BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

INGEKUWA VIPI? January, 2, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 12:06 AM

 

Pichani ni Hamisi Mwinjuma aka Mwanafalsafa(MwanaFA).Msanii huyu wa muziki wa kizazi kipya ni miongoni mwa wasanii ambao wanasifika sana kwa kuwa na mashairi makali na yenye ujumbe mzito nchini Tanzania.Pengine yeye mwenyewe alilijua hilo wakati anaingia kwenye fani ya muziki na ndio maana akaamua kujiita Mwanafalsafa.Hatujui,siku moja tutamuuliza.

Mwanafalsafa ameshatunga mashairi na nyimbo nyingi.Miongoni mwa nyimbo au mashairi hayo ni lile ambalo inasemekana ndio “lilimtoa”.Aliliita “Ingekuwa Vipi”.Humo alikuwa anahoji mambo kadhaa kama vile;

Ingekuwa vipi Yesu angerudi?Angemaliza vita ya Wapalestina na Wayahudi? lngekuwa vipi kama Osama angeutawala Ulimwengu?Wamarekani Uarabuni wangekuwa Sungusungu?Ungekuwa vipi ulimwengu kama kusingekuwa na dini?Dunia bila dhambi,Kipimo cha uovu nini?Polisi, mahakama na gerezani angeenda nani?Vipi kama Wazungu wasingeingia Afrika? Magari, ndege, Reli na nguo, nani angeleta?Na bila biashara ya utumwa wangekuwepo black Americans? …na mengineyo.

Unaweza kuusikiliza wimbo huo wa MwanaFA kupitia EastafricanTube kwa kubonyeza hapa.

Advertisements
 

13 Responses to “INGEKUWA VIPI?”

 1. kali Says:

  mbona kama anataka kudondoka, shairi kama sentensi dah

 2. matty Says:

  Wimbo mzuri una mistari iliyotulia, nampongeza anajitahidi sana…..hilo pozi mbona kama anatutega!!!!!!

 3. asaki Says:

  vp F.A ulikuwa unamtamani mpiga picha nini? naona ulimi nje.i BUT CONGRATS UKNOW MUSIC REALLY APPRECIATE

 4. sthugs4j Says:

  ni kweli kijana anajitahidi sana na ana kipaji kizuri cha lugha. Nashangaa kwa nini hajiendelezi kielimu katifa fasihi ya lugha. Kama kawaida wanasanaa wa kizazi kipya elimu ni suala walilolisahau…ingawa pesa wanazopata zingewafaa kielimu na si lazima waende mlimani hata nje ya nchi au chuo kikuu huria..tujali elimu jamani!

 5. Upendo Furaha Says:

  Ninampongeza sana Mwana FA.
  Big up.

 6. Edo Ndaki Says:

  KAZI NZURI …B…

  Nakupongeza kwa kuona pia umuhimu wa shule ingwa naamini pia wapo wasanii ambao wanapenda shule ila mazingira yana wabana..

  Vipi wadosi bado mnawapigia magoti?kwanini Mwana FA msivae viatu vya Ngwair,Mox na Sugu?

  Itasadia kufanya mapinduzi ya biashara..mpigeni mdosi chini sio kulalamika tu wadosi wanawaibia bila kuchukua hatua

 7. Ed Says:

  Good job MwanaFa, nadhani katika so called Tanzania celebrities huyu ni mmoja ya wenye akili. Kijana amaweza kwenda kuchukua degree yake ya computer sababu he knows bongo flava will not take you to the promise land. Good Job son

 8. BongoSamurai Says:

  Ingekuwa vipi kama wazungu wasingekuwepo duniani, ingekuwa powaaaaaaaaaa…! Teh tehhhhh..!Mwana FA nakupa big up mistari imetulia….

 9. mbongo Says:

  Wabongo hacheni kumisifia Mwana FA,hinyo nyimbo maishairi yake yalikuwa ya kucopy kutoka ktk nyimbo ya Fedro star american musician kutoka kundi la onexs,Jamaa aka copy and paste.hiyo siyo ubunifu wake.na mwana Fa anasifika kwa kucopy nyimbo za watu.ingekuwa vipi alikucopy toka wimbo DAT Be em”

 10. wakunyumba Says:

  na wewe una wivu tu, hata kama amecopy si inatuhusu nini, jaribu kumpa mwenzenu moyo sio unamponda tu,
  wabongo kwa dhararu tu hatujambo

 11. kay Says:

  wewe unayejiita sthugs4j usikurupukie mambo usiyoyajua na kusema kwamba hajaenda shule kwa taarifa yako amegraduate last year ifm tumemaliza mwaka mmoja.usipende kuongea vitu usivyokuwa na uhakika navyo na kuwagroup watu wote kwenye mkumbo mmoja na vilevile jaribuni kujifunza kuappreciate kazi za watu na kama hauko interested navyo ni bora ukae kimya na sio kuponda bila sababu.

 12. pakamafia Says:

  sio wivu nyinyi wabongo mnasema hayo mashaili ya maana,yako wapi unaona utumbo mtupu,anasema ingekuwa vipi Osama siujuhi awe raisi wa dunia umeona jibu utumbo mtupu na wala aina maana yoyote saa nyingine wabongo mnaniuzi kupenda ujinga kama wamarekani,ndiyo maana kuito ulaya sio raisi kwani hapa kama ujinga wanakwambia ukweli lakini marekani na bongo hata ujinga unamaana.

 13. Roc Boy Says:

  Kweli maudhui wa ‘Ingekuwa Vipi’ yanafanana na wimbo wa Fredro Star unaoitwa “What if” (na sio Dat be dem, kama mchangiaji mmoja alivyosema hapo juu). Lakini kusema ame-copy ni ujinga. Hivi mnajua maana ya ku-copy?

  Bila shaka B alipata ‘insight’ baada ya kuusikiliza ule wimbo; pia hata ‘Perfect B*^%h’. Ni kama mistari miwili mitatu tu ndio inayofanana. Lakini jamaa kajitahidi kuzungumzia mambo yanayotokea kwenye jamii yetu na dunia kwa ujumla. Mbona Cassidy ameimba ‘I am a hustler’ baada ya ‘kuiba’ mstari kutoka kwa Jay-Z. Just give him a damn break!! Fredro made a good song, B made a dope joint, you dig?

  Halafu, mnachodai na hoja zenu hazimaanishi kuwa jamaa sio creative. Kuna nyimbo kibao za jamaa zimesimama na zina mashairi ya maana. Alikufa kwa ngoma, list ndefu….


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s