BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI #04 January, 27, 2008

Filed under: Photography/Picha,Swali kwa Jamii,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Jiji la Mwanza(pichani) ni mojawapo kati ya miji inayokua kwa kasi sana nchini Tanzania.Kama ambavyo unaweza kuona katika picha hii,majengo mapya yanazidi kunyanyuka jijini Mwanza. Swali kubwa ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni je,ukuaji wa jiji kama hili la Mwanza unaenda sambamba na uboreshwaji wa miundo mbinu na huduma za msingi za kijamii?

Picha hii ilipigwa na MichuziJR kutokea kwenye paa la hospitali ya Bugando.Hii ndio picha yetu ya wiki hii.

Advertisements
 

7 Responses to “PICHA YA WIKI #04”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Nakumbuka wimbo wa Dr Remmy….aliimba
  mwanzaaaaaa ooohhoo mwanzaaaaa eeeheeee..,
  mwanza ni mjii mzuriiiiiii…,
  mwanza ooohoo mwanzaa eeeheee,
  mwanza nitarudi tenaa .

  Hakina Bc leo mmevuta hisia zangu haji katika hilo jiji la miamba au mawe..Rocky city zamani tuliita zoo na kabla ya kuja kwa ngozi nyeupe lilijulikana kama Nyanza.

  Hakika jiji la mwanza linazidi kubadilika kama ulivyodokeza.Na ninaona serikali kwa ujumla inajitahidi sana katika kuboresha miundo mbinu ukichukulia na siku za awali.

  Mfano barabara zote kuu ziingiazo katika jiji la mwanza naona kwa sasa zimewekewa mkeka..mfano nyerere road iendayo mkoani Mara.Kenyatta road iendayo mkoani shinyanga.Na pia barabara nyingi ndogo ndogo mfano kuelekea chuo cha SAUT na sehemu mbalimbali.

  lakini kubwa ya yote,mwanza kuna watu wanakula MAPANKI(masalia au mabaki ya samaki),sio kwamba ni utamaduni au kwa kupenda ila ni kutokana na hali ngumu ya maisha.

  Wenye viwanda vya samaki bado hawaja wajibishwa vya kutosha kuchangia maendeleo ya mji wa mwanza achilia mbali wanaongoza katika kuchafua mazingira ya ziwa victoria na mazilia ya samaki.

  Bado namuunga mkono Hubert Sauper…kwamba wenye nguvu ndio watakao neemeka katika jiji la mwanza.

  Asante na poleni kwa maelezo maelefu.

  asante michuzi jr maana nimeweza kuona fasta kwenye picha yaki,jengo la ccm mkoa,uwanja wa nyamagana n.k kwenye hi picha.

  jpili njema

 2. Edwin Ndaki Says:

  BC habari ya kusikitisha nimekutana nayo asubuhi hii.Celebrity John Lubungo,mwandishi wa habari mkongwe wa ITV na Radio One amefariki dunia kwa ajali ya gari akitokea Mbeya kueleke nyumbani kwake Tunduma.

  Habari zaidi
  http://ippmedia.com/ipp/alasiri/2008/01/26/107120.html

  mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi.Amina.

 3. ben Says:

  jiji la mwanza limetulia,nadiliki kuhama dar kwa sababu ya msongamano wa magari ambapo mwanza hakuna kitu kama hicho.

 4. Liz Baraka Says:

  Kweli jiji la miamba linapendeza wasiwasi wangu ni suala la miundo mbinu maana huku Dar tatizo ni hilohilo la miundo mbinu lakini kila asubuhi maghorofa yananyanyuka.

 5. Baba Koku Says:

  Aisee, turudishiwe hela zetu za almasi na dhahabu tuongeze magorofa … Mwanza wampunjwa sana.. Miaka ishirinin bila lami? wasukuma wastarabu sana.. Moshi ingefanywa kama Mwanza, mambo yange enda vingine..

 6. Debra Says:

  Yaani wee Edwin Ndaki umefikishwa hapo manake kama nakuona na tabasamu ulilojaza kwa uso wake wa kitizii!!
  Dahh ila kiukweli Jr hapo sawa

 7. ramadhan Says:

  MWANZA TANZANIA


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s