BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 05 February, 3, 2008

Filed under: Photography/Picha,Swali kwa Jamii,Tanzania/Zanzibar,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:10 AM

 

Picha ya wiki hii imepigwa na ni kwa hisani ya Mpoki Bukuku.Pichani ni mafundi wa barabara wakiifanyia ukarabati au kuipiga msasa barabara ya Nyerere(zamani Pugu) inayoelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.Hii inakwenda sambamba na maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani George W.Bush nchini Tanzania hivi karibuni.

Swali gumu ni kwamba hivi kwanini siku zote huwa tunasubiri mpaka kuwe na “ugeni” fulani ndio tutengeneze au tukarabati vitu mbalimbali kama inavyofanyiwa hii barabara?Kwanini? Hii ndio picha yetu ya wiki hii.

Advertisements
 

8 Responses to “PICHA YA WIKI # 05”

 1. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  Moja ya maana ya halisi ya DHANA YA UMASKINI ni SEASONABILITY yaani kuishi kwa mitizamo na vitendo vya ki-MAJIRA! Hatufikiri juu ya kuwa na maisha ya muendelezo.

  Tuna umaskini wa mipango na hivyo tunawezasema kuwa tuna u-MAJIRA wa mipango pia.

  Leo Rais anatembelea Babati basi watu hawalali, ndio barabara inakwanguliwa usiku kucha mpaka na wafanyakazi waugue na watu wote wapate mafua ya vumbi. Halafu akishapita basi tunasubiri MAJIRA ya ujio mwingine pengine wa Waziri Mkuu, wa Rais wa Marekani au wa Papa au sijui wa …………

  Hasara ya mipango ya namna hii sio tu kuwa husababisha maumivu ya ghafla makubwa kwa watu wanaotengeza hizo barabara au kupaka rangi shuta shuta na wanaoishi maeneo hayo; bali zaidi TUNAENDELEZA UTAMADUNI WA KUFIKIRI KUWA BARABARA NZURI NI KWA AJILI YA WAGENI AU WAKUU FULANI BADALA YA KUONA KUWA HAKIKA NI MUHIMU ZAIDI IWE NzURI KWA WATUMIAJI AMBAO NI WANANCHI WANAOKAA MAENEO HAYO NA KUITUMIA KILA SIKU!

  Mwisho huwa ni tendo la kuwadanganya wakuu kwamba hali yetu huwa ni nzuri kiasi walichokikuta wakati si kweli.

  WANANCHI WANAPASWA KUNGÁMUA HIYO DANGANYA TOTO NA TUSI HILO KUBWA NA KWA KUTUMIA MAHAKAMA ZA JAMII (MIKUTANO YA WANANCHI) WANAPASWA KUKATAA KWA NGUVU ZOTE KAZI ZOZOTE ZENYE MWELEKEO WA KUWAPENDEZESHA WAKUU NA WAGENI BADALA YA KUWATAKA HAO WAKUU WAISHI NASI MAISHA TULIYONAYO ILI KWA PAMOJA TUFIKIRI NAMNA GANI TUTAWEZA KUTATUA MATATIZO YETU KWA USHIRIKIANO.

  Viongozi shupavu na makini hutambua na kuwaumbua viongozi wachovu wanaotaka tuishi ki- MAJIRA MAJIRA. Hii haiitaji uwe na FBI kutambua kuwa maendeleo yanayooneka ni ya ki- Majira. Hata pua yako tu inaweza kunusa kuwa hii rangi au hii rami imepakwa hivi karibuni! Hata tairi za gari lako nazo zinaweza kukusaidia kuwasiliana nawe kwa namna kwenye lami ya wiki hii hata nyuso za wafungwa au wanafunzi au wanakijiji na mawasiliano ya maungo yao (Kinesics) huweza kukueleza kama hali uionayo wakati huo ni ya kila siku au ni ya kupandikizwa katika MAJIRA ya ujilio wako.

  Je, mnakumbuka Baba wa Taifa (RIP) alivyo n’goa ile migomba iliyopandwa masaa machache kujaribu kumpendezesha juu ya kilimo cha kufa na kupona? Je unakumbuka jinsi Mratibu wa Kisomo cha Elimu ya Watu Wazima alivyoumbuliwa kwa kuwagawia wazee madaftari mapya na kuwambia kukopi na kukariri notisi za ‘pamba ni fedha, uhuru na kazi, ushirika na maendeleo’ masaa machache kabla ya ziara ya Mkuu?

  WA KULAUMIWA ZAIDI SI VIONGOZI NI SISI TUNAOKUBALI KUTUKANWA NA KUONGOZWA KI-MAJIRA MAJIRA!I

 2. mdunger Says:

  huo ndio utamaduni wetu kwani nakumbuka hata mashuleni hukarabatiwa wanavyokuja viongozi wa serikali.Ili tufanikiwe tuombe kila mwezi waje wageni wa dizaini ya Bush.

 3. Gervas Says:

  Mi nafikiri ni ka-utamaduni ketu wabongo. Maana utaona issue hii inaanzia nyumbani. Kuvalisha watoto nguo nzuri akija mgeni, au siku ya siku kuu, au kubadili menu mgeni akija, au kuvaa vizuri siku ya sikukuu au kwenda auti. Hivo hii tabia inaenda mpaka hapa tunapojadili. Hii ni kutojiamini, kutojikubali, hii ni ukweli wetu tuko hivo naweza iita ni asili yetu. Ni sawa na kuishi maisha ya album, yaani mtu ukitaka kupiga picha lazima upendeze kwanza, upige pamba..kwa nini? hivo mi sishangai sana hao wanachokifanya saizi. Maana hiyo fedha ingetumika kukarabati sehemu korofi ya barabara pale singida, au daraja hatari la kule moro ambapo wananchi wanavuka mto mkubwa kwa kamba!!!

 4. Pope Says:

  “MGENI NJOO MWENYEJI APONE”
  Msemo huu ni wa wahenga walilijua hilo ndio mana ukawepo mpaka leo.
  Matatizo ya Cash budget unafanya kilichoko mbele ya macho yako kwa wakati huo hakuna mipango endelevu.
  Makampuni ya madini yote yako Dar yapeni waraka kuchangia maendelea kama Botswana yanalazimika kuchangia moja ya nyanja za maendeleo ya kijamii ama Elimu, ama Matibabu au Ujenzi wa Barabara kwa nini isiwe na kwetu kama hawataki si waondoke?

 5. Matty Says:

  Kweli jasili haachi asili!!!!mpaka mgeni aje ndo tunaanza kukimbizana???siku zote walikuwa wapi???bora hata wangeacha hivohivyo huyo Bush aone mabarabara yetu yalivyo mabovu tu!!!

 6. lugano kasambala Says:

  Kama ndio mpango huo tunaombea wageni wa namna hii wawe wanakuja mara kwa mara. Tena napenda wawewanapitia njia ya Tabata kupitia shortcut ya vingunguti machinjioni. Unaona bwana! ikiwezekana pia wapitishwe njia ya kinyelezi au munaonaje? wadau kwa wale walowahi kupita maeneo hayo.

 7. Albert Says:

  Ujenzi kama huo umekuwa maradhi sungu Tanzania na mabadiliko yake yatachukuwa maelfu ya miaka Na hata ukiangalia hiyo picha utaona kuna ukosefu wa kiongozi kufuata maadili katika sehemu za kazi kama hizo kwa mfano ukiangalia huyo Bosi katikahiyo picha hapo unaweza kujiuliza huyu bosi anafuata maadili ya kazi hiyo swali hapa hivi HivyoTanzania hakuna kitu Health and safety Angaliyeni huyo bosi kivazi alichovalia jee alikuwa hajuwi anakwenda kutembelea eneno la kazi na lina miko yake? tunapoanza kuacha mambo mepesi na ndio makubwa yana haribika na hiyo ndio intuletea kuwa na mabarabara mabovu kila kukicha Tutazidi kuwasifu na kuwashangaa wazungu kwa maendelea Halafu yake tunasema eti tutawakuta siku moja ,labda watusubiri na hata kama watatusubiri basi Hatutawafikia (Wafrika Tumehafilika )Viongozi waoneshe mfano na sio ( Majionesho)

 8. hater Says:

  Ah, huu ndiyo ujenzi wa barabara? come on now……. tunayeyushwa vibaya…


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s