BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

UCHAGUZI KENYA…KASHESHE TUPU! December, 30, 2007

Filed under: Breaking News,Developing News,Siasa — bongocelebrity @ 2:56 PM

 

Majirani zetu Kenya hivi majuzi walipiga kura za kuchagua Raisi na wabunge wa nchi yao. Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo (ECK) imemtangaza Mwai Kibaki(pichani) kuwa mshindi wa uchaguzi huo.

Hata hivyo utata mkubwa bado umegubika kuhusiana na uchaguzi huo,matokeo yake na mengineyo. Ushindi huo unapingwa vikali na aliyekuwa mgombea wa chama cha upinzani (ODM), Raila Odinga. Tayari Mwai Kibaki ameshaapishwa.

Habari hizi unaweza kuzipata kwa undani zaidi kwa kubonyeza hapa na hapa. Ukitaka kuona video mbalimbali kuhusiana na mchakato mzima wa uchaguzi huo bonyeza hapa.Kenya itaendelea kuwa salama? Tusubiri tuone.

Habari hii bado inaendelea.

Advertisements
 

23 Responses to “UCHAGUZI KENYA…KASHESHE TUPU!”

 1. PAUL LABAN Says:

  JAMANI WA AFRICA DEMOCRASIA TUTA JIFUNZA LINI?UCHAGUZI WA KENYA MIMI KWA MAONI YANGU BINAFSI UMEENDA VIZURI TENA TUME YA UCHAGUZI MWAKA HUU ILIKUWA NI NZURI WAZI NA YA HAKI SASAKWANINI WATU WAKATAE MATOKEO? HII INAONYESHA KWAMBA WA AFRICA TULIO WENGI HATUJUI DEMOCRASIA TENA KAMA TUTAENDELEA HIVI KAMWE MAENDELEO YA AFRICA YATAKUWA KITENDA WILI RAILA NA WAFUASI WAKO KWANINI MSIKUBALI MATOKEO MKAIJENGA KENYA?MNATUFUNDISHA NINI SISI KIZAZI CHA SASA?MACHAFUKO YANAYO TOKEA NCHI YOYOTE YA KIAFRICA HII YOTE NI UROHO NA TAMAA ZA MADARAKA ZA VIONGOZI WENGI WA KENYA MSIDANGANYE NA VIBARAKA WA WAZUNGU KAMA RAILA ODINGA

 2. Kyiteyi-teyi Says:

  MJALUO HAWEZI ONGOZA KENYA KATU!!

 3. Mkata Issue Says:

  HAKUNA CHA VIBARAKA HAPA.
  KABLA HUJATAPIKA HUMU, ULIZA MASHIRIKA NA VYAMA BINAFSI VYOTE VILIVYOSIMAMIA AU KUANGALIA MIENENDO YA UCHAGUZI AMBAVYO HATA AVIKUWA NA INTEREST YA NANI ASHINDE / ASHINDWE UONE WANASEMA NINI JUU YA HIYO TUME YA UCHAGUZI NA MAAMUZI YAKE.

  HATA HIVYO NI VEMA UTUMIE PIA BUSARA KUFIKIRI KWA NINI WAGOMBE WENGI TENA WALIOKUWA MAWAZIRI WA KIBAKI WALITUPWA NJE SASA NDO IWEJE KINARA WAO APENDWE???

  WAKENYA KUWENI TU WATULIVU; MSIUANE WENYEWE KWA WENYEWE WALA KUHARIBU MIUNDO MBINU YENU MAANA HILO HALITAWASAIDIA.
  NASHAURI TU KUWA MUMKATAE HUYO RAIS (KWA KURA YA KUKOSA MATUMAINI TOKA SIKU YA UCHAGUZI NA KUTANGAZWA KWAKE NA KUAPISHWA KWAKE (HARAKA HARAKA ) BILA NGUMI WALA MAPANGA NA AJENDA (BAJETI NA MISWADA) YOTE YA SERIKALI YAKE IKATALIWE HUKO BUNGENI BASI!! MPAKA KITAELEWEKA!

 4. Kimori Says:

  Judging from what I read and hear from different sources of infromation, the rigging was obviously done by ECK!

  It is quite evident that if almost 20 ministers of Kibaki were voted out there is no way Kibaki himself would have been voted in!

  If almost 100 seats in the perliament went to ODM and only around 35 to PNU there is no way PNU’s candidate would win the majority of votes!

  I think most of people were even shocked to hear that a ‘democratically elected’ president Kibaki was sworn in just a few minutes after the results were announced…this is a drama! Was he not confident of the victory?

  As Kyiteyi-teyi puts it, “MJALUO HAWEZI ONGOZA KENYA KATU!!”, it seems there is a long way to go as far as tribulism is concerned in Kenya! Stepping down in Africa needs a lot of courage even if you can’t walk, you can’t talk, you can’t write, you can’t read,…..yet swearing in with a bible or a Quran in your hand!….It seems we need some more Mugabe’s!

  Happy new year to all visitors and Editor!

 5. Ni vigumu sana kuendesha kenya ukizingatia ya kwamba wabunge wa chama cha upinzani wameongezeka maradufu

  Richard Mufumbya
  http://www.jacofoods.blogspot.com

 6. matty Says:

  Ni sawa ameshaapishwa Kibaki wakenya wakubali matokeo lakini wengi wetu tunakuwa na maswali yanayokosa majibu kwamba mara tu baada ya matokeo tayari anaapishwa hata JK MTANI WAKE WA JADI hajapewa invitation, hakuna cha kukagua gwaride wala nini au ni utawala wa MABAVU?
  Hapo hakuna democracy wala nini maana Rais anang’ang’ania Ikulu yenye neema hata kama hajashinda du kaziiiii kweli kweli je tutafika??
  Mimi siko upande wowote ila ni mtizamo wangu tu!

 7. Upendo Furaha Says:

  Wakenya: Uchaguzi umekamilika. Rais ni Emilio Mwai Kibaki.
  Tulieni, unganeni muijenge nchi yenu.
  Mungu Ibariki Kenya, Mungu Ibariki Afrika.

 8. amina Says:

  mwai kibaki kaiba kura wazi wazi yani mi nilikua nafatilia kwa karibu kabsa haya maswala mi silipendi na limke lake yanafanana kama vifaru

 9. GERVAS Says:

  CHONDE CHONDE RAILA ODINGA JE WAFURAHI KUONA WAKENYA TAKRIBAN 42 WAMESHA POTEZA MAISHA KWA SIASA ZAKO ZA TAMAA UCHONGANISHI NA KIKABILA?NI KWANINI BASI KAMA ULIKUWA NA NIA NJEMA KWA WALIO KUPIGIA KURAWASIPOTEZE MAISHA KIRAHISI TENA WASIONE MATUNDA YA SIASA ZAKO SAFI?NI LINI BASI VIONGOZI KAMA NYINYI VIBARAKA MTAKWISHA AFRICA?ONAWALIO TULETEA DEMOCRASIA KAMWE HAWAPINGI USHINDI WA WAGOMBEA WENZAO.MBONA CHAGUZI YA MAREKANI RAIS BUSH ALIKOSA UWAKILISHI KUPITIA CHAMA CHAKE TAWALA KWA KUPOTEZA KURA NYINGI LAKINI WAPINZANI HAWAKUSEMA AMEIBA KURA?NI LINI BASI TUTA ELIMIKA KUHUSU SUALA HILI?KAMWE SISI KIZAZI KIPYA HATUTA KUBALIANA NA KIONGOZI KAMA WEWE KENYA IPO NA ITAENDELEA KUDUMU

 10. BongoSamurai Says:

  Kibaki, hata kipofu ameona kuwa umeiba kura na kukimbilia ikulu.Damu ya wakenya inayomwagika itakufuata kila unapokwenda na mwisho wako utakuwa mbaya…..,nasubiri kuona mwisho wako.
  Ulionyesha tangu mwanzo kuwa haukuwa tayari kushindwa ila sauti ya wengi ni sauti yangu Mungu…,cha moto utakiona…
  Mungu wabariki wakenya wote na uwajalie moyo wa uvumilivu.

 11. kijiwe Says:

  AMINA: lol i like your comment because its funny lakini siyo fresh kusema hivyo katika kadamnasi.

 12. Ney Says:

  MWAI KIBAKI, THE SOO CALLED KENYAN PRESIDENT. SHAME ON YOU!
  MM NI MTANZANIA, NA NIMEKUWA NAFUATILIA SANA UCHAGUZI WA KENYA,

  LAKINI SASA KINACHOONEKANA NI KWAMBA, KIBAKI KAIBA KURA, NA KAWAHI KUJIAPISHA ILI AINGIE IKULU. HADI VYOMBO VYA KIMATAIFA VIMETANGAZA KUWA WAMEIBA KURA. ISITOSHE CHAMA CHAKE KINA VITI VICHACHE SANA BUNGENI KAMA 35 ONLY, ILIHALI ZAIDI YA 100 NI VYA UPINZANI.
  HIYO NI WAZI KUWA WANANCHI HAWAKIKUBALI CHAMA CHAKE NA YEYE MWENYEWE.

  YAANI INATIA AIBU SANA, KWA MTU MSOMI KAMA KIBAKI, NA UMRI WOTE HUO BADO ANAKUWA NA UROHO WA MADARAKA KIASI HIKI, NA KIASI CHA KUIKANA DEMOKRASIA.

  WANANIUZI SANA HAWA VIONGOZI WA THIRD WORLD COUNTRIES, WANAVYOPIGANIA MADARAKA, BILA KUJALI MAHITAJI YA WANANCHI. NINGEKUWA NA UWEZO NINGEWACHAPA VIBOKO VILE VYA POLISI.

  ZAMANI TULIDAI UHURU KUTOKA KWA WAKOLONI, NA KULALAMA SANA KUWA WANATUNYANYASA, LAKINI LEO SISI KWA SISI TUNAMALIZANA.

  INATIA AIBU KUJIITA RAISI ILI HALI WANANCHI HAWAKUTAKI KWA ASILIMIA KUBWA KAMA HIYO.

  NAWAOMBEA WAKENYA WAMALIZE HIZO TOFAUTI, MAANA WANANCHI WA CHINI NDIO WANAOATHIRIKA NA MAUAJI HAYO. HASA WAKINAMAMA NA WATOTO PIA VIJANA, ILI HALI WAO WAKO WANAKULA KUKU KWA MRIJA!!

  HUYU KIBAKI NI FISADI MWINGINE, SHAME ON YOU KIBAKI

  MUNGU IBARIKI AFRICA

 13. amina Says:

  kijiwe kausha basi mwanangu nilikua na hasira ndo mana nikaandika hivyo …ila we huoni ye na mkewe wanavyofanana?kwikwikwi

 14. ANNA ULOMI Says:

  MMMMHHHHHHHHHHHHHHHH KAZI KWELI KWELI.TUNAWAOMBEA AMANI NA UTULIVU

 15. nova Says:

  Tulizeni jazba mnapotoa comment !

 16. trii Says:

  hili jamaa kibaki jizi kweli aibu yani hata mtoto mdogo anajua kuwa kaiba kura.aibu sana,watu wanakufa kwa ajili yake.

 17. Mama wa Kichagga Says:

  Vita mbaya jamani? Hasa kwetu akina mama na watoto!

  Kama alivyosema mtoa mada mmoja TZ tutie maji, aina ya miundo mbinu tulionayo basi ikitokea hapa kwetu itakuwa tabu (Naomba Mungu ipite mbali).

  Hapa najiuliza maswali mengi yasiyo na majibu:

  1. Kama Kibaki kweli kaiba kura?

  Je, hii East African Community tunayoiunda na ubovu huu uliopo kwa viongozi wa juu wa nchi husika utazaa matunda?

  Jibu la karibu ni no! Kila mtu akae nyumbani kwake hadi tuhakikishe tumebadili tabia zetu mbaya za ubinafsi na kung’ang’ania madaraka! Au Jamaa anakataa matokeo anaamua kuua jamii ya watu maskini hovyo!

  Jamani si waangalie wa TZ wanavyostaafu kwa raha zao? Uganda mmmmmmmmm nk sasa hapa EAC ikiingia madarakani na kiongozi hana uzoefu na damu ya kustaafu si itakuwa hadi afe? MMMMmmmmmmmmmmmmmmmm hapa inabidi tujiandae vema kabla ya kucheka na kukubaliana.

  NB: Tusihubiri wala kushabikia vita ! NI MBAYA SANA.

  Nawaombea Mungu jirani zetu wa Kenya waweze kumaliza tofauti walizonzo.

 18. matty Says:

  Kwa mtazamo wangu.
  Huyu Kibaki anataka utawala wa mabavu na ukoloni wakati watu walishapata uhuru wao long time, jana alinimaliza kwenye taarifa ya habari alipokataa kuongea na waandishi wa habari inamaana aliogopa maswali yenye ukweli ndani yake na majibu hana.(KIBAKI iga mfano wa jk pls)
  Nadhani itamuwia ngumu sana kumuongoza punda kwenda kunywa maji wakati hana kiu, amani haipatikani kwa upanga hata siku moja.
  Enyi wakenya mjueni Mungu aliyewaumba na mtaona kuwa kuuana ni dhambi kumbwa leo watu wanakatana mapanga kama ilivyokuwa Rwanda na Burundi, siamini kama KIBAKI ni rais mwenye upendo na nchi/watu yake unless otherwise analakejambo ambalo anataka kulitimiza pale.
  Raila alipoojiwa alikubali wakae pamoja wazungumze lakini mkuu hataki kusikia huo ujinga,nway God will tell him!
  Hapo tunatakiwa nasisi watz tujifunze sana.
  Nawaombea kwa Mungu azilaze roho za marehemu wote walioaga dunia katika uchaguzi huo na mungu wape uvumilivu ndugu,jamaa na marafiki.
  MUNGU IBARIKI EAST AFRICA NA AFRICA KWA UJUMLA.

 19. mama koku Says:

  kila mtu anajua kwamba kibaki ni mwizi wa kura za wananchi wa kenya, hivi unakubali vipi kuapa uku umeshika kitabu cha mungu (biblia/msaafu) ili hali ukijua wewe ni mwezi??

  Kiama yako kibaki iko hapa hapa duniani, roho za wakenya zilitoka zote utazilipia siku yako ya hukumu ikifika, watu wameuana makanisani kwa ajili yako, inawezekana wapi mtu mzima wa miaka 76 ukawa mwizi? hainiingii akilini hata kidogo.

  Ndugu zangu wakenya, punguzeni jazba, mnachinjana wenyewe kwa wenyewe na kuchomeana nyumba wakati odinga na kibaki wanalala kwenye full kipupwe……..

  Mrudieni muumba wenu, nyinyi nyote ni ndugu kabila kitu gani? sie watanzania tunamshukuru sana baba yetu wa taifa hatuna hiana hata mmachinga alituongoza tungekua wakabila (BMW) hasingetuongoza maana kabila lake ni kati ya makabila madogo na yasiyo na maendeleo hapa tanzania.

  Mungu wabariki wakenya wote na mungu ibariki Africa Mashariki

 20. wakunyumba Says:

  jamani, kama wizi huu umepiliza kwa kweli, uzuri hata mwenyekiti wa tume ya uchaguzi alivyoulizwa kama kibaki ameshinda kasema haujui bali alishinikizwa humuoni kama kapindua tu matokeo huyo, kabla hawajanza kuua raia kwanza wangempiga mawe huyo aliyetangaza matokeo

 21. Ney Says:

  Naanza sasa kuammini usemi wa Baba yetu ya Taifa kuwa,

  “HAKUNA DHAMBI KUBWA INAYOTAFUNA VIBAYA KAMA UKABILA NA UDINI”. NA “YEYOTE ANAYEKIMBILIA IKULU TUMUOGOPE KAMA UKOMA”(J.K. Nyerere)

  Kwa kipindi kile nilikuwa bado mdogo, nilikuwa sijui Nyerere ana maana gani, sasa ndio naelewa alikuwa ana maana gani, Nyerere ni kiona mbali.

  Walianza kudharauliana kikabila siku mingi sana, wakikuyu wanajiona bora zaidi ya waluo ama makabila mengine. HAta huku ulaya, utasikia yule mluo yule mkikuyu, kwakweli huwa sipendi japo kwa wale waliokaribu yetu sana tunabishana nao mara kwa mara waache hako ka tabia. hali hiyo ya ukabila ni tofauti sana na watanzania ambao huwa tukikutana huku ugaibuni, mradi unaongea kiswahili na unatoka Tanzania mtu wala hana Muda wa kukuuliza wewe kabila gani, sana sana tu atakuuliza umetoka Tanzania sehemu gani, na mnaweza kaa miaka wala hujui kabila la mtu.

  nadhani haka ka mtindo ni kazuri, na nawaomba watanzania wenzangu kweli tusijejiingiza kwenye hali ya ukabila ama udini, na kama ipo, basi tuipinge ingali bado changa, tusiisubiri hadi ianze kututafuna.

  Swala la ukabila Kenya, halijaanza this time, ni zambi waliyoianza siku nyingi na ndio inawatafuna sasa. nasikia pia uchungu sana kuona majirani zetu wanauana kwa ajili ya UKABILA na uroho wa kuingia IKULU. nashukuru pia kuwa huwa Maraisi wetu wanatoka kwenye makabila madogo hiyo imetusaidia kuona kuwa kumbe ukabila sio ishu, na kipaji cha uongozi ni cha mtu binafsi sio kabila.

  Mwisho Naombeni sana, East Africa community, hapo ilipofika inatosha. MM sitaki nchi yangu Tanzania iungane na na nchi kama hiyo ambayo inabagua watu kikabila. Tusubiri hadi hapo watu watakapoelewa nini maana ya uongozi na kuheshimu democrasia.

  Watanzania tudumishe amani jamani, Vita ni mbaya sana kama alivyosema MAMA WA KICHAGGA hapo juu.

 22. Ed (USA) Says:

  Nikiwa mwafrica ninakereketwa sana na masuala ya nyumbani. Sijajiingiza kiundani kwenye siasa lakini nimekuwa nikisoma na kutafiti kujua wapi tunatoka, tulipo na tunakoelekea. Yaliyotokea kenya yameanza kunifunua macho kuona niliyokuwa siyaoni au kuyapuuzia huko nyuma.

  Nimekuwa na kawaida ya kupinga siasa za machafuko zinazopelekea watu kupoteza maisha na mali zao. Nimekuwa ninashindwa kuelewa nini chanzo cha machafuko kimsingi, japokuwa kumekuwepo dhana kuwa wapinzani ndio chokochoko ya mambo yote. Uchaguzi wa kenya umeanika mambo hadharani na mwenye macho unajionea wazi wazi. Haileti maana kumlaumu Odinga kwa machafuko iwapo upo ushahidi wa udanganyifu wa kura.

  Uvumi wa wizi wa kura ulitokea hata huko nyumbani Tanzania lakini hata mimi sikuamini nikajua hii ni kawaida ya bwana Mrema na jamaa zake kubwabwaja kila wanaposhindwa. Kinachonishangaza tunakiri tuna tatizo la rushwa na masuala mengine kama ujambazi na madawa ya kulevya, lakini tunakanusha kwa nguvu kubwa udanganyifu wa kura! Imefikia mpaka kusoma kwenye news media kuwa kuna hakimu kakamatwa akipokea rushwa na mengine mengi wanavyovurunda waendeshaji serikalini. Ninajiuliza, hivi iwapo tunalindana kwa masuala nyeti kama rushwa na madawa, vipi kwenye udanganyifu wa kura ambapo kunatoa mwanya wa kuendeleza kulindana?

  Maoni yangu kwa hali ya siasa ya huko nyumbani ni kuelewa kuwa watu hufikia mahali wanachoka kuvumilia uozo kwa kisingizio cha kudumisha amani. Amani ina maana gani iwapo inakingia kifua wachache na kuleta matabaka huku ikiwaonea wengine?

  Niliwahi kuangalia TV news nikiwa huku jamaa wakimhoji kiongozi mmoja wa kiafrica juu ya matatizo wanayopata wananchi wake kuishi maisha ya ukimbizi katika nchi yao. Jamaa bila kujua kuwa jamaa wanatape za video live akabisha hadharani kuwa huo ni uzushi wa wazungu na hakuna matatizo katika nchi yake. Baada ya mahojiano yale kuisha, jamaa wakaonyesha matukio live ya wananchi wanavyoteseka katika ile nchi wakati viongozi wanaishi maisha ya kujipendelea.

  Matatizo ya kenya ni fundisho kubwa kwetu watanzania na iwapo viongozi wetu watakuwa na busara wanaweza wakaepusha kama haya yanayotokea kenya.

 23. tonny Says:

  Bara la Afrika tunatia aibu katika jamii ya Kimataifa.Mtu ukishindwa katika uchaguzi mkuu kwa nini usiwe mstaarabu ukakubali matokeo kwamba wapiga kura wamechoka na wewe hufai na wameamua kuongozwa na mwengine atakaye waletea hali bora zaidi ya maisha?Na wewe uliyeshindwa bado ukaendelea na maisha yako kama kawaida badala ya kung’ang’ania madarakani kwa njia zisizo za kidemokrasia na kusababisha maafa na machafuko makubwa ya kisiasa katika nchi iliyojaa amani na upendo?Kuapishwa harakaharaka kwa Kibaki kuwa Rais wa Kenya kumethibitisha zaidi kwamba hakupata kura za kutosha kumwezesha kuwa Rais na kwamba mshindi halali wa uchaguzi huo alikuwa Mheshimiwa Raila Omollo Jaramogi Odinga,upende usipende huo ndiyo ukweli wenyewe ndugu zangu wa Kenya!Kigugumizi cha Tume ya Uchaguzi Kenya ,ECK, kimeletwa na nini iwapo Kibaki alishinda kihalali?Kumbuka Mawaziri wengi wa Kibaki walidondoshwa kwenye uchaguzi,chama cha Kibaki kiliishia kupata theluthi moja ya wabunge walioshinda uchaguzi kupitia chama cha Raila,spika wa bunge na naibu wake katoka chama cha Raila,huyo wa kumchagua Kibaki ampite kiongozi wa ODM walioipitisha kwa wabunge wengi zaidi atatoka wapi?Jamani hebu tutumie hata common sense tu,hilo litawezekana?Wasiwasi wa nini kwa mafisadi wa Kenya?Raila hatalipiza kisasi,kwasababu keshajifunza tokana na makosa na hataendesha serikali yeye peke yake,yuko na wenzake wenye Busara nyingi na utu wa kuthamini maisha ya watu wengine!Taifa la Kenya litajengwa na vijana wa Kenya wasiojua ukabila na udini ni nini, waliozaliwa baada ya uhuru na kulelewa katika mazingira huru yenye kuthamini utu na siyo ukabila,yenye kumuabudu Mungu na siyo udini,na yenye kutanguliza mbele na kuthamini Utaifa wa WanaKenya kwanza na siyo ubinafsi na ulafi wa madaraka!Mungu ibariki Kenya, Mungu wabariki WanaKenya!Ufisadi una mwisho wake,na mwisho wake ndiyo hayo mateke ya hivi sasa!Wanakenya wapenda haki lazima mtashinda!GOD BLESS ALL KENYANS!Tuko pamoja nanyi!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s