BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PROF.ISSA SHIVJI February, 4, 2008

Filed under: African Pride,Elimu,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 8:57 AM

 

Profesa Issa Shivji,mmoja miongoni mwa wasomi na wahadhiri wanaoheshimika sana nchini Tanzania.Wale waliopitia Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam wanatambua zaidi mchango wake.Swali gumu ni je tunawasikiliza kwa makini wasomi wetu wakitoa shauri mbalimbali za kujenga na kuendeleza nchi?

Picha kwa hisani ya Bob Sankofa

Advertisements
 

6 Responses to “PROF.ISSA SHIVJI”

 1. Gervas Says:

  Mimi nafikiri kulikuwa na haja ya kuwa na chombo maalum kikawa kama ndo kisima cha busara ambapo development plans za nchi na swala zima la kuutokomeza umasikini zingekuwa zinachukuliwa toka chombo hiki, kwani ni wazi kuwa mbali na kusoma sana wana experience inayojengwa na tafiti mbalimbali. Tatizo utaratibu wetu wa kukiachia chama kinachotawala kuplani maendeleo ni hatari maana siasa siku zote inafuata interest na sio maslahi ya wote. wasomi kama hawa wanatizamwa tu mpaka wanakufa na knowledge zao walizozijenga miaka mingi, ukitizama kuna research, report,seminar nyingi lukuki zilizokwisha fanywa na wasomi wakapendekeza, haya yote huishia dust bin. Maana ukitizma siku zote ushauli wa wasomi huwa haufuatwi bali politics ndo inatawala. watu wanakalia ku-focus ni kitu gani wafanye ili wachaguliwe tena uchaguzi ujao!! Haina maana watu hawa kuachwa tu, it is at this point where they have to be fully utilized!!

 2. Mwana wa mkulima Says:

  Kwa kweli huyu bwana ni hazina ya taifa sema tuu watawala wetu hawalijui hilo na hata kama wanalijua ni mafisadi hawawezi kulikubali hilo. Shivji Is just an incredible professor. Ni mtu ambaye yuko katika ulimwengu wake kwa kutetea haki za wanyonge na wakulima. Ohh Issa, be blessed and Iam sure Almighty will reard you for your untiring efforts to wrestle the syatem..

 3. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  PROF. SHVIJ,
  HESHIMA YAKO!

  GERVAS NAKUBALIANA NAWE KABISA!

 4. Mr. Upendo Furaha Amani Says:

  Tatizo la Taifa letu la Tanzania ni SIASA. Wasomi watasikilizwa pale ambapo “wana muelekeo fulani” ambao utawanufaisha wanasiasa fulani. Kuna tafiti nyingi zimeshafanyika, kuna shauri nyingi zimeshatolewa na wasomi mbalimbali hapa Tanzania, lakini kama kuna 1% zilizo fanyiwa kazi, ni kushukuru, maana nyingi zinaonekana kunyang’anya baadhi ya Wanasiasa TONGE mdomoni. Mie kwa ujumla ninaunga mkono hoja kwa kusikiliza kwa makini shauri wanazotoa wasomi wetu na kuzifanyia kazi.

  Samahani BC.; nichekeshe kidogo:
  Hivi wale wanaosema Miss Tanzania 2007 Richa Adhia si Mtanzania;
  Je huyu Mheshimiwa Profesa Issa Shivji ni wa wapi?

  Watanzania Tupendane, Tusibaguane kwa lolote iwe ni kwa Asili, Dini, Rangi, Kabila au kwa lolote. Sisi sote ni watoto wa Mama Tanzania.

 5. juma Rioba Says:

  Issa Shivji simtofautishi sana na wanaharakati wengine kama hayati Seithy Chachage, Haroub Orhman na wengine. Elimu ya kweli haimtenganishi msomi na jamii yake. Hawa wamethibitisha haya kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa kwa kutumia silaha kali ya “mawazo yao”.
  Wengine wakishapata elimu kiduchu tu ama senti kiasi basi hawana ‘shirika’ tena na wananchi walio wengi.
  Kumbuka kwamba kwamba ‘mafanikio’ yanakuwa mafanikio pale ambapo kuna mafanikio.mafanikio ya mtu mmoja katika jamii ni sawa na punje ya haradari katika dimbwi kwani hayaonekani na pia,mara nyingi, hayadumu.Tupiganie utaifa na tuambiane ukweli.

 6. NYANGE MTORO Says:

  Mzuka sana napenda kuwapa big up viongozi wa awamu ya nne kwa kiwango kikubwa wamechemka kwani hata kidogo hawatumii mawazo ya wasomi wetu mfano prof Issa Shivji ni miongoni mwa wasomi ambao selikari inayo tuongoza kwa kufurahia kuona wananchi hatuna elimu haimtumii vizuri Issa ni mkali mi nakili hilo angalia bunge letu vilaza wamejaa angalia baraza la mawazili vilaza pia wamejaa wakuu wa mikoa na wilaya ndo usiseme mjomba akikujua unakupa.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s