BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

“MR.HANDSOME” January, 14, 2008

Filed under: Burudani,Filamu/Movie,Muziki,Sinema — bongocelebrity @ 12:10 PM

 

MWANAMUZIKI nyota wa muziki wa kizazi kipya, Banana Ally Zorro(pichani), baada ya kutesa vilivyo katika anga la muziki hivi karibuni anatarajiwa kuibuka kivingine katika filamu mpya ya ‘Kibongo’ inayokwenda kwa jina la ‘Mr. Handsome’, imefahamika. Habari zaidi bonyeza hapa.

Advertisements
 

35 Responses to ““MR.HANDSOME””

 1. Edwin Ndaki Says:

  Kila la kheri kaka ..endeleza kipaji.

  Tupo pamoJAH…

 2. Nerra Says:

  Yaani Banana unatisha!! Endeleza kipaji na please endelea kujiheshimu na kuheshimu ndoa yako hivyohivyo yaani nakufagilia mpaka nasikia kulia but God will show you the way……….. tunazidi kukuombea!

 3. Kajura Hamisi Says:

  WaTZ bwana..sasa huyu yanki ana kipaji gani? Hakuna msanii yeyote wa Bngo Fleva aliyena kipaji, tusibishae bila saababu.

 4. amina Says:

  ma filamu ya kibongo michosho

 5. shally Says:

  kuimba wewe,movie wewe,ndoa wewe,
  mmh kwa vichwa vya kibongo hamna kitu hapo.

 6. shally Says:

  kwa hiyo umeamua kuuza sura baba kazana wewe ndoa changa hiyo umeshaanza mr handsome kichwa chako kina akili kweli wewe badala ukae kwanza na mkeo mjadili family mpya au mlikuwaga mnakaa pamoja kwa hiyo umefanya kupasha kiporo dizaini unaonyesha umeshamzoea punguza pepe umeshasahau ulikuwa famous bachelour unajifanya umezoeaga unachemsha dogo.

 7. shally Says:

  ngoja ukakutane na kina johari wa ray,na mainda wa max, na nora wa ngwizukulu uone mambo wako bush wale wanahunt hata kenge.

 8. Matty Says:

  Ana Kipaji lakini hizo nywele kwanini usiziache kawaida kuliko kupaka marelaxaz au bila hiyo mikogo sauti haitoki???umeoa punguza madoido kichwani bwana.

 9. Kekue Says:

  Huyu kijana anaimba vizuri sana mwe!! unajua mtu anapofanya kitu kizuri jamani msifieni heee!!!! sema tu apunguze make-up!!!! sasa ni kichwa cha familia!!!! Lakini ana kipaji na banana endelea, ALL DA BEST BANANA and your kiburudisho pamoja na yule mtoto wako!!!

 10. Any Says:

  Watanzania bwana! sasa kijana wa watu kakosa nini mpaka mnamshambulia kwa maneno? Hiyo ndio diversification! kuamua kufanya shughuli mbali mbali za kiuchumi wala si ajabu anaweza kucheza sinema, akaimba, akauza kahawa, akalima chochote kile anachoona kinaweza kumuingizia kipato ili mradi havunji sheria za nchi!

  Halafu mambo mengine kuhusu maisha yake na ndoa yake its none of our business! Who are we to instuct him what to do and what not to do anyway?!! Haya mambo ya kutaka kujua mambo ya ndani ya maisha ya watu ndiyo yamewafikisha wasanii na watu wengine wanaojiita maarufu mahali pabaya wala mtu asiniambie eti kwa kuwa msanii ni kioo cha jamii basi ndio muwe na haki ya kujua ashakum si matusi mpaka nguo yake ya ndani aliyovaa!!

  Tumenogewa na udaku mpaka basi lol! give these people a break and not a mental breakdown!!

 11. Edwin Ndaki Says:

  Nimekusoma…Any…nimependa mchango wako….

  Kula kumi m2 wangu..pamoJAH

 12. queen Says:

  mchangiaji hapo juu umesema kweli hata mimi nimeshangazwa na maneno yaliyokuwa yakimtoka huyo jamaa sijui ni wivu binafsi au kamtupa nnje! huwezi kumsema mtu ukaingilia hadi maisha yake na kumpangia nini cha kufanya,kwani wewe ni Mungu? kila mtu anafanya kile anachopanga mwenyewe na akili yake, kila mtu anahaki ya kujiamulia kukaa au kuvaa chochote anachoona anakipenda na kinamfaa katika hii dunia mradi havunji sheria. sasa wewe unakerwa na huyu kijana eti atulie na ndoa,ooh kapasha kiporo, hata kama sio shughuli yako kumrekebisha ana uhuru wake.Mwache handsome boy ni mzuri kwa mama na baba yake na kwa mkewe wewe ulie tuu.Ringa mwanangu nakufagilia japo hunijui sikujui ila siwapendi watu wenye viroho vya wivu.

 13. Mama wa Kichagga Says:

  Watanzania tubadilike muda unatutupa mgongo ndugu zanguni!

  Mimi sioni sababu ya kujadili watu na maisha yao ya binafsi, mavazi, malazi, hobby ili mradi yale yote unayoweza kuyaona ni ya binasi katika mtizamo hasi (negative visions).

  LETS STOP BE JUDGEMENTAL TO OUR PEOPLE.

  Binafsi mie siipendi tabia za kusema sema wengine na kuwabeza kwa muonekano wao kwani ni mbaya sana.

  Tabia hii mara nyingi inatokana na ufinyu wa akili ya mtu. Ukiona wewe mara zote unapenda kujadili wenzio vibaya kwa ajili ya wivu wa kijinga jinga au wee kila mtu unamkosoa huna la kusifia ujue fika unatatizo la ufinyu wa akili ama ubongo wako unahitaji marekebisho kidogo.

  Kumbuka wenzetu walishafanyia haya mambo utafiti na kugundua kwamba “SIMPLE MINDS DISCUSS PEOPLE”. Tubadilike na tuondokane na huu ujinga. Unajua umaskini upo wa aina nyingi sana: MAWAZO/FIKRA, CHAKULA, KIPATO NK. Ukiangalia kwa undani utagundua kwamba umaskini wa MAWAZO unachangia umaskini wa aina nyingine na ni wa kiwango cha juu.

  Sioni sababu ya maneno yote machafu hapo juu kwani kijana ameamua kuisha anavyotaka yeye na anavyojua inampa raha yake binafsi sasa wewe na “KAFIKRA” kako finyu unaanza kupepeta oooooooooooooooooooo eeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, WACHENI TAFAZALINI. Nyie ndo wale watu wakionawapendanao mnaanzisha zogo “MWANAMKE KAMKALIA”! Sasa kama kamkalia wewe hutaki inakuhusu? Je akimlalia itakuwaje?

  TUACHE UJINGA NA TUJIFUNZE KU-WAKUBALI WATU KAMA WALIVYO NA WATAKAVYO SIO KAMA TUTAKAVYO SISI.

  YEYE ANAPENDA NYWELE YAKE AWEKE RELAXER FINE, WEWE HUPENDI USIWEKE ZAKO!

  NI LINI TUTAJIFUNZA KUHESHIMU UHURU WA MTU BINAFSI JAMANI?

  WHERE ARE BRAVE MEN AND INDEPENDENT WOMEN?

  WAPENDWA TUELIMIKE NA TUACHE UJINGA WA KUWAKWAZA WENZETU KWA MAWAZO, KWA MANENO NA KWA VITENDO.

  BANANA LIVE YOUR LIFE TO THE FULLEST! RELAXER IKIISHA WEKA KALI KAMA NI CHAGUA LAKO VINGINEVYO FANYA RE-TOUCH UKIONA VIPI NYWELE ZINAKATIKA NYOA ZIKUE UPYA KISHA WEKA RELAXER!

  TUMEZIDI HADI TUNATIA KINYAAA

  PLEASE ENJOY YOUR LIFE!

 14. Lucy Says:

  Mi nakubaliana na wachangiaji wa mwisho… unajua watu wengine wao kwa vile ni ‘danda’ head hawawezi fanya mambo mengi kwa wakati mmoja basi wanadhani kila mtu hawezi… mfano ukikuta anaendesha basi hata kuongea hawezi… ukikuta anaongea na simu basi hata kuandika hawezi… ukikuta yeye ni administrative officer basi hata computer hataki kujifunza kuitumia kitaalamu zaidi (kwa kutumia programs mbalimbali) zaidi ya kuchapa kawaida (kwa kutumia word process) hawezi kufanya vitu vya field ingine kama budgeting/planning, evaluation nk. Siku hizi hata makazini employers wanataka mtu mwenye ujuzi wa aina nyingi (multiskilled)… we ukikalia profession yako ya aina moja hutaki kujua mambo mengine basi utabaki lofa tu… watu watakupita na wanakuwa exposed na mambo mengi unabaki unashangaa. Ukiwa multiskilled unajipa avenues/opportunities nyingi zaidi… Sasa kama Banana anaweza ni vizuri zaidi kwa sababu ukiwa msanii kuna siku utazeeka kitu kimoja kisikusaidie sana katika kujikimu kimaisha… Akiweza kufanya mambo yote hayo na hata akaamua kuinvest ni poa tu. Hao watu wanaompiga madongo wana walakini katika kufikiria… Kwa wanaomfahamu Tyra Banks ni presenter, anahost talk show, ni model, ni mwimbaji, ni actress hayo ni machache nayoyakumbuka kwa sababu nilisoma documentary yake zamani kidogo. sasa kuna madhara gani kama mtanzania anajaribu fields mbalimbali? watu muache wivu… ila sishangai kwa watanzania… mtu unapojaribu kukwea juu watu lazima wajaribu kukushusha kwa sababu ya viwivu visivyo na maana… Hata private life yake sisi haituhusu. Anavyomanage nyumba yake baada ya ndoa we waitakia nini? kama ni nywele mkewe huyo kayajua hayo hata kabla hajaolewa so she was prepared! sisi wa pembeni ndio vinatukunaaa! ah! please leave him alone…

 15. twin Says:

  Huyo anayejiita Shally ana lake jambo, huo ni wivu na chuki binafsi inaelekea alimtaka akatolewa nje! Sijui huyo Shally ni mwanamke au mwanaume vyovyote vile wivu sio dawa mamaaa, mwache Suzy Walele Banana ajili vyake kwa raha zake. We ulie tu!!!

 16. Nerra Says:

  Nawaunga mkono Any na Queen kwa nguvu sana huyu anayejiita Shally sijui ni mwanamke au Mwanaume lakini sijawai kuona mtu wa ajabu kama wewe! Ebu rudia kusoma hiyo michango yako kwa Banana alafu uone wewe ni mtu wa namna gani! Jaribu kuwapa moyo vijana tafadhali wivu mwingine ni wa kitoto!

 17. mme wangu Says:

  He!! Makubwa!!! sasa mnasema hakuna haja ya kumuinstruct what to do sijui nini.. sasa hii picha imewekwa hapo ya nini si kila mtu anatoa ushauri wake kulingana na anavyomuona huyu Mr. Handsome!!!

  Sasa mbona wakati alivyofunga harusi picha yake ilitolewa na watu wakawa wanamshauri, wanampongeza nk, basi BC asiweke picha ya mtu hapa!!! acha watu wamshauri bwana He!!!!! Hapa ni full kujiachia, kila mtu aseme the way anavyojisikia!!!

 18. BongoSamurai Says:

  Mama wa kichagga, pamoja na wachangiaji wengine wenye mawazo chanya, nawaunga mkono 100%, ni kweli wengi wetu hatuna hulka ya kumsifia au kumpongeza mtu anapojaribu kufanya jambo lenye kuleta tija maishani zaidi ya kumponda na kumkatisha tamaa…,hapa tulipo ndio matokeo ya ufinyu wa fikra zetu….!
  Kila la kheri Banana maisha ni kujaribu, bila kujaribu hakuna kufanikiwa…

 19. punani Says:

  Bongo kuna wanamuziki watano tu wa kizazi kipya ambao muziki wao utadumu mpaka uzeeni.Banana ni mmoja wao anasauti nzuri sana ya kuzaliwa sio ya kulazimisha na ni ya kurithi. kufanya mambo mengine ni utashi wake kama atafanya vizuri ni juu yake. Kama mnaolalamikia nywele zake mna ujuzi mzuri wa mitindo hiyo picha ni ya zamani sasa hivi ana dreads huwezi kufumua dreads uweke dawa nywele ni lazima utazikata ikiwa zimefikia urefu aliokuwa nao banana na zimesha Lock. Shally wewe lazma ulipigwa buti ndio maana unakijiba. angakuwa sio msanii mzuri kweli ningekuamini lakini kwa huyu hizo ni chuki binafsi. Suzy kapenda ua na boga lake waacheni muendelee na maisha yenu yaliyo bora(kama mnayo basi)

 20. nusrat Says:

  banana(mr handsome) endelea na mambo yako achana na hao wakosaji, hayo yote ni maneno ya mkosaji tu, mijitu mingine wivu tu unawasambua. banana fanya unachojisikia kufanya, imba, act, na chochote unachotaka kufanya hayo ni maamuzi yako wewe mwenyewe ili mradi tu humtukani mtu. wewe nI bonge la star unatisha mdogo wangu, wakimbize kwa sanaaaaaa, na mwenye wivu ajinyonge!!! KEEP IT UP!!!

 21. any Says:

  Acha ajichie kudadeki! ata akivaa WIGI poa tu. next time weka weaving kabisa.

 22. Nerra Says:

  MMe wangu sikiliza kama umeelewa vizuri sio kwamba watu wasimwongoze ni nini cha kufanya hapana, ila ni jinsi watu lugha wanazotumia kucritisize mfano “unauza sura tu wewe!” au “bongo hakuna muziki usituletee michosho!” n.k unataka kusema huo ni mwongozo utakaomsaidia msanii wa kitanzania? amemsaidia nini hapo kama sio maneno ya chuki na wivu tujitahidi kuwa makini na wastarabu kwa faida ya vizazi vijavyo kama tutaweza.

 23. amina Says:

  jamani mi sina la kusema nacheka tu hata kumshauri banana nashindwa nitashushuliwa….hangi mwaya

 24. mmy Says:

  Ndio kaka kaza buti Hongera sana kwa kujituma.
  Achana na uyo shally asikuumize kichwa siku azigandi
  i wish u all the best in you life

  Mmy

 25. Kekue Says:

  Amina usiogope kusema kile unachojisikia shosti!!!! Wewe sema wakikushushua is up to wao!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 26. amina Says:

  we nerra kazi yako kujifanya unawapa moyo vijana tu hata kule kwa ali choki umejifanya umenikosoa kama ulivomkosoa mwenzio hapa..mi kwa banana sina tatizo kabsa ila toa comments zako tuone za maana usiandikeandike tu na kushushua wenzako kwani hapa lango la jiji kwenye tarabu?wewe toa comments zako kwa banana kaa kimya siyo uingilie visivyokuhusu

 27. amina Says:

  we nerra unajifanya yesu kristo eeeh

 28. unknown Says:

  Kwa kwei Banana ni Handsome.mbona mnakuwa hivyo?after all,beauty lies in the eyes of the beholder. hao wanaoropokwa hapo juu ni wapuuzi.hivyo vi-gal /boy friends vyao vikoje???? hebu wekeni sura zao hapo tuwachambue.hata wengine wenu hamuwezi thubutu kutuma picha zenu kwenye blog hii.

  Mwacheni mtoto wa watu afanye mambo yake na Mungu atambariki.Kazi kwenu waosha vinywa

 29. janet Says:

  wewe shally mbona usiimbe au kuigiza kama unaona ni rahisi? acha wivu, aoe aimbe aigize vinakukera nini au ulitaka akuoe wewe? too late anampenda suzzy wake! watanzania WIVU ACHENI!! banana imba hata taarabu kama unaweza usiskilize maneno ya wanafki mbona wao hawafanyi unachofanya wewe mpaka wajidai kukuchambua ivyo? kuwa na amani na mkeo suzzy kwanza mmependezana mno! na wewe amina acha mdomo, ivi ni yupi uliewahi kumsifia? kila mwanamziki wewe humtaki imba wewe basi wivu tu huoni aibu

 30. Nerra Says:

  Thanks Amina kwa kuniita yesu kristu kwani natamani siku moja ningefanana na yesu kwani ndio tegemeo langu la maisha yangu, na pia pole kwa kukukera lakini naamini ujumbe unakuingia ndio maana unajibu kwa jazba pooole. MSG SENT!

 31. braza du! Says:

  acheni kuponda washkaji, mcheza kwao hutunzwa bwana eeh! Hebu mtunzeni basi acheni kuropoka kama wehu! BANANA Kip it ap mai frendi, achana nao wasiopenda maendeleo ya mtu

 32. annabell Says:

  macelebrity wote wanafatwafatwa sijui watu wengine mnalalamika nn! l just wish him all the best to do what he thinks he can do it better…..lakini bado nasubiri manewz yake tele tele na macelebrety wengine pia!!!!!!!hii blog iendelee…cheeerzzzz

 33. Hellen Says:

  do u know u r my favourite artist in Tz or mayb dawhole East Africa?????am so proud of u n pliz kip it up ok….lea familia yako vizuri coz u have married such a pretty wife(Suzzy) n i wish u ol da best…….every gal in tz wud wish 2 have u my dia…..

 34. liz Says:

  mhhh kazi kweli kweli

 35. zaina seif Says:

  Hey handsome! Big up, wanaochonga wache wa chonge wewe songa mbele mchumba. au sio? kila la kheri Banana


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s