Hiyo ni mfano wa barabara chache tu nchini zinahitaji ukarabati, na si kutengenezwa?! Inashindikana!

  Mimi nadhani, muda upite tu. , Kama mistake Watanzania huwa tunafaya nyingi. Lakini misatke ya sasa hivi ni babu kubwa. NIna amini mnaelewa!

 10. Kimori Says:

  Nani anafikiria kuwa nchi ina rais?….niulizeni mimi…

 11. Ana Says:

  mzee kimori au sijui kamori sijui ndiye yule wa NBC?? samahani kama nimekosea. Hebu tupe data zinazoonyesha kuwa nchi haina rais.

 12. Recho Says:

  Hakuna raisi balakala ya watoto wao kulinga wanabahati ulaya Haki sawa kwa wote.Serikali ya Kikwete ni ya wakoloni weusi

 13. majita Says:

  Anna, yule Kamoli Jimogi aliyekuwa Director wa NBC miaka ya 90’s alitokea BoT alishapigika na maisha kinoma.nasikia ndie JK anataka kumfanya Gavana wa BoT baada ya Balali.

 14. sado Says:

  we mpand anjia umeongea point na kweli, wajiandae kucheza mdundiko uko ikulu, wananchi mna haki sawa, kama nchi zingine, na kweli wajiandae kucheza mdundiko.

 15. kaso Says:

  nyie ndio wapiga kura, mna power tanzania, mmemchagua huyo kamanda, kama hampendezwi muulizeni.

 16. soso Says:

  majina mengine hapo juu hata hayafai kabisa, ni baadhi tu ya hayo majina, kwanza haina haja ya kuwapigia kura, ni bora kutafuta mtu mwingine kabisa, we mwenye hiyo list, umekosa kazi nini, weka jina lako

 17. zibo Says:

  yaani mwenye hiyo list namuonea huruma sana tena sana. Hana kazi nini, badala akatafute wasomi toks IFM, maccountant wako wengi sana, ameamua kutundika hiyo list, unadhani wanajali basi, unawapa sifa tu, we mwenye list nenda IFM, au wanafunzi toka nchi za nje, wakow engi, pia wako wengi waliofanya kazi bot, na benki zingine,w atanzania mnachekesha sana.

 18. fukara Says:

  Unajua watanzania ni wanafki (baadhi yetu) ,naomba tujue kwamba ,hatma ya tanzania iko mikononi mwetu.
  Nitawarudisha nyuma kidogo wakati wa kampeni za uchaguzi.
  ” Mh.Dagama ” ktk kampeni zake alifikia hgatua ya kujiona anakubalika na kusema
  Nanukuu” akina mama najua kurazenu ninazo sasa kazi nikuwahimiza waume zenu kwamba ikifika siku ya uchaguzi,waopia “MWISHO WA KUNUKUU.
  mIMI NIKO uGHAIBUNI NA NINAONA KWAMBA Dagama alijiamini hadi kufikia kuleta usanii.
  Sasa kutenda kosa si kosa ,balikurudia ndo…..
  Nilijua maadam yuko nahawa mafisadi hakuna jipya
  sasa Watanzania tubadilike na tusifanye ajizi.
  Huku nilipo naona aibu kujiita mtz maana hakuna lakujivunia
  Nawatakia merryx-mass&prosperous new year

 19. fukara Says:

  bot ATAMWEKA RAFKI YAKE dr>charles kimei KWA KIGEZO KWAMABA ameiendesha CRDB vyema maana nilipokuwa Sweeden nilimsikia akimtaja kwamba watz walipokutana naye na kusema kunautaratibu ilituweze kuweka fedha zetucrdb na kuinufaisha nchi.Nainda nyumbani ishaaalah kuona mambo jinsi yalivyo na nitatoa ripoti as soonj as possible
  kila la kheri
  FFUKARA

 20. sango Says:

  watanzania badala ya kutangaza magazetini, kuwa watu mliomaliza accounting, ombeni kazi bot, au wasomi wengi tu wako mitaani, mnabandika hayo majina, kweli wewe mwenye list uwe unafikiria kabla hujaweka hiyo list hapo juu. Wahitimu wa accounting wako wengi sana tena sana, tanzania, jamani mtafika, nendeni idara za hesabu na serikali, kabla ya kurukia hao watu, weka sifa zajo hapo, na wewe eagle umesoma nini?

 21. kiso Says:

  jk leo anang’oa huy, kesho anakimbia marekani, yyani amenichanganya sana simuelewi kabisa kabisa, sijui nyie watanzania wenzangu, naomba ushauri, kama atarudia haya haya miaka inayokuja, lazima kuwe na serikali ya mpito, hamna kuogopa, hasa hasa nyie watu wake wa karibu, mnamshauri vipi huyo jamaa jamni, hatari sana.

 22. nick Says:

  miaka miwili imepita na kila dalili zinaonyesha kuwa kikwete is a boogy man. maamuzi yake mengi yamekuwa ni ya kuwalinda viongozi wabovu kwa kutumia tume za uchunguzi kuchunguza vitu ambavyo hata mtoto mdogo anajua kinachoendelea(tume za kuchunguza mayai viza) ktk mikataba ya madini harufu ya rushwa kila mahala lakini hakuna atua anayochukua bali ni kuunda tume kufanya bogus investigation lengo likiwa ni kuwalinda viongozi wabovu. sababu ya kusema kuwa rais kikwete ni boogy man ni kwamba rasi kikwete ni actor mmoja mzuri mara nyingi amekuwa akiact kama vile anafanya kitu fulani kwa nia ya kuwaonyesha watu kama anachukua hatua fulani ukiingia ndani utagundua hakuna anachifanya isipokuwa ni ku act tu. nina mifano mingi kudhibitisha haya ninayosema mfano mzuri ni pale baada ya kuapishwa rais alizunguka maeneo mbali yakiwemo muhimbili na soko la tandale, alipofika soko la tandale alijifanya kuwaomba wabiashara kupunguza bei za vyakula, hii ni ajabu kwani kikwete anajua wale ni wafanyabiashara wana gharama chungu wanazozingia ktk kufanya biashara na nia yao ni kupata faida ili waweze kukaa kwenye biashara una maana gani unapokuja kwenye biashara ya ntu na kumweleza apunguze bila kutaka kujua hali halisi ya biahsara yake. kikwete anajua wazi kuwa hilo aliwezekani isipokuwa lengo lake ni kuwaonyesha wananchi kwamba anajali huku akijua kuwa siyo kweli. alipokuwa muhumbili alishangaa sana kuona wagonjwa wanalala chini, mshangao ule ulikuwa ni wa ajabu kwani hakuna mtu asiyejua kuwa wagonjwa wanalala kwa miaka na hata Kikwete mwenyewe analijua hilo isipokuwa kuwaonyesha wananchi kuwa anajali wakati si kweli anajifanya kushangaa(boogy man). juzi kuunda tume ya uchunguzi wa richmond ni ktk hali ya kuwaonyesha wananchi kuwa he is doing something lakini si kweli kwa maana anawajua wote walioiibia serikali ktk issue ya richmond lakini ili kuwaonyesha wananchi kuwa anachukua hatua ndio kuunda bogus commision huku akijua wazi hazina nguvu za kisheria. juzi ktk safari yake ya marekani aliwakuta mahujaji wanasota uwanja wa ndege ili kuaonyesha mahujaji kuwa he is doing something ndio kujifanya siondoki mpaka mahujaji waondoke huku akijua wazi kuwa siyo kweli ni kuwazuga mahujaji kwa maana kikwete kama rais anao uwezo wa kumpigia simu mkurugezi wa ATC na kupata maelezo yote ya safari ili kuja nini kinaendela na hakuna haja ya kujifanya kuwa hata yeye aelewi kwanini mahujaji wamekwama. kwahiyo ktk miaka hii miwili yake ya uongozi Rais kikwete amtuthibotishia kuwa yeye ni boogy man na siyo mtendaji kwa maana hata hivyo hakuwai kuwa na record yeyote ya kuwa mtendaji kabla ya kuwa rais.
  NAWATAKIA HERI YA CHRISTMASS.

 23. ISMA KABENGO Says:

  MIAKA MIWILI YA KIKWETE HAKUNA KITU CHA MAANA CHA KUJIVUNIA,SHILLINGI IMEZIDI KUPOROMOKA HII INAASHIRIA UCHUMI HAUKUI,UMASIKINI UNAZIDI KUONGEZEKA,TUME NYINGI AMBAZO HAZINA MAJIBU WALA KUTATUA MATATIZO YA WATANZANIA,AHADI ZISIZOTEKELEZEKA,RAIS KUSAFIRI SANA NJE NAFIKIRI HUYU NI RAIS MPENDA KUSAFIRI SANA NJE KULIKO RAIS YOYOTE KATIKA HISTORIA YA TANZANIA KWA KUTUMIA FEDHA ZETU WALIPA KODI

 24. Kimori Says:

  Ana, Tafadhali usinichanganye na mtu mwingine yeyote….Jina langu hapo jhuu linasomeka vizuri kabisa wala hustahili kuulizia tena!

  Kwani wewe kwa imani yako hata bila data unaona kweli kuwa nchi ina rais?… Au yawezekana uko nje ya nchi kama akina Balali na wenzake maana hii mitandao inatumiwa sana na walio nje ya nchi ambao hawajui ni kwa kiasi gani maisha ya wananchi ni magumu hapa nchini! Nchi inatia huruma!

 25. Ana Says:

  Majita, Kamoli tena kurudi BOT? tumekwisha; mzee huyo hana msaada wowote ktk kukuza uchumi wa nchi wala kwa Watanzania binafsi. Ukimya wake hauuziki popote!!

 26. BongoSamurai Says:

  Mhh maskini Tanzania nakuonea huruma maana uko mokononi mwa mafisadi wanaojiita viongozi……..!

 27. fukara Says:

  yaani we acha tu,alipokuwa kwenye thifa ya kitaifa mjini Dodoma,alimtuma mkewe kwenda kuwa pooza mahujaji pale airport.
  Nadhani mama huyu hakupanda treni!! aliruka na pipa nakama ujuavyo gharama za mafuta ya ndege ilivyo panda
  kwenda na kurudi,lakini analipa nani…….mimi fukara ,akarudi Dodoma.
  Baadaye rais akapanda pipa kwa lengo hilohilo….
  Sasa labda mnisaidie ndugu zangu maana Uk.ndege za viongozi zinaruswa kwa mpango maalum.
  Nasikia ni “MCHUMI”-Economist.Sasa kamahilo dogo tu anashindwa kuliangalia sembuse hatma ya maisha ya mafukara Bongo kweli yatajulikana kwa kipindi cha uongozi wake?
  Watanzania mlioko home MNAVUNA MLICHO PANDA tena na bado hiyo ni trella tu .bado yenyewe isubirini.
  Maana mlizani mchezo wapinzani walipo wasii msiirudishe CCM- ‘ mmechuammeweka waaaaaa’

 28. Upendo Furaha Says:

  Kwa Ujumla Ninampongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutimiza miaka 2 Ikulu.
  Ninamuomba Mungu ampe Maisha Marefu na Ufanisi katika kazi hiyo “Ngumu” ya Uraisi.

 29. Papaa Says:

  Miaka miwili ndo imepita…tumaini letu tulilonadiwa kuwa limerejea inaonekana sasa limepotea!

 30. Desert Eagle Says:

  soso, sango hii ni elimu kwenu maana inaonekana mnaufinyu mkubwa wa kuona, kuchambua na kutafakari mambo,

  Hapo BOT hakuna hata mtanzania mmoja anaejua nafasi za kazi zinatangazwa na kutolewa vipi,,acheni kuropoka waulizeni wazee wenu watawaambia yanayoendelea BOT.

  Mimi sijabahatika kusoma sana kwa sababu kiwango changu ni sawa na cha rais wangu (BA Economics),,, Hao mnawaita wenye degree za Accounts waambieni waende waka-apply hapo BOT halafu watawahadithia

  Nyie inaonekana ni walewale watafuna kodi zetu na hamna uchungu na matatizo yanayotukuta sisi walala hoi,, inatakiwa tupige kelele pamoja ili mambo yabadilike pale BOT

  Enyi wadogo zangu (Kifikra+Kiuchambuzi) mambo yafuatayo ndo yamenifanya kutoa hiyo orodha, kama kuna mtu nimemuonea naomba mniambie kisha mnitajie idara yoyote ya serikari yenye watoto wa vizito kama BOT,,,

  (1) Ajira za BOT hutolewa kwa watu wachache na maalum
  (2) BOT ni sehem pekee ilioajiri watoto wengi wa vigogo.
  (3) BOT hiyohiyo inakabiliwa na shutuma kubwa na ya aibu
  (4) Mishahara ya BOT ni mikubwa kuliko idara yoyote ya serikali kwa mujibu wa takwimu za ERB

  Sisi vijana nchi yetu tukufu iko mikononi mwetu, kama na sisi tunakua WANAFIKI,MAKUADI na VIFUATA-UPEPO kama kina soso na sango, ipo siku wote tutaikimbia nchi yetu maana itakua ni “MAPIGANO KATI YA WATOTO wa vigogo na WATOTO NA MASIKINI”

  Naomba tujaribu kumfikilia na kijana mwenzetu alieko kijijini na sio sisi tu, Hali kama hii itatuletea matatizo sisi wenyewe vijana.

  Mwisho kutokana na ufinyu wa busara waliouonyesha “soso na sango” ninawasemehe katika jina la “NYERERE” la sivyo ningewatukana tusi ambalo linge-zidhuru familia zenu.

  “”Vijana ni Jembe kali lililoelekezwa ktk udongo Mfinyanzi” (Mao Tse Tung)

 31. Renee Says:

  Well, well, well! Tutamkumbuka Mzee Mkapa!
  Wakati wa kampeni na hata uchaguzi niliwaonya vijana wengi kuwa mtu huyu hatufai, sasa matokeo mmeyaona, bado mtampa kura kuwa raisi wenu kipindi kijacho? He doesn’t have to be there for ten years you know!

  I cry for my country and the future for my children/grand children!!

 32. Renee Says:

  By the way, afande JK anatakiwa apunguze uzito, hii kula kitimoto ugenini na kusahau kufanya mazoezi zi halali kwa afande wa nchi<<>>>

 33. Shwain Says:

  kazi ipo apo akiyanani,Jamani kumbe wa tz mpo makini naona mmeshaanza kuwatabili atakaye mrithi Balali,Ila mwenye nacho asiongezewe bali asiyenacho apewe,Nafasi ichukuliwe na mwinge kabisa tofauti nawaowafikilia.Ni hayo tu.

 34. Upendo Furaha Says:

  Ndugu zangu nimesoma maoni yenu kwa umakini kabisa. Ninachoomba mkumbuke kuwa hata mmoja wenu angekuwepo ikulu (Rais), ingekuwa anayofanya JK ni nafuu 100%. Ndugu zangu Watanzania tukumbuke: Nyerere alipoacha madaraka 1985, miaka 2 baadaye wananchi walimkumbuka. Mzee Ruksa alipomaliza muda wake 1995, miaka 2 baadaye Wananchi walimkumbuka. Vivyo hivyo Mzee Mkapa amemaliza muda wake 2005; mnajifanya eti mnamkumbuka na mwaka jana tu wakati Kasi mpya inapamba moto mlikuwa mnamtukana.
  Kuna wimbo mmoja unaimba hivi: “Ee Jamani, Mwanadamu hatosheki hata ukimpa nini Milele hataridhika”
  Raisi wetu Jakaya Mrisho Kikwete ni “Supa” na Tunamuombea Mungu ampe maisha atawale hadi 2015.

 35. soso Says:

  sawa bwana eagle, hapo umeongea naona sasa umeweka na wewe cv yako, kwa nini ujirudishe nyuma namna ivyo, tafuta na wewe jinsi yako utakavyochangia katika nchi, weka mambo yako kwanza, sasa ndio hapo tuhoji kwa nini, wapewe nafasi watu wengine, ndio hapo sasa, una kazi gani na ewe mwenzetu, jina lako na wewe peleka panapohusika, sio majina ya watu wamekusaidia nini hao jamani, merry x-mas.

 36. Matty Says:

  Jamani naona bora nchi iuzwe ili tugawane mshko au mnasemaje?? te te te……2 years !!!!!!maana tunakoelekea ni —– badala ya +++ samahani nina maswali mengi siyaelewi vizuri naomba mnisaidie.
  -kwani huyu boss mshauri wake ni nani??
  -anafanya kazi gani??na anaelimu gani??
  -Suala la ajira kwa vijana limefikia wapi??
  -maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi??
  -anangoja nini kuwaadabisha balali, mafisadi na wauza kete sijui flour??
  -anangoja nini kung’atuka ikulu yenye neema
  -mgogoro wa kisiasa znz umefikia wapi??

  Hayo ndo yanayonitatiza jamani ndani ya 2yrs.

 37. Desert Eagle Says:

  soso mdogo wangu, tatizo sio kupeleka jina langu linapohusika, tatizo hakuna ninaemfaham wa kunisaidia,
  mie kwa sasa ninajishughulisha na biashara ya kuchukua MAEMBE hapa Geita vijijini na kuyapeleka Mwanza mjini

  Tatizo linalonikwamisha ni soko, kodi kubwa na miundombinu mibovu. Kama Mzee wako anahusika na maamuzi ya kitaifa mwambie anisaidie mimi na jamii ya mwanza haka kabarabara ka Kamanga-geita maana huku kunakila aina ya mali na mazao

  Hao watu nilio-waanika hapo juu kama ni ndugu zako samahani sana mdogo wangu maana najua na wewe unafaidika kwa njia moja ama nyingine na ndio maana unakua mkali unaposikia sponsor wako wanatajwa hadharani.

  Kwa ufupi kutaja majina ya hao watu au hata ninapotaja lako sifaidiki na chochote, ila hapa ni mjadala tunajalibu kujenga hoja kwa vielelezo na sio kuropoka kama wewe.

  Nisiongee sana maana naweza nikakutukana na hoja yangu isitokee kwenye web yetu tukufu,

  Ndugu yangu soso kwa mara nyingine nakuomba uzingatie haya yafuatayo;
  (i) Usiwe mbinafsi kwa kuwatetea ndugu zako wanaokuweka mjini.
  (ii) Jaribu kua mzalendo japo inaonekana umesha-pandikizwa damu ya kifisadi (Ubinafsi).
  (iii) Tembelea vijijini uone vijana wangapi wanaoteseka na maisha na hakuna dalili ya kutoka kesho wala kesho kutwa
  (iv) Uliza hapo Dar mjini kuna Graduate wangapi hawana kazi na dalili za kazi hazipo
  (v) Tafuta mtu wa BOT na muulize ni wafanyakazi wangapi pale wanaingia kwa taratibu za sheria ya nchi
  (vi) Kisha muulize ni wangapi wanavigezo na wangapi hawana vigezo??? Wapo wana degree gentralmen class na kuna 1st class kibao ziko mtaani zinauza sura

  “”Soso jaribu kujenga hoja kama mtu uliefaidika na “MMEM” la sivyo watu wakikufahamu watakuchinja maana wewe unatusaliti vijana ambao tunaangalia watoto, wajukuu na vitukuu vyetu baadae wataishi vipi na sio kuuliza huko kutaja majina kumenisaidia nini”” soma hadithi za “MAKUADI” alizozisimulia marehem Chachage

 38. fukara Says:

  Yaani hii picha JK anawapungia kwamba mtajiju
  mtachukua mtaweka wa 2010

 39. mwalimuzawadi Says:

  Desert Eagle, na wengine wenye nia ya kweli ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa vitendo

  Naomba kukukumbusha, Tanzania ni kama msafara wa mamba, na kenge wamo. Utawaona kwa maneno na tabia zao. Wengi wao wawajui tofauti ya kutoa hoja na kulalamika. Wengine wamezoea kucheza na akili za watu (kama wanavyofanya ndugu zao watawala wa sasa)

  Ila nafarijika na kuaamini hutachoka kuwaambia ukweli

 40. fukara Says:

  Tumeona ya kenya sasa yanakuja tanzania
  MAGEUZI

 41. Mama wa Kichagga Says:

  Ndugu zangu samahanini maana sijaona kitu cha kuchangia hapa! JAMANI NARUDIA FIKRA ZETU ZIMEKAA KUSHABIKIA CHUKI NA HUKUMU KWA WENZETU TU.

  Naomba msaada kwenye tuta: HEBU TUJIULIZE:

  1. Hivi hapa tunachangia nini? maana hata mada yenyewe haijatulia au tunachangia picha ya RAIS akipunga mkono wa X-mass?

  2. Nanukuhu mada “Miaka miwili, unasemaje? X-mass njema: Miaka miwili ya nini? Kama ni miaka miwili ya utendaji wa Rais ripoti tumeipitia au tumeiona? au baada ya kuona picha ya Rais akipunga mkono basi tukaanza kububujika kama maji ya chemchem ili mradi kila mtu anatoa mada yake ndogo ndani ya mada?

  3. Kazi tunayo kwelikweli! FIKRA FIKRA tuwe waangalifu wajameni. Hivi IP address yako ikachukuliwa ukafolenishwa kuwasilisha hii hoja yako uliyoileta hapa utakuwa na nguvu angalau ya kukumbuka sentensi moja? Au unajidai unatumia cafe hutajulikana? Usijidanganye kwa fikra zako finyu maana kama hoja yako ni potofu kiasi cha kuleta tabu mwenye cafe akikamatwa na wewe unalo maana na wao wako katika biashara sidhani kama atakuruhusu utumie kifaa chake bila kuchukua tahadhari ya picha yako bila wewe kujua (In-Built computer webcam). Hivyo nakusihi ndugu yangu changia hoja zisizo za matusi na zenye kuijenga nchi na zenye ukweli ili siku kikikuwakia upate pa kujishikilia, EPUKA KUKURUPUKA KWA KUSIKIA HADITHI ZA VIJIWENI ZISIZO NA TAKWIMU KWANI UTAUMBUKA. Ni hayo tuu kwa wale wasiofahamu technolojia hii ya mawasiliano.

 42. Desert Eagle Says:

  Mama wa Kichaga kwa mara ingine ninakusamehe maana umeonyesha ni jinsi gani ulivyo mtumwa wa “UBINAFSI” na ndio maana kila hoja inayowekwa hewani inayohusu wa-TZ wengi unakua mkali sana,

  Anyway jaribu kua unafikila na kuchambua mambo kwa upana na sio kukurupuka na kusema hujaona cha kuchangia, then unachangia

  Kama ungekua unabusara zaidi ya wana BC basi usingeandika chochote na kukaa kimya kwa sababu hujaona point ya kuchangia na ukatafuta maada inayoendana na busara zako ukatoa mchango wako, hapo ninge kupa grade ila kwa sasa Mama wa Kichaga umejichukulia Aibu na kuivaa kama nguo ya ndani,

  Hizo unazoziita hadith za vijiweni ndio ukweli wenyewe wa mambo kwa taarifa yako maana taarifa za kitaalamu huwa zimejaa uongo, kwa mfano kashfa za BOT zinawataja watu flani ndio wahusika lakini wananchi wote (vijiweni) wanafaham ni kina nani na lini walihusika na Ubadhilifu,

  Jaribu kutoa mchango wako kwa utashi na hekima ya juu zaidi kama jina lako lilivyo (Mama) la cvyo utakua unadhalilisha wengi bila wewe kuona.

  Mwisho nakuomba kwa niaba ya wote ambao tumechangia hapo awali ututake radhi kwa kutukashfu kwamba “tunachangia picha ya RAIS akipunga mkono wa X-mass?”” Tafadhari sana tumia Hekima, umri na jinsia yako wakati unataka kutoa mchango

 43. Mama wa Kichagga Says:

  Pole wee mwewe wa jangwani (D Eagle).

  Nakuambia hili jina LANGU na kabila lenyewe ni lilelile linatakutoa roho! Naona usiponiona kwenye maoni basi roho yako haitulii maana hupati wa kupambana nae haya nimekuja sema yote hapa!

  Nakushukuru umejileta mwenyewe maana hoja yako ndo iliyonikera zaidi ya zote maana nikizijumlisha zote ulizowahi kuchangia hayo majibu yangu hapo juu yanakushabihia vilivyo!

  Pole kaka kukunwa kutamu ati, umeguswa kidogo tuu umechemka kama maji ya ugali hahahaaaaa sasa hio Mao yako utaiongozaje? Labda uongoze wanyama wakuogope kama kuliko Simba aogopwavyo na wanyama wengini.

  UNGEKUWA UMEELIMIKA WEWE UNGEANGALIA PROBABILITY YA KUINGIA IKULU ILIVYO NDOGO KABLA YA KUWAKASHIFU WENZIO
  Sasa rudi kwenye hoja yako ya awali katika mada hii uniambia itamuondoaje mwananche wa kawaida kwenye umaskini?

  NI IMANI YANGU KUWA MWAKA 2008 UTALETA HAPA HOJA NA MICHANGO YA KIMAENDELEO NA SIO HUU UPUUZI WA VIJISERA NA VIJIMIKAKATI VYAKO VISIVYO NA MWELEKEO. KAMA WEWE KIDUME CHA MBEGU KWELI WEKA ANWANI YAKO WAZI NA MIKAKATI YAKO HAPA TUICHAMBUE KWA HOJA BILA MATUKANO WALA KUFANYA HUO U-MAO-TSE ULIOKO KATIKA SERA ZAKO.

  Kwa vyovyote vile hii ilikuwa kama mada chokozi tuu ili kuweza kutambua fikra za watu mbalimbali na upeo wao katika kuona mambo.

  Wenye akili zao timamu utawagundua hapo juu kwa hoja zao, ziwe ni kuhusu nukuhu husika ama mkono wa rais.

  Bahati mbaya sana kuna mijitu mingine sijui ikoje ikiona mafanikio ya wenzao haiachi kutafuta sababu na kukosoa kila kukicha imekuwa ndio kazi yao na wanaendelea kuwa maskini siku hadi siku. HIVI WEWE KWANINI UONE WENZIO KILA SIKU WANAKOSEA TOKA AWAMU HII HADI AWAMU YA NNE” WEWE UMESHAFANYANINI KWANZA TUKICHAMBUE HAPA”

 44. amina Says:

  aahh tumechoka bwana bora nchi iwe kama somalia kila mtu aiongoze familia yake

 45. Mama wa Kichagga Says:

  BC kheri ya mwaka mpya 2008.

  2008 uwe wa mafanikio na maendeleo, sina mengi kwa leo ngoja niupokee mwaka kwanza kwa kusikiliza hotuba ya Rais kwenye TV.

  Tusameheane kila mmoja wetu hasa pale ambapo mtu aliguswa hisia zake visivyo hasa viongozi wetu na ndugu yangu Mwewe wa Jangwani

 46. kijiwe Says:

  Heri ya mwaka mpya wadau wa BC.
  jamani jamani watanzania tuache please mambo ya kugombana humu ndani.
  kuna kitu inabidi tuelewe wazi kuhusu hizi nchi zetu za kiafrika.
  kuna vitu vinaitwa systems katika dunia hii na most of the african countries(tanzania in particular) tume adopt kutoka kwa wamarekani.
  system hizi hizi(tofauti kidogo maana kulikuwa na less corruption na wizi) zilikuwepo kabla hata ya mwalimu kung’atuka.
  ubaya sasa ni kwamba sasa hivi inakuwa worse sababu kuna a lot of resources zinaflow out of TZ na kuna mijitu kibao ipo katika channel.
  unajua kama tungedhibiti hizi resources kabla mambo hayajaharikibika i mean tungekuwa na stable system ya kucontrol hizi resources wala hakungekuwa na matatizo ya kuchagua reis yupi au kufanya nini maana majority wangekuwa na say i mean not chama tawala wala some few individuals like the way it is sasa hivi.
  mfano mzuri ni botswana.i stayed there for a couple of years hawa jamaa wana chama kimoja kimetawala tangu uhuru wao miaka ya 60 which is almost like sisi na ccm yetu ila difference yao ni moja.resources zao(diamonds in pariclular)zinakuwa controlled na a specific board in conjuction na botswana defence force.yaani jiwe likitoka shimoni hata liwe dogo vipi linaposafirishwa kutoka machimboni linasindikizwa na kifaru na mitutu kibao pamoja na helikopta angani inacheki pia.
  sasa these guys they know that this is the shit which is giving us loot kwa hiyo lazima tuwe na system ya uhakika.
  nakuambia mpaka tunapoongea sasa hivi kila generation inayukuja botswana inajua kuwa chama cha BDP(chama tawala ndiyo chama poa)sababu ya uchumi umekuwa stable for years.
  i mean really kama tungekuwa na the way ya kucontrol resources zetu walahi kusingekuwa na uvasco dagama
  i mean in botswana rais hawezi kusafiri kijinga jinga namna ile bila kujibu bungeni ni kwa nini anasafiri hivyo.
  eti anaenda kutangaza mkutano wa nini suvillian?jamani hiyo si kazi ya waziri wa utalii au mambo ya nje au hata mkurugenzi wa bodi ya utalii.mbona huyu jamaa anajifanya multi tasking wakati kuna watu kibao wenye uwezo wa kufanya mambo kibao?
  am so sorry wadau kwa hii barua ndefu nimepitiwa kidogo kwa hiyo msikonde!
  togather TUNAWAKILISHA!

 47. sino Says:

  jk, tanzania inakupenda ila umeanza uongozi wako kwa speed sana, baadhi ya viongozi wako, hawatendi kazi, wanajinufaisha kivyao kuwa makini sana na watu wako wa karibu.

 48. Mama wa Kichagga Says:

  Mimi sina chuki, sina kinyongo sijui wewe jirani yangu?

  Kwa mawazo yangu na ninavyoamini kama ningechangia mkono wa Rais kupunga kheri ya X-mass basi ningesema hivi: Mkono kaupunga kwa furaha na unaleta matumaini na hamasa, sio mchezo kupungiwa na Rais ati achilia mbali kupiga naye picha!

  Kama ningengeamua kuchangia miaka miwili ya Rais JK madarakani ningechangia hivi:

  A. Kwanza kama nilivyoongea mwanzo mada hii ni tata na hakuna taarifa ya kutosha kuichambua – hakuna ripoti ya utendaji iliyowekwa hapa ama sijaiona ili niweze kutoa uchambuzi fasaha na wa kuijenga nji yangu.

  B. Kwa maana hiyo hapo juu (A) nitaamua kuchukua hotuba ya mwanzo kabisa ya Rais wakati alipofungua Bunge kwa mara ya kwanza kama kielelezo cha mchango wangu hapa maana mimi naamini hoja yenye nguvu ni ile inayoambatana na taarifa/takwimu sahihi na sio chuki, majungu, tamaa dini, kabila wala ushabiki wa mtandaoni ambao hautanijenga mimi, wewe wala Mtanzania mwenzangu!

  – Ripoti kamili/hotuba soma hapa

  http://www.jakayakikwete.com/tanzania/articles/38/10/Hotuba-ya-Rais-wa-Jamhuri-ya-Muungano-wa-Tanzania/Page10.html

  Sasa nachangia Hoja kamili kwa kigezo cha hotuba husika:

  1. Kwa mtizamo wangu ni mapema mno kusema Rais kashindwa kutekeleza sera zake maana mikakati yake ya utekelezaji iko katika kipindi cha miaka mitano

  2. Ktk mipango mikakati ya Rais (ukurasa wa 10 – 13 ambayo ipo 10).

  – Mkakati Na. 7 ni muhimu sana na ndio unaomfanya Rais na office yake kuwa na safari nyingi za ndani na nje ya nchi ktk kuutekeleza mpango huu – Sioni kama ni sahihi mtu kukurupuka na kuanza kumbatiza jina Rais wako “VASCO DA GAMA” Kwani kapanda mashua kwenda ng’ambo? Jamani someni habari mbali mbali na tovuti ili kupata habari wacheni ujinga na kujilundikia chuki eeeeeeee Mangi oooooooo Rais ooooo sijui nani mwisho utadai hata kivuli chako kinakufuata fuata kila uendapo bila kutafakari kikiondoka na wewe duniani haupo!

  3. Mkakati namba 1, 2, 4, 5, 6, 7, 9, na 10 Rais na uongozi mzima wamefanikiwa kwa asilimia kubwa sana kama sio 97% basi 95% tena kwa muda mfupi – tusubiri taarifa kamili (labda itakuwa na confidence interval ya +&- 10)

  4. Ukija kwenye mkakati namba 3 na 8 utagundua kuwa bado hapa panahitajika kazi kubwa kwani hii ndio sehemu inayogusa mwananchi mmoja mmoja na ni sehemu mtambuka (Cross-cutting section). Mikakati hii miwili inahitaji marekebisho ya makubwa ktk sekta nyingine ili ufanisi uweze kuonekana kwa mtu wa kawaida ama “maisha bora kwa kila Mtanzania” mfano:

  Inahitaji
  a) Kuwepo na miundo mbinu bora na endelevu (Barabara, umeme, mawasiliano, nk)
  b) Kukua kwa pato jumla la uchumi la taifa (viwanda, kilimo, nk)
  c) Kukua kwa shughuli za kilimo (chakula na kusafirisha nje)
  d) Kuwepo madaktari na wataalamu wa kutosha wa sekta ya afya na kuwepo na vitendea kazi vya kutosha (hospitali, zahanati, maabara za kisasa nk)
  e) Kuwepo kwa mashule ya kutosha, walimu na vitendea kazi

  Niruhusuni ninukuhu namba 3 na 8 hapa kama zilivyo kwenye hotuba:

  – (3) Kuondoa Umaskini, Ujinga na maradhi
  – (8) Kujali masilahi na mahitaji ya makundi maalumu katika jamii (wanawake, vijana, watoto, wazee, walemavu na yatima)

  NB: Mkakati namba 8 umeshafanyiwa kazi ila bado uhamasishaji na mipango mikakati mingi inahitajika katika kutekeleza mkakati huu ambao ndio wewe na mimi tutakapoona tumegushwa moja kwa moja.

  SASA NDUGU YANGU UNAPOMUHUKUMU MWENZIO HAJAFANYA KITU, UNATAKA HADI MTU ATOKE KUZIMU AKUAMBIE USOME TAARIFA ZA SERIKALI NDIO UAMINI KAZI INATENDEKA?

  KASI UNAYOITAKA NI SAWA ILA SIO RAHISI KAMA UNAVYOFIKIRI KTK UPEO WAKO

  MIMI NINA IMANI KUBWA YA MAFANIKIO YETU ILA TUMPE RAIS MUDA ALIOPANGA NDIPO TUMUULIZE KAFANYA NINI NA KWA VIPI KATUGUSA.

  ISIPOKUWA: WALE WABOVU MIMI NAITA VIBUYU, VIRAKA WANAOMWARIBIA UTEKELEZAJI WAKE INABIDI AWATAMBUE HARAKA SANA NA AWAPANGUE HARAKA KAMA KUPEPERUSHA KARATASI YA TIARA VILE KAMA ANATAKA KUBADILI HISTORIA NA HALI YA MAISHA YA MTANZANIA

  Hasa wala rushwa na wapokeaji mimi siwapendi kabisa maana hao ndio wanaoturudisha nyuma. Binafsi namshukuru Mungu katika umri huu nilionao 42+ sijawahi kupokea, kuomba wala kutoa rusha na ndio maana ninauchungu na hawa wezi wakubwa wa nchi yetu!

 49. TK Says:

  Nampenda!… Na wala siogopi kusema!

 50. niko Says:

  kwa wkeli kikwete ashughulikie hao watoto waliowekwa bot, maana watoto wengi tu wanahitaji ajira, waliosoma, ni vizuri kikwete afwatilie kwa makini sana, maoni ya watu wa bot, kwani ni benki ya taifa zima hiyo.

 51. Mama wa Kichagga Says:

  Niko,

  Nimependa ulivyoitoa hoja yako, muungwana ataelewa na wahusika wakiiona sidhani kama watasita kuifanyia kazi.

  KICHWA YAKO IMETULIA NDUGU HUPAYUKI NA ASANTE SANA NIMEKUKUBALI

 52. sabuni Says:

  KAMA MIAKA 2 HAITOSHI KUMCHAMBUA JK, ULITAKA IWE MINGAPI, 10? USICHEKESHE UMATI.

 53. MPILI Says:

  KAKA WENGI TULIJUA TOKA KIPINDI KILE CHA MWANZO ULIPOTAKA KUWANAFUU WATANZANIA LAKINI NAFASI AKACHUKUA ALIE ONDOKA SASA TUNJIONEA WENYEWE NILKUWA HAPO NYUMBANI MUNGU AKUZIDISHIE AKUPE MWANGA WA KUWANYAMBUA KABLA HAWAJAKUPA KAZI NGUMU KWANI WACHACHE NDIO WANAOKUANGUSHA LAKINI MUNGU BABA ALIE MBINGUNI YU USIKU NAMCHANA KUKUSAIDA KWANI HATA SIKIA KILIO CHETU.HAKIKA MDA NI MDOGO LAKINI WATANZANIA WENYE IMANI TUTAKUPA MUDA ZAIDI
  Na Mpili


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s