BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 03 January, 20, 2008

Filed under: Photography/Picha,Swali kwa Jamii,Watu na Matukio,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:10 AM

 

Picha ya leo ilipigwa na mwanablog mashuhuri, Maggid Mjengwa, pale Mtaa wa Jamhuri jijini Dar-es-salaam wakati wa majira ya Xmas mwaka jana(huu tulioumaliza majuzi). Kama inavyoonyesha, jamaa yupo kazini akipaka rangi kwenye hilo jengo/ghorofa katika mazingira ya kazi ambayo ni hatari sana! Itazame picha kwa makini uone ni mambo mangapi ya kiusalama wa binadamu yamekiukwa.Nani wa kulaumiwa katika hili? Ni jamaa,mwajiri wake au serikali?

Hii ndio picha yetu ya wiki hii.

Picha kwa hisani ya Maggid Mjengwa.

Advertisements
 

13 Responses to “PICHA YA WIKI # 03”

 1. benjamin Says:

  Hii ni hatari sana,
  Viongozi wa nchi hii wanakaria kula pesa zitu wanaacha kushugulikia mambo muhimu yanayoweza kupoteza maisha ya watu.

 2. Edwin Ndaki Says:

  Amana hakika hii picha inatia uzuni na uchungu sana.

  Naamini huyo kaka anajua kabisa hatari au dhahama inayoweza kumkuta.Lakini kutoka na hali ngumu ya maisha anajikuta hana jinsi inabidi atumie kamba yake na hiyo miti kutengeneza ngazi.

  Hapo unakuta kapewa tender ya kufanya hiyo kazi na hana vifaa.Unafikiri bank gani inaweza kumdhamini aweze kununua vitendea kazi wakati anatokea kwenye familia kama za kwetu sisi wakina Edo Ndaki za daraja la chini.

  Akifikiri anahitaji kulipa kodi ya nyumba,chakula,watoto waende shule.Anaona potelea mbali bora kufa natafuta riziki yangu kihalali.Hata tukimlaua tunakuwa tunakosea.

  Yanayo mkuta huyu fundi ndio yanayowakuta pia MADEREVA wa mabasi.Anaweza kuona gari lina matatizo aua matairi “vipara” akimwambia bosi wake.Jibu analopewa kama hawezi kuendesha gari basi aachei kazi anapewa mwingine.

  Hakika serikali na wadau wasimamizi na watunga sera,lazima kuwabana hawa wakandarasi wawe wanajari usalama wa wafanya kazi wao.Na kuwachukua hatua kali wale wote wanao kiuka.

  Pole kaka.Tupo pamoja.

 3. Pope Says:

  1. Mtaa wa Jamhuri majumba ni ya NHC, kama ni matengenezo lazima kuna mkandarasi aliyepewa kazi na NHC,

  1a. Tender imetolewaje kwa mkandarasi mwenye vitendea kazi duni liasi hiki?

  b. CRB wammempaje (kama ni mwajiriwa wa Kampuni) huyu mwenye Kampuni ambaye ni muajiri wa huyu fundi mangungu?

  2. Jamaa hana Kofia (Hellment)

  3. Site Safety Boot

  4. Ngazi

  aaaaaaaaaah bwana we bora liende

 4. Dar-Hotwired Says:

  Aisehh!!! yaani pengine jamaa hana choice ila kufanya kazi apate chakula. Hapo hamna health & safety hata kidogo. Kuna watu wengine duniani ambao kama sio mungu sijui mambo yangekuaje.

  Nway, u gotta do what you gotta do to get paid.

 5. Mkweli Says:

  NI LAZIMA KWANZA KILA MTU AJIFUNZE KUYALINDA MAISHA YAKE IKIWEMO KWA;
  KAZI HATARI
  UKIMWI
  NK
  TUJIZOESHE KUSEMA ‘NO’

  NINAMLAUMU HUYO FUNDI KUWEKA TAMAA MBELE MAUTI NYUMA

 6. Mkweli Says:

  NYONGEZA…

  NAKUMBUKA WAKATI NIKIWA HUKO NYUMBANI (TANZANIA) KULIKUWA KUNA TANGAZO LINALOELIMISHA MADHARA YA KUFANYA KAZI ZA UJENZI BILA KUFUATA TARATIBU ZA KAZI, IKIWEPO UTUMIAJI WA VIFAA VYA KUJIKINGA NA AJALI. HII ELIMU ILIKUWA NADHANI INATOLEWA NA CRB BURE KABISA KWA WANANCHI KUPITIA TV, TENA KWENYE VIPINDI VINAVYOANGALIWA NA WATU WENGI.
  TAASISI ZINAJITAHIDI KUTOA ELIMU, HUYU FUNDI HATAKI KUFUATA TARATIBU, IKO HAJA YA HUYO FUNDI NA WAHUSIKA WENGINE WAWAJIBISHWE.

 7. Muwasilishaji, tafadhali naomba kujua ndugu yetu huyu alikuwa akifanya kazi hii ghorofa ya ngapi au niulize ni urefu wa mita ngapi kutoka ardhini?

 8. Kekue Says:

  Da!! Haya maisha haya!!!!!!!!!! Hiyo kamba yenyewe sasa, yani ikikatika hapo ni habari nyengine lakini sasa afanyeje na familia nyumbani inataka kula, kuvaa bado yeye mwenyewe mh!! lakini ishaalaah ipo siku nyota yake itang’ara!!! watu wanatoka mbali sana!! Pole kaka!!!

 9. Kemmy Says:

  Jamani maisha duni, hali ngumu mtu anawaza atakula nini, ataishije, watoto watasomaje, watatibiwaje wakiumwa???ndo yanayopelekea kufanya kazi katika mazingira magumu namna hiyo, tuelewe ile si tamaa ila ni kutokana na hali kuwa ngumu.
  Mungu awasaidie wote wanaofanya kazi katika mazingira ya namna ile.

 10. Matty Says:

  Du!!!!!!!mungu amsaidie ni uchumi mgumu!

 11. Upendo Furaha Amani Says:

  Kazi ni shughuli halali inayompatia mtu kipato.
  Huyu anatafuta kipato chake.

 12. mdunger Says:

  Inatia huzuni,inaonesha aliyempa kazi alitaka cheap labour ili kupunguza gharama.ifike wakati tuwawajibishe wote wanaohatarisha maisha ya wenzao.yule fundi yuko katika unyonge na tajiri ametumia hiyo nafasi kujaribu kumuua!pole kaka.

 13. BongoSamurai Says:

  Watanzania wengi tumekuwa ni watu wa kutafuta riziki kwa namna yeyote ile hata kama ni ya kuatarisha maisha yetu.Hii ni kwa sababu ya ugumu wa maisha tulionao wengi.Jamaa kwa upande mmoja ana makosa ila kwa upande mwingine pia hana kosa maana naamini aliyempatia hiyo kazi alistahili pia kumpatia vitendea kazi madhubuti.Waajiri wengi hawazingatii usalama wa waajiri wao bali wanajali maslahi yao, hata la huyu jamaa halinishangazi sana ila linanisikitisha sana.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s