BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HERE COMES MR. AND MRS. BANANA December, 31, 2007

Filed under: Bongo Flava,Familia,Mahusiano/Jamii,Maisha,Muziki,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 8:41 AM

 

Jana ndio ilikuwa jana.Kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa,Banana Zorro na Suzy Walele jana walifunga pingu za maisha.Pichani ni Banana Zorro akimlisha keki mkewe Suzy Walele.Sherehe hiyo iliyofana ilifanyika katika ukumbi wa Msasani Beach Club jijini Dar-es-salaam.Banana na Suzy wamefungua ukurasa mpya.BC inawatakia kila la kheri.Kwa picha zaidi endelea hapa

 

Ukiolewa au kuoa mwanamuziki jambo moja liwazi.Atakuimbia sana tu.Banana hakusita kufanya hivyo kwa mkewe Suzy hapo jana.
Sherehe bila kutakiana kheri kwa cheers inakuwa haijakamilika. That was the moment.Did you notice who was the best man?
Ukweni hapaendeki mikono mitupu.Banana akikabidhi keki kwa wakwe zake,Mr and Mrs Walele.
Maharusi wakiwa na baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki katika picha ya kumbukumbu.
Picha zote kwa hisani ya MichuziJR.
Advertisements
 

30 Responses to “HERE COMES MR. AND MRS. BANANA”

 1. Chris Says:

  The good thing about this dude is that he knows what he’s doing.Very objective, doing what he believe. Hafati mkumbo km wengine. Hakurupuki,km other celebrities esp musicians.Inampa sifa sana.Ni mfano kwa wengine na hiyo ndo inafanya hata miziki yake iwe mizuri.

  All the best in ur new marital family. Chris…. Holland

 2. patricia Says:

  hongereni sana

 3. queen Says:

  Ama kweli mmependeza. Mungu aibariki ndoa yenu idumu itenganishwe na kifo.

 4. Mama wa Kichagga Says:

  Hongereni sana maarusi Bwana na Bibi Banana. Mmetimiza ndoto zenu na sasa nyie ni kisiwa. Fanyeni mambo yale yanayo wapa nyie furaha.

  Mtunze ndoa na nyumba yenu kamwe msiwaruhusu watu wengine kuvunja ndoa yenu. Mambo yenu ni yenu wawili tuu hata chumba cha pili kisijue.

  Hongereni sana

 5. Edwin Ndaki Says:

  HERI YA MWAKA MPYA 2008 BC.

  Pia nawatakia kila la kheri na afya njema wauzuliaji wote wa kijiwe chetu hiki.

  Sitaweza kuwataja wote..MAJITA,TANZANIA DREAM,ANY,MATTY,KIMARO,QUEEN,DINAH…nawengine woote…

  2008 hakuna kulala mpaka kieleweke.mmeona kwa jirani kenya kunawaka moto lazima na sisi tujipange.

  Thanks God its 2008

 6. kinono Says:

  Mmependeza sana vijana hongereni kuamua kukaa pamoja mungu awabariki sana nawatakia maisha mema.

 7. Michelle Says:

  Kwa kweli hongerani sana,sasa muwe waangalifu sana, maana marafiki watajitahidi sana kuwavuruga, Wazazi nao hasa wamama huwa hawatakikuachilia watoto wa kiume usiwe mama’s boy,kuna jamaa moja lilifanya hivyo kwa mkee wa lenyewe,kwa sababu ya mama ambaye alikuwa hata amelikataa kuwa si toto lake lilipooa kalivunjia ndoa,baba wa kijana ni balozi wa nchi za huko scandinavian maana ni twambombo walishaachana na huyo mzee,sasa yule mama anauza tu huko Dk, baba naye anaendelea kuzaa tu na wabongo hata ingawa ni mzee sasa, sasa angalieni sana msiendekeze wazazi na marafiki.

 8. any Says:

  heri ya mwaka mpya na wewe edwin/edu. na wengine wooooooooooooote. hata Dinah wa dinahicious.. na kila la herikwenu in this year.

 9. Nay Says:

  Hongera bwana na Bibi harusi, sie wasahili tunasema mtango na utangae wende ndani ukazae, upate ndume na jike.

  Ninawatakia kila la kheri katika maisha yenu ya ndoa, mjue ndugu wa mke na mume, muishi vizuri na majirani zenu, maana jirani ni wa shida na raha!

 10. Any Says:

  Ingawa hapa sio mahala pake lakini ngoja niseme.

  Bwana Edwin Ndaki, hilo balaa la kuana Kenya mungu apishilie mbali, huo moto ukishawashwa wewe uko Ufini na ndugu zako wako ghorofani watakaokufa ni ndugu zangu mie na masikini wengine ambao wanaishi Temeke, Mbagala, Tandika na Tandale na Manzese. Nyie mkishawasha moto mtakuwa mmejifungia kwenye mahekalu yenu.

  Siasa za ukabila na vurugu za Kenya hazikuanza leo, na hatutegemei kama tutaziiga. Walipokufa ndugu zetu Pemba, Maalim Seif na Prof Lipumba mpaka leo wanadunda wengine wamepoteza watoto, wazazi wengine kaka wao wamepoteza nini zaidi ya kukosa kuingia Ikulu? Hata huyo Odinga amefiwa na nani katika sakata lote hili zaidi ya sie wengine ambao jamaa zetu wanashindwa mpaka leo hii kurudi Kibera kwa sababu walitoka wakati fujo haijaanza kutafuta maisha na sasa hakuna hata usafiri wakurudi huko Kibera.

  Acheni ubinafsi na ushabiki wa mtandao, mkiambiwa mtoke muende kwenye maandamano mnajifungia vyumbani au maofisini mwenu. Wengi tumeona wakati kulipokuwa na maandamano ya fujo Dar afadhali hata huyo Prof Lipumba alishiriki nyie wenye kujua kusema hamkupanda ndege kuja kufa na sie. Acheni unafiki mnakaa kwenye viota mnasubiri sie tunaokaa kwenye mavumbi tufe kwa ajili yenu hatujaona hata mtoto mmoja au yeye Raila au jamaa za Kibaki waliyedhurika kwenye kadhia hii. Njia za kisheria ziko wazi badala ya kufuata sheria wanasiasa wako radhi watu wafe kwa maslahi yao! Tunataka tuwaone huku mitaani tutakapopokuwa tunapigwa mabomu ya machozi na nyie mje mlie na sie! Kama kweli vile!

  Hamumpati mtu ng’oooo tumeshawastukia!!!!!

 11. Papaa Says:

  Kila la heri bwa na bi harusi….kumbukeni ‘hamuanzi maisha’, mnafungua tu ukurasa mpya, maisha mlishayaanza zamani!

 12. any Says:

  du kumbe any tuko wawili.

 13. Upendo Furaha Says:

  Hongereni sana.

 14. Any Says:

  Hivi lilikuwa jina lako la urithi au la ukoo? Samahani kama unalilipia kodi.

 15. Edwin Ndaki Says:

  Rafiki yangu Any.. niliposema kwa hakuna kulala mpaka kueleweka nahisi hukunipata vema.

  Binafsi najua siasa za kikabila pamoja na ubabe na kuto kuwepo democrasia ya kweli ndio kuna pelekea yanayotokea kenya.

  Mi nilikuwa nawaomba watanzania wenzangu,tusikubali kuburuzwa na viongozi wetu.

  Yanayotokea Kenya kuna mengi sana ya kujifunza mbali na masuala ya ukabila.

  Utawala wa sheria hakuna.Kwanini serikali itoe baraka za kuua binadamu wenzetu kisa wanaipinga serikali.

  Kwa sababu yoyote ile SERIKALI DHARIMU,hazipasi kuwepo kwenye USO wa dunia.Heri ya mwaka mpya aluta kontinua…

 16. matty Says:

  Asante Edwin Ndaki kwa salamu za New year na mimi nawatakia wapendwa wa BC WOTE HAPPY NEW YEAR!!!
  Nawapongeza maarusi kwa hatua waliyofikia mmependeza sana naamini upendo utazidi kudumu ndani yenu, Mungu awabariki!

  Kaka Edwini Ndaki na Any hao wakenya wanaouana ni kweli ni tabala la chini watu wa hali fulani hivi hawaandamani hata siku moja na wako pale si kama wanatetea chama au haki yao,wengi wanatetea Raila (kwa ufahamu wangu) na wao ndo wanaokufa mwenzao na familia yake wanakula kuku kwa mrija.
  Ni bora wakubali matokeo kuliko kupoteza damu kiasi hicho!na Kibaki ajue malipo ya hizo damu zilizomwagika ni sawa na moto usiozimika.
  Mungu ibariki Tanzania, East Africa na Africa.

 17. mum Says:

  Hongereni sana kwa kuamua kufunga pingu za maisha. all the best.

 18. maryam kiosi Says:

  mimi maoni yangu kuwa sijamjuwa yupi mwanamme au mwanamke maana naona mmoja amesuka na mwengine ana maziwa sasa yupi mwanamme kati ya hawa wawili
  naomba ufafanuizi

 19. Abdi Mkwizu Says:

  Mungu aibariki na kuilinda ndoa yenu. Katu msiruhusu mahasidi waingilie ndoa yenu. HONGERA MAHARUSI

 20. Neoemmanuel Says:

  I am your big fan Banana, I should’ve been in Dar for the wedding.

  All, same “ongera, rafiki yangu”.

  Emmanuel(Brazil)

 21. Neoemmanuel Says:

  I am your big fan Banana, I should’ve been in Dar for the wedding.

  All the same “Hongera kwa kumpata wako.., rafiki yangu”.
  Yes”Mwanzo wa kutimiza ile nthondo yako, au siyo…”
  Wish you happy married life.

  Emmanuel(Brazil)

 22. Rodney Says:

  Hongera sana. Epuka kuruka ukuta wakati husika

 23. EasyS Says:

  Congratulations!!!
  Mengi yatasemwa, lakini kumbuka kuwa familia yako ndiyo ngao yako. Watakao kashifu au kusema ovyo si katika familia yako hivyo ni haki yao kwani hakuna waliofurahi zaidi ya familia na walio karibu nawe. You’ve taken the biggest step in your life, take it easy. Just remember that a strong marriage is built on Love, Trust and Respect. Always love, trust and respect each other as you’re each others’ best choice; Let no one come between you; Evaluate your friends and their advices. And please, let your married life always be a Honeymoon. All the best

 24. OrgZigda Says:

  Congratulations My Man G{}d bless you and ya wife mungu awepe ndoa yenu ya salama na amani hawaondolee husda kheri na fanaka muwe nayo amein.

 25. striclygospel Says:

  im ur fan dude congrats

 26. nusrat Says:

  HONGERENI SANA, TENA SANA, M’MUNGU AIBARIKI NDOA YENU, NA MUISHI KWA AMANI NA UPENDO, MSIKILIZANE NA MUHESHIMIANE. NA M’MUNGU AWAJAALIYE WATOTO WALIOWEMA NA WENYE KHERI NA NYIE. MTANGULIZENI M’MUNGU KWA KILA JAMBO. INSHAALLAH!!!!!!

 27. Imaculada Says:

  Hey bro congratulations! We are happy cz u are………. Mwah

 28. Alhaj meddie Says:

  eeeh bwana eeenh kila la kheri

 29. Jane Says:

  We Banana ndio ushakua mbaba tena mambo yakuruka ruka uyaache ala.
  Nawatakia kila la kheri Amani ya Mungu ipitayo fahamu zote iwafunike iwahifadhi ktk maisha yenu yote ndani ya noa yenu.

 30. lightness Says:

  Hongereni sanaaa
  Mwenyenzi Mungu awatangulie


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s