BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PM MSTAAFU NA MISS TANZANIA January, 22, 2008

Pichani ni Waziri Mkuu Mstaafu,Jaji Joseph Sinde Warioba akiteta jambo na Miss Tanzania 2007,Richa Adhia, walipokutana jumamosi iliyopita nyumbani kwa Balozi wa Palestina nchini Tanzania,Yusufu Habab,huko Oysterbay jijini Dar-es-salaam.

Jaji Warioba na Richa Adhia walikuwa ni baadhi tu ya wageni walioalikwa kwenye chakula cha mchana nyumbani kwa balozi huyo ikiwa ni lunch maalumu ya kutunisha mfuko na pia kuwafariji watoto takribani 30 wanaopata msaada mkubwa wa kimalezi kutoka katika shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Mitindo House(TMH) shirika linaloundwa na baadhi ya wabunifu wa mitindo nchini Tanzania wakiongozwa na Khadija Mwanamboka. Kwa picha na habari zaidi juu ya tukio hili bonyeza hapa na pia hapa.

Picha kwa hisani ya MichuziJR.

Advertisements
 

24 Responses to “PM MSTAAFU NA MISS TANZANIA”

 1. Majita Says:

  Nukuu ya Karne hii….
  “Sasa hivi SI wakati wa Wapinzani kukaa na kupiga kelele juu ya ufisadi ama mafisadi wa nchi hii.Hilo ni jambo dogo sana kuongelewa na wapinzani dhidi ya Serikali.Kuna changamoto nyingi sana zinazotakiwa kuongelewa muda huu juu ya maendeleo ya nchi.Kwa nini sasa wapinzani wasiongelee Kilimo na kuhamasisha wananchi juu kilimo ili kutumia mvua zinazonyesha sasa??”………

  Huwezi kuamini.Tamko hilo lilitolewa na mhe sana aliyekuwa maarufu na kusifika SANA juu ya umakini wake dhidi ya Rushwa kutokana na kile kilichoitwa “Tume ya Warioba”

  hahahahahaha.LoL.
  “The Beautyfull One Are Not Yet Born”
  ©Majita

 2. Edwin Ndaki Says:

  Nampongeza K.Mwanamboka kwa kazi nzuri anayofanya kwa jamii.

  Ila ni changamoto kubwa kwa hao mamiss mfano Richa.Mara nyingi wakati wa kinyang’anyiro cha ulimwende wanapenda kutoa ahadi kibao jinsi ya kuitumia kijamii lakini inakuwa tofauti na hali halisi.

  Inapendeza kuona miss Tanzania akifanya kazi za kijamii kwa wingi na kusaidia harakati mbali mbali za kijamii.

  Hongera balozi wa palestina kwa kuwa moja ya chachu.

  wasalaaa.

  tutafika tu

 3. janet Says:

  kwakweli mimi ni mmoja kati ya wasio mkubali huyu mnaemwita miss tanzania.
  muhindi ni muhindi tu, wanafki, roho mbaya, wafitini kwanza hatuwatufai nchi yetu yenye utulivu na amani. mi ninasema haya kwani ninafanya kazi na wahindi mwaka wa tano sasa nawajua nje ndani, ivyo hata nikimuona huyo richa napata hasira sana.

 4. Edwin Ndaki Says:

  BC..ina maana bado unafanyi kazi maoni yangu au umeyaweka kapuni au haka kakopyuta kangu ndio kimeo maoni hayajafika.Maana ni muda alafu naona ze kimya.

  Ene wei tutafika tu.

  Kikubwa hongera sana kwa K.mwanamboka na wenzake wote.Ni mfano mzuri kwa maselebriti wa kibongo kuitumia jamii.

  Wasalaaam

 5. Matty Says:

  Bora MAJITA ametoka out of topic maana mimi nikimuona huyo Richa nasikia kizunguzungu….najua mtasema ila meseji sent na ukweli ndo huo!!!!!!!!!!Janet bora ukubali matokeo te te te te te !!!!!!!
  Wanawake na maendeleo tufanye kazi tusonge mbele eeeeeeee nawapongeza sana wajasiliamali wetu kwa kazi wanayoifanya hasa wanapojitoa kwa wasio na wazazi (yatima).
  Mungu awabariki!

 6. janet Says:

  matty, bora wewe kizungu zungu mi natapika kabisa richa richa richa kila kona ndo maana kapigwa chini miss world!
  na hawa wakina lundenga nao mi hata siwaelewi sijui mwaka huu watatuletea kituko gani,

 7. janet Says:

  amina upoooooo……? richa vip unamkubali?

 8. Recho Says:

  Nani amkubaki richa hapo hanajipendekeza hili haonekani mtu wa mahana.Mwindi mbaya na nguo yake mbaya

 9. annabell Says:

  jamani haya ni maoni yangu tu,
  miss tanzania? mbona sioni huo umiss?tafadhali mliomchagua naomba mnipe mafafanuzi mnaonaga nn?for sure sidhani kama atatuwakilisha tanzania kwenye miss world i doubt!

 10. annabell Says:

  eehee hadi nimetoka nje ya somo
  waziri warioba umefanya jambo la maana kukutana namiss eti! nakuteta mambo mawili matatu! i dream ni ya kumsisitizia kuhusu asili yetu…asije akasema yeye ni miss india tanzania bure!

 11. anony Says:

  shame u people. It seems u have got nothing to do than discussing about her. Haiwasaidii lolote. hizo ni roho dhaifu mlizo nazo. She is miss TZ, nothing u can do to change it.
  Isitoshe siyo yeye aliyejichagua kuwa miss, Ni majaji. Ni vema mngewashambulia hao majaji na sio yeye.
  Kwani amewakosea nini yeye mpaka ikawa hivyo

 12. Ally Says:

  Huyu jamaa anasema anafanya kazi na wahindi mwaka wa 5!!badala ya kutuambia nabebeshwa box kisutu na wahindi mwaka wa anajifanya eti nafanya nao kazi acheni hz huyu ndio kishakua miss wetu hata mfanyeje shame on you people u cant change it.

 13. Matty Says:

  Anony nakujibu hivi! kama unamkubali wewe usilazimishe watu wamkubali sawa??yeye anatanga na kabila mara mama kutoka pemba, baba india mara baba anaasili ya moro na usukumani wewe kasema nani???na hao waliomchagua si ndugu zake tu!!!! huyo Lundenga naye kashaishiwa mamiss mwakani tusubiri mchina te te te te !!!!!!!!!Kashindwa huko Miss world kutokana na kukosa sifa halisi full stop! nadhani huyu ni miss kitongoji cha Kariakoo!!!!!!sina ubaguzi nasema ukweli ….msianze ohh ehh aiii racism no! kwanini tusiwe na mrembo mwenye asili halisi hata ngozi au nyele zionekane kipilipili sio hizo zake kama rasta sijui weaving mwe mwe mwe jamani hata akisuka twende kilioni wala hazikai.

 14. Kekue Says:

  Matty sio meseji sent, hii ni meseji delivery inaweza ikawa sent lakini isifike!!! Hapa imefika!! Hongera Khadija Mwanamboka!! mambo ya kuchikuchi kotae nilishachoka!!!!

 15. kijiwe Says:

  anony who? patel,gupta,ghella au?
  let us know jamani maana kila mmoja hapa ana some sort of identification ni wewe tu unatuletea anonymity – ni dalili za paranoia !
  usimaind 🙂

 16. kijiwe Says:

  To ALLY on behalf of MATTY
  Inaonyesha jinsi ulivyokuwa na negative thoughts about others which indicates your weakness “kufikiria kila mtu yupo step one kama wewe” LOL
  acha kudiss watu ambao hata huwajui wanafanya nini hapa planet earth ebo!
  Matty alikuwa anashare her life experiences na wahindi hakuwa anatoa hadithi ya kuwa ana level gani ya maisha.
  humu BC watu wanadiscuss mambo mbalimbali ya kijamii,kiuchumi na kisiasa na siyo kuchunguza huyu anabeba box au ana run 6 digit account.ukienda kwa mwendo huo utachoka mwenyewe maana kuna kila aina ya watu katika mtandao.
  halafu wewe Anony please acha kutupangia what to do with our lives “everybody for herself/himself GOD almighty for us all!”

 17. kijiwe Says:

  Duh kaaz kweli kweli
  Matty sorry nimekuchanganya na Janet unajua wazushi wengine humu ndani wanatuchanganya
  Naomba kusahihisha my latest post.
  ——————————————————
  To ALLY on behalf of JANET
  Inaonyesha jinsi ulivyokuwa na negative thoughts about others which indicates your weakness “kufikiria kila mtu yupo step one kama wewe” LOL
  acha kudiss watu ambao hata huwajui wanafanya nini hapa planet earth ebo!
  Janet alikuwa anashare her life experiences na wahindi hakuwa anatoa hadithi ya kuwa ana level gani ya maisha.
  humu BC watu wanadiscuss mambo mbalimbali ya kijamii,kiuchumi na kisiasa na siyo kuchunguza huyu anabeba box au ana run 6 digit account.ukienda kwa mwendo huo utachoka mwenyewe maana kuna kila aina ya watu katika mtandao.
  halafu wewe Anony please acha kutupangia what to do with our lives “everybody for herself/himself GOD almighty for us all!”
  ——————————————————

 18. Matty Says:

  Nimekusoma Kijiwe!!!!!!asante Kekuu kwa kunisaidia kumbe msg delivered…

 19. anony Says:

  Hey matty and kijiwe, nobody pursuade u to praise her. Hii inaonyesha ni jinsi gani mlivyo na uwezo mdogo wa kuelewa kilicho andikwa. Comment inamainisha wazi kuwa acheni kumkashifu binti wa watu kwa maneno yenu ya kibaguzi. Maana she has done nothing wrong to u. Ata kama haumkubali its ok hakuna anayepinga kwa hilo, lkn sio kukaa na kuanza kumsimanga na kumkashifu pasipo kosa lolote. Hii pia inaonyesha ni jinsi gani mlivyo na uwezo dhaifu wa kufikiria na kuamua cha kuongea.
  najua mtacomment ktk hili lkn sishangai maana inaprove jinsi mlivyo mailliterate. And never expect me to come back and argue with u, coz I cant do so with illeterate one. Gud stuff………!!!!!

 20. Matty Says:

  Anony,hapa kila mtu anamtazamo wake usitake kulazimisha watu wafate mtazamo wako na huwezi kunibadili mimi kama mimi!!!!!!!

 21. kijiwe Says:

  ———————————————————————————————
  TO ANONY
  hivi wewe umejiona very literate mpaka unaanza kuwaita watu ambao hata huwajui iliterate?sikiliza wewe watu wana freedom ya kudiscuss kitu chochote wanavyotaka either iwe pros au cons it does not matter because every human being is entitled to a freedom of expression.
  wewe umekuwa nani mpaka uwalazimishe watu kusema huyo binti this or that?watu wanapochangia mada wana uhuru wa kusema wanachotaka it is a way of expressing their feelings towards a particlular matter then you get few who get really touched by the topic then wanaongea zaidi but whatever they say is their opinion au feelings sasa wewe umekuwa nani mpaka utulazimishe kumkubali?
  maana hata katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge kuna watu wanapiga kura za ndiyo na wengine wanapiga kura za hapana and life goues on na watu wanaendelea kuongea!
  halafu please tuheshimiane sijawahi kuitwa iliterate tangu nimezaliwa na kama unataka i can drop my cv in here wewe unafikiri ningeishi botswana(10yrs),south africa(5yrs)and now sweden kama professional kama ningekuwa iliterate?
  EBO?
  —————————————————————————————————

 22. Upendo Furaha Amani Says:

  Mie ninampongeza Mh. Waziri mkuu mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba kwa kuendelea kuwa mshauri wa mambo mbalimbali ya kitaifa.
  Richa Adhia ni Miss Tanzania 2007, huyu ni Mtanzania wa “Kabila la Kihindi” kama wewe ulivyo mtanzania wa “Kabila lako”. Hivi ndugu zangu watanzania, mnajua kuwa historia inasema kuwa, wenyeji wa nchi hii ni “Wasandawe” na “Wahadzabe” tu? hivyo makabila mengine yote hawana tofauti na wahindi maana wote ni wakuja.
  Ninawasilisha.

 23. Mama wa Kichagga Says:

  Upendo,

  You made my day! hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.

  1. Nampongeza Waziri Mkuu mstaafu Nd. Joseph Sinde Warioba kwani kama asingeshiriki vema katika kupanga sera ya elimu kwa wote wakati ule basi nisingeweza kuwa hapa leo.

  2. Pongezi kwa dada yangu Kh. Mwanamboka kwa kuthubutu kufanya mambo mazuri kwa jamii.

  3. Pongezi kwa Miss TZ kwa mafanikio yako – hata kujaribu kitu na kushindwa ni mafanikio vilevile.

  4. Lundenga na wenzio: fuateni haki ktk maamuzi na wengine jitahidini kukubali matokeo tusije ishia msituni buree.

  5. Wahindi naamini mnasoma hapa na mmeona sura yenu ilivyo machoni pa Watz walio wengi – badilikene na wacheni mambo ya kijinga jinga kwani binadamu wote “RANGI YA DAMU NI NYEKUNDU”. Mimi nawapenda Wahindi wa Bombay- wana utu kidogo maana rangi zao wamechanganyika weusi au weupe au maji ya kunde. Mtambue fika watu wameshazichoka tabia zenu zilizotajwa hapa na zile ambazo hazikutajwa. Hakuna sera ya ubaguzi iliyowahi kudumu duniani.

  Ni haya tuu

 24. johari ally Says:

  mambo mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 18 natafuta marafiki wa kuchati nao katika computer sibagui rangi wala kabila . napendelea kuruka kamba kusikiliza mziki kuchati na marafiki kusafiri.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s