BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MIZIKI YA MJI WA MOROGORO January, 18, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Haya tena,ni siku yetu nyingine ya kuendeleza jadi. Wikiendi ndio inabisha hodi.Wakati wa familia,wakati wa kuburudika.Leo tunarudi tena mkoani Morogoro,mkoa ambao una sifa ya kipekee linapokuja suala la muziki hususani “Zilizopendwa”.Sina uhakika kama Morogoro bado kuna sifa hiyo hivi leo.

Sasa,ni wazi kabisa kwamba sio rahisi ukaongelea mji wa Morogoro na muziki wake bila kumtaja Hayati Mbaraka Mwinshehe.Ukifanya hivyo itakuwia vigumu kueleweka.Shauri yako.Kwa kuzingatia hilo,burudani yetu ya leo inatoka kwa si mwingine bali Mbaraka Mwinshehe na kundi zima la Moro Jazz Band.Wimbo unaitwa Miziki ya Mji wa Morogoro.Pata burudani.Ijumaa Njema.

Advertisements
 

5 Responses to “MIZIKI YA MJI WA MOROGORO”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Pumzika kwa amani.

  Hakika kwenye kuushika huo mpini nakupa mia mzee wangu.

  Pamoja na tungo nyingi maridhawa …

 2. Mdau Says:

  Wimbo haujamalizika huu unacheza kwa 15seconds only ebu fanya mambo tupate flavor ya ijumaa maana ndio mambo ya weekend haya…full kujiachia

 3. Mangapwani Says:

  BC,yaani mimi mnanikosha sana na hizi oldies za kwetu.You have no idea how much I enjoy these stuffs.Endeleeni hivyo hivyo.

  Mdau,mbona wimbo mimi nimeupata full kabisa.Maana mpaka zile nga…nga…ngaaaaaa..za mwisho.Si unajua tena miziki yetu ya kale.Sio siku hizi miziki inaisha kama vile umeme umekatika ghafla.

 4. Upendo Furaha Says:

  B.C. Big-up. Mnatuburudisha sana wadau wa Blog hii.
  Endeleeni kutupa viburudisho ambavyo hata vilipokuwa vinaimbwa wengine (kama mimi) tulikuwa hatujazaliwa, lakini ni vizuri na vinatangaza U-Tanzania wetu vilivyo.
  Ninawatakieni kila la heri katika kutuhudumia “Waswahili” wenzenu.
  Ukweli nyimbo za huyu “Mzee wa Moro Jazz” nikizisikia, zinanikonga roho (moyo) sana.
  Nyimbo hii ya “Mziki wa Mji wa Morogoro” kwa wanaousikiliza kwa makini una mafundisho mazuri sana ya “Watu wanaoingia hata makazini (kama wakubwa fulani) wanabadili mwelekeo wa sehemu ile na wanaanza kuingiza maslahi yao; Watu kama hao ndio Marehemu Mubaraka Mwishehe Mwaruka anawaita “Wachafuzi”.
  Nchini kwetu Tanzania kuna “Wachafuzi” kuanzia ngazi ya Serilali za Mitaa hadi Serikali kuu (kwa Mawaziri). Isipokuwa katika Ngazi ya Wilaya, ndio inanuka kabisa, maana baadhi ya Wakurugenzi wanapenda kuingiza maslahi yao, Mkurugenzi kama hana elimu ya juu akiona mkuu wake wa Idara au mfanyakazi mwingine anataka kwenda kusoma elimu inayozidi ya kwake anamkatalia, wakurugenzi wengine wanapenda wao ndio wawe ndio wasomi zaidi wilayani. “Je tutafika”
  Ninawashauri Wakurugenzi wa Wilaya zote nchini waangalie mfano wa Rais wetu (JK), Amezungukwa na Mawaziri ambao ni Maprofesa na Madaktari wa falsafa; Rais wetu anajua kuwa wasomi ndio nguzo ya maendeleo kwa karne hii ya sayansi na teknologia.
  Samahanini kwa kutoka kidogo nje ya Mada.
  Mungu Ibariki Tanzania; Mungu Ibariki Afrika; Mungu wabariki Walimwengu.
  Nawasilisha.

 5. tonny Says:

  Hivi kweli hapa Bongo hatuna MaProducers ambao wanaweza kutengeneza DVD Documentary ya Mbaraka Mwinshehe na Muziki wake wote toka alipokuwa Morogoro Jazz hadi Super Volcano hata ikibidi kwa kuwatumia baadhi ya Wanamuziki aliokuwa nao ambao bado wangali hai na kwa kutumia Nyimbo zilezile zilizo rekodiwa na Radio Tanzania na nyinginezo alizorekodia Kenya?What the hell are you waiting for?Mpaka watu wa nje watupige bao hata kwa hili?Lets be serious.Watoto zetu na vizazi vijavyo vina haki ya kuelimishwa kuhusu Wasanii mashuhuri kama Mbaraka walioliletea sifa kubwa Taifa letu katika fani ya muziki wa dansi.R.I.P. Maestro Soloist National Mbaraka Mwaruka Mwinshehe.Bado unatuliza kwa tungo zako mahiri na nyuzi mithili ya Franco Wa Makiadi Luanzo Lwambo.Kitoko mwana mboka!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s