BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

JK AVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI,AKUBALI OMBI LA EL February, 7, 2008

Filed under: Breaking News,Developing News,Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 2:51 PM

 

Habari zilizotufikia hivi punde zinapasha kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete,amekubali rasmi ombi la kujiuzulu la aliyekuwa Waziri Mkuu,Edward Ngoyayi Lowassa.Rais pia amelivunja Baraza la Mawaziri.

Advertisements
 

28 Responses to “JK AVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI,AKUBALI OMBI LA EL”

 1. kijiwe Says:

  safi sana vunja mpaka hiyo mikono na midomo iliyocheza hayo madili

 2. mwalimuzawadi Says:

  Sasa JK apange makuwadi tena aone. Safari hii tutawakataa kwa kuzomea kama hawafai. Pia ana nafasi ya kufinya baraza, watu ni wengi sana, 60?

 3. Big up JK. Huo ni uamuzi wa ukweli kabisa. Huku niliko nafurahishwa sana na mambo yanavyoenda nyumbani huko. Naanza kupata imani ya kurudi bongo one day. Daima naamini wewe uko safi sana. Ila hao jamaa ndio walikuwa wanakulet down sana. Kwa mwendo huo TZ itaenda fresh sasa.

 4. Kimori Says:

  This was the only expected move.

  I hope this time the president will use the golden opportunity and a bit of wisdom to trim down his cabiinet.

  It has been a delight for many Tanzanians, that at least there is a beam of light at the end of the tunnel. We need people who are competent and result-oriented and not the rogue ministers as the prvious ones, because we have lost the past two years without tangible results.

  Take time and pick among the 38 million Tanzanian a well-organised team, which can steer forward our country – a big reshuffle is required.

  Remember the following quote from Eleanor Roosevelt, “One’s philosophy is not best expressed in words; it is expressed in the choices one makes… and the choices we make are ultimately our responsibility”.

  We really need genuine changes.

 5. mathias Says:

  Kazi ni kubwa na inaitaji ujasiri mkubwa, tunachokiona na kukisikia uwenda ikawa moja ya kumi ya mambo yote. Ikiwa Mungu atafungua milango na kuta za hawa mafisadi, nchi hii watu watatafutana! Kuna wengine tunawaona kama kondoo kwa muda huu lakini ukweli ni kwamba ndani ya chama kumejaa mafisadi wa kutupwa hakuna sehemu utasogea ukawa salama pasipo kuwa karibu na fisadi. Mie naogopa ata kuchukua kadi manake ile kuitwa tu mwanachama tayari harufu ya ufisadi imekupata. Tunaitaji wananchi wa kweli ili nchi hii isonge mbele. Watu ambao hawajawai kuhusika kwa namna moja au nyingine na serikali za mafisadi zilizopita ndo tunaowaitaji. Itanishangaza kama baadhi ya mawaziri watarudi maofisini.

 6. Msukuma wa shy Says:

  Edo ndaki mcheki edo mwenzio hapa anabanjuka tuhttp://www.eastafricantube.com/media/2448/Ze_comedy_-_Waziri_Mkubwa/

 7. Chris Says:

  Tunataka sura mpya kbs kwenye baraza jipya.

  Lkn sura mpya zitakuwa ni meaningless kama hawa mabwana akina Lowassa, Msabaha, Karamagi,Mkapa etc hawataadabishwa. They’ve to pay for what they’ve done.

 8. stimela Says:

  safi sana mzeee wakazi JKkanyaga twende!,narungu lako liwafikie wote waliohusika,inasikitisha kuona nchi inaporwa na wachache bila huma!!,Faza jk hakuna cha tume,wala nini haohao watawataja na wenzao,awali dagaaa waliangaliwa kwa jicho kubwa wakati papa na nyangumi wakitafuna ile mbaya zamu yao sasa Faza,mie nukupa big up sana mzee

 9. Adeel Says:

  Hongera sana mzee JK, angalau na sisi tulioko huku ughaibuni tutajisikia kuwa tuna serikali inayofuata utawala wa sheria. Ila tu tunakukumbusha Rais wetu usingoje mpaka akina Zito Kabwe na Dr. Slaa watikise bunge ndio ufanye kweli. Watu wa kazi unao huwatumii?.
  Kama Lowassa anadai hahusiki basi atutajie wanaohusika, yeye si ndio kinara wa mawaziri?

 10. Edwin Ndaki Says:

  Kwa stahili hii..

  Leo napat anguvu kuandika..TUTAFIKA sasa..

 11. Herman Ngonyani Says:

  JK ukitaka heshima yako irudi weka urafiki na uanamtandao kando kwani sio marafiki wala wanamtandao waliokupa hayo madaraka ya urais bali ni sisi wananchi ambao kuna kipindi unatusahau na kutudharau eti ni ni kilele za mlango zisizokuzuia kulala.

  Kwa kiwango kikubwa ugumu huu wa maisha ya watz ni matokeo ya ufisadi na ubinafsi uliokithiri wa baadhi ya mawaziri wako pengine ni nafasi yako nzuri sasa kufanya kweli.

 12. mdau Says:

  Kujiuzulu haitoshi, inabidi wakamatwe uchunguzi ufanywe na ikibidi wafilisiwe ili hela yetu irudi, ikiwezekana wanyongwe hadharani ili iwe fundisho kwa wengine.
  Na kashfa nyingine zoote zifanywe kama hiii,benki kuu,buzwagi,meremeta,iptl,kiwira zipo nyingi mno.
  Mungu waangaze mafisadi wote, amin

 13. Liz Baraka Says:

  Safi sana lakini sheria ifuate mkondo wake, ingekuwa mwananchi wa kawaida, kwa ushahidi ule, saa hizi yuko keko, ukonga au segerea. Natumaini baraza jipya litakuwa na mawaziri wachache, wasomi, na wachapakazi, na halitaangalia uswahiba.

 14. lugano kasambala Says:

  Hongera sana mh. rais wetu kwa uamuzi wa kukubali maombi ya mh. lowasa, sasa huu ni wakati mzuri wa wewe mh. kujipanga upya na kufanya mambo mapya.

  Sio siri wananchi tulikuwa tumeanza kupoteza imani na serikali yako kumbe si kosa lako ni kosa la baadhi ya mafisadi wenye uroho wa mali. pole sana mheshimiwa wetu kwa yote.

  Tunachoomba haya mambo yasiishie kwenye kujiuzuru tuu, hapana utunaomba hawa watu wachukuliwe hatua za kisheria bila kujari ushkaji muliokuwanao. Tafadhari yapeleke kisheria, ushkaji baadae. Hata ikitokea wamefungwa utaenda kuwacheki ukonga kama vp!

 15. salekio Says:

  mungu amjalie rais wetu, akaweze kufanya maamuzi yenye busara katika kuchagua baraza lake. i hope this time nitaona sura ngeni nyingi, na baraza lenye watu wanao stahili hata kama ni kumi ni bora kuliko watu 60 ambao kila kukicha wanatafuta mianya ya kufanya ufisadi

 16. Kaka K Says:

  Mh.Raisi, hicho ulicho fanya ni sehemu ndogo saaaaaaana ya mambo uliyoyaahidi wakati wa kampeni na ndo maana waliona wewe ni mwenzetu. Sasa basi mimi nitatoa hongera zangu mara baada ya uteuzi wa team mpya na kisha nini kitafuata kwa hao makuhani wa ufisadi. Sikatai kuna mambo yatafanyika kulinda maslahi ya chama ila 90% iwe ni kwa ajili ya nchi na wananchi wake masikini. Kila kitu unacho mkononi ni wewe tu sasa kufanya kazi kama itakayo jenga heshima ya nchi na yako binafsi kwenye uso wa mataifa mengine. Mwisho, ukisikia minong’ono ujue kuna jambo pia watu si wenda wazimu wazushe vitu visivyo na uhakika na hili basi likupe changamoto usimwache hata mmoja aliyehusika kutia nchi umasikini usio na kifani.

  MUNGU IMULIKE SERIKALI, MUNGU WABARIKI WATANZANIA

  Kaka K

 17. LWABULINDA JOSEPH Says:

  AIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU
  KAKA YANGU JK MWALIMU MAREHEMU JK ALITWAMBIA WATANZANIA WOTE BILA KIFICHO KUWA EL UTAJIRI ALIONAO NA UMURI WAKE VITU TOFAUTI HIVYO HAFAI KUWA KIONGOZI WA NCHII WEWE UKAWEKA PAMBA KWENYE MASIKIO SASA AIBU HII UMEKILETEA CHAMA CHETU NA WATANZANIA KWA UJUMLA. SASA NAFASI UNAYO YA KUREKEBISHA MAKOSA USITULETEE UOZO TENA

 18. amina Says:

  haya vunja hilo baraza weka manyang’unyangu mengine..hawa wote mafisadi hadi vyama vya siasa vipige kelele.wao wenyewe wanalindana na bado spika sitta hafai

 19. tonny Says:

  Rais Kikwete,hii nifursa yako pekee kufungua ukurasa mpya wa kisiasa hapa nchini.Bara zima la Afrika na Dunia nzima macho yao yote yame elekezwa hapa Tanzania.Kwa nini?Kwa sababu pamoja na matatizo na mapungufu ya kisiasa na kiuchumi yaliyopo nchini,Tanzania bado ni kielelezo cha mfano bora wa Mwelekeo wa Bara zima la Afrika katika karne kadhaa zijazo.Kiswahili kina nafasi kubwa ya kuja kuwa lugha pekee asili itakayo zungumzwa na Watu wengi zaidi wenye asili ya Afrika na wageni watakao penda kufanya biashara na Afrika.Tanzania ni kielelezo cha Ukombozi wa kisiasa barani Afrika.TANZANIA HAS A HISTORIC ROLE TO PLAY IN AFRICA.Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.MAGEUZI NA MABORESHO YA DHATI KATIKA NYANJA ZOTE YAANZE SASA.Ili Tanzani tuwe Mfano Bora kwa wenzetu wote barani Afrika katika Utawala Bora na Mahusiano ya Kijamii.Nina mengi ya kusema.Lakini itoshe kwa kumuasa Rais Kikwete haya machache yafuatayo:Uamuzi wa Lowassa ni mchungu lakini Siasa ndivyo zilivyo.Kilchobaki ni kusonga mbele hakuna kurudi nyuma.Usifanye haraka ya kutangaza Baraza lako jipya la Mawaziri.TAKE YOUR TIME DEAR PRESIDENT!Watanzania tupo tayari kusubiri bila ya serikali hata kwa wiki mbili.Heri uchelewe kuteua Mawaziri wapya lakini uteue wachache na walio bora KULIKO kuwahi haraka haraka kuziba hizo nafasi na kuteua Mawaziri wasiokubalika na hawafai katika Uongozi wenye dhamana ya Uwaziri.Wazee wangu wote wenye umri mkubwa waweke pembeni.Na kama ni wazuri kiasi hicho kwamba huwezi kuwa mbali nao basi wawe washauri wako katika nyanja mbalimbali lakini siyo Uwaziri au Makatibu Wakuu.Uteuzi utakao ufanya sasa ndiyo utakao kuhakikishia ushindi wa kutakata katika uchaguzi mkuu ujao 2010!Kila utakaye mteua ndiye atakaye kuwa tafsiri na kielelezo cha fikra,tabia,dhamira na mwelekeo wako Mh.Rais!Watanzania watakutathmini wewe kupitia wale utkao wateua kuwa Mawaziri na katika nafasi nyeti za Uongozi.Kwa jinsi utakavyo lishughulikia kikamilifu na ipasavyo suala hili moja tu la Richmond ndivyo litakavyo punguza hasira ya watanzania katika matatizo mengine yaliyo bakia ya Buzwagi,Benki Kuu na mengineyo.Na watakuelewa makusudio yako nakukubali kuwa na subira katika hayo mengine.Usiogope kufanya kazi na sura mpya za viongozi ambao hawajapata kusikika katika nyanja za kisiasa.Ndiyo maana nikatoa ushauri kwamba katika hili asikusukume mtu.Wewe binafsi ndiye uliyeubeba Msalaba huu wa kuwavusha Watanzania.Utakabiliwa na majukumu mengi ya Kitaifa yatakayo hitaji marekebisho na mwanzo mpya.Lakini pia utakabiliwa na majukumu mazito zaidi ya kuhakikisha kwamba Viongozi wenzio wa nchi za Barani Afrika waliotoka nje ya mstari na kuzitumbukiza nchi zao katika migogoro mikubwa zaidi ya kisiasa, wananufaika na kisima cha hazina ya busara za kisiasa kilichopo Tanzania kilicho chimbwa na mababu zetu na kuja kuboreshwa na Mwalimu Nyerere na kuendelezwa na viongozi waliofuatia na kulindwa na watanzania wote katika ujumla wao kwa manufaa ya vizazi vijavyo.Tukumbuke Tanzania tunayo ijenga sasa ni ya watoto wetu na vizazi vijavyo,siyo yetu.Tanzania yetu ilishapita ni ile tuliorithishwa na mababu zetu!Wote tunaijua.Mrejee Muumba Wako,Sali na Umuombe kwa Dhati atakushushia MWANGA!

 20. Dada wa Kihaya Says:

  Safi sana Mkuu, vunja vunja tu hata wakimaind kimpango wao!
  Watoe wazee wote weka vijana wachapa kazi ikibidi changanya na wapinzani kidogo ili kuleta ladha halisi ya democracy ,kama CCM wameshindwa unadhani what next?

  Hapa ndo huwa nachoka na siasa za bongo!UFISADI hata aibu hawana hawa MAHARAMIA!uongo uongo, utapeli unafiki mwingi wa kichinichini tu!
  Pls Jk wafilisiwe hawa watu, haina haja ya kucheka nao ushawapa nafasi wamezichezea kifisadi badala ya kufanya kazi kwa maslahi ya wananchi wote wanajinufaisha!
  NAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA KATIKA UTEUZI WA PM NA MAWAZIRI SAFI.

 21. noah gondwe Says:

  Sio siri J.K ana kazi ngumu, tatizo kubwa ni kwamba CCM wanabebana sana na yote tunayaona bungeni. Kipindi kile Mh Zitto Kabwe alivyoleta hoja ya madudu ya Karamagi wenzake walimtetea, ila sasa naona wana CCM wameanza kuchochwa. J.K anatakiwa awe strong kwenye maslayi ya nchi na sio ya kichama. Huyu Karamagi na wenzake wote akaunti zao zichonguzwe na ikioneka wamejilimbikizia mali, zote zirudishwe serikalini. Nakupongeza sana Raisi wangu Kikwete kwa kuvunja baraza lako la mawaziri ila pongezi zangu za dhati na kwa moyo wote ni pindi utakapowawajibisha hawa mafisadi wa nchi yeta. HAKUNA CHA URAFIKI KWENYE MAFISADI WA NCHI YETU.

 22. Dinah Says:

  Madau hapo hakuna haja ya uchunguzi wala kuendesha kesi hao ni moja kwa moja kufirisiwa alafu jela kifungo cha maisha. Mambo ya uchunguzi (mwingine) na uendeshaji wakesi ni kupotezeana muda na pesa. Tume iliyowaanika ilifanya uchunguzi na kupata kilichopatikana.

  Hivi Kogoda yuko wapi? 🙂

 23. Dinah Says:

  AlafuThis time Kikwe punguza mawaziri wasio na mpango (kila waziri anakuwa na makamuwake basi) mambo ya “Waziri sijui wanini katika ofisi ya nini inayoshughulikia nini” ni kuchezea senti za mvuja jasho, punguza uwingi ili ku-save pesa tupanue barabara.

  Kila lakheri Kaka!

 24. Bangusilo Says:

  SISI TULIWAPENDA LAKINI RICHMINDS ILIWAPENDA ZAIDI NJINA LA ……. LIHIMIDIWE

 25. Dinah Says:

  I meant Waziri wa nishati na madini wa miaka ile Mr Kigoda.

 26. Mama wa Kichagga Says:

  BC

  Jamani tunapoongea hapa tupige picha kule vijijini! Achilia mbali mijini ambako watu wanashindwa kumudu hata mlo mmoja! Hela waliyokuwa wanalipana kwa mwezi @ mtu mmoja ingetosha kabisa kuwalipa social benefit allowance WaTZ milioni 4 @ mtu sh. 30,000/mwezi sawa na sh. 120,000,000,000 kwa nchi nzima!

  Hii changamoto [wind of change] lihamie ndani ya mawizara na idara zote za serikali na watu binafsi kama kweli tunamedhamiria kupambana na ufisadi kwani huko ndiko visima na chemichemi za ufisadi. JK yaani ni vijikundi vya mafisadi vimejitega kila mahali vikiamini bila mission town maisha hayaendi. Watu wanaishi kama mtoto wa mama na mototo wa kambo yaani ni unyama unyama tuu. Chunguza utapata majibu haya yote na kuzidi.

  NB: Mh. JK Watu wanahasira si vijijini si mijini si maofisini maana mambo yanayotendeka na hali ya maisha ilivyo ni mabaya sana.

  Wito: Chagua baraza la mawaziri ambalo linaweza kuueleza umma wa Watanzania wamewahi kuufanyia nini hadi waweze kupata hizo nafasi na pia WATAWAFANYIA NINI WATANZANIA TOFAUTI NA WENZAO WALIOWATANGULIA?. Ikiwezekana unapompendekeza mtu kabla hujampitisha awasilishe ripoti ya utendaji wake kwa maandishi na mkakati anaotarajia kuufanya.

  KWANINI TUSIUTANGAZE MWAKA 2008 KAMA MAALUMU KWA KAMPENI YA KUPAMBANA NA UFISADI TZ? YAANI KAZI KUBWA IWE HIYO ILI MWAKANI TUFANYE KAZI KTK MAZINGIRA YA HAKI?

 27. radhia kalombola Says:

  hao wote mafisadi! sasa chenge ajiuzulu,MWALIMU NYERERE ALIMKATAA LOWASSA KWA KUMFUKUZA IKULU KIPINDI KILE YUKO HAI…watu wanajifanya wajanja kumrudisha tena…walaumiane wenyewe…maana wanapendeleana 2.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s