BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BALALI YUKO WAPI?YUKO HAI? January, 11, 2008

Filed under: Developing News,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 4:28 PM

 

Kama unafuatilia mambo yanayoendelea nchini Tanzania, ni hakika kwamba utakuwa umesikia kuhusu taarifa ya hivi majuzi ya kufukuzwa kazi aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu nchini Tanzania, Daudi Balali.Mambo yanakuwa magumu zaidi zinapoibuka taarifa mbalimbali kuhusu alipo Balali.Yuko wapi? Soma zaidi kuhusu habari ya utata huo kama ilivyoandikwa na Tanzania Daima kwa kubonyeza hapa.

Advertisements
 

45 Responses to “BALALI YUKO WAPI?YUKO HAI?”

 1. Kimori Says:

  I want to believe sincerely that the president has revoked the appointment of the Governor Balali due the corruption scandal which has been so long being debated throughout the country as was reported by Honourable Luhanjo and not because of his “deteriorating” health condition.

  I solemnly presume that there is something mysterious going on. We first heard of Governor tendering his resignation to the president just as report was submitted asserting that he (the governor) could not perform his duties as required. Then after a little while the Government denied receiving such a letter of resignation and even persistently refused to inform the public of Governor’s whereabouts leave alone mentioning the hospital in which he is admitted for more that five months now! Surprisingly, up to now there is no any top official who knows where is Balali!…Quite ridiculous!

  However, it remains to be a gimmickry for the president to pretend to be serious in issuing controversial rulings on the matter. I am really enraged that Balali and his company will still walk freely after such a huge squander of taxpayers’ money! I don’t see any reason as to why some can praise the actions taken after the BoT report, because there is no action at all! It is the same old politics and no a glimpse of hope for the nation!

 2. fukara Says:

  We acha tu
  unajua hili ni dili Limbu alisha sema atachukuliwa
  atawekwa waaa
  kwa maslahi ya mafisafidi sasa yetu macho
  Na uchungu sana a mimi
  ,waheri

 3. Majita Says:

  Yuko kwake Washington-USA.Unauliza yuko hai!!Kwani alikuwa anaumwa???Mbona hatujasikia ajali yeyote.Baada ya kuandika barua yake ya kustaafu kazi na Ikulu kuikubali kwa mtindo wa KimajitaMajita jamaa alirejea kwake kupumzika.

 4. Dinah Says:

  Serikali ya Marekani na Tanzania washirikiane wamrudishe Bongo ili apatiwe kile kinachostahili…..kufungwa kifungo cha maisha au kifo kama inawezekana ili iwe fundisho kwa mafisadi na wezi wa mali ya uma wengine.

  Nina uhakika kabisa sio Balali tu bali kuna anaepaswa kufukuzwa kazi bali hata wale Mawaziri waliokuwa wakimuunga mkno au kwa kiswahili chepesi kumtetea, hao wapambe (Mawaziri na wabunge waliokuwa wakimuunga mkono) watoke adhalani (in public) nakuomba radhi Taifa kwa utovu wao wa nidhamu kwa kumtete Fisadi Balali.

  Tukiendelea hivi na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria watu kama Gavana na wengine wengi wahalibifu na wala rushwa(wezi) ikiwa ni pamoja na Majaji na Viongozi wengine kwenye Wizara mbali mbali nchini Tanzania, hakika tutafika mahali.

  Heri ya mwaka mpya!

 5. Dinah Says:

  Nimekumbuka hii, wale wote waliokuwa madarakati kama waziri na watendaji wengine wa Wizara ya fedha wakati yeye ni Gavana wafukuzwe kazi pia na wachukuliwe hatua za kisheria.

  Naona Serikali za UK na US wanaunga mkono (nimesoma habari zao muda huu) hii kitu na wanataka wachukuliwe hatua za kisheria hivyo sio mpaka wazungu waseme ndio tufanye hima kuwatimua wale wote “waliouchuna” yaani wale ambao hawakuchukua hatua za kisheria wakati huo na walikuwana uwezo wa kufanya hivyo

  Ni wazi kuwa hatuhitaji kupoteza pesa za mvuja jasho (mlipa kodi) kwenye uchunguzi mwingine au kuendesha kesi wakati kitu “kipo cheupe “. Timua wote, binafsisha mali zao, weka jela kisha tuanza from scratch.

 6. Zafanana Says:

  Huyu bwana alitaka kujiuzuru, kakini raisi alikataa, ili baadae amufukuze – Kwani ingekuwa soo, Tanzania ingekosa pesa toka Millennium Challenge – US na GBS – EU.
  Serikari haina wanauchumi wakereketwa-Visionaries, hata hao maprofesa na madokita ameweka, Kazi kusoma magazeti nakuongea kwenye simu

 7. Ally Says:

  Jela miaka laki nane huyo kwa nn ss tunaenda mbio wao wanakula pesa za zetu na watoto wao?wanasomesha watoto zao shule za maana wanawapeleka ngambo kusoma we mbonde kabwela mlipa kodi unangaa tuu sharubu hapo fungilia mbali kama hwa nchi itanyoka tuu hiyo lkn kama tutaendelea kuoneana haya sijui nilisoma nae bagamoyo au maskani 1gogo vivu tutaendelea kuburuzwa hivi mpaka mwisho wa dunia.

 8. Matty Says:

  Msela anadunda kwa raha zake huko aliko mihela ashachukua kibao na serikali inamficha asijulikane aliko ili mimi na wakina majita tusije tukamvamia kwa hasira (du!!! natania jamani).
  Ni bora BOT ianze na alif waliopo tokea enzi hizo wachunguzwe upesi na wapelekwe njia panda ya segera (segerea) ili iwe fundisho kwa wengine, sioni haja ya kumfukuza kazi mwizi, kwanini asipelekwe jela kama wengine maana nayeye ni mhalifu tu.
  Anaumwa????? nini???kalazwa???wapi????

 9. Sinzia Says:

  Kuna kipindi serikali iliwahi jigamba sana kwa kulipa madeni ya nje na sisi walalahoi tukapiga makofi maskini bila kujuwa….kumbe walikuwa wanalipa madeni hewa!!!! Hapa anaeyehumia ni sisi walalahoi ambao ndio walipa kodi wakuu.

 10. johnruta Says:

  Sasa huyu Balali ataendelea kulipwa mshahara wake ama vipi?
  Maana Magavana wa BOT hulipwa mishahara yao for their life time hata kama akistaafu ugavana.
  rate ya mishahara yao huwa sawa na mshahara wa Gavana aliyepo madarakani.
  kazi ipo hapo!!!!!!!!!

 11. Baba Koku Says:

  my bro Balali si here with me in Mwanza…

 12. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  Hivi sisi ni lini tutapata mtu asimame hadharani kama Marion Jones kuwa tayari kunyangánywa medali, rekodi ya dunia na fedha na kuhukumiwa lakini akiri na kuwa muwazi kuwa alifanya makosa? Upendo wangu kwa huyu dada umeongezeka mara dufu. Moja ulikuwa ni ule muonekano wake wa ucheza na sasa zaidi ni ushindi wake dhidi ya uongo na udanganyifu!

  Yaani Tanzania hakuna mkubwa anayekosea?
  Ni mapambano na ubishi mpaka mwisho kama katika vilabu vya Yanga na Simba. Mabishano na kutotubu yameendelea na kuambikiza hata Miskiti na Makanisa. Kiongozi bomu Kanisani yuko tayari hata kununua wakristo ili wamchague tena!
  Kwenye siasa ndio makao makuu ya kuhifadhi wabovu ilimradi mtu awe na investments hata kama ni za mikopo ya benki!

  Mzee Balali, I extend my lovely invitation at this minute through my keyboard, usimame mbele ya Watanzania ukiri matatizo yote yanayohusiana na ubadhilifu ndani ya BOT kwa kadili unavyojua. Utasamehewa na kuheshimika na kila Mtanzania. Na Mungu pia atakufutia makosa yakoyote dakika hiyo hiyo kama alivyoahidi. Ewe Mrs. Balali fanya kama Mume wa Marion alivyokuwa amemshika Marion akitubu na hata baada ya hukumu. Kumbuka maisha yenu ni zaidi ya fedha za hapa duniani, ni zaidi ya umaarufu wa hapa duniani na hakuna amani popote mtakapokuwa hata kama mngepangishwa katika jengo refu kuliko yote duniani la Mnara wa Taipei lenye urefu wa futi 1,670 huko Taiwan na kila kitu ndani, mtapata utulivu wa Viyoyozi lakini kamwe hamtapata AMANI YA ROHONI!

  Na ukianza wewe, wengine wote itabidi waseme kwa uwazi walivyoshiriki mchezo mchafu dhidi ya kidogo tulichonacho Taifa duni kimaendeleo. Utarahishisha kazi ya Wakaguzi na Wachunguzi na hata utumishi wa rais.
  Baada ya ushindi huo mkubwa wa hatua hiyo sote tutaruka na kuimba bravo Balali, bravo Balali, ubarikiwe zaidi Balali na usisahau kunikumbuka katika maombi mimi Nyakatakule kijana mdogo sawa na wanao!

 13. Bablii Says:

  Nyakatakutle,

  Umenifanya mpaka machozi yamenitoka, umeshawahi kuandika kitabu cho chote cha hadithi? Una mtiririko mzuri wa habari, lugha nzuri na fasaha na una uwezo wa kuchora picha kichwani mwa msomaji juu ya habari unayoizungumzia. Hakika comment yako imetulia pamoja na ukweli, na umakini juu ya maudhui yenyewe lakini pia fani imetulia. Umefanya ni comment juu ya comment yako badala ya FISADI BALALI.

  Big up bro ni mwandishi mzuri sana.

 14. Edwin Ndaki Says:

  Jamani hii sirikali ina watu wanaakili sana.Usije hata siku moja ukafikiri mikataba mibovu wanayoingia,eti hawafahamu madhara yake.Hapana.

  Utakuwa unajidanganya.Ni ufisadi ndio unawafanya wanatusaliti.Sasa leo hii tunaulizana Balali yupo wapi?Wakti majuma machache yaliyopita serikali ilisema anatibiwa na gharama zinalipwa kwa fedha ya walipa kodi.

  Ina maana wanataka kutuambia kwa miezi mitano wanalipa pesa zetu kwenye hospital wasiyoijuia kweli?

  Najua Balali akijitokeza na kuja kuweka mambo hadharani,sijui nani atapona kwenye hao vigogo.Usishangae na Mzee Lupaso naye yumo kunduni,mawaziri na hata Vasco.

  Ninacho jua mimi kwa ufahamu wangu.Serikali ikimuitaji Balali afikishwe mbele ya sheria wanaweza.Ila wanaogopa atawataja.Ndio maana wameona wamfiche.Kuna Internpol police dunia nzima anaweza kuletwa fasta tu.

  Kama alivyosema wamai Majita,Balali kajipumzisha Usa.

  Bado nauliza nani serikalini mwenye ubavu wa kumvisha paka kengere?Dawa sio kutwambia Balali ni paka sisi ni panya.Mfungeni sasa kengere muone cha moto.

  wasalaaaaam!!! mlipa kodi kwa ajili ya kulipa madeni ya nje mkapa aliyokuwa anajisifi kila mara.

 15. Ndugu zangu,naomba ieleweke kuwa Balali hajafukuzwa kazi,bali cheo chake alichokuwa nacho awali(ugavana) ndiyo uliotenguliwa na Mh.Rais.Kwa hiyo ni kama tumefanyiwa mazingaombwe.Kama akipona,basi anaweza kurejea nchini na ataeendelea kuitumikia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nafasi nyingine ambayo atapangiwa na Wizara ya Fedha ambayo ndiyo mwajiri wake.Tumepigwa changa la macho na sirikali,alipaswa kimsingi afukuzwe,lakini ugavana wake tu ndiyo uliotenguliwa,na si ajira yake

 16. BongoSamurai Says:

  Mazingaombwe, kiini macho…!
  Inanisikitisha sana sana sana na kunihuzunisha jinsi hawa tuliowakabidhi dhamana ya kutuongoza walivyotugeuza wadanganyika na mazingaombwe yao bila kusahau viini macho kila kukicha..,kuanzia IPTL, Richmond,Radar, mikataba mibovu ya madini na sasa hili la BOT…!
  Hivi ni lini watanzania tutaamka toka kwenye huu usingizi mzito tuliolala…?!
  Hili la kutengua ugavana wa Balali ni changa la macho na usanii wa hali ya juu..!Tusubiri kinachofuata (kuwajibishwa kwa wahusika) kama kitakuwepo…!
  Mungu ibariki Tanzania.

 17. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  Bablii, chozi lako halikutoka si tu kwa ajili ya usanifu wa kiuandishi bali pia inaonyesha jinsi ambavyo suala hili la BOT limetugusa sote kwa hisia kali.
  Hata hivyo ni kwamba hata katika hasira ya kilichofanyika bado mawazo ya hekima yanayojali makusudio ya kurekebishana makosa, utu wa mtu na maendeleo endelevu ya mwanadamu ndiyo yanatakiwa kutolewa.

  Asante sana mdau Bablii kwa kunitia moyo. Sijaandika kitabu chochote lakini mimi hupenda kuandika makala na kutoa mawazo mbalimbali katika mitandao na nipatapo nafasi vyuoni. Pengine bado kitambo kidogo nitachapisha kitabu changu (samahani kwa lugha ya kiingereza) na tutajulishana mara kitakapokuwa hewani.

 18. Tokomile Tulivu Says:

  Kwa kweli kwa muda wa miaka mingi sasa viongozi wa serikali ya Tanzania wanatufanya sisi wananchi tulio wengi ambao ndio tulio wachagua kuwa ni wapumbavu, ninasema hivyo kutokana na hili sakata la BoT ambalo hivi sasa linazungumzwa kwa sana, kwa kweli kashfa hii anatajwa Balali
  peke yake. Ukweli kutokana na uzoefu wa vipi Tanzania mambo yanao wahusu viongozi yanavyozimwa hasa yakihusiana na wizi, rushwa, uonevu na hata mauaji. limekua ni jambo la kawaida. Balali alikuepo BoT kulinda na kutetea maslahi ya wakubwa wenziwe, na kamwe sio walala hoi. Imedhihirika hii baada ya kuona dili imeshitukiwa akafanyiwa mpango aondoke nchi haraka sana kwa kisingizio cha kwenda matibabuni Amerika. Hivi sasa serikali inagwaya gwaya ikiulizwa habari za Balali. Kwa taarifa zenu wabongo wenzangu hiyo ndio imetoka! Balali ameshasevu, hakuna cha kurudi au kurejeshwa Tanzania kukabili mshitaka, tunajua kuwa huo ni mtandao wa kula mapesa ya uma unaohusisha viongozi kibao wa ngazi za juu pia. Kumbukeni 2010 haipo mbali mtakuja kutueleza nini wananchi, ukitilia maanani kwamba habari hizi za BoT zilikua zinajulikana zamani, lakini ngoma ilizimwa hadi hapo Viongozi wa Upinzani walipoanza
  kuipigia kelele serikali. Kila kukicha tunaambiwa serikali haina fedha, kumbe walojuu wanayaeka kwenye “personal account”
  zao huko Ulaya bila ya noma wala nini, bado kuna maswala ya ununuzi wa rada, mikataba ya madini ya kimizwengwe ambayo wananchi wa Tanzania tumeyeyushwa. ” Unaweza kuwafanya baadhi ya watu kuwa wajinga kwa muda, lakini huwezi kuwafanya watu wote wajinga nyakati zote”

 19. Mama wa Kichagga Says:

  Nyakatakule hoja zako zinanifurahisha sana halafu za kiutu uzima na maadili kebekebe, wachilia mbali mpangilio wa hoja zako. Keep it up man!

  Hicho kitabu kikiwa tayari tafadhali usiache kukimuvuzisha hapa ili nasi tukifaidi.

  Mimi nakubaliana na wewe kabisa kuhusiana na suala zima la kukiri makosa mbele ya hadhara au vyombo vya habari. Haijalishi itakuumiza vipi ila utakachokipata kikubwa katika maisha yako ni UHURU NA AMANI YA MOYO huku wengine wakipata mafunzo ya namna ya utendaji na uwajibikaji bora. Laiti kama Balali angekuwa ni mume wangu ningeomba msamaha kwa niaba yake ili kuupooza umma wa Watanzania na kuwatia moyo.

  Historia inatukumbusha kuwa hakuna jambo jema kama kuomba msamaha. Mfano mzuri ni ule ulioonyeshwa na Clinton wakati akiwa rais alivyokubwa na kashfa “YA NGONO OFISINI”. Jamaa alipoamua kukubali kosa tena mbele ya familia na umma aliwekwa ktk vitabu vya kumbukumbu kama muungwana na baada ya pale hakuna mtu anayekumbuka makosa yale. Na kwa kuwa alikiri hadharani angalia sasa hivi ilivyo faida hadi ndani ya familia mama anathubuti kusimama majukwaani kugombea urais wa nchi na yeye mumewe anaambatana na mkewe kwenye kampeni bila woga maana ni MTU MUUNGWANA. Tatizo ninaloliona hapa ni pale mtu anapoamua kubonyea na kuzania eti watu watasahau baada ya muda LA HASHA Watanzania wa leo sio wa miaka ya 60 – 90 wamebadilika sana kifikra na hata kiutendaji.

  Hoja ya Nyakatakule ni muhimu sana hapa.

 20. Ed Says:

  Kuna kitu kinaitwa Jurisdiction katika sheria, uwezo wa kumshataki mtu katika circuit fulani ya mahakama. Balali is not Tanzanian citizen, so there is no jurisdiction while he is not in Tanzania. Hizi kelelee kelele hazisaidii kitu, JK and another cheaters knows what they real doing.

  Poor Tanzania, 2008 resolution ni kukana Uraia wa Tanzania na kuchukua wa nchi yoyote

 21. kijiwe Says:

  Jamani ee hebu tuachane na hii issue ya huyu jamaa maana no matter what we can say or think huyu jamaa hawamrudishi ng’o unless serikali ya kijeshi inashika madaraka(which sioni kama itatokea karne hii).hivi jamani mmesahau majita aliongelea about FREE masons?
  hao watu hawaguswi ni kama laana fulani hivi the only way to deal with this issue is to clean clean clean the rotten system otherwise ni mambo ya santana kumpigia mee gitaa!

 22. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  Mama wa kichaga asante sana. Hata nawe umenikuna vilivyo maana maneno yako ni ya kishujaa sawa na yale ya Esta alipomkabili Mfalme ingawa haikuwa wakati (zamu) yake na akaliokoa Taifa la Israel.
  Unajua watu wengi tunafikiri kuwa siku zote kukiri kosa ni kitu kisichotakiwa kabisa maishani au kwamba ni kushindwa kabisa. Hili si kweli maana kinyume chake ndio kweli.

  Akina Mama wana uwezo mkubwa katika ku-‘influence ‘ maamuzi ya akina Baba na kinyumeche pia. Pengine ni vema tufikirie mkakati wa namna akina mama walio karibu na Mrs. Balali wamshauri ili kufikia uamuzi huu wa busara tunaoupendekeza hapa.

  BC asante kwa kutufungulia ukurasa huu. Mama wa Kichaga Unafaa sana, nimekukubali kwa hoja na msimamo wako pia!

 23. Papin Says:

  Ufisadi wa nchi wa namna alivyofanya huyu bwana Balali unahitaji adhabu kali ikiwezekana ya KIFO manake mijihela hiyo yote aliyoitia hasara ni watanzania wangapi wameendelea kufa kutokana na huduma mbovu za afya ambapo hiyo mipesa ingeweza kwa njia moja au nyingine kudumisha miundombinu ya afya. Wale wote waliohusika ni lazima wawajibishwe kisheria ikiwa pamoja na kufilisiwa mali zao,kuchapwa viboko mbele ya hadhara na kufungwa maisha.

 24. shally Says:

  naona kosa la balal ni kubwa kuliko la nguza viking hivi kama walibaka kwa staili hii balal katubaka tena mbele ya wakwe zetu

 25. Kekue Says:

  Someni gazeti la THIS DAY la jana!!! ni kuhusu hili sakata la Dalali!!

  Jamani hivi mmesikia huyu anaeitwa Johnson? (Yuko kwenye orodha ya kina balali) can u imagine ndo mwenye tender ya kusupply magari haya ya fire Tanzania nzima na ni kwamba kila msafara wa raisi huyu jamaa humkosi yani ni mtu ambaye anajuana na raisi kabisa, ni mtu na hela yake, uliza ana miaka mingapi tobaaa!!!!! sasa tusubiri Dalali aletwe nchini nyooo tutakesha na kuandika maoni huku kwa BC!!!!!

  Kuna mwengine yeye kaagiza Range Rover new model unajua ni sh. ngapi? bei yenyewe ya Vogue ni kasheshe bado kuileta tena kwa ndege!!! hela za wajinga si zipo kuna shida gani? wathubutu kwenda kumkamata, na sio kwamba hawamjui wanamjua fika!!!! Yani ni bora hata hizo pesa walizochukua wangejenga mashule yao tukapeleka watoto na mahospital au wangewekeza katika magari ya abiria haya makubwa wakasaidi hata hii adha ya usafiri hapa kwa Kandoro!!! kuliko kuzitumia namna hii!! I fell to understand!! Ngoja nikale zangu niachane na kuumiza kichwa changu wakati hata Balali hawajui yuko wapi though kalazwa na anaendelea vzr ss sijui wanajuaje km anaendelea vzr kwi kwi kwiiiii!!! hivi ni kwanini wanatufanya hatuna akili kabisa Y?????? Kwa niniiiiii! Waendeleeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!! mama wa kichaga shimbony????? Ebu BC fanya mpango haya maoni yetu utafute gazeti ambalo litaandika atleast kwa wiki mara 2 labda yanaweza kufika kwa walengwa manake ni wasomaji wazuri tu wa magazeti!!!

 26. Upendo Furaha Says:

  Ni kweli Balali amefanya kosa ambalo linaonekana.
  Hebu tujiulize sisi wenyewe kuwa ni makosa mangapi tunafanya ambayo hayaonekani na hakuna mtu aneyetuhukumu???
  Kuna msemo mmoja unasema hivi: – “Ukiona mwenzako ananyolewa, …….”
  Tujiangalie sisi wenyewe kwanza kabla hatujaanza kutupa lawama za kila aina kwa Balali maana: “Hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe”.
  Naomba kuwasilisha.

 27. shally Says:

  ina maana hakuna aliyenunuliwa rav 4 na muheshimiwa vicky kamata nani kakuingiza bot???????????????????????
  lipeni fadhila pamekucha sasa

 28. Mkata Issue Says:

  Nani anauliza kuhusu la Vick Kamata kuwa BOT?
  Sijawahi kufeli hisabati toka nilipokanyaga unyayo wangu Nyasho P/S!

  BOT inazungumza juu ya MAENDELEO hivyo;
  1. BOT= MAENDELEO;
  Vicky kaimba, AKINAMAMA na MAENDELEO hivyo pia
  2. AKINAMAMA = MAENDELEO; Relating and Replacing MAENDELEO, unapata
  3.BOT = AKINAMAMA
  Na kwa vile Vicky ni subset ya AKINA MAMA (wanaovutia), hivyo

  4. Vicky ni subset (inayovutia) ya BOT

  QED

 29. Dullah Says:

  Empty leader, empty profile, empty head fisadi!

 30. Mama wa Kichagga Says:

  KEKUE,

  NASHICHA BANA – KYEEDU KIUUMU! Asante kwa salamu!.

  Kekue wacha watu wanunue magari usiwe na wivi usiokuwa na sababu maana kwa kuwa na magari watalipa kodi, watapeleka garage, watanunua mafuta n.k angalau kuongeza na kufanya mzunguko wa hela uendelee kuliko walimbikizaji wasiotumia wa hela! Pia gari ni bidhaa muhimu kila mmoja wetu anaihitaji kuwa nayo hata mimi ningekuwa na Range ningefurahi sana – Moshi masaa 5 tuu!

  Leo naomba niyaelekeze majeshi yangu ya maombi mbele ya Mungu ili yeye alete msaada wa haraka katika kuwezesha viongozi na watanzania wote kwa ujumla:

  1. Kuijua na kuitenda haki katika ngazi zote za utendaji hasa mahakama, makazini, maeneo yanayotoa huduma (HAKI ITALIOKOA TAIFA)

  2. Kuwa na uchungu wa maisha ya kila Mtanzania na hasa wale wanaohitaji zaidi (Vijijini, wamama, watoto, na wasiojiweza) – KWA KUFANYA MATUMIZI YA FEDHA NA MALI ZA UMMA KTK MISINGI YA MAADILI

  3. Kumuweka Mungu kama kiongizo ktk utendaji wetu wa kazi ili haya majanga ya rushwa, kunyanyapaa (makazini, maeneo ya huduma nk), umaskini, maradthi na ujinga – TAIFA LIWEZE KUENDELEA (HILI LINAHITAJI MAFUNGO NA ALBADIR TENA IANZIE BUNGE LIJALO)

  4. Kuwapa viongozi wote na waongozwaji ufahamu wa kutambua mema na mabaya na kutenda yaliyo mema tuu na pia kuwakumbusha daima KUWA HAPA DUNIANI NI KITUO CHA DALADALA (TENA KITUO KISICHO RASMI – UKIPAKI VIBAYA FINE) MAANA SAA NA WAKATI WOWOTE WAWEZA KUTOWEKA.

  5. AWAPE UFAHAMU NA UWEZO WANAWAKE WENYE NAFASI ZA JUU ZA UONGOZI AMA MOJA KWA MOJA AMA KUPITIA NASAFI ZA WAUME ZAO – KUTENDA MEMA MAANA AMA KWA HAKIKA WAO WANAWEZA KUWA CHACHU KUBWA SANA YA KULIOKOA TAIFA LETU. Wakisimama wanawake watatu tuu (nasema 3) wenye nafasi za juu kwa moyo na utashi – uchungu wa maisha ya wanaohitaji zaidi katika jamii naamini taifa linauwezekano wa kubadilika katika kipindi kifupi sana na kuondokana na maadui wetu wa maendeleo (ujinga, marazi, umaskini, afya duni nk).

  Nawapa changamoto hawa kinamama wasijisahau wakawekeza ktk mavazi na utambulisho (mimi ni mama fulani, mimi dr, mimi sijui nini nk) wakasahau wanao wajibu mkubwa kwa jamii na taifa lao na wafahamu wazi kuwa WANALO DENI KUBWA LA KULIPA MBELE YA MUNGU KWA NAFASI WALIZOPEWA – “WALIZIFANYIA NINI WALIPOKUWA DUNIANI? SWALI LA KUJIBU MIAKA 50 IJAYO” MAANA WOTE TUTAKUWA TUMESHAFARIKI WAKATI HUO”.

  KUMBUKENI NA SOMENI HABARI ZA WANAWAKE WENGI WA ZAMA ZA MWANZO WALIOTUMIKA KUYAOKOA JAMII/MATAIFA YAO AMA FAMILIA ZAO KWA KUSIMAMIA HAKI (MFANO: Esta, Abgal/Abigaeli, Hillary Clinton na wengine wengi).

  Kama hamna sera za msingi basi msiogope kuwatumia/kuwashirikisha wanawake/kinamama wenye uwezo katika sekta mbalimbali katika kutekeleza chachu ya maendeleo!

  NB: Navutwa kuamini kuwa wanawake wa KITANZANIA HATUJASIMAMIA NAFASI ZETU VIZURI HASA KATIKA KUENDELEZA TAIFA LETU! HEBU TUWE KITU KIMOJA, FAMILIA MOJA TULIOKOE HILI TAIFA LETU! HEBU RAIS JARIBU KUTEUA WAZIRI MKUU MWANAMKE HATA KAMA NI NAIBU TUONE PENGINE ITABADILISHE MWELEKEO WA MAENDELEO MAANA TANGU 1961 (MIAKA 45 YA UHURU) JAMANI HATUJAFAA TUU! JE, URAIS JE?

  “JAMII YENYE MAENDELEO YA JUU KATIKA HISTORIA YA KUUMBWA KWA ULIMWENGU HUU NI ILE INAYOTHAMINI MICHANGO YA WANAWAKE KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAENDELEO/UTENDAJI”

 31. amina Says:

  he vicky kamata mpakanjia yupo BOT?Makubwa haya kuongea vizuri kwenyewe hajui

 32. Matty Says:

  Mama wa Kichaga na Kekuu shimboni!!!!!!te te te te te !! hata kama sikijui ila nimejisikia na mimi kuwapa hi ya kimila si unajua tena! watani wangu wa jadi, safi sana mama wa kichaga unatoa point zilizoiva inabidi wanawake tuamke na tuwe mfano kwa jamii sio kujilimbikizia mali kama mkewe balali migodi anaimiliki yeye tu!!!!!!.
  He Amina makubwa Vicky Kamata mpakaway???kivipi???nae inamaana yupo BOT??? nishachoka kama mastaff wenyewe ndo hao!!!!!!

 33. John. Says:

  Balali and his WAJANJA like Sarah Martin Simbaulanga used their brain and pen to steal while Kasusura and his Crime mates used their muscles to steal but they are all thieves and they need harsh punishment.Suprising enough Kasusura,Simbaulanga etc was ransacked throught the world and brought to justice while Balali is still enjoying life in unknown hiding under the pretext of being sick.This country has Discrimination even on suspected thief……While kibaka who grabed up wrist watch or even cell phone worth less than 50,000/= is brought up to Mob Justice and they send him quickly to the grave yard but Balali who stole Bilions together with his Colleagues are Still enjoying at Posh residence…what a shame of justice in this world!
  Stambuli

 34. Mama wa Kichagga Says:

  Mimi kusikia Vicky Kamata yuko BOT (kama ni kweli) hainipi tabu hata kidogo maana binafsi naichukulia kama changamoto ya maendeleo.

  Kitu kimoja tunapaswa kukielewa ni kwamba maendeleo ni mkusanyiko wa shughuli ndogo ndogo nyingi sana kama vile: mhudumu wa ofisi, dereva, katibu muhtasi(secretary), wasaidizi, wafanya usafi, wataalamu wa chini, kati, na waandamizi, uongozi na kiongozi mkuu – “GAVANA”, mfanyabiashara, mkulima, dalali nk nk.

  Kwa harakaharaka hapa lazima Vicky atakuwa katika kundi mojawapo la utendaji hapo BOT. Tusimnyanyapae isipokuwa kama hana kundi la kiutendaji kati ya hayo hapo ndio tuanze kuhoji ???? Vinginevyo nampa hongera kwa ajira yake mpya na ajitahidi kutoa mchango wake mahali alipo kwa uaminifu na WENGINE TUWACHE WIVU NA FIKRA POTOFU KWA JAMII.

  Tuwe tayari hata kufanya kazi serikalini na watu wa mataifa mbalimbali ili tuweze kupata changamoto za maendeleo kutoka kwao na tuawache fikra kuwa “watu fulani tuu ndio wanafaa/takiwa hapa” au ni thithithiii tu NO hatutaendelea.

  Angalia mataifa yaliyoendelea zaidi au yaliyopo ktk ulimwengu wa pili wa maendeleo – kazi zinafanywa na mtu yeyote multi-skilled & multicultural bila kujali kabila, dini wala uraia wa mfanyakazi, au taifa linakuwa na mipango ya kuwasomesha kwa makusudi wananchi wake kwenye mataifa makubwa ili kupata ujuzi unaokusudiwa na kuongeza changamoto za maendeleo.

  Mfano mzuri ni Botswana, Namibia, na Afrika ya Kusini wakikuona hata kwa kusikia unaujuzi wanaouhitaji basi watakutafuta na watakuajiri kwa gharama yeyote utakayohitaji ili kuendeleza nchi yao – angalia madaktari na wataalamu wetu wengi wameishia huko kutafuta matawi ya juu maana nyumbani miti imekauka na hakuna sera muafaka.

  Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa sana la manesi kuajiriwa nchi za nje kutoka hapa TZ wakati hospitali, zahanati, na vituo vyetu vya afya vikiendelea kukumbwa na uhaba wa wataalamu hao kila kukicha. Hapa mimi nazani tupitie na kuangalia upya sera zetu za ajira na zinginezo ili kukidhi mahitaji ya jamii.

  “FOR ME VICKY TO BE AN EMPLOYEE OF BOT IS OK – IT DOES NOT HARM ANYTHING” LET US STOP BEING TOO JELOUS & JUDGEMENTAL

  I WISH TO SEE BRAVE MEN AND INDEPENDENT WOMEN IN TZ”

 35. Kekue Says:

  Mama wa kichaga mimi sina wivu, ila ni jinsi hawa watu wanavyotumia hela za wananchi kwa kufanya mambo ya ajabu badala ya kusaidia wananchi!! Umenipata ??? Kwani Balali alivyotoa hela kwa watu wakafungua makampuni si ajira zilitoka sasa tunawaonea wivu kwa kufungua makampuni??? au serikali inavyosema hao watu watafutwe wawajibishwe ni kwamba wanawaonea wivu kwa kufungua makampuni wakati wananchi walipata ajira????!!!

  nawakilisha!!!

 36. trii Says:

  huyu na wengine wengi serikalini ndo wanao kula hela za watz na kufanya kuwe na tofauti kubwa kati ya maskini na matajiri,tena BOT na serikali hebu walipeni wazazi wetu hela zao za EAST AFRICA COMMUNITY wamefanya kazi miaka kibao alafu mnawazurumu hivi hivi.hela mnazibania benki hadi wajanja wanajigawia kwa kulipa madeni hewa.

 37. mdunger Says:

  Balali ni sampuli ya mafisadi wa nchi hii!Mimi pia nashangaa kwa nini hajakamatwa,lakini sishangai kwani sijawahi sikia fisadi wengine wamekamatwa na kushitakiwa,hivyo na uhakika Balali nae hatakamatwa la kama wananchi tunaweza kumsaka,kumkimbiza na kumhukumu(kama tunavyowakimbiza vibaka mitaani).

 38. msema kweli Says:

  Mbona nilidhani huyu mama wa kichaga anatoa mada za mana! sasa hapo kekue ana wivu gani kusema hao wabadhirifu wa hela mmoja kanunua vogu na kaleta kwa ndege na ni kwamba katumia pesa wa wananchi!! He!! mama taratibu!!! kwa hiyo Balali mali alizonazo tunamwonea wivu?? I fell to understand what is mama wa kichaga talking about!! Aya ndo BC maoni mbali mbali!!

 39. Mama wa Kichagga Says:

  Kyekue na Msemakweli,

  Asanteni kwa hoja zenu na ukosoaji.

  Nawaomba msome vizuri mada yangu hapo juu jibu lipo – Chuki sitaki toeni hoja za kuleta muafaka au pendekezeni njia mbadala.

  Kama hoja yangu imewauzi shauri zenu maana mie siangalii kwani tuna mitizamo na peo tofauti katika kuona na kupambanua mambo/vitu.

  Haya leteni sera/mapendekezo yenu nini kifanyike na kivipi? Pia hutakiwi kumzania mtu kuwa anatoaga mada za maana badala yake uwe unasoma hoja anazotoa kama ni za msingi au la bila kusahau kuna ubinadamu pia. Kama ukigundua zina mgogoro basi changia kwa hoja ili kuisaidia jamii hasira na maneno ya mkato mkato hayatatufikisha popote.

  Mimi issue ya Balali nilishaichoka na ndio maana sitaki kuiandika andika kila saa maana sheria tayari inachukua mkondo wake hivyo naona kuendelea kuitaja kunanipotezea muda/nguvu yangu (ni mimi sio nyie – waweza kuendelea). Pia tusisahau mfumo mzima wa ufisadi ni uozo mtupu! Pengine uchunguzi wa kina ukifanyika na sisi wengine tunaojiona wasafi hapa tupo ndani yake! La msingi watu wabadilike na waelekee kulijenga taifa na sio vinginevyo!

  Kuhusu Vicky wala sitamtaja tena hapa maana sioni kama kuna hoja ya nguvu hapa ukizingatia yeye sio muhusika mkuu katika mada hii tunayoiongelea – tumechomekea tuu kama mtu anayeulizwa swali la mtihani 1+2 = ? anaanza unajua 30-27 +7 _7 +0 _2+2 inaweza kuwa ndio jibu au labda 57-4 nk. Hapa maana yangu ni kwamba tunatafuta majibu kutoka mbali mno wakati jibu liko moja kwa moja.

  Vinginevyo kama mnafahamu kuwa mchakato wa ajira yake ulikuwa na mizengwe, basi muvuzisha hapa kama mada tuichore (comment) kwa ujumla wake maana issue za ajira za kinyemela sizani kama ni BOT tu hili ni tatizo la mfumo uliopo (kuna za kikabila, ndugu, kimaliwazo/wapendwa wetu, kidini, kichuki, kieneo, za 10% nk) ambazo zote ni chukizo kwa jamii!

 40. Mama wa Kichagga Says:

  Trii,

  Samahani ndugu yangu mimi huwa sili haramu nakula kalamu! Swala la EAC hata mie linanigusa moja kwa moja maana MAREHEMU BABA YANGU naye ni muathirika katika malipo hayo na kwa kuwa hakuwa hai wakati tunafuatilia haki ya baba (ambapo alifanyia kazi maisha yake yote) tuliambulia 175,000/= gawanya kwa wanawake 2 (mama zangu) na watoto wa marehemu 13 na wajukuu 21!

  NDUGU SIJAWAHI KUIBA HATA PENSELI SHULENI, SIIBI SASA HIVI NA “SITAKAA NIIBE KATIKA MAISHA YANGU” – MUNGU WANGU NDIYE SHAHIDI NA HAKIMU WANGU.

 41. Mama wa Kichagga Says:

  SIMPLE MINDS = DISCUSS PEOPLE

  BIG MINDS = DISCUSS ISSUES

 42. kijiwe Says:

  jamani kwa nini msiende kugomania ubunge maana you are taking this issue too far halafu sioni hata kama itakuwa na positive output maana BC kauchuna.Tehe tehe!

 43. shukrani Says:

  mimi naona balali wamwache tu mzee wa watu kajizeekea japo billione.hakuna kuhukumiwa balali sababu nimechoka na maigizo ya nchi hi.
  mmemwandama balali je mzee dito aliyemsambaratisha dereva yameishia wapiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
  acheni upuuzi huo
  kinachotakiwa tufanye kama kenya tu kila mtu achukue rungu lake tuingie barabarani mimi nimechoka na maigizo ya wakubwa nataka maigizo ya akina kanumba na akina joketi.
  haya ya benki kuu tuchapane mabomu ,mapanga then tutaheshimiana.
  mimi sina hata kiatu pesa yangu yote balali katimka nayo.watu

 44. nifer Says:

  Yaani nimesoma maoni yote hadi nachanganyikiwa!, roho inaniuma, kichwa kinanizunguka, yaani sipati picha.
  Ukweli utafikia wakati tutawaiga watani wetu wa jadi, kila mtu panga mkononi tukachinjaneeee kama wendawazimu.

  Ukimya wa watanzania utakuja kuwatokea puani hawa mahayawani tunaowapa madaraka alafu wanatung’ong’a!
  OLE wenu mafisadi ipo siku jua la mbingu ltawashukia.

  Ila na nyie watoa mada wengine mnaniudhi, kinachowafanya muache kuzungumzia mada iliyopo mezani na kuanza kupondana na kukashfiana ni nini?

  Au na nyie ndio hao hao wanaokula uji wa mgonjwa?

  BC tafadhali tafuta mahali pa kuandika hayo maoni (yenye maana) kwenye gazeti lolote hata la mzee wa tindikali (mwanahalisi) kwenye barua za wasomaji watasoma tu na ujumbe utawafikia

  Kazi njema

 45. Stidia Says:

  Balali anatembelewa na Mkuu wa usalama wa taifa huko hospitalini USA!!. Ilishatokea kwa kiongozi yupi akalazwa hospitali ya nje, Mkuu wa usalama akamtembelea? Tunaelezwa kivivu na kufikiri kivivu!!. Naam huyo akamweleze Luhanjo alikolazwa Balali. Mh Zakia Meghji kudanganywa na wasaidizi wake hakujaanzia hazina, kulianzia Maliasili na Utalii, si alitoa agizo la kusitisha usafirshaji magogo nje likakwama, baadae ikagundulika Makampuni yasafirshayo magogo ni ya wakurugenzi wake, hama yake mwenyewe.

  Ni nini kitamzuia asiendelee kudanganywa kwa utaratibu huo, Kikwete anajua udhaifu wa huyu mama, Huyu mama inatosha kesha tuvulia nguo bado kumvua bosi wake!! Hivi Tanzania nzima Rais amekosa akina mama wengine wa kuchukua nafasi yake, mbona wenye uwezo wengi?

  Wananchi wametulia tuli!!, Wanahabari pia!! Rais Kama ni Kitete kumfukuza Zakhia,Mramba na Mgonja, alazimishwe kuwaondoa.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s