BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

TUMUITE NANI? January, 17, 2008

Filed under: Siasa,Swali kwa Jamii,Tanzania/Zanzibar,Wanawake na Watoto — bongocelebrity @ 12:06 AM

 

Mke wa Raisi huwa tunamuita First Lady au kwa tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi Mama wa Kwanza. Je, mke wa Waziri Mkuu,kama alivyo mke wa Waziri Mkuu wetu,Mama Regina Lowassa(pichani) tutamuitaje au tunatakiwa tumuite nani?Msaada tafadhali.

Advertisements
 

38 Responses to “TUMUITE NANI?”

 1. Kim ramsay Says:

  kwanza ni vizuri kuwaenzi wake wa viongozi wetu.Nafikiri kwamba mke wa raisi angeitwa mama kiongozi na mke wa waziri mkuu akaitwa mama kiongozi waziri au!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 2. Matty Says:

  Mh!!!!swali gumu lakini mama mzuri anaonekana mpole hata watoto wakikosea home hawachapi!!!!!!!!!

 3. Edwin Ndaki Says:

  Samahani naenda nje ya mtundiko tafadhali.

  BC ….kuna habari iliyovunjika mbona hamjatupa.

  Dr.Balali afutiwa visa yake ya kumuwezesha kuishi Usa.

  Ebu tafuteni tumwagieni hiyo nyuzi.

 4. twin Says:

  Sijui tumuite nani kwa kweli, ila huyu mama nampenda na namfagilia sana .Kwanza anapenda elimu na ana masters ya maendeleo ya jamii na uchumi kama sikosei. Big up mama!!

 5. KionaMbali Says:

  Huyo ni THIRD LADY, kwa kuwa “second lady” ni mke wa Makamu wa Rais
  Nawasilisha

 6. Zzz Says:

  Naaah,in a country that has a President AND a Prime Minister,the Prime Minister’s wife will only be known as-‘the Prime Ministers wife’,since the said wife does not have any whatsoever executive,judicial,or legislative powers.

 7. Msukuma wa shy Says:

  Mama wa pili

 8. Rodney Says:

  Mama wa Tatu (Kionambali, 2008)

 9. Upendo Furaha Says:

  Aitwe: “Mke wa Waziri mkuu”. Kwa kimombo “PM’s Wife”. Maana hata kama Waziri mkuu ni Mwanamama, Mumewe ataitwa Mume wa Waziri Mkuu.
  Naomba niulize Swali:
  (a) kama mke wa Rais anaitwa “First Lady” Je nchini Liberia Mume wa Rais anaitwa nani?
  (b) Kule Uingereza Mume wa Malkia haitwi “King” bali anaitwa “Prince”; Je, ni kwanini?
  Nawasilisha.

 10. Mtanzania Says:

  Haya mambo ya kuita mke wa Rais “First Lady” ya Ki-Amerika. Watanzania hatuna jina kwa mke wa Rais, lakini kama kawaida yetu tunajaribu kuiga kila kitu hata kama hakina maana katika mfumo wetu wa maisha na mendeleo yetu ya kijamii. Sikumbuki kusikia Mama Maria Nyerere akiitwa First Lady! Why now all over the sudden we call Mrs Kikwete First Lady? Let’s stop this! It adds nothing to her responsibility as the wife of a President, nor diminish her.

 11. Kaka Yenu Says:

  Upendo Furaha(Jan 17,2008 at 1:07pm posting) (1) Mume wa Rais Mwanamke (as in Liberia example you gave) ataitwa “Fist Gentleman”. (2)In your UK question, kuna ufafanuzi ufuatao: Tawala za kifalme zina “vyeo” viwili vikubwa: King (kama mwanaume) au Queen (kama mwanamke) , fuatilia hii: Mtawala falme za UK (UK Monarchy) wa leo wa ni mwanamke, ndio maana anaitwa”Queen” (na mumewe ataitwa ‘Prince’ kwa sababu yeye siye mtawala/kiongozi wa Falme/monarch NA amezaliwa kutoka kwenye familia zingine zenye uhusiano wa kifamle–vilevile huitwa “the Duke of…”). Mkuu wa falme za UK kwa sasa na Queen Elizabeth II. Mwanae mkubwa ndio wa kumrithi, ikitokea ni wa kiume ataitwa King (baada ya kurithi madaraka) ama Queen (na kuuvua u-princess kama ni wa kike). As is now, Prince Charles ndio next inline tayari kumrithi mama yake. Normally two condition has to happen for him to take over, (i) Queen Elizabeth II akifariki (ii) Queen akionekana amezeeka mno/mgonjwa kiasi cha kutoweza kuendelea kuendesha monarchy. Endelea kujielimisha kwa kutembelea toviti ya falme hii at http://www.royal.gov.uk/ Naomba kuwakilisha

 12. Kekue Says:

  Aitwe tu Regina Lowasa, Hicho kitenge/Bazee sio hela za walipa kodi?? mmh!! na mimi mchokozi!!!!! au kile cha Salma tu ndo kilikuwa cha hela za walipa kodi?? coz alishambuliwa hapa bc palikuwa hapatoshi. Tehe tehe!!!!!!!!!!!!!!!!

 13. amina Says:

  mtanzania bravo..mi sina cha kuchangia

 14. Upendo Furaha Says:

  Asante ndugu yetu na mdau mwenzetu wa B.C. “Kaka Yenu” kwa kutoa ufafanuzi wa suala la “First Lady” , “First Gentleman” , Queen, Prince na King. Kazi njema.

 15. Mama wa Kichagga Says:

  BC,

  Ni kweli kabisa alivyosema “Kaka yetu”, mwanaume anaitwa “First Gentleman” kama alivyo yule wa nchini Liberia na wengineo duniani waliobahatika na bahati hiyo.

  Kwa kuwa mfumo wetu wa utawala ni ule tulioachiwa baada ya uhuru ni sawa kabisa Kaka alivyochangia. Hatuwezi kusema tunaiga bila utaratibu hadi hapa tutakapoamua kuubadili mfumo mzima ambapo itakuwa kazi kubwa kuunda na kuujaribisha mfumo ambao haujafanyiwa kazi.

  Ukiangalia taarifa hapa kwenye mtandao (kiambatanishi chini) Utapata taarifa muhimu sana kuhusiana na hili na pia utayaona mataifa mbalimbali ambayo yamewahikuwa na viongozi wanawake katika nafasi za juu kitaifa, Urais au Waziri Mkuu. NB: TZ bado hatumo kwenye orodha maana wanawake wetu bado hatujaamuakuwapa nafasi ama tunawahofia sijui, ila muda ni hakimu siku moja itakuwa. Sasa endelea na mitandao hapa chini:-

  http://www.oph.gov.au/mrspm/

  http://www.filibustercartoons.com/charts_rest_female-leaders.php

  NB: Naomba Mungu mwaka 2010 angalau TZ tumpate rais mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi yetu tukikosa basi ANGALAU TUAMBULIE WAZIRI MKUU – Italeta changamoto nzuri sana ya maendeleo kwa wakati huu na vizazi vijavyo na pia itatuwezesha kuingia kwenye vitabu na kumbukumbu za dunia kama mtandao unavyoonyesha hapo juu.

  Hainiingii akilini tunapoimba wimbo wa “TZ ni nchi ya “AMANI AMANIIII “HAKI HAKIAAAA”, “USAWA USAWAAAA” NK wakati ktk historia ya TZ hatujawahi kuwa na mwanawake hata mmoja ktk uongozi wa juu. Au wimbo huu hii ni kwa jinsia moja tuu (wimbo dume?)?

  Ni muda wa kubadilika kifikra na kimtizamo na kutenda yale tunayoyahubiri kwa vitendo hata mambo ya rushwa na ufisadi naamini yangepungua kama sio kuisha kabisa maana hadi ung’ang’aniza kukwida “11 figures” itakuwa kazi, yaani 1 ongezea sifuri 11! hahahaaaaaaaa sicheki nalia INGAWA ZOTE NI KELELE

 16. Matty Says:

  Kekuu unanikumbusha kuhusu mavazi ya mafirst lady sijui ma 3rd lady wakati wanakula hela za walipa kodi na kuifilisi BOT yetu, sipendi uchokozi na wewe!!!!!!!!kwi kwi kwi ….hajaona nini maana huwa ni mkereketwa nambari 1.samahani kama niko out of topic.

 17. Upendo Furaha Says:

  BC,
  Mama wa Kichagga, Asante sana kwa mtandao unaoonyesha Maraisi, Mawaziri wakuu, na Mawaziri wa mambo ya nje wanawake duniani (isipokuwa hawakuonyesha nchi zinazoendelea kwenye upande wa mawaziri wa mambo ya nje maana tungemuona M-Tz mwenzetu Dr. Asha Rose Migiro).
  Ni vyema na haki kuwa na Rais mwanamke maana wanawake nao ni viongozi wazuri kama wanaume. Lakini jambo la kumuomba Mungu ili Tz impate Rais mwanamke mwaka 2010 sio sawa (mimi sikubaliani nalo), maana Ikimpendeza Mungu akimjalia maisha JK bado atakuwa ana kipindi kingine cha miaka mitano kwa mujibu wa katiba.
  Mimi na wewe tumuombe Mungu Tz ipate Rais Mwanamke itakapofika 2015.
  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika; Mungu wabariki Walimwengu.
  Nawasilisha.

 18. Mama wa Kichagga Says:

  Upendo Furaha,

  Uko sawa nilipitiwa kuandika (nilimaanisha 2015 sasa nikajisahau nikaandika 2010) maana kimsingi miaka 5 ya mwanzo huwa ni ya kujifunza mipangilio ya ofisi, kukamilisha mikakati iliyotangulia, kupanga, kupangua na kuweka mikakati mipya, nk na miaka 5 inayofuata ndio unafanya utekelezaji. Uko sawa kabisa ndugu yangu.

  Ila ikiwezekana kama mwanya upo sio mbaya maana sio kwamba wanawake wataendelea kuongoza kwa miaka 46 ijayo (hahaha kama wanaume walivyoanza 46 ya mwanzo) isipokuwa tunachohitaji ni changamoto kutoka kwenye jinsia zote mbili (Me/Ke) maana hii moja imeshafanyakazi peke yake ,uda mrefu (ngazi za juu) huenda mchanganyiko wa jinsia ya upande wa pili ikaleta changamoto kubwa katika maendeleo kwa ujumla. Angalau Rais Me na waziri mkuu Ke hii haishindikani.

  Mimi mwenyewe nilishangaa KWANINI DR. ASHA-ROSE MIGIRO hayupo ktk taarifa hizi, nikaanza kujiuliza huenda pengine hatujawasilisha taarifa zetu au sijui nini maana kama ni kuhusiana na nchi zinazoendelea mbona rais wa Liberia yumo kwenye orodha?

  WAHUSIKA WAKIBAHATIKA KUONA HUU UJUMBE NADHANI WATAUFANYIA KAZI.

 19. kijiwe Says:

  Habari zenu wana BC. Naomba kutoa maoni yangu kuhusu hii mada

  Kuhusu suala la kuitwa First Lady,Mama wa kwanza,au whatever name you may tag her has got nothing to do with kuoga wamarekani or whatever.Hivi wewe(Mtanzania in particular) ulisoma Sekondari kwa kiswahili?Je ulisoma chuo kikuu kwa kiswahili pia?kama ni ndiyo basi nakuheshimu na sitotaka kuendelea lakini nina uhakika asilimia 90 kuwa kama umeenda shule ipasavyo umetumia kiingereza,umejifunza mambo mengi ya kijamii na kiuchumi kwa kiingereza na ulikuwa unavaa nguo na siyo majani ya migomba!
  Tuache unafiki kuhusu mambo ya first lady au whatever you can call it maana hiyo siyo issue kubwa katika matatizo yanayotukabili as Tanzanians maana ukisisitiza hii issue then acha kuiga kila kitu basi halafu uende ukakae Mikumi national park au serengeti.Hivi hujui kuwa ukoloni ndiyo umefanya mambo yawe kama yalivyo sasa hivi?mbona wachina wameendelea sana na wame chinalize kila kitu lakini bado wana mambo kibao wanaiga from western countries.It is because they know what time it is – IF YOU CAN’T BEAT THEM JOIN THEM!
  Kumaind vitu vidogo kama majina ya wake za marais au waziri mkuu inaonyesha CHUKI BINAFSI which will not take you anywhere.I mean really what has vitenge na majina got to do with maendeleo yetu?
  Hivi ukiambiwa kuwa huyo mama angeweza kuafford pamba hata kama asingekuwa na Lowassa ungesemaje?Because amesoma so probably angekuwa na uwezo at least wa kuafford kitenge.
  Narudia tena
  racial,gender descrimination(mama wa kichaga),chuki binafsi na wivu(matty,kekue,mtanzania)
  will not help by any means kutupeleka one step up will only increase the height of our ditch.hehehe
  msimaind lakini hii ni opinion yangu shoot back as much as you wish!

 20. frank Says:

  du! tusiwe na tabia ya ku linganisha mambo na kufanya yaendane mke wa waziri mkuu atabaki kuwa ka anavyoitwa,hawezi itwa vinginevyo.

 21. frank Says:

  jamani eeeeeee swala la kushitakiwa kwa balali ni tata sana yule bwana zile hela hawezi kuwa katumia yeye kwa majambazi wenye nyazifa kubwa tuu ndo sasa wana haha make jamaa yaliyomo kichwani mwake ni mengi,chonde chonde jamani .. tusikulupuke,afu wanao anza kugawana mali zake jamani tuwe makini.

 22. sponge bob squire pants Says:

  upendo furaha, nafikiri mme wa queen anaitwa DUKE, sina hakika, watoto ndio ma prince pamoja na wake zao. Not sure abt waume zao

 23. Upendo Furaha Says:

  Du! Mdau Kijiwe, naona umechambua ilivyo mwanawani. Big-Up.

 24. Matty Says:

  Kijiwe nakusahihisha sehemu moja pls usituweke katika kundi uliloweka pale juu sisi hatuumii na wake za mawaziri/prezidaaa mapedezee kuulamba wanaoumia labda umewasahau hebu rudia ile picha ya tarehe. 10 Dec 2007 inayomuonyesha first lady uone ni akina nani wana ubaguzi na chuki binafsi.
  Huo ujumbe wangu hapo juu kwa Kekuu labda hukuuelewa kwa walioelewa wameishia kucheka tu, mimi nataka wanawake na maendeleo ikiwa ni pamoja na kupiga pamba kwa kwenda mbele pale hela inaporuhusu!!!!!

 25. jay Says:

  aitwe “SECOND LADY”

 26. kijiwe Says:

  kumradhi Matty I got it , nakupa 5 🙂

 27. Kasule Guselya Says:

  Mke wa Rais anaitwa First kwa sababu mme wake kiitifaki anitwa VIP no.1. hivyo mke wa Waziri mkuu ataitwa 3rd Lady kwa sababu mme wake ni VIP no. 3.Hayo ni mambo ya kiitifaki:

  VIP NO 1Rais
  vip no 2Makamu wa Rais
  VIP NO. 3 Waziri Mkuu.
  VIP NO.4 speaker wa Bunge.

 28. Mama wa Kichagga Says:

  KIJIWE

  MIMI HOJA YANGU IMELENGA ZAIDI KWENYE GENDER DISCRIMINATION NA KIMSINGI HILI SIO SIO SWALA LA KUFUMBIWA MACHO DUNIANI WALA TANZANIA KWA WAKATI HUU WA CHANGAMOTO ZA MAENDELEO! HILI NI TATIZO LILILOTOKANA KUTOKA MUDA MREFU KUFUATIA SERA ZA MIFUMO DUME ZILIZOKUWEPO/ZILIZOPO ULIMWENGUNI. HAYA TUYAONAYO HIVI SASA NI MADHARA YA MIFUMO HUSIKA.

  HILI NI JAMBO LINALOHITAJI KUFANYIWA KAZI KUBWA TZ NA NAMSHUKURU RAIS WA AWAMU YA NNE INALIPA KIPAUMBELE SUALA HILI KWANI LINAONEKANA NA HALIKWEPEKI KATIKA KARNE HII.

  http://www.nbs.go.tz/TZ_FIGURES/TZ_FIG_2006.pdf

  NB: ANGALIA UKURASA WA 6 WA TAARIFA HII – HUTAACHA KUKUBALIANA NA HOJA YANGU HAPO JUU UKISHINDWA BASI JUA TUKO TOFAUTI KIMTIZAMO NA HIYO NI SAWA TUU. NASISITIZA HOJA YANGU NI YA MSINGI.

 29. Matty Says:

  Ok,Kijiwe hii ishu imenichosha hebu twende kwenye ishu ya leo.

 30. kijiwe Says:

  MAMA WA KICHAGA
  nadhani hatuelewani kwa sana tuuu.mimi nimedokeza kuwa hayo mambo ya descrimination na nini offcourse ni lazima yazungumziwe ila kusema kuwa kila hoja inayoanzishwa humu ndani uitranslate ki “Gender” inanifanya nikufikirie vingine.I mean kama mtu kila wakati wa kuongelea different issues unasisitiza issue ya gender unakuwa unazidi kujidiscriminate mwenyewe its like mtoto anayesisitiza kuwa apewe candy wakati anajua fika kuwa candy anapewaga kila mara ila wakati wanataka kumpa biskuti yeye bado anasisitiza kuwa nakumbushia kuhusu candy.
  samahani kama hatuelewani ila point yangu ni kwamba ndiyo tunakubali kuwa wanawake wanatakiwa kupewa haki sawa na wanaume na najua kuwa huu ni mfumo mzuri sana maana nimeuona ukifanya kazi kinoma.nilipokuwa botswana most of the heavy weights katika kila kona sa system yao ni wanawake ukianzia mawaziri mpaka gavana wa benki.
  most of my former professors walionifundisha uni walikuwa wanawake.huku sweden kila kona katika system heavy weights ni wanawake.mimi na wife wangu tunagawana majukumu sawasawa except kumyonyesha mtoto 🙂
  so kwa kweli nakubaliana na wewe kuhusu hili swala la gender ila nakupinga ukiwa unabring it up all over again coz ina end up sounding like feminism which i dont think there is anything wrong with it but haisaidii in reality katika maendeleo ya bongo.kumbuka togather(whether female,male,boy or girl)TUNAWAKILISHA au siyo

 31. Roya Says:

  Inategemea Waziri Mkuu atakua nani, kama anaitwa Lowasa basi tumuite mke wa Lowasa, WM alipokua Sumayi aliitwa mke wa Sumayi.

  Tusijiongezee vyeo ambavyo havipo!

  Mbona sio mke wa Makamu wa Rais?
  Baadae itakuwa hadi mke wa Gavana wa BOT tumwiteje.

 32. shani nassoro ndege Says:

  mie napendekeza aitwe mama afrika inatosha .

 33. Mama wa Kichagga Says:

  Kijiwe,

  Mambo? Nimekupata na umejibu vema ila sijakuelewa FEMINISM NI NINI? NIFAFANUNULIE NA IONDOE KWENYE HOJA YANGU MAANA SIIJUI

  OK MAN!

 34. Duke Says:

  Kwa kweli bado tunachanganya mambo,na hasa kutokana na kuiga yasiyo tamaduni zetu,Tukiangalia kiuwajibikaji!kuna viongozi wa kike wanawajibika kushinda uyo first lady,na wa hazi ya kupewa jina hilo.MARIA NYERERE mbona hakuitwa jina hilo?Tuache ulimbukeni jamani.REGINA ni msomi pili ni mwajibikaji nzuri sana,Sina jina la kumpa ila naomba WAANDISHI WA HABARI wafikili kabla ya kukiandika kitu chochote maana jamii inajifunza mengi kutoka kwAO.

 35. kijiwe Says:

  Mama wa Kichaga
  mambo yanakwendaje. mi naona tuachie hii topic hapa as long as tunaelewana au siyo. feminisim ni kutetea maslahi sawa for wanawake

  feminism – A doctrine that advocates equal rights for women
  or the movement aimed at equal rights for women

  tupo pamoja mtani 🙂

 36. johnnie Says:

  Ooh? tabasamu hili kama mimi ndoo mwanae aah shule siendi ntashibaa busara tu. Mii na ona tumwite MAAMDOGOO au mnabongajeeee?

 37. Jane Says:

  nawapa big up sana yote yanawezekana kwa majadiliano..

  cha msingi hebu tuangalie hili la ufisadi wa RICHMOND hatimaye lowasa kujiudhuli..

 38. Jane Says:

  tujadili na hili


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s