BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MPOKI AND JOTI January, 29, 2008

Filed under: Burudani,Comedy/Vichekesho,Television — bongocelebrity @ 12:08 AM

 

Mpoki(kushoto) na Joti(kulia) baadhi ya wasanii wanaounda kundi maarufu la Ze Comedy ambalo kila Alhamisi jioni huwavunja mbavu watanzania wengi kupitia kituo cha luninga cha EATV.

Advertisements
 

36 Responses to “MPOKI AND JOTI”

 1. Nerra Says:

  Congrants Mpoki na Joti mna kipaji cha ajabu kwani Joti aweza kua mtoto, kijana na mzee ni kipaji cha ajabu! mungu awabariki mje mpige hatua zaidi ya hapo.

 2. twin Says:

  walianza vizuri, ila Joti anaboa anatumia sana lugha ya matusi ambayo ni kinyume na maadili ya mtanzania, anaudhi sana, ajirekebishe mbona wenzake hawaongei matusi? au anafikiri kuongea matusi ndiyo kupata umaarufu zaidi. Ni bora Masanja ukarudi kwenye position yako manake wengine tume- loose interest kabisa kwa ajili hiyo. Wanashindwa kuelewa kuwa kipindi hicho kinaangaliwa na watu wa rika mbalimbali. Rekebisheni lugha please.

 3. Matty Says:

  Mdebwedo!!!!!!!!!acheni kulewa sifa umaarufu ni kama maua fanya kazi, jenga nchi sorry imean jenga mambo yako!!!!

 4. Edwin Ndaki Says:

  Joti ama hakika ni kipaji kikubwa sanaaa.

  Kila pande analopewa kuigiza ni balaaa …

  Na ukimpeleka kwenye lafudhi za mwambao ..aaa swadaktaaa hapo ndio mwake.

  Hongera sana Joti..ila mpoki na wewe unafuatia fresh

 5. gee Says:

  hawa jamaa wana kipaji sana. hongereni kwa hatua mliyofikia.
  kila alhamis mishe mishe zote nahairisha kuwahi kipindi chao. keep it up guys.

 6. mkata issue Says:

  siku moja nilisoma maelezo fulani mtandaoni kuwa eti ‘hawa jamaa wanajificha chini ya kivuli cha vichekesho lakini wamedhaminiwa kuwamaliza vyama vya upinzani Tz!
  Binafsi nilidismiss hiyo kauli kama udaku.
  Jamani sijui kama wenzangu nanyi mliwahi kusikia hilo au kuna mtu ana uhakika na hilo lililosemwa basi atumwagie hapa uchambuzi wake ?
  Kama ni udaku basi wazushi walegee, nanyi mzidi ktunukiwa! Lakini kama ni kweli basi hamtafika mbali maana mapigo ya Mungu huja hata nyumbani kwa Farao sembuse Wasanii?

 7. Nawakubali kwa vichekesho Mpoki na Joti. Keep it up. Wewe Mpoki mbona macho yako mekundu unavuta bangi nini?

 8. haika Says:

  Yaani nyie kweli mnachekesha.
  Mpoki siku hizi kitambi kikubwaaaaaaaaaaaaa. Mashavu. misuli nk.

  Nawe babu joti uchawi uwache wengine tumeokoka kumloga Masanja wetu mpaka akawa tumbili hujisikii vibaya? eti wataka kipaji chake kife wewe utaadhibiwa na mungu.

  Tena tabia yako mbaya mtaani kwetu umetuaribia watoto. mwanangu ana miaka 2 nikirudi kazini ananiambia mamaaaaaaaa, mama,,,, ona nini sianashtua kijoti,,,, joti Nitakuletea umleeeee wewe,

  ni mtazamo tuuuuuuuuu. ila kazi nzuri

 9. Kwa vichekesho nawakubali sana. Keep it up. Ila wewe mpoki mbona macho mekundu sana unavuta nini brother? punguza jicho linatisha hilo!!!!!. other wise I like your comedy

 10. maya Says:

  Guy let just be onest ni wazuri na wanafunika sana lugha za matusi ni nyie waswaz mna zitafsiri wenyewe kwa hi waacha watupe raha sana sie tusio jua tafsiri zenu yie. kwa kweli mama ima ana nikuna sana jot akiwa msicha kwa ujula woote nawapenda nsana na wapongeza sana sana . na ngoja alihamisii iii kwa hamu naivi valentine imekaribia mbavu zangu naziaandaaaa ata kama hakuna wa kuni valentine raha tuta ipata in side zecomedy

 11. Askofu Says:

  Kwa mujibu wa falsafa niliysomea kwa muda mrefu nimeweza kugundua kuwa hapo juu kuna mtu anatafuta mchumba. Mtu huyo ana jinsia ya kike kwa mujibu wa jinsi alivyojitambulisha, sipendi kumtaja jina ila kama mkipitia maoni yaliyotangulia kwa ufasaha mtaweza kumgundua.

  Vinginevyo ni kuwa hawa vijana wanajitahdi katika kazi yao na Mpoki kama kweli unavuta bangi jitahidi kuacha kwa sababu haitakujenga bali kukubomoa muda si mrefu ujao. Kuhusu Joti pia nakushauri utumie maneno ambayo hayatawakera kikundi fulani cha wanajamii. Mf. kuna kipindi ulihoji kuhusu watu wanaoishi Upanga au Kigogo, hapo sikuungi mkono kabisa.

  Nawakilisha.

 12. Upendo Furaha Amani Says:

  Ninawapenda wana vipaji vya ajabu Mungu kawajalia. Wangekuwa majuu wangekuwa matajiri kama akina “Fresh Prince” na wengineo.
  Kuhusu aliyesema kuwa ameokoka hivyo aache mambo ya kichawi ni kuwa kama kweli umeokoka, soma kitabu chako kitakatifu vyema maana “Vitabu vyote Vitakatifu” vimezungumzia uchawi, hivyo Uchawi ni sayanzi ambayo ipo na “Mungu aliiumba”
  Ushauri wangu kwa hawa vijana: Wasibweteke kwa elimu walio nayo, kama inawezekana waongezee ili wawe “figa” za kimataifa.
  Nawasilisha.

 13. Mossy Says:

  You guys are the BEST!

 14. Mama wa Kichagga Says:

  Kazi yenu ni nzuri sana na mbarikiwe sana. Mpoki havuti wala kusokota, ni macho yake aliyopewa na mwenyenzi. Ila Joti sasa hawa watoto vipi? Anyway wacha wafurahie maisha kwani enzi za “Break Dance” za kina Wako Jaco watu wazima hasa vijana walitembea hadi mabega upande – KISA RAHA YA BREAK DANCE. NI KHERI TUU.

  Mpoki msalimie sana Binti MPAPAI

 15. Kijana Says:

  sijui kama ni maarufu sanaaaaaaaaaaa kama tunavyowafagilia maan sijui kama kuna watu ambao wanaoangalia kwa sana zaidi ya akina mama na watoto ambao hawana shughuli ,ningehimiza zaidi wawe wanatuletea vitu vya msingi zaidi kuliko hv vya sasa

  Nawakilisha

 16. lugano kasambala Says:

  mupo safi keep it up,
  munatisha.

 17. SAfiiiiii sana keep it up!
  NAwakubalii…..huku kwetu siku ya alhamisi mabaa yote yanavuna ile mabya kwani siwatoto si wazee…..
  Mnatusaidia kusahau machungu jamaniiiii
  TUMEWAKUBALI SI KIDOGO ILA MSILEWE SIFA>>>>>Sawa jotii

 18. ANNA GABRIEL Says:

  Bravo!!!!!!!! i real appreciate your work.Nowadays on Thursday i try to be at home early so that I’ll not miss ze comedy.

  Keep it up guys.

 19. Pope Says:

  KWA WASIOWAJUA NENDA HAPA

 20. Mchunguzi Says:

  Ila Joti uache kabisa kuigiza mwanamke.
  Viguu vyako vimekomaaa! Mpaka mtu anajua kabisa kwamba yule sio mwanamke halisia.
  Au la ukiigiza mwanamke vaa suruali au max.
  Natumaini umenielewa.
  Nawasilisha

 21. amina Says:

  juzi joti kaweka mitambala kwenye maziwa ilikua inaonekana pale anaendesha gari mmmhh

 22. zawadi Hji Says:

  mko juu ile mbaya,achaneni na hao watu wanaotafsiri vibaya maneno ya Joti,hata kama watoto wanaangalia,wanajua anaamanisha nini?acheni hizooooooooooo!!!!!!!!! na mpoki jaribu kupunguza shedo ukiwa unaekt mawnamke

 23. Simon Kizito Says:

  In short…hiki kipindi choote ni upuuzi mtupu tu. Hawa jamaa wote wala hawachekeshi hata kidogo. Nilikuwa Bongo mwaka jana, kipindi nipo pale kila mmoja alikuwa anasema hawa jamaa ni kiboko, nami siku ya siku nikajitolea kuwaangalia, yaani niliboreka ile mbaya. Vitu vya kijinga karibia wabongo wote wanacheka (yaani filthless humour). Yaani mpaka leo hii sielewi tu kwa nini wabongo wanapenda hiki kipindi. Filamu za kibongo pamoja na stupid comedies like this (except Mze majuto, Mze Small, na Onyango) ziko nyuma sana tena ile mbaya…Tutafika kweli huko tuendako? Yaani vitu vya kijinga Bongo ni dili mfano wa hii comedy na Bongo Fleva.

 24. Upendo Furaha Amani Says:

  Du! Simon Kizito.
  Ndugu yangu, unajua kuwa Mdharau kwao ni Mtumwa? Kama wanaboa, Je wewe upo wapi uwe unawapa watanzania burudani isiyoboa kama ya kwao? Kumbuka kuwa: Hata Roma haikujengwa kwa siku moja. Huu ni mwanzo mzuri. Miaka ya sitini, sabini na themanini tulikuwa hatuna runinga, sasa zimekuwepo inabidi tuanzie mahali ndio tuendelee na kuwafikia hao unaowaona kuwa hawakuboi.
  Inaonekana huishi Tanzania, sasa ndugu, Tanzania bara (Tanganyika) tulitawaliwa na Waarabu, Wareno, Wajerumani (Wadachi) na hatimaye Waingereza; Je Sisi Watanzania tumewatawala akina nani?
  Du! sikutegemea kuwa mtanzania halisi atadharau watu wa kwake na kusifia wengine, bila kutambua kuwa naye hana tofauti na hao anaowaona kuwa wanaboa.
  Tuipende Tazania Nchi Tuliozaliwa.

 25. Joyce Says:

  wewe Simon kizito acha kujishaua kama umeishiwa kaa kimya ndio maana wakaita commedy umewah kuona wapi commedy ina mambo ya maana aim yake ni kucheksha at the same time na kutoa ujumbe ndan yake. kama wewe ni kilaza ulishindwa kuelewa what do they mean kaa kimya kukaa kwako huko ukibeba box basi ndio iwe tabu siku nyingine uwe unakaa kimya bwana kuliko hizo pumba alaaaaa

 26. owner Says:

  we zawadi na wewe acha kushadadia matusi ya Joti, ndiyo watoto wanajua ndiyo maana huyo mdau hapo juu aka coment. Mpaka aje atukane mbele ya mkweo ndiyo utajua. Au wewe watoto wako ndiyo wale wanaosonya watu wazima kwa hiyo hata wakisikiliza matusi we poa tu. Hongera!

 27. amina Says:

  huyu simon kizito vipi?keshajiooona…sasa wewe unatakakufanananisha na fresh prince?eti anawaua hadi akina mzee small he..kama we unaangalia wayan brothers huko shauri yako tuachie sie mdebwedo wetu bwana,bora useme hizo filamu za kibongo hata mi nitakuunga mkono lakini hivi vitu vingine eti na bongo fleva inaboa mmmh..we vipi?usijifanye unamjua sana jay zee kwenda huko

 28. owner Says:

  We Zawadi acha kutetea ujinga huo, watoto wasijue anamaanisha nini na wakati naongea live. Nashangaa unavyodadia hiyo lugha anayotumia Joti. Mi namuunga mkono mdau hapo juu. Joti atumie lugha safi siyo hizo lugha zake za ajabu zisizo na maadili. Nina wasiwasi watoto wako ndiyo wale wanaosonya watu wazima!!

 29. amina Says:

  owner bravo..mi mwenyewe nilisikia sikumoja joti anasema sijui nini sijui nini vile tena nimesahau

 30. Madoline Okeyo Says:

  Joti umetuharibu watoto hapa shuleni kwetu kila mtoto anatembea kijoti joti hasa sisi tunaosoma grade 1,2 and 3 walimu noma unawajua? wakiona mtu anatembea kijoti joti utachapwa.
  Mpoki story zako hazifanani na ukweli yaani wahaya ndio wanatembea na simu mbili mbili na perfumu?
  Nawapenda sana sipendi kukosa kipindi chenu na mimi nataka kuwa kama nyie.
  BIG UP MY Bro!

 31. nice kz Says:

  hongereni sana the comedy ninawapenda mnatupa vitu poa, hope the day pass mtakuwa juu zaidi kwenye comedy .

 32. Pot Says:

  Lakini wakati mwingine mnatuchosha maana mkazania habari ya siasa basi ni hiyo hiyo tu tunataka vichekesho , matukio yanayohusu jamii msikazanie siasa .. kwani hiyo the comedy ni show mliyoiiga marekani inaitwa CHAPEL SHOW chini ya Divid Chapel . hailengi siasa peke yake ni kama vitimbi .. ikumbukwe mambo hayo tuliyaanza miaka ya nyuma tena kwenye magazeti .. kama mnakumbuka katuni za Jemes Gayo (mchoraji wa kingo) ana makala inaitwa huu ni mji .. haina tofauti na the comedy ,

 33. mohamed pâpa Says:

  mimi nampenda joti namasanja mkandamizaji kibala naspid ni ko uo faransa

 34. sada Says:

  joti umezidi kutumia lugha za matusi punguza kidogo wengine tunaangalia na watoto wetu unatufanya tukichukie kipindi

 35. salome Says:

  joti ovyooooo sikuizi umezidi matusi


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s