BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

OLIVER MTUKUDZI NDANI YA TZ HIVI KARIBUNI January, 29, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,News,Sanaa/Maonyesho,Tamasha,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 1:31 PM

Mmoja kati ya wanamuziki magwiji na maarufu barani Afrika,Oliver Mtukudzi “Tuku” kutoka nchini Zimbabwe anatarajiwa kufanya maonyesho “live” jijini Dar-es-salaam na Arusha hivi karibuni.Hii ni nafasi adimu kwa wapenzi wa muziki,hususani wenye mirindimo ya kiafrika kwenda kumuona “Tuku” kama ambavyo wapenzi wake hupenda kumuita,akifanya vitu. Kwa undani wa habari hii bonyeza hapa.

Bonyeza player hapo chini umsikilize Oliver “Tuku”Mtukudzi katika wimbo wake maarufu Todii.

Advertisements
 

12 Responses to “OLIVER MTUKUDZI NDANI YA TZ HIVI KARIBUNI”

 1. Kalimah Says:

  BC…heshima kwenu wazee.Napenda sana mnavyotoa habari zenu.Nadhani hii ndio blogu pekee ambapo nikitaka habari kwa uhakika na iliyofanyiwa utafiti najua nitaipata.Huo wimbo mlioweka nadhani ndio utambulisho mzuri wa Tuku.Hyu sio mwanamuziki wa kimchezo mchezo.Lazima niende kumuona Tuku.

  Keep it up guys.I admire your work.

 2. Edwin Ndaki Says:

  “Todii-what shall we do?”…

  Yaani kati ya watu ambao naweza kuwataja ni mwagwiji wa sanaa Barani afrika,basi Tuku namueshimu sana.

  Kwanza upigaji wa gitaa pamoja ba uwezo wa kuchanganya vionjo vya kiasili na sauti yake.

  Natamani ningekuwepo karibu na hapo japo na mimi nimshuhudie moja kwa moja.

  Wasanii wa nyumbani kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwa Oliver,jaribuni kuhudhuria onesho lake litawasaidia sana.

  Siku njema

 3. mkata issue Says:

  WAPI OLIVER!! WAPI OLIVER!! WAPI OLIVER!!
  WIMBO UNAITA KAMA POP CORN VILE!!

  MH! JAMANI!

 4. Mama wa Kichagga Says:

  BC,

  Asante sana kwa kuugusa moyo wangu! Nyumbo za Ntukdzi nazipenda sana. Nilimpenda sana pale walipomshirikisha katika Kanda ya ya filamu ya mama mjane Neria. Yaani hata sikuweza kujua wanaongelea nini ila wimbo ulitosha kunipa hisia nini kinafanyika. Hivi kuna nakala ya Neria kwa Kiingereza au Kishwahili? Nijulishe!

 5. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  DU! KILA NISIKIAPO SAUTI NA MIDUNDO KAMA HII HUSEMA NASHUKURU MUNGU KUWA MWAFRIKA !!

  HIKI NDICHO KICHWA PIA KILICHOTEREMKA NA SAUTI YA KUMFUTA MJANE CHOZI KATIKA SINEMA YENYE TUZO YA KIMATAIFA YA NERIA!
  PIA NYIMBO ZAKE KAMA ‘CHARA CHIMWE (KIDOLE KIMOJA)’, DAME RINETAPIRA (MANENO MATAMU) ZINANIKUNA SANA!!

 6. tonny Says:

  Pongezi nyingi sana kwa waandaaji na Promoters wa ziara ya Mkongwe Oliva Mutukudzi toka Zimbabwe!Maonesho yasiishie DAR na Arusha tu,kumbukeni miji mingine mikubwa kama MWANZA, MBEYA nA DODOMA kwa kutaja michache.Nao pia wana kiu kubwa ya kuwashuhudia Nyota Wakongwe wa Kimataifa kam Mutukudzi aki perform LIVEEEE!.Ni gharama lakini KAAMPUNI YA BIA isisahau kwamba ina wateja nchi nzima!Otherwise muziki wa Oliva Mutukudzi nimeukubali, Umekubalika na wengi.Ni muziki pure african in content, hana tabia ya Copy & Paste, anajituma, anajiamini, mbunifu, hakika ni Balozi mzuri wa Muziki wa Afrika katika majukwaa ya kimataifa. Endeleeni hivyo hivyo waje wasanii wengine wengi wa kimataifa kabla hawajtutoka! BigUp.

 7. Upendo Furaha Amani Says:

  Karibu sana Oliver Mtukudzi “Tuku”; nchini mwetu Tanzania. Watanzania wenzetu wajifunze kutoka kwako siri ya mafanikio yako katika sanaa hii ya Muziki.

 8. punani Says:

  Ukimsikiliza vizuri sauti yake inafanana sana na ya chidumule sijui amefikia wapi na muziki wake wa injili haujasikika sana.Ila “tuku” yuko mbali sana natamani ninekuwa bongo lazima ningeenda kumwona.Sauti yako ni jinsi unavyoinadi hivyo wenye sauti Jide,banana stara,mr paul,mandojo na domo kaya msindwe wenyewe kupata ushauri kutoka kwake

 9. Chris Says:

  Speechless wen it comes to the music giants like Tuku.Nasikia anaishi uhamishoni, is it? Tena for political reasons. Km ni kweli serikali za kiafrika hz…. Kweli ukiona mwingine ananyolewa ww tia maji…

 10. Michelle Says:

  mhh, na nyie naye unafiki mtupu, mara hivi mara hivi, mbona hajui mziki huyu Oliver jamani,huko zimbabwe toka lini wakajua kuimba? ila mambo ya kunyang’anya waume za watu mhh hayo wanaweza. acheni umbeya.

 11. tonny Says:

  Promoters wa Tanzania WAKE UP!Tayarisheni TUZO YA HESHIMA ya kumpa Ndugu yetu MUTOTO YA AFRIKA Oliva Mutukudzi kwa kuthamini mchango wake katika kuendeleza Muziki na Utamaduni wa Kiafrika!Tanzanians we should always show the way to our fellow africans.Tuko nyuma kiuchumi lakini hatuko nyuma katika kila kitu wazee! Nyie Vipi,he!The Time is Now.God Bless.

 12. DUNDA GALDEN Says:

  MWANA MUSIC MKONGWE NI MAHILI SANANAKUMBUKA KWA MALA YA KWANZA NILIMUONA PALE KISIWANI ZANZIBAR KWENYE TAMASHA LA NCHI ZA MAJAAZI ENZI ZILE.NA NILIPOKUWEPO KULE NYUMBANI NILIKWENDA KWENYE ONYESHO LAKE AKIWA JUKWAANI NA KAKA JIKHO WALIKONGA MOYO NAFSI ZETU.
  CHAFOSA IGODENI


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s