BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JOHN POMBE MAGUFULI December, 29, 2007

Filed under: Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:10 AM

Ukiongelea viongozi wa kiserikali nchini Tanzania,hususani kutoka kwenye Baraza la Mawaziri, ambao wamewahi kutokea kupendwa sana na wananchi,huwezi kumuacha nje Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Pombe Magufuli(pichani). Unajua kwanini anapendwa?

Picha ya UN-HABITAT/World Urban Forum

 

12 Responses to “JOHN POMBE MAGUFULI”

  1. John. Says:

    He is agreat guy but sometime Mnafiki.Hata kasi yake si kama ile aliyokuwa nayo wakati wa awamu ya Tatu.Inaonekana alikuwa anafanya kazi kwa sifa au kwa malengo fulani sasa ameona malengo yake yametimia au hayajatimia na hayawezi tena kutimia ndio maana anafanya kazi kwa spidi ya konokono sio kama alivyokuwa awamu ya Tatu-He worked hard sijaona bado cheche zake.

    John.

  2. mama koku Says:

    Ni mchapa kazi na hapendi wazembe, ila sijui kwanini sikuhizi kwenye hii wizara ya Ardhi amekua mpole ghafla, inawezekana vigogo wengi ndo waliogawa viwanja vya watoto vya michezo na open space, labda anashindwa aanzie wapi, lakini bro tunakufagilia sana, najua ungekua kule kule (wizara ya miundo mbinu zamani ujenzi) hii barabara ya sam nujoma ingekua imeshakwisha siku nyingi, bora JK akurudishe kwenye wizara yako, may God bless you big times, happy new year

  3. mama koku Says:

    big up bro….. wewe ni kijana wa kazi, mungu akubariki kwa mwaka huu tunaokwenda kuanza hivi karibuni

  4. mkata issue Says:

    risiki tekingi Lidaz ar fyu; zis iz wani ovu zemu!

  5. Joachim Says:

    Hamna kitu! Mbabaishaji sana. Tatizo la sisi wabongo huwa tunapenda sana kushabikia mtu anayeropokaropoka hovyo! Mfano kama alivyokuwa mzee wa Kiraracha, Mrema. Watu walimpenda sana lakini kume hakuwa na chochote. Ndo Magufuri alivyo.
    Subiri uone atakavyoishia kisiasa. Atakwisha sasa hivi.

  6. Desert Eagle Says:

    Ebwana hata mie naungana na wadau hapo juu kwa kutoa sifa zake zinazomfanya apendwe na watu
    (i) Anajua porojo (propaganda) ambayo ni moja ya sifa muhim ya mwanasiasa yeyote mzuri
    (ii) Ni mchapa kazi mzuri anaesimamia upande wa sheria
    (iii) mara nyingi amejitoa kwa masirahi ya wengi kwa mfano viwanja vya kule mbezi vilivyokua vinashikiliwa na wachache, uwanja wa Nyamagana bado ameshikilia msimamo na viwanja vingi vya wazi kavinusuru kutoka mikononi mwa wabinafsi wa nji hii

    BUT, ktk serikali hii makucha yake hayapo tena nadhani nikwa sababu yeye na Da Gama waliwahi kupingana ktk mambo flani wakati wa Mkapa na vilevile yeye hakua mwana-network kwa hiyo hana kauli ktk serikali hii kama ilivokua kwa BWM,

    Otherwise, the guy is good na kila siku hua nasema NYERERE angekuwepo nadhani huyu ndie angekua chaguo lake maana alipenda wenye sifa kama zake

  7. TanzanianDream Says:

    Kila mtu anakosea so was him(kwenye nyumba za serikali)…Ila besides he’s one guy anaejitahidi kuwa responsible zaidi jamii…
    Yupo wizara ambayo inamfanya awe kimya kwahiyo kumskia ni accordingly lkn bado kama unafatilia utajua kama anawajibika au hawajibiki…..

    Otherwise i think he would make a Good PM anywhere in the 3rd world countries…..n’ may be in further levels………

    “Tanzania wenyewe tunaweza sema wachache wanatuharibia”

  8. Upendo Furaha Says:

    Ni Mchapakazi.
    Wizara ya Ardhi ni ngumu sana (naweza kusema kuliko wizara zote). Hivyo basi, Hata JK alipompeleka huko anajua kuwa ni yeye pekee atakayeweza kuondoa uozo ulioko kwenye wizara hiyo kama livyofanya kwenye wizara ya kazi wakati ule.
    Ninampongeza sana na Mungu azidi kumpa hekima na maarifa ya kuongoza.

  9. matty Says:

    Huyu kiumbe anajitaidi sana data za barabara wakati ule zilikuwa kichwani, hapo alipowekwa mhhhhh ni pagumu jamani mfano watu wanauza viwanja mara 3,4,,5 kila siku kwa watu tofauti na matajiri wananyang’anya masikini ardhi zao panahitaji ufumbuzi si wamtu mmoja kwenye sekta yake ukizingatia kesi zinazoongoza ni za ardhi nadhani kazi kubwa anayo.
    Mungu akubariki ulitakiwa uwe PM lakini jamaa akampa classmate wake…usijali akiingia Mrema Ikulu yenye neema nawewe utapata UPM, ili nasisi wa kina matty tuwe masecretary wako.

  10. mama koku Says:

    nina wasiwasi na mchangia hoja ‘joachim’ nahisi sio mtanzania, kama unamuhita huyu muheshimiwa mbabaishaji na wale wanaozunguka tanzania na mawaziri kumi kwenye ndege kisa waende kujibu hoja za wananchi huko vijijini utawahitaje? sasa huyu baba ameingia wizara ya ardhi huwezi kuamini, ukienda unahudumiwa kwa muda mfupi mpaka unashangaa, hakuna tena mambo ya njoo kesho na wale watu waliokua wanajaa kila siku wameisha kumbe wale ndo walikua wanashirikiana na wafanyakazi kuuza viwanja mara nane nane, kwani ukimpa sifa john pombe magufuri utatoka ngozi? BIG UP JOHN POMBE MAGUFULI, MIE NAKUFAGILIA SANA

  11. Reg Miserere Says:

    Kaka Pombe kazi anaiweza…. sema sio binadamu wote wana ridhika na kazi ya mtu.

    Mama Koku, nadhani Joachim ana lake ….

    Big up mwalimu Pombe… wanafunzi wako wanakukumbuka sengerema wanatamani urudi ukafanye kazi…

  12. Kay Says:

    Jamni hivi mnakumbuka kwamba Magufuli amejaribiwa kupigwa ndumba mara kadhaa. Kasi hajapunguza kwa kupenda – amelazamika. Hivi mnadhani yeye hayapendi maisha yake jamani. Kwa hiyo tusimlaani sana. Tumuonee huruma.


Leave a comment