BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

TAARABU NA MIPASHO,KITU KIMOJA? January, 19, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Swali kwa Jamii,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:10 AM

 

Bi.Sabbah Muchacho(pichani-on focus)ni mmojawapo miongoni mwa waimbaji wa taarabu au muziki wa mwambao walio maarufu sana katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Ni mmojawapo kati ya waimbaji mahiri ambao kundi maarufu la East African Melody linajivunia.Hivi kuna aina ngapi za muziki wa pwani? Je taarabu na mipasho ni kitu kimoja? Kama unaufahamu kuhusu hili tafadhali saidia kuelimisha jamii.

Wakati huo huo bonyeza hapa ili kupata burudani kutoka East African Melody katika wimbo wao Hamtuwashi.

Picha kwa hisani ya Issa Michuzi.

Advertisements
 

16 Responses to “TAARABU NA MIPASHO,KITU KIMOJA?”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Duu!mambo ya vidole juu.

  Hapa ufahamu wangu ni mdogo sana.

  Ninachokumbuka tu tuliwahi kuwa waimbaji bora kama Sitti Binti Saad na hayo ni kwa mujibu wa marehemu Shaaban Robert.

  Mwingine ni b Kidude,ila hawa wengine hama hakika sifahamu wanaimba aina gani ya taarabu.

 2. Matty Says:

  Haya sasa huyu nae anavaa kulingana na umbo lake madodo yote nje why??kwa mtu mzima du!!!!!au kitambaa kilikuwa kidogo/fasheni/madoido??sijui Kiona mbali umeshamuona??? Taarabu ni zile asili ambapo waimbaji wanaimba huku wamekaa na mipasho ni modern taarabu ambapo wanaimba huku wakicheza/kutamba na vidole juu!!!!!!! kwa ufahamu wangu jamani.

 3. Upendo Furaha Says:

  Wadau “Kekue” na “Mama wa Kichaga” mmelumbana sana kwa Stara Thomas; Je kwa huyu Sabbaha Muchacho, ambaye “Hayavaa blauzi” mnasemaje.
  Mungu tusaidie Wanaume.

 4. KionaMbali Says:

  Tehe teh tee!
  We Matty naona unataka kuanzisha topiki nyingine sasa.
  Na huyu nae naona anavaa kulingana na umbile lake pia.
  Tehe teh tee.
  Taarabu nayo ina evolutions zake kama mambo mengine yoyoyte yale kwa hiyo hata hiyo staili yao ya sasa ndio mambo yaevolusheni za taarabu hizo.
  yote sawa tu. Hamna noma wala nini.

 5. Mama wa Kichagga Says:

  Upendo,

  Mimi kwakweli sio mtaalamu sana wa mambo wa taarabu ingawa mara kwa mara nakumbana nazo kwenye mashughuli. Kwa ujumla mie nikisikia mdundo unaopendeza kama wa “Utajiju” japo sielewi maana yake nafurahi tuu.

  Kuhusu mavazi yake mi naona hilo ni chaguo la mtu binafsi anavyojisikia na kwangu ni sawa tuu maana mavazi kwangu hayana nafasi katika suala zima la maendeleo.

  Kuhusu wewe kuona sehemu ya mwili wa Ke na kuanza kufadhaika sielewi nisemeje maana naona kama vile utakuwa na katatizo na ushirikiano wako wa akili na kuona (Psychological Problem).

  Sasa kila kitu ukionacho ukitaka kukila si itakuwa tabu ndugu yangu? Jifunze kuona bila kula, tembelea maeneo ya fukwe zetu na maeneo ya michezo ili uzoee kuwaona wanawake miili yao. Baada ya muda utazoea tuu ndugu yangu na ukiona tena wala hutatizama mara mbili kwani utaona ni kawaida.

  Jichanganye zaidi na watu wa jinsia zote ili kuwa na uzoefu. Kwa sisi tuliopita jeshini (Me na Ke) ukichunguza hatuna hayo matatizo maana wote tulikuwa tukivaa vibukta/vichupi muda wote tukazoeana na hakuna ubakaji uliowahi kuripotiwa kutokana na mavazi. (Mara nyingi shule za jinsia moya ya Ke au Me huwa na adhari za kisaikolojia kama hii).

  JIFUNZE KUUZUIA MWILI NA MAWAZO YAKO YASIELEKEE KWENYE MRENGO WA KUSHOTO

 6. Upendo Furaha Says:

  Mama wa Kichagga,
  Nikisoma mada zilizopita (hasa ya Stara Thomas) inaonekana kuwa unafahamu maandiko matakatifu (hasa Biblia).
  Je unajua kwamba imeandikwa “Wanawake wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, ….? (1Tim 3:9).
  Umenishauri sana niende bichi kuangalia bukta, na vichupi ili niyaone haya mambo kuwa ni ya kawaida. Na pia umesema kuwa ninyi mliopitia jeshini mlikuwa mnaacha mapaja nje na hakuna uliyesikia amebakwa. Sawa ninakubaliana nawe. Lakini unaona kuwa kwa maumbile ya kike ni vyema mwanamke akaye maziwa au mapaja au sehemu zake nyingine zinazosisimua wanaume ziwe nje ???
  Mie ninawasifu sana wenzetu wenye asili ya kisomali huwa wanasema kuwa: “Mwili wote wa Mwanamke ni Uchi” Je hili nalo unasemaje?
  Mama wa kichaga, ukiwa unafurahia uumbaji wa Mungu, pia angalia na utafakuri yafuatayo:
  (1) Kati ya wanyama wote wanaoonekana kwa macho yetu (akiwemo mwanadamu) ni kwa nini Wanawake wa Kibinadamu ndio wazuri, lakini wanyama wengine ni Wanaume wazuri? Na hao wanyama wengine, wanawake ndio wanafuata wanaume na sio wanaume wanafuata wanawake kama tulivyo wanadamu?
  (2) Ni kwa nini Vitabu vyote “Vitakatifu” vinakazia Mwanamke kuvaa mavazi ya kujisitiri?
  (3) Hivi “Mtengeneza sumu” ya kuua na “Mnywa sumu” ili afe, ni nani mwenye kosa kubwa?

 7. Nai Says:

  Taarab hakuna tafauti yeyote sema taara ya sasa ni mipasho juu ya mipashooooooooooooo

  Mipasho- vidole juuuuuuu wambia watu “Talijua jiji bisho” ” usohaya ujioni uso umekuparama” ” Taal Taratibu ma mdogo eti unarusha roho wamrusha roho nani” and sooo on. Hizi sasa ukisikiliza we utachanganyikiwa na kurusha madongo kwa wenzio. Mangumi ndo yatembeayoooooo

 8. Kekue Says:

  Sichezi mbali na Matty, Taarabu unatulia lakini mipasho mwanangu lazima ujizungushe kidogo he! namna hiii eee weeeee!!!Pendo sitaki uchokozi!!!!!!! Matty siku hizi hakuna watu wazima na watoto yani tunatoka droo na kama vipi watu wazima wanatuzidi!! manake du!! lakini kalipuka aaa kama noma na iwe noma!!!!!

 9. Kemmy Says:

  Dini zipo lakini hatuzioni,Kama kusingekuwa na dini kila mtu angevaa anavyotaka hata ukitembe uchi hamna wa kukuuliza.
  Ukifatilia vitabu vya dini vinaongelea mwanamke ajipambe lakini si kwa mtindo huu wa kuacha maziwa nje no!!!!!!!
  Huyu ni mzanzibari halisi mchana anavaa ninja style na baibui huwezi kumjua usiku iz like above style.
  Jamani acheni mungu aitwe mungu, vinginevyo mavazi yatawamaliza wanaume kwa tamaa, huyo mama kama anamume na mumewe anamruhusu avae hivyo na atoke du!!!!kazi kweli kweli!!!!!!nawakilisha wamama!!!!

 10. Matty Says:

  Kekuu ni kweli kalipuka ila mimi nilizani fundi kakosea mshono au kitambaa hakikutosha te te te te!!!! aliyempa kitambaa ndo kamchagulia huo mshono!!!!!

 11. lily Says:

  mnaozungumzia hiyo nguo ni washamba, cha msingi imevaliwa wapi ,saa ngapi na kwenye function ipi . Thats all.Mimi sioni kama huyu kavaa vibaya sana .BC next time tuletee fashion za nguo tuzijzdili.

 12. Kekue Says:

  Lily kula tano !!!!!!!!!!!!!!!!!!

 13. linda Says:

  Lily hakuna mshamba hapa upo!!!!!!!kila mtu anamtazamo wake ndo maana wewe ukaitwa lily na mie ………..

 14. Upendo Furaha Amani Says:

  Lily;
  Kwa kiswahili sanifu, Mshamba ni mtu yeyote asiyejua kitu fulani. Hata wewe ni Mshamba wa vitu ninavyovijua nawe huvijui. Kwa mfano mimi ninajua kutengeneza bomu la Nyuklia, na ninajua asilimia mia kuwa wewe hujui hivyo wewe ni Mshamba.
  Lakini kuhusu nguo aliyoivaa Bi.Sabbah Muchacho, inaonekana wewe unaiona kuwa ni mtindo wa nguo. Lakini kumbuka maziwa ya mwanamke ni kati ya “Nyeti” za binadamu, kama unaona ni vyema uache maziwa yako nje kama huyo Bi.Sabbah Muchacho, basi endelea bali ujue kuwa Unajidhalilisha mwenyewe na unadhalilisha utu wa Mwanamke.

  Linda: endelea na kuielimisha jamii dada yangu.

  Nawasilisha.

 15. Linda Says:

  Lily, imagine wewe ni mwanaume halafu mkeo anatoka out (anaenda rusha roho)na nguo ambayo inaonyesha maziwa nje utafurahi???lazima tujisitiri hasa wanawake kwani ukivaa nguo ambayo haionyeshi maziwa unapungukiwa nini???
  Upendo furaha amani ni hayo tu dada yako nawakilisha!!!!!

 16. Mukubwa Says:

  NI KWELI MMEONGEA MENGI SANA KUHUSU NGUO NA TAARABU.LAKINI MNACHO SAHAU NI KWAMBA, MNAONGELEA MAADILI SEHEM AMBAYO SIYO YA MAADILI.KWENYE TAARAB HAKUNA HESHIMA NDO MAANA MTU HUWEZI KWENDA NA MKWE WAKO.
  SAWASAWA TU SABAH KUVAA NGUO YAKO.KWA SABABU KWENYE TAARAB HAKUNA USTAARAB.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s