BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

AFRICA MOKILI MOBIMBA January, 11, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Sifa moja ya muziki mzuri ni kwamba ukiusikia tu unajikuta na wewe unamumunya mumunya maneno yake huku ukitingisha kichwa,mguu,bega,kiuno,ukirusha mikono hewani na kutamani kunyanyuka ucheze.Muziki mzuri ni ule ambao tune yake hukaa kichwani kwako daima,haikutoki. Hata ukiusikia bila maneno au kwa ala tupu(acapella) unautambua.Isitoshe,wakati mwingine haijalishi kama unaelewa maneno yaliyomo au la.

Leo tunahama kidogo kwetu.Tunataka kuthibitisha kwamba muziki ni lugha ya dunia(Music is a universal language). Wimbo unaitwa Africa Mokili Mobimba.(Africa Worldwide/ Afrika duniani pote).Wimbo huu umeimbwa na kurudiwa na bendi kadhaa za DRC kiasi kwamba kuna utata fulani kuhusu nani hasa alikuwa mtunzi au mwenye wimbo huu.Pamoja na hayo wanamuziki kama Dr.Nico,Tabu Ley Rochereau(pichani) na Dechaud(kaka mkubwa wa Dr.Nico) ndio wanatambulika zaidi kuhusiana na wimbo huu. Bendi kama Rumbanella Band imewahi pia kuurudia wimbo huu na kupata nao mafanikio.Pata burudani.Ijumaa Njema.

Shukrani F.T.Mtimkubwa kwa wimbo huu.

Advertisements
 

6 Responses to “AFRICA MOKILI MOBIMBA”

 1. john Says:

  Geff !
  Huu wimbo ni classic !
  Popote niusikiapo hutamani kucheza
  Siku njema kwako na wasomaji wote
  Mr Dar

 2. Edwin Ndaki Says:

  Kaka Fidel mimi nasema Kiitosi kwa kuturushia ilo dude.

  Wasalimie Helsink.

 3. mpita njia Says:

  Sasa hapa kweli Mzee Pascal Tabu Ley ni mwanamziki
  mkubwa Afrika!Lakini sasa Bongo Celebrity ?tena inageuka
  Kongo Celebrity!habari za huyu bwana hapa sio mahala
  pake!au sasa hii bongo celebrity ya wabongo inaelekezwa
  wapi jamani?????

 4. Paukwa Says:

  BC endeleeni kutupa burudani.Mpita njia mimi nadhani wewe hujui muziki.Kama ungekuwa unajua usingehoji kwanini BC wameweka kitu kama mokili mobimba.Isitoshe wamesema kabisa kwamba wanavuka mipaka…sasa hujaelewa nini hapo?BC mwendo mdundo..achaneni na wapita njia.

 5. amina Says:

  jamani africa mokili mobimba ndo nini mi nimezaliwa mwaka 85 sijui kitu

 6. Freddy Macha Says:

  Ni muhimu kuzungumzia muziki wa Kikongo hata kama si wa Wabongo. Kwanini? Sababu nyingi.
  Mosi.
  Muziki wa Kitanzania penda usipende katika miaka 40 iliyopita umekuwa ukinukuu na kuathiriwa sana na hawa majirani zetu. Bendi kubwa kubwa za zamani kama Atomiki Jazz, Morogoro Jazz, Tabora Jazz, Kilwa Jazz , Dar Jazz, Msondo, nk zilichukua (kiduchu) kile wanamuziki tunachokiita “licks” yaani vipande vya mamelodi katika upangaji sauti, magitaa hata Sax. Uigaji huu ni muhimu katika maendeleo ya muziki wa Kitanzania, si kwa ubaya (kuiga kila kitu ni vibaya) ila kwa kuwa wasanii huigana na kupeana mahamasa (inspiration). Leo kwani huu muziki wa kizazi kipya ni nini? Si hiyo “hip hop” ya Marekani (iliyoanzia kwa marehemu James Brown ambaye naye alichukua vitu kutoka Naijeria na kwa Waafrika)? Hiyo moja.
  Pili.
  Ili kufahamu asilia ya muziki si vibaya kuwataja baadhi ya magwiji wa Kiafrika. Mbona BC ilishawataja akina Mbaraka Mwinyishehe na Balisidja katika safu zake nyuma? Sasa kumtaja Tabu Lei kuna ubaya gani? Wapigaji muziki (Hasa waaimbaji) kama Patrick Balisidja na King Kiki ( Mzaire aliyehamia Bongo na ambaye anaimba pia Kiswahili) waliimba kwa mtindo wa Tabu Lei ambao tuliuita wa “Kichiriku” (yaani mwanaume kuimba sauti ya juu sana, Wazungu huita “falseto” au “soprano”.)Uimbaji huu unaghani (kama wanavyoghani waimbaji wa Kiarabu, Kihindi na Kihispania); kwa hiyo ni muhimu kuujua. Haina maana kuwa BC inatukuza wageni. Ah ah. Inafahamisha. Hilo ndiyo lengo la mablogu kama haya.
  Tatu.
  Wazaire ni Wabantu kama sisi. Uimbaji na upigaji wao wa muziki kiasilia unakaribiana sana na wetu. Na si tu Wakongo. Vile vile, Wakenya na Wazambia. Miziki yao inafanana fanana. Nazungumzia kiasilia hapa…katika ngoma, katika na umbuji wa muziki, kwenye chimbuko. (Msikilizeni Mwanamuziki wa Kizaire, mpiga kibodi, Ray Lema ambaye katafiti muziki wa mbilikimo wa Kikongo na ngoma za kiasilia. Lema anatufahamisha kitu kimoja. Chimbuko letu ni muhimu. Waafrika Magharibi wanaendelea kutuzidi kwa kuwa wanatafiti asilia zao).
  Nne.
  Wimbo huu wa Afrika Mokili…unazungumzia hekaya na kulilia bara Afrika (kuna msomaji aliyezaliwa mwaka 1985 juu kasema haujui wimbo una maana gani) ulitungwa katika kipindi ambacho Waafrika walikuwa ndiyo wanapata Uhuru na ghasia na kasheshe za mwanzo wa miaka ya 60 kali sana. Kati ya matukio makubwa yaliyotokea yalikuwa mauaji ya kikatili ya Waziri Mkuu mteule wa Kongo, Patrice Lumumba aliyeuawa kama kuku (afadhali hata kuku unamuua awe kitoweo); alipigwa, akatukanwa, akapigwa risasi kisha wakatekeza maiti yake kwa tindikali (sulphuric acid), 1961.
  Mmoja wa wanajeshi wa Kizungu aliyemuua alisema miaka mitano iliyopita katika mahojiano Ubeljiji(walikuwa Wabeljiji) kuwa alichoweka kama kumbukumbu kilikuwa pete yake Lumumba kidoleni. Pepe Kalle mtunzi wa wimbo huo alikuwa akiilia Afrika na hususan Lumumba, akina Ben Bella, na matatizo ambayo bado tunayo leo.
  Sasa basi kuna ubaya BC kuonyesha kitu kama kile? Bara letu linatuhusu wote, ingawa hii blogu ni ya Watanzania hakuna ubaya kuonyesha matukio muhimu. Kwanini? Kwa sababu yanatuhusu. Maafa yaliyowapata Wazaire (na sasa Wakenya, awali, Waganda) huwa yanatuathiri sana Wabongo. Wamejazana Bongo wakimbizi toka huko. Nkrumah aliita hii itikadi Pan Afrikanism.
  Namalizia kwa kukutaka msomaji usikilize wimbo huu ulivyokuwa awali,. Mtunzi wake ni Pepe Kalle:


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s