BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

SUMU YA TEJA,HAPPY BOXING DAY December, 26, 2007

Filed under: Burudani,Muziki,Sanaa/Maonyesho — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Kama wewe ni mpenzi wa muziki wenye ujumbe mkali huku ukisindikizwa na mirindimo yenye kuleta burudani muafaka,basi kwa Vitali Maembe(pichani) utakuwa umefika. Wengi tunamfahamu kama Sumu ya Teja jina ambalo sio lake bali la wimbo wake maarufu uliompa umaarufu. Vitali ambaye pia ni mchoraji mzuri ni matunda ya Chuo Cha Sanaa Bagamoyo. Unaweza kusikia nyimbo zake ukiwemo Sumu ya Teja kwa kubonyeza hapa.

Wakati huo huo BC inawatakia Happy Boxing Day.

Picha kwa hisani ya Mroki

Advertisements
 

6 Responses to “SUMU YA TEJA,HAPPY BOXING DAY”

 1. kiso Says:

  asante kaka mungu akubariki maishani, nasikiliza wimbo wako.

 2. Ana Says:

  Maembe hongera sana.
  Jamani nje ya topic kidogo.

  MICHUZI USITUMINYIE 2008 VINGINEVYO TUTAHAMA !

  Kama kawa Issa Michuzi amechemsha huko kwenye blogu yake mpaka akatupiwa taulo eti alidhani Boxing Day inahusiana na masumbwi akakurupuka na kuandika habari za Japhet ambaye ubingwa wake wa Dunia haupo popote katika rekodi za dunia. Tunamuelewa sana Michuzi anapotumia tungo kama mai hasband wako na majina kama ukerewe, A-town, n.k Lakini kwa hili si utani wala hasijifanye kuwa alikuwa anachekesha maana huwezi kuweka post nzima na picha ya watu kwa utani. Michuzi Jr mtupie taulo huko ndugu yetu kwenye hii link:
  http://issamichuzi.blogspot.com/2007/12/boxing-dei.html#comments
  La pili ni kuwa Michuzi (senior) ambaye ndiye huwa anamtumia taarifa zote Mzee Mwanakijiji wa USA (Mpelelezi) ana utofauti mkubwa sana na Michuzi (Junior) ndio maana wengine tumeamua kuhamia huku kuliko kwenye blogu yake ambayo ana amua bila sababu kuzuia comments za watu na wakati hujaandika matuzsi yeyote kama nilivyoandika sasa.
  Michuzi (senior) inabidi ukue kiuandishi, hoja zijibiwe kwa hoja na siyo kumminyia mtu comments zake. Hapa sina haja ya kuomba eti haya niliyoyaandika yawekwe ni dhahiri yanawekwa maana ni kwa ajili ya kuboresha namna ya kuhabarisha watu na pia sijaandika tusi lolote.
  Kama nimeongea vibaya naomba msamaha na nisahihishwe hapa hapa.
  N.B nendeni jambo forums muone jinsi ambavyo huyo mzee Mwanakijiji pamoja na mazuri yake mengi amejikweza kiasi mpaka anaonekana kuwa yeye ndiye chanzo cha habari zoooote na kwamba yeye hasahihishwi na pia kuwa anajua kila kitu cha fani zote ulimwenguni kuanzia uvuvi wa dagaa mwanza hadi ubunge hadi thesis defence hadi mapenzi ya mfano hadi hard science fiction! Hadi Leo yeye anajiita mpinzani wa kweli lakini utambulisho wake haujulikani na kuna mtu aliandika hapa mambo yake lakini yeye akatetewa kuwa hana haja ya kujibu wakati motto yake at KLH News ni kuwa kila kitu kinazungumzika na hoja hujibiwa kwa hoja.
  Mimi napenda kusoma na kujifunza mambo ambayo wengine huandika lakini sipendi mtu anapojinyanyua mpaka karibu kujivika uungu mdogo katika fani ya uandishi.

  Samahani kwa kuwapotezea muda wakati wa siku ya kupeana zawadi.

 3. Edwin Ndaki Says:

  Hakika huyu bwana namkubali ni msanii mzuri sana.

  Tukiacha hayo samahani msaada kwenye tuta.

  HIVI NINI MAANA YA BOXING DAY.

  Nisaidieni wajameni maana wengine tulisha jizoelea kudandia tu sherehe kwa sababu ya utandawazi.

  Boksing ya kupigana mangumi yaani nakozi.

  Au boksingi kwa wale tunaobeba MABOKSI huku mitaa ya kati.

  Au boksi lile la barua.

  Pia ni sherehe ya kidini au historia yake ikoje.

  Ni mimi mwenzenu mvivu wa kufikiri.Nawatakieni siku njema haijalishi ni boksi au vumbi day.

 4. Tarimo Mkurugenzi Says:

  Edwin Ndaki,
  Maana ya Boxing Day unaweza kuipata hapa http://en.wikipedia.org/wiki/Boxing_Day. Furahia

 5. Nathan Says:

  Ebwana mimi naunga mkono hayo yote ya wadau kuwa msanii huyu Maembe ni mkali sema tu mimi huwa nashangaa nasikia anasoma pale chuo cha Sanaa Bagamoyo lakini huwa hamalizi kwa kufeli sijui ni kweli hili au tunadanganwa.
  Ila tuache utani mimi nampa Big Up sana kwa mwaka huu jamaa anae jiita Father Kidevu wa http://www.blog.co.tz/mrocky news zake za uhakika na anaimudu kazi kwa blog za kibongo toka bongo huyu amewin.
  Thanks

 6. DUNDA GALDEN Says:

  oya maembe funika wote hapa tumeukubali ujumbe lakini wapi bint Malingo?mpe Hi RAS TUNTENGE pia na Mpili pia Maco Sawe wa B.S.A
  CHAI GODA NEVER DIE


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s