BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 16 December, 30, 2007

Filed under: Photography/Picha,Serikali/Uongozi,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:20 AM

 

Kila mwaka hutokea picha moja ikatokea kupendwa,kuzusha gumzo,kusababisha tafakari mbalimbali nk. Kwa mwaka huu,picha unayoiona hapo juu inaweza kabisa kuwa miongoni mwa picha za namna hiyo.

Picha hii ambayo inawaonyesha baadhi ya viongozi wakiwa ‘off guard” ilipigwa na Mroki Mroki wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya Mapinduzi Zanzibar tarehe 12 Januari mwaka huu. Hii ndio picha yetu ya wiki hii.

Picha kwa hisani ya Mroki

Advertisements
 

7 Responses to “PICHA YA WIKI # 16”

 1. Upendo Furaha Says:

  Duh! walikuwa wemechoka sana.
  Inaonyesha Hotuma iliyokuwa ikitolewa na Mheshimiwa mmojawapo ilikuwa ya muda mrefu sana.
  Nawapa pole, maana maisha ya binadamu hayakamiliki bila usingizi.

 2. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  Wakati mjadala mkubwa ulielekea kuonyesha UZEMBE WA WANAUSALAMA KUTOKUWA MACHO; mimi bado pia nachangia upande wa pili na wa tatu wa shilingi kwamba:-

  1. Picha inatuonyesha kuwa sote hata askari au kiongozi wa ngazi ya juu tu binadamu na tunahitaji kupumzika vya kutosha. Kuna watu wengi (hata mimi) wanalala masaa machache sana mawili au matatu tu kila siku. Hiyo ni hatari kwa afya zetu na matokeo yake ndio yanaweza kuwa kama haya. Unakuta mtu anasinzia mahala kama hapa au hata kanisani au msikitiki mpaka ana’polute’ hali ya utulivu kwa kutoa ukelele kama mashine ya kutengeneza juisi.

  2. Mara nyingi sana baadhi ya wazungumzaji, wahubiri, wanaotoa hutuba na hata walimu wanaboa sana badala ya kuwafanya wasikilizaji wawe na hamu ya kuwasikiliza. Sina haja ya kuwataja walioboa au wanaoendelea kuboa lakini niwakumbushe kuwa kuna watu kama marehemu Luther King, marehemu J.K.Nyerere, marehemu Ask. Nyamko Sarya, marehemu Mwalimu wangu Elisha Nyamara wa Nyakato s/m, marehemu Okeyo- mwenyekiti wangu wa DUSA, mwalimu Bibi sabina Gheleja wa Mzumbe university, Dk. Abagi – mkereketwa wa mada ya Maendeleo na demokrasia, Bill Hybes – gwiji wa uongozi na utawala mtangazaji bibi Umlikheir (wa DW- idhaa ya kiswahili), n.k maana orodha haiishi.
  Hakika nilishuhudia / naendelea kushuhudia watu wakikataa kuondoka ukumbini au darasani au kanisani au katika makusanyiko ambapo hao watu walipokuwa wakiwasilisha ujumbe fulani. Yaani inakuwa kinyume na hiyo picha hapo juu kwamba pindi MC tu anatambulisha Mhutubu hapo unaona watu wanaamka kutoka usingizini au ndipo unaona watu wanakimbia kuchukua nafasi ili wamsikilize huyu mtu.

  Naelewa kwamba, kuwa na mvuto katika kuwasilisha hotuba ni kipaji cha kuzaliwa lakini pia kinaweza kuboreshwa!
  Ebu wahutubu muwe mnajiandaa vizuri, jalini muda mliopewa (hotuba ndeeeeefu huchanganya watu), zungumzieni kwa undani yale yaliyo katika wigo wa taranta zenu, mjitahidi kuielewa hadhira mnayoongea nayo kabla hamjatoa uhalo wa kauli (verbal diarrhoea). Zaidi ya yote kumbukeni kanuni ya muhimu ya mawasilano isemayo kuwa;
  ‘UKUBALI WA UJUMBE UNATEGEMEANA SANA NA PICHA (ILIYOJENGEKA) YA MTOA UJUMBE KWA HADHIRA YAKE JUU YA ANALOLIELEZA’.
  Hapa msisitizo ni kuwa tusiwe wanafiki; tuzungumze tunayotenda vinginevyo wasikilizaji watasinzia maana wanajua ndo porojo zako za kila siku!

  Nanye Nyakatakule Unyilisya Echalo

 3. BongoSamurai Says:

  Kazi yenu kulala tuu ndio maana hatuendelei….! Kwa staili hii hata ktk maofisi yenu nadhani huwa mnalala pia bahati mbaya ni kuwa hatuwaoni….!
  Mungu ibariki Tanzania.

 4. Kimori Says:

  Hunger?…Boredom?…Overeating?….Frustrations?…It might be one of these!….a reproach to all top bosses!

 5. wakunyumba Says:

  yaani jamani haingii akilini hata chembe, ina maana msemaji alikua mvutoless sana na hotuba yake, maana haiwezekani watu wote wauchape usingizi kiasi hicho hii aibu wajameni, duuu, balaa yaani polisi si tunasikia kazi yao kulinda usalama popote sasa hapa hata kama mtu anataka kuzuru kweli watapona hapa? jamani tuwe tunamaliza mausingizi yetu usiku, au kama ni umri basi mjiuzuru ili mpate muda wa kulala mpishe vijana wakae hapo, inakera sana.

 6. Matty Says:

  Ona wanavyokoroma!!!du viongozi wenyewe ndo wanaota kuchukua chao mapema namna hiyo!!!!!!!!hotuba inaelekea ilikuwa ndefu sana.

 7. pakamafia Says:

  mijitu mizee achieni ngazi kwa vijana.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s