BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HAWEZI KUMUACHA NGALULA! January, 25, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:10 AM

What a week! Wikiendi ndio ishapiga hodi tena.Tarakimu za kwenye kalenda ndio zinazidi kutukumbusha kwamba mwaka 2008 ndio huooo tushaanza safari ndefu ya kuukata.Hapa BC mambo ni shwari kabisa.Kama kawaida leo ni wakati wa kupumua kidogo,kupata burudani na kutafakari mawili matatu.Nadhani utakubaliana nasi kwamba wiki hii ilikuwa na changamoto,maoni na mijadala mingi zaidi.Hiyo ndio inavyotakiwa,mijadala,maoni na pia maono mbalimbali bila tu, kuvunjiana heshima,kutiliana chuki,fitina,umbea wala matusi.Tunajenga jamii.

Burudani ya leo inatoka kwa Orchestra Maquis.Wimbo unaitwa Ngalula,utunzi na uimbaji wa Tshimanga Assosa. Mwenyewe anasema ashamzoea Ngalula wake,hawezi kumuacha kwa sababu yeye ndio anajua shida na raha zake zote.Upo hapo?Sikiliza jinsi Dekula Kahanga maarufu kama “Vumbi” anavyocharaza gitaa.Mtindo unaitwa Sendema.Pata burudani,hapo ulipo nyanyuka ucheze kidogo.Wikiendi Njema.

Burudani hii ya leo imeletwa kwenu kwa udhamini wa;

Advertisements
 

11 Responses to “HAWEZI KUMUACHA NGALULA!”

 1. tonny Says:

  Nimpongeze kwa dhati kabisa Mkongwe Mwana Kitoko, Mwana Mboka, Mukulu, Supremee, Mvumilivu wa Wavumilivu na Mchapa Kazi Hodari Ndugu na Rafiki yangu Tshimanga Kalala Assossa kwa tungo zake zilizoshiba na za kuvutia toka enzi za kina LipuaLipua, Kamale, FugaFuga, Maquis, Bomoa hadi Bana Balembi Bana ba Maquis!Mungu akubariki na akupe nguvu mpya ya kuendelea kuchapa kazi kwa moyo uleule!Riziki ni popote ndugu yangu.Pengine nikushauri tu kwamba kutokana na ukongwe ulionao na muda kututupa mkono hebu sasa ufikirie kuanza kupakua Kipaji chako kwa vijana wanao chipukia na wenye mwelekeo na vipaji vya kuwa wanamuziki pengine kwa kuanza kuwa na kikosi cha pili cha vijana wadogo watupu katika bendi yako. Mpaka hapo ukija choka kabisa utavuna matunda yake ndugu yangu Assossa! Usisahau kuwa na Studio yako mwenyewe.Siyo lazima uwe na Cash mkononi.Zunguka kwa wadau ambao wamekuwa wakifaidika na jasho lake kisha KOMAAA NAO MZEE!tunakupenda na tutaendelea kuuheshimu muziki wako Assossa!ningesungumsa sana lakini kiswahili yangu iko small small!tehe tehe tehe1BRAVO ASSOSSA bravo michuzi.com!

 2. Edwin Ndaki Says:

  Asante saaaana BC,kwa kuendeleza maburudani ya kufa mtu hususani mwishoni mwa juma.Yaani nakumbuka sana RTD”Radio Tanzania Dsm”

  Nyimbo nzuri sana hizi.Imefika wakati wangeziweka kwenye chupa”kideo” inakuwa inapendeza zaidi.

  Pia wimbo umebeba ujumbe.Kuvumiliana inapende sana.Sio ka kosa kadogo tu tayari mmemwagana.Eti kisa umekuta sms kwenye simu ya mwenzi wako ..presha juu utafikiri kashfa ya BOT.Kama huna kifua unatafuta nini kwenye simu ya mpenzio..mfano tu.

  Wadau wote…wasomaji..watoa maoni nawatakieni wiki endi njema ..ila mkumbuke kuna ndugu zetu huko kusini mwa Tanzania wamekubwa na janga la njaa.

  Mshukuru sana Mungu kwa kila unachokipata.
  Na kumbuka unaendelea kuziona hizi ijumaa sio kwa bahati mbaya au ujanje.Zitumie vema kujenga jamii bora.

  Ene wei,tutafika tu.

 3. Dinah Says:

  Samahani natoka nje ya mada, nadhani umesoma hii habari.

  http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2008/01/25/106999.html

  Kuna uwezekano wowote wa kuiweka hapa ili watu waone ni jinsi gani mtz wa kawaida ambe ni mtoto na mwanamke asivyo na haki mbele ya polisi!

  Hivi Polisi wetu hawakufunzwa binu nyingine za kupata ukweli kama vile kuuliza maswali ya “kuiandishi”, kula deals za kisheria na mtuhumiwa, kuhsawishi kwa kutumia maneno n.k. ili kufungua mashitaka zaidi ya kuwapiga watumuhiwa?

  Mbona akina Balali ambao wanasababisha vifo vya watu wengi kutokana na umasikini hawasumbuliwi kama haka katoto kalala hoi kalikoua mtoto mwenzie bila kukusudia?

  Kilichonisikitisha sio kuuawa kwa mtoto bali ufuatiliaji wa kesi ili kufungua mashitaka dhidi ya mtuhumiwa. Ktk hali halisi Polisi waliotoa kipigo wanapaswa kufunguliwa mashitaka na huyo Mama mwajili anakesi ya kujibu kwa vile ameajili mtoto na alikuwa akimnyanyasa kisaikolojia na bila shaka kimwili. 😦

 4. Edwin Ndaki Says:

  Dinah..duu ni habari ya kusikitisha sana kuuwawa kwa huyu malaika.

  Ingawa na polisi nao mbinu wanayotumia siyo njema.Lakini kwa mfumo wa bongo jinsi ulivyo na vitendea kazi,wakati mwingine polisi inabidi watumie njia ya kichapo kupata ukweli fasta.

  Hapa bongo polisi wetu wanatambua hawapaswi kumpa kichapo hivyo mtuhumiwa,ila kutokana wingi wa kesi mbalimbali na hawana nyezo ili kuokoa muda,hakuna MAMBO ya Ulaya sijui kumpa mshtakiwa kitu anachopenda mfano fegi n.k ndio maana inabidi watumie suluba kupata ukweli fasta.

  Si umeona huyo muuaji alivyotoa ushirikiano fasta baada kula kichapo.Ingawa Rajabu anaweza kuwafungulia kesi hao maafande waliompa suruba.

  Ene wei ,Tufafika tu Dinah …hiindio bongo

 5. Upendo Furaha Amani Says:

  “Ngalula, ananielewa vizuri kuliko mtu (mwanamke) yeyote”
  Yakale ni dhahabu; ukishaishi na mtu (hasa mkeo kwa wanaume na mumeo kwa wanawake) hata kwa muda mfupi, mfano mwaka mmoja tu; ukweli ni kuwa hata mkiachana, hutapata tena mwingine kama yeye. Maana kila mwanadamu ana mapungufu yake.
  Nawasilisha.

 6. Farida Says:

  Huu utunzi umetulia kupita maelezo, yote ni katika hali ya maisha ya kila siku ya mwanadamu, kuwa hana maamuzi kutokana na kuwa mtu wake ameshamzoea, shida na raha zake anazielewa, hivyo anaona ni ngumu kuachana nae!! Ujumbe mzuri sana huu katika maisha yetu ya ndoa. Nakupa big up Asosa!! Japo nipo mbali lakini siachi kuburudika na tunzi zako, kama “Aisha”, makumbele, Fransica n.k.
  Cha matata – UK

 7. DUNDA GALDEN Says:

  KINACHONIFANYA NISHINDWE KUAMUA.PAMOJA NA VISA VYOTE LAKINI MTU ANAVUMILIA TUU UBEBWE VIPI TENA?KUMBUKA AKICHOKA HUYO!LAZIMA TUKUBALI YAKALE SI MCHEZO MPAKA UVUNILIVU ULIKUWEPO KWA WANA NDOA LAKINI KWA SASA BAADHI YETU UKILIKOLOGA KIMPANGO WAKO YOTE WAKATI UMEKUWA UKUTA UNAFANYA UMALAYA KIGEZO TUMEKAA MDA MREFU TEH TEH KIBUTI TUU NGALULA
  DARWIN=CHAFOSA CHAI GODA

 8. mariam kabula Says:

  HUWA NATAMANI JUMAMOSI IFIKE NIENDE PORT VIEW NIKAMUONE ASSOSA. KWA KWELI NAMPENDA SANA ANAIMBA VIZURI. NAMSHAURI WAWE SMART WAWAPO JUKWAANI

 9. hans Says:

  hakuna mtunzi mzuri kama yule anetunga nyimbo nyingi na zote zinavuma na kupendwa na mashabiki, kwangu tshimanga kalala assosa hana mfano. ninazo nyimbo nyingi sana zake toka fukafuka, lipualipua hadi za marquiz original. jamaa namkubali sana

 10. Hanny Mrembo Says:

  HILO GITAA LINA NI KUNA MPAKA,SIJUI NIMPE NINI JAMAA HUYU.ASSOSA NI KIBOKO KWA KUTUNGA MASHAIRI NINAVYO SIKIA NYIMBO HII NGALULA THAT IS CLASSIC TZ MUSIC

 11. BATTY JULIUS Says:

  KIKOSI KIZIMA CHA SENDEMAA KATIKA ALBAM NGALULA;
  WAIMBAJI NI CHIMANGA ASSOSA,MUKUMBULE PARASH,MUTOMBO AUDAX,ISSA NUNDU NA KABEYA BADU.
  SOLO GUITAR:DEKULA KAHANGA”VUMBI”,SECOND SOLO:MBWANA S.KOCKS(marehemu)RYTHM:WILLIAM MASELENGE(marehemu) BASS:BANZA MCHAFU(marehemu).
  TROMPETT:KAUMBA KALEMBA NA NGOYI MUBENGA(wote marehemu) SAXOPHON:MUKUNA ROY,BERRY KANKONDE(marehemu) CONGAS:SEIF SAID,DRUMMS:MATEI JOSEPH
  KINONDONI LANG’ATA ILI KUWA KIVUMBI NA JASHO SENDEMAAAA,TWENDE MBELE RUDI NYUMA,KUSHOTO KULIA


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s