BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

FORMERLY KNOWN AS THE EAST COAST TEAM January, 31, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 12:10 AM

 

Pichani ni baadhi ya wasanii wa kundi lililokuwa likijulikana kama The East Coast Team lililokuwa na makazi yake Upanga jijini Dar-es-salaam.Kundi hili limeshasambaratika.Unadhani kwanini makundi mahiri kama hili ambalo lilikuwa linaonekana kuwa lenye mafanikio huishia kusambaratika?Umoja sio nguvu tena?

Picha kwa hisani ya AY

Advertisements
 

13 Responses to “FORMERLY KNOWN AS THE EAST COAST TEAM”

 1. ziko Says:

  kusambaratika kuna sababu nyingi, kutoelewana kati ayw atu au pia kama wanaona hamna maendeleo, zipo sababu nyingi.

 2. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  SI KWA WASANII TU;

  ULIKUWEPO UMOJA ULIOJUMUISHA MAGWIJI WA TAALUMA, NA TENA WENYE VIWANGO VYA KIMATAIFA. PIA ULIJENGWA JUU YA MSINGI MZITO WENYE SERA NA TARATIBU MURUA. WATENDAJI WALIBIDIKA NDANI YA MAZINGIRA MAZURI YENYE FEDHA NA MALI ZISIZOHAMISHIKA ZA KUTOSHA. MIZIZI YAKE ILIKUWA MIREFU NA MIZITO; UMOJA HUU NDIO ULE ULIOUNDWA NA MAAMIRI JESHI WAFAWIDHI WENYE KAULI ZA MWISHO KATIKA ARDHI ZETU. HUU SI MWINGINE BALI NDIO ULE MUUNGANO ULIOJULIKANA KAMA EAC.

  JE MBONA UMOJA HUU WA AFRIKA MASHARIKI ULIKATIKA KAMA WAYA WENYE UMEME UKAENDELEA HATA KUCHAPA WATU WOTE WALIOKUWA KATIKA MZINGO WAKE?

  HAPA NDIPO NADIRIKI KUPANZA SAUTI YANGU NIKINENA KUWA,
  HAKUKOSEA MZEE WA HEKIMA MFALME SULEIMAN KUPITIA KOHELETH ALIPOANDIKA,

  “KWA KILA JAMBO KUNA MAJIRA YAKE….;
  WAKATI WA KUUNDA UMOJA NA WAKATI WA KUSAMBARATIKA (Paraphrased)”

  LAKINI BAADAYE ALITOA TENA CHANGAMOTO AKINENA;

  “JE MTENDAJI ANA FAIDA GANI KATIKA LIKE ANALOJISHUGHULISHA NALO?” (Yaani ama katika kuungana pamoja au kuachana)

  Kumbe kusambaratika kunaweza kuwa ni tukio la kishujaa la kusifiwa au lenye athari chanya katika maendeleo ya mwanadamu pia. Hivyo ni vema kabla ya kuhukumu tufanye uchambuzi wa kina kutathmini maisha ya WASAMBARATIKAJI binafsi na maendeleo ya usanii kati ya sasa na walivyokuwa pamoja ndio tuseme kuwa walijilisha upepo chini ya Mbingu.

  Sababu za vikundi vya muziki kusambaratika zipo tu nyingi katika maisha. Nakudondosheeni NNE tu ambazo hujitokeza mara kwa mara:-

  a. Kukata tamaa kutokana na Kutofikia matarajio yao (unmet expectations). Unajua kuna watu wengi ambao huungana (kwa mioyo tu bila vichwa) wakiwa na matarajio tofauti kabisa na uhalisia. Mfano vijana wanaweza dhani kuwa wakiungana wakatoa Album yao basi ikianza kuuzwa tu wataukata bila kufikiria malipo ya gharama na pia muda halisi wa kazi mpaka kikundi kitakapoanza kutengeneza kweli faida na hadi kufikia utajiri wanaoufikiria.

  b. Mafarakano yasiyosuluhishwa (Unresolved Conflicts) kutokana na ukinzani wa kifikra na uelewa ndani ya wana kikundi (Wasanii) hii inaweza kutokana hata na matukio ya aibu ya kugombea wapenzi au kugombea umaarufu au pia ugomvi kati ya wenye Asasi/ vyombo vya mziki na Wasanii wenyewe nk

  c. Uendeshwaji wa vikundi / Asasi bila kufuata misingi ya menejiment iletayo ufanisi ambazo hujumuisha uwepo wa demokrasia, malipo ya haki, mipango, uwajibikaji na ruhusa ya kuendelea vipaji. Haijalishi kikundi ni cha familia moja au la, hizo kanuni ni nyeti sana.

  d. Kushindwa kuendesha asasi kutokana na ukosefu au upungufu wa fedha. Vikundi vingi huishia kuwa na mikopo na madeni kibao kiasi cha kufika kufirisiwa.

  Nyakatakule anaomba kuwasilisha!

 3. Matty Says:

  Swali!!kwanini mnatengana wakati umoja ni nguvu??
  lakini mnajitahidi napenda nyimbo zenu wote! hasa
  GK – Hawa ndio simba wa Africa
  AY-rusha mikono juu kama hufagilii mambo ya kishamba na FA- Unanitega!!!!!!aaaaambona miguu iko nje heeeeeejamani wengine siwajui fresh hasa bro mwenye red t-shirt ~~!!!!!!kazeni butzzzzzzzz mazee!!!!muoe sasa kama banana na nyie!!!!kuliko kusarandia vitotozzz mitaa ya sea view!!!!!!

 4. Dinah Says:

  Ikiwa Umoja ni nguvu kwanini wanatengana?

  Umoja wao haukuwa wa kufanya kazi pamoja, umoja wao ambao uli-base zaidi kimagharibi (waliiga kama kawaida) ulikuwa wa ushindani au kwa kiswahili chepesi ubaguzi, walijibagua na wale wa Uswahilini labda kwa vile wao walikuwa mabraza duh na wale wengine ni wangoto, wasela, wagumu (which cms like mtindo wa Rap really).

  Japo kwa wenzao wa US walikuwa wakijigawa hivyo kutokana maeneo watokayo, utashi na wanavyoghani…… Mfano kughani kwa P Didy, Hayati Big popa (hawa all was about themselves a.k.a misifa)ni tofauti kabisa na ule wa Snoopy D, Dr dree(walikuwa wakichanganya misifa na real life)……vilevile hao wote wanaghani tofauti kabisa na Common auwale walioimba “can I kick it”?(hawa wana-base kwenye real ife na mistari yao imekwenda shule), vilevile ukimsikiliza DMX anaghani kivyake na alitoka na kundi lake pia.

  Thank god Pdidy na Snoop wameua tofauti zao na hata kufanya kazi pamoja ili kutogawa mashabiki wao hasa baada ya vifo vya marafiki zao 2Pac na yule Ndimbo (big popa).

  Nikirudi kwenye swali, kwa vile umoja wao haukuwa ume-base ktk kazi nadhani walihisi wanazibana kisanii kwamba wewe kila leo una-korebo/kolebo na wenzako (chagua sahihi) lakini hakuna unachokipata na mbaya zaidi kipaji au uwezo wako unauwawa taratibu.

  Umoja ni nguvu ikiwa nyote mnamalengo au lengo moja la kimaendeleo sio kushindana kimavazi, aina za magari na wapi mnaishi.

  Wkd njema!

 5. Matty Says:

  Asante Dinah Kwa jibu i get u!!!!swali la kizushi! hivi wewe ni Dinah Marios?au Dinahicious…mamaaa maloveddavi??? nakutania usijibu maana hapa wazushi hawakawiagi kurusha makombora.!!!!!!!!!

 6. Dinah Says:

  Poa, Ila ngoja niweke sawa kuhusu jina langu (M-Jamaica ukikosea kutamka jina lake inakuwa vita) sasa na mimi huwa naudhika kuona watu wanatamka tofauti au even kuliandika tofauti.

  Napenda watu wajue tofauti ya jina langu ambalo ni Dinah (with h) si lile Dina (without h).

  Jina langu linatamkwa kwa kuvuta kidogo ile “i” kama unavyotamka “e” unatamka “Dena”

  Na jina Dina (bila h) kama Dina Marios linatamkwa kama unavyotamka mlo wa jioni kwa kiingilishi kwamba Dinner/Diner na unalitamka kama linavyoandikwa Dina au Dinna bila kuvuta “i”.

  Asante!

 7. BongoSamurai Says:

  Bongofleva na wasanii wetu bongo kazi kweli kweli..
  Kuwa kwenye kundi ina maana kuwa pamoja na kushirikiana katika kufanikisha malengo yenu yaliyowaleta pamoja. Lakini pale mnapokuwa pamoja kama kundi na papo hapo wengine kujiamulia au kufanya mambo bila kuzingatia muundo uliowaleta pamoja hii inaweza ikawa ni tiketi tosha katika kulisabaratisha kundi au muungano wowote ule.
  Kila la kheri naamini sasa kila mtu yuko kivyake, hakuna kubaniana mambo yatakuwa poa.
  Au vipi washkaji…

 8. Dina Says:

  Ha ha ha ha Dinah umeniacha Hoi…

 9. agogo Says:

  well well Eastcost unajuwa watu wanaponda kuhusu jamaa kujitenga lakini sio kwamba wamijitenga na watoto wa uswazi imetokea wana mawazo yaliyokuwa yamefana angalia style yakina juma nature na Ay,Falsa au GK ni tofauti thats y kuna R&B na hiphop and funky music ,lakini hamuoni hata wao wamekuwa sasa wametengana! kwa ufupi kwanza tanzania waimbaji ni wachache sijawaona walionifurahisha , kunatofauti ya kuwa muimbaji na kupenda kuimba sasa wabong wanapenda kuimba ,mfano bongostarsearch kweli kunamuimbaji meona tokea ianze kama wanatafuta seriously washindi wachukuwe wanaimba lugha yoyote maana if uo want to help some one is to be in an international level mtu yoyote aneimba lugha zote mbili either swahili & english ingekuwa nzuri zaidi. jamani ni maoni to msianzee

 10. ugele Says:

  mwaya unaweza zaliwa na nduguyo tumbo moja na msielewane sembuse wasanii, mtaungana baadae, msigombane tuu

 11. annabell Says:

  daah siamini hii ni uzuni,come up guys acheni hizo inabidi tukomae au vipi?

 12. Franco Says:

  mimi naona GK alikua anajiona yuko top sana so wasanii wengine kwenye kundi hawawezi kufanya lolote na anaujua mziki kumbe hamna kitu so guyz keep it real kuweni pamoja even if hauwezi ukakamua maji kwenye jiwe yakatoka au siyo ila you must force in one way ya BIG LOVE kamavipi


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s