BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

RUSHWA NI ADUI,NANI ALAUMIWE? January, 3, 2008

Filed under: Mahusiano/Jamii,Mawazo/Tafakuri,Sheria,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:16 AM

 

Rushwa ni adui wa haki, ni adui wa maendeleo.Natumaini sote tunakubaliana na hilo.Rushwa ni mojawapo ya matatizo sugu sana yanayozikabili nchi zinazoendelea ulimwenguni ikiwemo yetu ya Tanzania.

Ndio maana nchini Tanzania kuna Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inayoongozwa na Dr.Edward Gamanya Hosea(pichani).Lakini swali au maswali magumu yanabakia.Nini chanzo cha rushwa?Nani wa kulaumiwa kuhusiana na tatizo hili?Je,wewe umeshawahi kutoa au kupokea rushwa?Ilikuwaje? Unashauri nini kifanyike?

Picha kwa hisani ya Issa Michuzi

Advertisements
 

19 Responses to “RUSHWA NI ADUI,NANI ALAUMIWE?”

 1. mama koku Says:

  kima cha chini cha mshahara ni shs 65,000/= hachana na hiyo labda ndo unapata laki na nusu 150,000/= umeme tu (kwa mtu wa kawaida mwenye fridge pasi, tv na taa za ndani) si chini ya shs 40,000/= housegirl shs 25,000/= bado sijakwenda kwenye chakula na school fees, hata kama wewe ni mchumi kuliko mpare bado bajeti itagoma tu, na hakuna msaada mwingine zaidi ya kula rushwa kwa kwenda mbele. kwa maoni yangu, hizo nyimbo za rushwa ni bora tu wangenyamaza kimya, maana nasikia huyo hosea ndo brigedia wa rushwa tanzania.

  Dawa pekee ni kuboresha mishahara ya watanzania, wenzetu kenya na uganda mtu anaefanya kazi anamaisha japo hata kama si mazuri sana lakini hana hofu ya kula, kusomesha watoto wala kulala, maana mishahara inatosha, lakini sio kwetu tanzania, mfanyakazi ndo mtu masikini kuliko wote, sasa unategemea rushwa ukiandika kwenye gazeti na kuiundia tume itasaidia nini? VIONGOZI WETU PUNGUZENI SIASA JAMANI TUNAUMIA……….

 2. mama koku Says:

  Hivi takukuru ndo hao hao pcb? kazi yao kubwa ni kukamata mahakimu na police wanaopokea rushwa ya shs 30,000/= mpaka 100,000/= hivi kweli mtu mzima na akili zako timamu hiyo nayo unaita rushwa?

  Wanaokula billions wanaachwa, unategema rushwa ije kuisha kweli Tanzania? hachana na kuisha, hata kupungua haiwezi kupungua, sana sana inaota mizizi.

  Hayo ni maoni yangu mimi, mtanzania ninae ipenda nchi yangu, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Africa

 3. Mpenda Usawa Says:

  Jamani tuwe wakweli.
  Huyo Hosea ye mwenyewe anajihakikishia kwamba ni mtu safi hajawai hata siku moja kuwa na uhusiano na huyo mdudu anaeitwa Rushwa?
  Let us be Frank and Honest.
  Nawasilisha

 4. matty Says:

  Hiyo takukuru yenyewe imejaa rushwa nadhani ndo maana haiishi hata sikumoja na chanzo chake ni tamaa, chuki, wivu na ubinafsi.
  Mfano mtu anamgonjwa hospital nesi anadengua (analeta pozi) kumhudumia mgonjwa yule mwenye mgonjwa anaona ili mgonjwa wangu atibiwe ni bora nimshikishe kitu kidogo nesi ili huduma itolewe, sasa hapa anayetia kishawishi cha Rushwa ni yule mhusika pale hospitalini.
  Mfano mwingine unaenda sehemu kuomba kazi unaqualifications zako na mashahada kibao, ukifika utazungushwa weeee na kama ni msichana hapo rushwa ya ngono ndo itakapotake place ikiwa boss ni mwanaume au lasivyo utoe kidogodogo ndo kieleweke.
  Hakuna dhambi kubwa kama ya rushwa na kuwanyima haki zao za kimsingi wanyonge.
  Mungu ibariki Tanzania!

 5. mohamed Says:

  Mzee Hosea ile likizo ya kirisimasi uliyowapa waleeee mwaka uleeee haijaisha? Mzee chemka vinginevyo hutoeleweka!

 6. Jumanne Says:

  Jamani,nadhani swali muhimu lililoulizwa hapo juu ni kwamba je umeshawahi kutoa au kupokea rushwa?Mbona wachangiaji wenzangu mnalikwepa swali hilo?Yaelekea sote tuna mchango wetu katika mdudu rushwa.

  Mimi nimeshawahi kutoa rushwa.I guess sijawahi kupokea kwa sababu sijawa katika mazingira yanayoniruhusu kufanya hivyo.Nimewahi kutoa rushwa pale muhimbili hospitali ili mgonjwa wangu(baba yangu alikuwa amelazwa) ahudumiwe vizuri.

 7. mama koku Says:

  Hata hamjuhi nini maana ya rushwa…. hiyo ya muhimbili, mahakamani ambayo unampa nurse elfu 10,000/= nayo unaitwa rushwa? unazani takukuru imeundwa kwa ajili ya hivyo vijirushwa? mie nilizani wachangia mada ni watu wanao elewa kumbe ni watoto wadogo (under age) nurse ataachage kukudengulia wakati hajaacha chakula cha watoto nyumbani? mshahara wenyewe ukipokea tarehe 25 mpaka ikifika tarehe 5 ya mwezi unaofuata umeshaishiwa unaanza kukopa, unategemea aje mgonjwa uanze kumkimbilia? kwani ndugu yako huyo…. big up nurses

  Kwa taarifa yenu rushwa inayozungumziwa hapo mfano mdogo ni ile ya aliyekuwa balozi wa italy (somebody mahalu if am not mistaken) mtanisahihisha kama nimekosea jina na nchi maana mie sio mwana siasa.

  Hizo za kumpa nurse na hakimu elfu kumi msije kuzizungumzia tena kwenye blog ya jamii… kama hamna point nawaomba muwe wasomaji

  mwananchi, mpenda nchi yangu Tanzania

 8. Karim Mussa Says:

  Mama Koku,
  Mambo mawili;kwanza yaelekea wewe ndio hujui kabisa maana ya rushwa.Kama hiyo elfu kumi wewe unaiona sio rushwa ndio maana tatizo lipo hapa lilipo.Ni watu kama wewe wanaojidai wajuaji ndio wanaoongoza kwa kutoa na kupokea rushwa.Rushwa ni rushwa tu,yaweza kuwa ya shilingi moja au hata bilioni moja.Yaweza kuwa ya ngono,busu au chochote kile kingine.

  Pili,mbona unakwepa swali?Umewahi kutoa au kupokea rushwa?
  Mimi Karim Mussa nishawahi kupokea na kutoa pia.Nilitoa ili nipatiwe kifurushi changu pale posta bila vitambulisho thabiti(mzigo ulikuwa wangu lakini) na niliwahi kupokea rushwa ili nimsaidie mtu kupata bank statement ambayo hakustahili kuipata.Mama Koku,zote hizo ni rushwa.

 9. Upendo Furaha Says:

  Ama kweli, “Rushwa ni Adui wa Haki, Sintapokea wala kutoa Rushwa”.
  Hawa TAKUKURU ninawapongeza kwa kazi kubwa nanayofanya.
  Tatizo ni kwamba wanapambana zaidi na rushwa za “Wala Sungura” badala ya “Wala Nyati” .

 10. Majita Says:

  Nimewahi kupokea SANA tu na kutoa rushwa SANA.Nilitoa rushwa kwa mara ya mwisho Arusha baada ya kukamatwa na ofisa wa PCB-TAKUKURU nikipokea rushwa.Ilibidi nitoe rushwa kwa PCB ili mambo yaishe na kweli baada ya kumpa mrungula hakunipeleka kokote mbali na kunipa warning ya kupunguza kasi.

  Eti PCB walitetea RICHMOND eti hapakuwa na rushwa katika mkataba huo.Mmmmh kazi ipo.Sasa bunge linaunda tume ya nini wakati PCB keshasema Richmond ni wasafi?????

  Polisi na mahakimu hawapokei rushwa.Wanapewa tip tu

 11. tish Says:

  Mie nishatoa rushwa tena mbele ya polisi wa takuru nae aliipokea sasa nifanyeje na nilikuwana shida ya haraka? nyie nendeni pale mnazi mmoja kwenye chanjo yani hadi raha unatoa harafu unapata yellow card, bongo tambalale bwana

 12. kimk Says:

  Tatizo la rushwa si mshahara,kwa maana ya kuwa hata hao wenye mishahara minono kama wabunge na wenye vipato kama wafanya biashara ndio watoa rushwa wakubwa. Jambo la msingi hapa ni kuwa hakuna utashi wa kushughulikia rushwa kuanzia ngazi za juu hadi chini. Vyombo vya kuhughulikia rushwa kama takkukuru na polisi vinawajibika kwa baadhi ya viongozi.Hivi takukuru itaweza kumchunguza Rais au waziri mkuu maana ndio hao walimpa mkuu wa taasisi hiyo kazi. Matokeo yake zile rushwwa kubwa zinazotikisa taifa kiuchumi na kimaadili zinaundiwa maneno matamu kama takrima,kuundiwa tume,kushughulikiwa na mamlaka husika n.k. Sasa mimi kama mkuu wa kaidara kangu nina sababu gani ya kumkabili askari au mwalimu ‘anayejikimu’ kwa 30,000 kama wale wenye mishahara ya mamilioni bado wanakula rushwa za umeme,madini!!!!

  Hakuna njia nyingine isipokuwa kuwa na chombo huru ambacho hakina uhusiano na Rais wala serikali katika utendaji wake.Hii takukuru ni chombo cha kuwaosha ‘papa’ kama tulivyoona Richmond na kuwahukumu walimu,matabibu na trafiki. Huwezi kumsafisha mtu kama wewe ni mchafu.Ingawa tunasema rushwa ni rushwa iweje rushwa ya 30,000 ihukumiwe na ileya IPTL na mikataba mibovu iachwe?

  Na mwisho kama viongozi wanachaguana kwa jenda,na urafiki ni nani atawawajibisha wakila rushwa? kwani mumesahau kuwa kuna bodi imesema fulani ndiye mhusika,je ameshughulikiwa vipi. sasa mimi kwanini ni jali na kukekea rushwa kama wale wanaohubiri hawatendi wasemayo.

  Tatizo si mishahara,ni kukosa utashi na viongozi wasafi ambao watasimama na kuikemea kama akina Mwl.Nyerere na sokoine. Jiulize utakamata vipi wala rushwa kama una biashara za migodi ya makaa na biashara ukiwa ofisi kuu ya nchi.
  Takukuru si lolote si chochote ni chombo cha kuwasafisha wakishasafisha mali zetu.

 13. mama koku Says:

  Karim Mussa,

  Soma paragraph ya mwisho ya majita na upendo

 14. wakunyumba Says:

  huyo bosi wa masuala ya rushwa nasikia ndio mkingaji mzuri lakini ndio maisha ya tanzania hayo

 15. matty Says:

  Mama Koku, labda wewe ndo hujui maana ya Rushwa,mimi nakubali sijawahi kutoa rushwa ila siku moja nilijuta pale niliposhindwa kutoa rushwa ili mzazi wangu atibiwe hospital na hatimaye akafariki inamaana ningetoa rushwa nurse angekuwa karibu hata kumsikiliza mgonjwa anajisikiaje(hata kama asingepona ni mipango ya mungu ila at leat nurse alikuja kuliko unamuita anadengua).Si tukwamba uwaite watu(under age) ***kabisa wewe!!!!!!!labda wewe ndo under age.
  Rushwa ni rushwa tu!! hata iwe sent 5,10,20 nk. acha tuanze na huku kwenye jamii yetu hususani hospital pananiboa sana, wewe unaiona elfu 10 ndogo wakati bibi yako kijijini hana hata sabuni ya kufulia na akitoa hiyo elfu 10 kumpa nurse si atakuwa kapoteza mtaji wote wa dagaa sasa utaniambia hiyo si rushwa???
  MAMAKOKU TAFUTA MAANA YA RUSHWA NDO UJE KUCHANGIA SIO KUKURUPUKA TU…RUSHWA NI RUSHWA TU HATA BUSU KAMA ALIVYOSEMA KARIMU MUSA.

 16. Mercy Says:

  Mama koku ambacho huelewi ni nini??inaelekea wewe ni mtoto wa Mafisadi wakubwa hapa bongo ndo maana unaikataa rushwa ya elfu 10.
  Suala sio ya kuanzia millions, rushwa ni rushwa tu!!!!!!!!!!!
  mimi nishatoa mara kibao hapo Hospital ili mdogo wangu atibiwe haraka ili tuwahi kuondoka maana daladala ukichelewa usiku ni za shida hasa za kwenda Mbagala, uwezo wa taxi sikuwa nao sasa what do say!!!!!!!

 17. Kimori Says:

  The way I know is that PCCB is Prevention and Combating of Corruption Bureau. I think the key word here of this government entity is CORRUPTION and if you look at the definition of corruption you will find that corruption is a general concept describing any organized, interdependent system in which part of the system is either not performing duties it was originally intended to, or performing them in an improper way, to the detriment of the system’s original purpose.

  However, going deeper to elaborate corruption, I found out that there are various forms of corruption and the ones which attracted my attention are:

  1.Political corruption, which are dysfunctions of a political system or institution in which politically elected officials seek illegitimate personal gain through actions such as bribery, extortion, cronyism, nepotism, patronage, graft, and embezzlement. “Rent seeking” is a closely related term in economics. Again in this type of corruption I met the word bribery, which I think most of people are interested in.

  What is bribe?…To my view this is where the main problem lies, especially for low-income people. The bribe is the gift bestowed to influence the receiver’s conduct. It may be any money, good, right in action, property, preferment, privilege, emolument, object of value, advantage, or any promise or undertaking to induce or influence the action, vote, or influence of a person in an official or public capacity.

  It is generally considered unethical. In most jurisdictions it is illegal, or at least cause for sanctions from one’s employer or professional organization.

  For information bribery around the world is estimated at about $1 trillion (£494bn) and the burden of corruption falls disproportionately on the bottom billion people living in extreme poverty, which I think I am part of. Everybody at any time of his/her life has been involved in giving or receiving bribe and I am one of them.

  2.Another type of corruption is the so called Bureaucratic corruption,, which relates to mainly to nepotism and pecuniary corruption by bureaucrats that pushes up the cost of functioning of public offices, penalizes the public exchequer or clients or both.

  3.It will also be interesting to know that there is Police corruption, which is a type of bureaucratic corruption that infects police departments, and includes misuse of authority in addition to bribery. Police misconduct is a closely associated phenomenon.

  I beg to submit!

 18. Majita Says:

  KWA MATTY NA WENZAKO:-

  RUSHWA ni kitu chochote kitolewacho kwa hiari kwa mtu mwenye nafasi fulani ili ku-influence msaada (favor) wa aina yeyote.Inaweza kuwa hela,mali,utu ama situation fulani.

  Mimi nafikiri Tanzania tatizo kubwa la rushwa ni TAFASIRI halisi ya neno rushwa.Mfano:-
  1:Mwalimu akifaulisha sana wanafunzi wake ama wanafunzi wakimsifia mwalimu kwa ufundishaji wake na mzazi akachukua jukumu la kumpa mwalimu huyo zawadi ETI wanasema mwalimu kachukua rushwa.
  2:Polisi akifanya kazi nzuri na raia kuamua kumpa zawadi ETI wakubwa wanaita rushwa.Kwa mujibu wa PGO-Police General Order ETI kama askari wa cheo cha chini say PC akitaka kupokea hiyo zawadi,inatakiwa ipelekewe IGP na huyo IGP aitangaze ndo imwendee huyo polisi mnyonge.Assume wewe uko majita na unataka kumpa motisha huyo Polisi wa majita ya sh.10,000/=guess what??unatakiwa uipeleke Dar HQ kwa IGP.Mifano ni mingi.Huo ndo urasimu.

  Waliosoma education watakubaliana na mimi nini tofauti ya motisha,zawadi na adhabu.Wale wa sheria na madakitari nao watakubaliana na mimi kuhusu dhana ya Zawadi.

  Tanzania kinachofanyika ni kushughulikia tips,zawadi,na motisha.Wale wala rushwa wanaachwa bila kuguswa.Kimsingi wanaopokea rushwa ni wakubwa.Nina mifano halisi na hai.Tutawasema ma-traffic police lakini hatujui wala RUSHWA.

  Leo namshangaa sana MATTY kwa kumhoji mama koku kuhusu kutoa 10,000/= tu.Amesema kwa jazba kuhusu bibi yake muuza dagaa.Ni wiki juzi tu huyohuyo MATTY alimshaabikia mama Salma Kikwete kuhusu kuvaa matenge. sishangai hao ndo watanzania halisi.Sasa Matty!!!yale matenge ya mama Kikwete uliyoyashaabikia ni bei gani na hizo 10,000/= ni bei gani?????Je! kwa maana ya rushwa tunasemaje kuhusu mavazi ya mama kikwete????

  Ukiwa nchi nyingine say Marekani,utasikia maneno tips yakiwa common sana.Ukienda say bar au hotelini mbali na gharama zooote utakazoandikiwa kwenye bill LAZIMA utakumbana na tips.Ndo maana utaona bar-maid wa USA ana maisha bomba tu kwani anaweza kutengeneza hata $5,000/= kwa night kutokana na tips tu,lakini Tanzania tunaita RUSHWA.

  Mimi nasema hivi,nyie PCB sijui TAKUKURU acheni kushughulikia tips,shughulikieni rushwa.Acheni vi shilingi 10,000/= hivyo.Nyie wakubwa mnachukua mamilioni ya rushwa kila siku na PCB mkiwa miongoni mwao na kukaa kusumbua wanyonge tu.
  MKOME.
  Majita

 19. Matty Says:

  MAJITA, mimi nimetoa mfano mdogo tu!jinsi mzazi wangu alivyofariki baada ya kushindwa kutoa kitu kidogo hospital,hapo ukiniambia hiyo ni tipu/zawadi nakuwa sikupati vizuri.(inamaana tipu/zawadi inatolewa kabla ya kazi au baada ya kazi??)
  Kuhusu Kitenge cha mama salma kinahusiana vipi na rushwa inamaana yeye hana elfu 10 yake binafsi ya kununua kitenge?????(narudia tena dingi anatoa mshiko heavy wa mboga kinachobaki maza anatinga mwilini)huna haja ya kudhania kitenge alichovaa amekula rushwa kumbuka viwalo anavyotoka yupo teacher…. MAJITA KILE KITENGE NI BEI NDOGO MNO RAFIKI YANGU WALA HAKIUZWI MILLION.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s