BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

YAMEANZA KUTIMIA,LOWASSA AJIUZULU! February, 7, 2008

Filed under: Breaking News,Developing News — bongocelebrity @ 7:38 AM

 

Aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Ngoyayi Lowassa(pichani) ameamua kujiuzulu Uwaziri Mkuu kufuatia kuhusishwa kwake na kashfa ya Richmond.Habari hii bado inaendelea,tutaendelea kuwaleteeni kadri taarifa zinavyozidi kupatikana.

Advertisements
 

52 Responses to “YAMEANZA KUTIMIA,LOWASSA AJIUZULU!”

 1. Sinzia Says:

  Amefanya jambo zuri,tunategemea na wengine waliohusishwa na scandal hili wajihuzulu. Mh.Nazir Karamagi safari hii huna la kujitetea….kuwa mstaharabu,nawe step down. Mikataba mibovu ya madini ilikuhusisha na wewe,lkn ukakataa na ukatishia kwenda mahakamani. Sasa huna la kutueleza….step down please.

 2. BongoSamurai Says:

  Asante kwa kuwajibika sasa rudisha pesa zetu.

 3. Recho Says:

  Safi sana kujiuzulu kwani umekuwa mkweli kwa watanzania natumekusamehee kutoka na kujitoa mwenyewe.Mungu hakubaliki

 4. mwalimuzawadi Says:

  Baba safari njema, nakutakia kila la kheri PALE tu utakaporudisha pesa zetu, ili Mtanzania atue mzigo uliomtwisha kwa faida yako, mke wako na watoto.

  Mafisadi wengine, wafuate tu maana mlango umeshafunguliwa, hatutawashangaa. Ila pesa warudishe, la sivyo watapata walichopangiwa kupata…malipo duniani

 5. ab Says:

  wakati sasa umefika wa wewe kurudisha ulichochukua na sio tu kuodoka navyo

 6. kijiwe Says:

  Nina zinga la swali kama mtakumbuka few days ago JK alisema kuwa viongozi wote wa serikali au wabunge wenye ma business wachague moja either kuwa na biashara au kuwa katika politics.

  ze swali:
  JE HIYO NI KUWAPA KAMWANGA KUWA SASA TAMBAENI WASHKAJI SOO LIMEBUMBURUKA MTADAKWA NA UMMA!!
  AU
  HIYO NI KUWAWEKA SAWA ILI AWEZE KUWABANA VIZURI NA KUWAWEKA KIZIMBANI?

  COZ AS LONG AS THEY ARE KAMA AKINA SISI ITAKUWA EASY KUWABANA..

  NAWASILISHA

 7. Kijana Says:

  du jemedari kaanguka na kazi alizozifanya zimeishia hapo ,ila aliemsababisha ni kj na yey kujifanya kiherehere cha kuleta maendeleo bila kuangalia wanakoenda ,wengi waliangalia pale pale waliposiomama tu na ndo linaloikumb anchi kwa sasa ,sio kama enzi ya mzee wetu mkapa .hawa walikuja kwa kasi mno na sasa ndo inwaumbua bila kujijui ,so watafuata wengi sasa mpaka tutaogopa

  Nawakilisha

 8. ab Says:

  kuondoka ilikua nin lazima ,swali ni lini utarudisha mali ya watanzania uliyojipatia kwa njia ya ufisadi,
  na hao wenzake waliotajwa sijui wanasubiri nini kung’oka;

 9. Mwana wa mkulima Says:

  Recho tafadhali! Lowassa arudishe pesa zetu…then aende Monduli akachunge ng`ombe wake! Hivi Watanzania tuko namna gani? no wonder Mkapa alitwambia sisi ni wavivu wa kufikiri. WE ARE DAMN HOPELESS!! Now I can prove this. Yaani Lowassa kujiuzulu inaonekana kama katufanyia favour? He is a big time thug should go na apelekwe mahakamani (sadly hakuna wa kumshtaki maana Mwanyika na Hosea nao ni majangili!). Huyu jamaa alistahili kufukuzwa kazi na kupoteza haki zako zote!

  Watu wanaishi kwa mshahara wa elfu sitini na wakati huo huo Kampuni hewa ya Richmond ya Lowassa tunailipa MILLION 152 KILA SIKU KWA MIAKA MIWILI? Ontop ya $$35 million TULIZOWAPA? Hivi unajua hawa jamaa i wauaji kuliko hata Interahamwe? Honestly, Lowassa ni jambazi! watu wanakufa njaa, shule mgogoro..na bado jamaa wanapeta! Jamani watanzania hatukuandikiwa kuwa maskini!!!! WE can be bettter people!

  I always say mjini unaona watu wanapeta..ohh we are doing better, or we are hard working…sasa hao wanaumbuka…mijitu ni mithugs mpaka inaboa….Kibaya wanawaibia watanzania ambao hata uji wa asubuhi hawaupati….Tanzanians we should wake up. Tumenyanyasika vya kutosha na hawa mafedhuli. Its time we confront them!

 10. ab Says:

  nafikili hata huyu spika nae hatufai kwani alikua mstari wa mbele kupinga hoja hiii, akidai ni ya kizushi akataka kukimbilia marekani, in short raisi avunje balaza zima la mawaziri na wale wanaonekana mafisadi wafirisiwe na si kuondoka tu, kwani kuondoka hakutupunguzii machungu yetu watanzani, ili iwe fundisho kwa wale waliosalimika na watakao pewa dhamana ya kuongoza nchi.napedekeza mama Anna makinda awe spika full, kamati ya ripoti ya buzwagi na BOT itoe ripoti kwa kuiga mfano wa richmond

 11. LWABULINDA JOSEPH Says:

  Muungwana ni vitendo huu ndio uungwana
  Umeshindwa kumsaidia rais

 12. JIMMY Says:

  KWANZA KABISA NIMSHUKURU MH. DR. MWAKYEMBE KWA KAZI NZURI ALIYOFANYA. NAAMINI KAKWEPA VISHAWISHI VINGI SANA VYA KUPEWA HONGO ILI ASIANDIKE UKWELI LAKINI HAKUTAKA KUWEKA MASLAHI YAKE BINAFSI MBELE. KASONGA MBELE.

  MIMI NINGEPENDA HAO WOTE WALIOHUSIKA WAOZEE JELA IKIWEZEKANA WAPIGWE RISASI HADHARANI ILI IWE MFANO KWA WENGINE WENYE TABIA KAMA HIYO AMBAO HAWAJAJULIKANA! AMEN!

 13. Majita Says:

  Naona sasa waandishi wa habari HOFU ya kumwagiwa TINDIKALI itapungua.Ila Mzee Mamvi mimi nataka tu chenji zetu.Sina mengi,ukikataa tutaonana Monduli na mimi nikuibie kidogo.Hope yule mdogo wako atapunguza nyodo

 14. Liz Baraka Says:

  Kujiuzuru tu haitoshi tunataka urudishe mapesa uliyojikusanyia kwa njia isiyo halali, mapesa ambayo ni jasho la watanzania.

 15. Bongo Pixs Says:

  ONLY GOD KNOW, Umefanya, ukufanya au umepakaziwa. Uongozi ni DHAMANA NA UNA KIKOMO CHAKE, TATIZO NI AINA TOFAUTI YA UKOMO,

  KULIA NA KUCHEKA ZOTE KELELE.

 16. Edwin Ndaki Says:

  Ngoja nijikumbushe ka wimbo ka Ndanda…

  Sasaaa wanaanza kuliaaa eheee Nuhuu..utufungulieee safinaaaa…aaaa
  kidedeaaaa ….

 17. Bongo Pixs Says:

  CLIK LINK YA BONGO PIXS UPATE MPYA MPYA DOM.

 18. any Says:

  Spika alijua kuna kidedea, au bosi alimwambia hamna cha safari wala nini hadi kieleweke.

 19. Jesse Says:

  Ninapenda kumpongeza mhe. waziri mkuu kwa kitendo chake cha kiungwana, ila hiyo haitoshi kwanza inabidi watu wote waliohusika kwa namna moja au nyingine wailipe fidia TANESCO kwa gharama ambazo zingewezwa kuepukika kutokana na hali ya mabwawa ya kuzalisha umeme kuwa katika hali nzuri, kwa kuwa menejimenti ilisha shauri kuwa mkataba usitishwe lakini kwa ujeuri wa mafisadi uliendelezwa kwa hiyo wao ndio wawe responsible kwa gharama zote ambazo zinalipa kwa kampuni ya fisadi Rostam kuanzia kipindi hicho.Pili gharama zote za kabla ya hali ya mabwawa kuwa nzuri inabidi waliohusika na mkataba na huu sio mkataba maana hakukuwa na capacity kwa second party ambao ni RIchmonduli walipe hao walioingia mkataba feki. Ambao ni Msabaha, Mwakapugi na wenzao wote

 20. hawa Says:

  sasa tanzania inaonyesha ni jinsi gani tulivyochoshwa na ukandamizaji wa wachache wenye fedha za kuiba,
  ombi langu ni kwa spika bado muoga hatakiwi kuongoza bunge,kwa nini kaahirisha safari ya marekani kwani hamuamini naibu wake?
  aliagiza ripoti isijadiliwe mpaka yeye arudi,kwani kazi ya naibhu spika ni nini? sio kukaimu madaraka yote bosi asipohudhuria bunge kwa shughuli yeyote ile?
  Bg up Anna makinda ,tukiwa na wanawake 10 tu ktk bunge letu fufufu kama wewe,maisha yataboreshwa haswaaaaaaaaaa
  keep it up

 21. Edwin Ndaki Says:

  BREAKINGS NYUZIIIIIIIII…..

  Waziri wa nishati na madini Karamagi kafutata nyayo za Lowassa naye kajipiga chini….

  Ene wei tutafika tu

 22. mwale9 Says:

  Nilihisi kitu fulani kutoka kwao, hawa viongozi waliojiona wasafi sana, watu wa maadili na utendaji mzuri na wa jitihada za pekee. Kumbe walitufunika macho na vi-kauli mbiu vyao vyo uongo ili wachume. Wanaaibika mmoja baada ya mwingine. Ona sasa Waziri mkuu mzima anakua mdogo kuliko vumbi. Yaan kumbe ni tapeli!! Sikujua. Afadhali ya wapiga debe na wamachinga ambao hufanya kazi halali. Rudisha mali zetu kusudi uende salama baba.

 23. Victor Manyahi Says:

  Swala hapa si kujiuzulu.Huyu ni mhaini aliyewaachia Watanganyika mzigo mkubwa wa bills za umeme. Huyu mtu hakuwa safi hata kidogo hata Mzee Nyerere hakumtaka hata kidogo.Kama kweli Serikali ya JK imeanza kuamka jambo ambalo nina mashaka nalo.Basi huyu kibaka na vibaka wengine wafunguliwe mashitaka mara moja ili iwe fundisho kwa vizazi vilivyopo na vijavyo.

 24. james humphrey Says:

  Watanzania bado tumelala sana.Mchungaji Mtikila aliwahi kusema Watanganyika wengi wana matatizo ya akili.Hivi mtu kuresign ndio watu wanafurahia.Lowasa, Balali and Co.Mkapa and Co, Rostam and Co. wote hawa maisha yao hayapaswi kuwa Masaki bali Gereza la Keko au Segerea milele.Uoza tunaouona kwa sasa ni moja ya mia moja. Bado ni alfajiri hata mapambazuko bado ikifika mapambazuko watu watajaa mitaani na bakora na mashoka kudai vyao.Hatuwezi kuona watu wakiishi kama peponi hali watu wengine wakiishi katika makabuli kwani Kenyata aliwahi kusema Tanganyikans are living corpses.

 25. O.J Says:

  TUME YA KUZUIA RUSHWA ILIKUA WAPI SIKU ZOTE HIZO? WAO NDIO WANGEKUA WA KWANZA KUJIUZULU, WAMEPEWA MADARAKA LAKINI WAMEJIWEKEA MIPAKA.. MBONA HATA SIKU MOJA AWAMTAJA WALA KUMKAMATA WAZIRI AU JAJI YOYOTE. NAOMBA JK ANGALIE AJIRA YA HAWA WATU

 26. Verbal Diarrhoea Says:

  Ikulu ilikuwa haijatulia! na mpaka sasa haijatulia!

  Msee Mimi nilikwisha kutoa nje ya orodha ya viongozi siku nyingi mbona.

  Eti unalalamika kuwa hukuitwa. Heri na wewe ulikuwa umealikwa na watanzania wote pia tukatoe maelezo tunayojua kuhusu Rochmond hivi na wewe hukwenda?Tena wao hawakukufukuza ila umejiwahi mwenyewe kwani unajua ulichofanya.

  Pili, hivi siku ulipomfukuza kazi Mhandisi wa Manispaa tena kwenye Luninga kisa eti kwa sababu ghorofa limeporomoka ulimuita? Mkuki kwa ngurue ekhe?

 27. Mtema Kuni Says:

  Kwa kweli ni vizuri akarudisha pesa za watanzania. kiongozi gani hana huruma kwa watu anaowaongoza hafai kuwa kiongozi akalala. yeye anachukua kila mwezi bil 2 wakati mtanzania anaongezewa bili kubwa ambayo hiyo pesa ingemsaidia mtanzania wa chini anyanyuke hizi mali anazo rudika anataka aingie nazo kaburini awaache kidogo watanzania au anataka kuwa kama mabutu

 28. kijiwe Says:

  spika alizima kwenda marekani kusafisha statement yake ya awali ya kujaribu kuizima hoja ilipowashwa.yaani washkaji mkiangalia kwa mapana kuna zinga la chain la ufisadi this is some mafian stuff.
  inatia machungu sana yaani jk inabidi alete capital punishment ili hii mijitu itolewe kabisa na system iwe clean

  free mansons wanaexist bongo na ndo hawaaa

 29. Dinah Says:

  Mfano mzuri, pamoja na kujiuzuru bado sheria ichukue mkondo wake na airudieshie Serikali (wananchi) alichochukua.

 30. eunice Says:

  huu ni mwanzo mzuri wa mafisadi kuanikwa hadharani,kikubwa kwa watanzania JK na serikali yake wazakalie kooni mafisadi warudishe hela walizochukua na wawajibike kwa kwa kuyafanya maisha bora kwa kila mtanzania yawe ni kwa wenye vyeo peke yao tu,MUNGU NA AWALAANI

 31. Reg Miserere Says:

  Karibu mtaani mkuu.

  Kabithi mali zetu zote uanze upya.

  Itaniuma sana kama utakuja mtaani kutulingishia na mali zetu wenyewe.

  Jamani napita tu!!…

 32. Jo Chancellor Says:

  Ndugu Lowassa umekuwa hujui kuwa watanzania wameanza kufunbuka macho. Viongozi wengine muanze kujisafisha. Kizazi chetu akitamuonea haya mtu kama Lowassa au Billali wake. Munao wasalitu watanzania wasio kuwa na hatia. Mungu aibariki Tanzania ilituendele kuwa na amani na pia nakuwa fichua wazi wa pesa za uma. Tanzania inaweza kuwa nchi tajili kwa kipindi kifupi kama wote tukiwa na uchungu kama kamati ya bunge ya sooo la Richmond. Mungu aibariki kamati hii kwa kujitoa bila kuogopa bwana mkuu Lowassa wetu kuwa watafukuzwa kazi

 33. Alfonso Says:

  Sasa mzee JK unawaona maswahiba wako? Ama kweli BABA WA TAIFA aliona mbali tangia 1995, na amekufa na maneno ya wahenga yamekufa! Yaani leo hii zimwi likujualo ndo limekutafuna hadi nywele!Sasa brother LOWA, kuwa muungwana urudishe hayo ma-%, watu wamelipa kufungiwa umeme tangia mwaka juzi na umeme hawafungiwi, kisa vifaa hakuna, kwa hiyo hata za bili na nyinginezo kutoka TANESCO mliamua kubugia? Jamani watanzania! BABA WA TAIFA alimtoa nduki brother Lowa wakati alipotaka kununua uraus 1995!Hapo watanzania inabidi kuingia mitaani na kudai kilicho chetu! Jamani nina uchungu na maisha yalivyo magumu kwa watanzania! Sasa, potelea mbali, kufa gari kufa dereva! ya rift valley ya kenya yananukia TZ! hakyamungu!

 34. Mama wa Kichagga Says:

  Hongereni kwa kujiuzulu kwa njia ya amani LAKINI TAFAZALINI SANA TINDIKALI NI MARUFUKU!. Chukueni hii kama changamoto kubwa ktk maisha yenu na tumieni huu muda kwa kutubu na kumomba radhi Muumba wenu YEYE ATAWASAMEHE. Sisi tutajitahidi ila ubinadamu na umaskini tulionao utatusumbua. Karibuni mtaani kwetu.

  Ni kheri wamejiuzulu wenyewe kwani wameonyesho uzalendo na ukomavu wa hali ya juu wa kiakili kulikoni wangebonyea na kuanza kuumiza watu vichwa kama B…………… ambaye bado asifikiri watu wa siku hizi wanasahau? No no umesakini umekithiri hadi mfumu wa fahamu wa kusahau umeingilia kazi ya kukumbuka.

  Naongana na wenzangu kuwa wahusika warudishe mali ya umma na wengine wasisubiri hadi ripoti zitoke ndio wajiuzulu, waunge body kama jeshini vile “fata fata fata fata fata fata fa……” mwisho wabaki watu wenye uchungu na ubinadamu na ujenzi wa Taifa letu.

  KWA WALE WALIOPO MADARAKANI NA NI MAFISADI OLE WAO MAANA MAANDIKO NA SALA ZA WANYONGE YANATIMIA SASA., NANYI MSISITE KUJIUZULU.

  Nasisitiza KUFILISIWA KUFUATE MARA MOJA!

 35. Joyce Says:

  Tehetehe jaman tunaomba mtuweke na clips basi ili tuone na siye kidogo basi tuliombali maana kweli tunakosa uhondooo.

 36. Zyb Says:

  Baba wa Taifa Mwl. Nyerere alishasema tena wazi wazi kuwa “WEWE LOWASA HUWEZI KUWA KIONGOZI WA NCHI HII” kwa namna anavyojilundikia mali!!!!!!

  Kweli inaudhi sana, yani watu wazima kabisa tunaowaheshimu wanaenda kutubebesha mzigo mzito kiasi hiki? Oooh TANESCO haiwezi kujiendesha, tunabebeshwa mzigo mziiiiito wanatupa mabill ya ajabu ajabu kumbe kuna millions zinamwagika bure kabisa.

  Mtu kuweka umeme kwenye nyumba yako eti ni anasa!! Maana ni pesa nyingi ambazo huna. Wakati umeme ilitakiwa iwe kitu cha kawaida tu kama kusikiliza redio kwa watanzania. Sasa kama sio hayo mamilioni wanayotupa huko kwa kina Richmond si TANESCO ingekuwa imefika mbali? Hizo milioni 152 kwa siku si mchezo, WAMENIUDHI SANA.

  Ajabu Lowasa anasema eti hakuitwa!!!! Wakati alikuwa na uhusiano wa karibu sana na mchakato mzima wa Richmond, kwanini pale mwanzo tu waliposema kuwa watu watoe chochote walicho nacho abt Richmond kuisaidia tume yeye asiwe wa kwanza kuieleza tume namna alivyoshirikiana na viongozi wenzie kuhakikisha inakuwepo!! Alisubiri aitwe? Ili aharibu ushahidi wote.

  Kapumzike salama maana hata ubunge sijui wananchi wako utawawakilisha vipi tena bungeni, kwa kipi kipya sana utakachowaeleza kwamba utawafanyia? Zaidi ya sherehe kuuuubwa za kila mwaka?

 37. al Says:

  ..cha muhimu huyu Bwana arudishe chetu,ataifishwe yeye na wahusika wenzake pamoja na adhabu kali za kisheria

 38. amina Says:

  ufadi hauwezi kuisha serikali yote chafu…waking’oka hawa wanakuja wengine basi tabu tupu..ila safi sana

 39. Dada wa Kihaya Says:

  Tumechoshwa!!!!machinga wanaharasiwa kama nini wapeni hiyo mihera wawekeze ili umasikini upungue Maharamia wanatafuna nchi tu, bwana bora wafilisiwe.
  Mwee tatizo hakuna hata wakuwaambia leo mnashtakiwa mahakamani! swahiba wake hawezi kumpeleka jela hata siku moja!
  Mimi nimechoka hiyo mihela ya Richimonduli ingekuwepo tungekuwa mbali jamani million mia hamsini per day times three yrs of work = ( ) hesabu zinanipiga chenga hebu nisaidieni, sikwambii hiyo Dowans sijui…. nikikumbuka mibilioni ya hela pale boT na makampuni 22 ya mfukoni ndo nachoka kabisa.
  PLS PLS JK SERIKALI IWAFILISI NA HUYO PM UTAYEMCHAGUA BORA HATA ASITOKE KWENYE BARAZA LILILOPITA.

 40. Reli Says:

  Mambo haya nilikuwa siyajui,hadi hiyo juzi. Na eti kuna watu wanampongeza “kwa ujasiri wa kujiuzuru”. Mwenye kustahili heshima noi Mwakyembe ambaye kama angeukubali ufisadi angeficha ukweli. Lowasa na MSHENZI tu. Hana uchungu na sisi na anatutafuna tukiwa hai, na hayuko peke yake!

 41. tonny Says:

  Jamani eeeeeeeeeeeeh!Miongoni mwetu hakuna aliye mkubwa zaidi kuliko MAMA TANZANIA!vyama vya siasa vitakuja vitaondoka, viongozi wa kisiasa watakuja wataondoka.Mother Tanzania atabakia palepale milele na milele.Tuooooooooombe!

 42. Tembo Says:

  Nyerere muungana! Nashangaa mpaka sasa hawajamkamata. Hivi hawaoni tunavyowateketeza wadokozi hadi wale wa kuku? Jizi linaiba halafu hatumpondi kichwa! Kajiuzulu. Akamatwe na atupwe jela. Kisha arudishe fedha zetu zote. Tuone kale kabinti kake, kama hataacha nyodo!

 43. Nkima Says:

  Mtenda akitendewa huhisi kaonewa. Eti kamati haikumtendea haki kwa kutomhoji. Nadhani Bw. Lowassa amesahau kuwa alimfukuza kazi Mhandisi wa Manispaa ya Temeke tena mbele ya waandishi wa habari na wananchi waliokuwepo eneo la tukio la kuporomoka jengo la Chang’ombe Village, march 2006. Bw. Lowassa hakumpa huyo Mhandisi nafasi ya kujitetea.

 44. Zanzibar Says:

  Kujiuzulu kwa Lowassa sio kitu geni kwetu. Mimi nina maswali
  1) Kwa nini CRDB ichukue dhamana ya kutransfer hizo hela wakati CITIBANK ili katakata?
  2) Hiyo kamati inaweza kuchunguza kwa njia ya benki CRDB walikuwa walipaji wa RICH MONDULI ?
  3) Tusisimame hapa tu pia kuna mkataba wa bandarini TICTS ichunguzwe?
  4) Kwanini serikali haiweki sheria kwa yeyote atakae patikana na hati ya kula RUSHWA au UBADHIRIFU mali zake na za familia yote ifilisiwe?

 45. mmy Says:

  Hongera bwana Lowasa kwa kujiuzulu. Pia umeonyesha ujasiri kiasi fulani kwa viongozi wa africa kujiuzulu bila kufukuzwa sio rahisi.

  Subiri kiendeleacho utajulishwa.

  tumebadirika kisiasa kwa kiasi furani watu wako wazi sana inapendeza sana

  i wish tanzania all the best

 46. Alfonso Says:

  Inafurahisha kwa kujiuzulu, lakini inasikitisha sana kwa kulalamika bila kuwa na sababu za msingi! mfano! Unasema taarifa iliwasilishwa kwa mbwe mbwe! je, ulitaka Dr. Mwakyembe awasilishe taarifa akiwa analia? kazi mlipa nyie kama bunge, alichofanya alifanya kwa niaba ya bunge na wewe ukiwa mbunge achilia mbali nafasi uliyokuwa nayo, hakuna haja ya kuonyesha chuki bro! la msingi wengi tumeelewa kuwa ukweli unauma! Pili unadai kuwa hukuta nafasi ya kuhojiwa, lakini kumbuka tume ilitoa nafasi kwa mtu yeyote mwenye maoni au taarifa apeleke kwa wakati uliopangwa na tume, kama ulikuwa na lolote, mbona hukwenda kwenye tume? Ungeonyesha uzalendo kama mtanzania namba tatu, lakini kwa mbwe mbwe zako ukasubiria waje kwako. Lakini usisahau ni chombo kikubwa ki-mamlaka ingawaje huenda ulikiona inferior kwako! Hakuna haja ya kulalamikia tume wala mwenyekiti wa tume, lalamikieni utashi wenu na tamaa zenu idha za mali au za kujipatia umaarufu kinyume cha taratibu! Dr. mwakyembe kufundisha sheria hakuna uhusiano na mliyoyafanya, hakuteuliwa kutafsiri sheria, kama sheria ilikiukwa thubutu kwenda mahakamani! Wanzania wote isipokuwa wewe watakuwa mawakili wa tume! UNGEPELEKA TAARIFA, AU UNGEMTUMA HATA KATIBU WAKO KAMA ULIONA KWENDA WEWE NI NGUMU!

 47. frank kasera Says:

  SASA BAADA YA KUJIUZULU NAOMBA TU SASA MASHITAKA YAFUNGULIWE KWA WOTE WALIOUSIKA NA KISHA PESA ZILIZOLIMWA ZIRUDUSHWE KWA WATANZANIA…….YAAANI VIONGOZI WA JK WANAMUANGUSHA SANA…….

 48. frank kasera Says:

  HATUTAKUBALI MPAKA WAUJUMU WOTE WAFILISIWE MALI ZAO ZOTE KWANI KWA MTAJI HUU HATUJUI WAMEZIPATAJE?? JE KWA NINI WASIPELEKWE JELA?

 49. Mr. Upendo Furaha Amani Says:

  “Aliposulubiwa Lowasa”
  Wakampeleka kwa SPIKA wakamuuliza wewe ni RICHMONDULI? hakujibu neno. SPIKA akaomba RIPOTI ndipo RICHMONDULI akasema NAJIUZULU. Wabunge wakapiga kelele wakisema ASULUBIWE! Spika akasema “nimsulibishe kiongozi wenu?” Wabunge wakapiga makelele “mwondoe! mwondoe! msulibishe!” Spika akasema mpelekeni CHIMWAGA hata yapata saa 11 wakamsulubisha RICHMONDULI, kulia KARAMAGIMBI, kushoto MSABAHAKI. KARAMAGIMBI akamwambia RICHMONDULI umefanya usanii mwingi jiokoe wewe nasisi pia. RICHMONDULI akalia kwa kimasai OONGAI PAPALAI, yaani MKUU MBONA UMENIACHA? kisha akazimia, akakata roho.

 50. Gerald W.Chegenya Says:

  Binadamu kukosea ni jambo la kawaida sana hivyo mh,ajipange upya na hatutasahau utendaji wake kazi,na wale wote kwa namna moja ama nyingine waliotokea kufurahia kwa mh,hatujui maovu yao hivyo sisi binadamu tutambue kwamba tunatofautia kiakili,kimawazo na kiujuzi pia,MUNGU IBARIKI TANZANIA.

 51. Ndugu yangu Gerald W.Chegenya nakusifu kwa comment yako nzuri Big up man!!! Umesema kweli
  Nina uhakika kama ni kweli kala hizo pesa basi kala na wengi sana na baba zetu wamo humo humo kama si ndugu
  Tujaribu kuangalia chanzo mpaka wakafikia kula hizo hela zote…Je JK alikuwa hajui????ainiingii akilini mtu wa chini yako kimadaraka afanye ufisadi kama huo na wewe ukae kimya tu eti unamuonea aibu!! BIG NO….let us look on the system
  Kuna siri kubwa sana imefichika hapo
  Kwanza kuvunjwa kwa baraza na kuundwa upya bado sio suluhisho.
  Na nyie mlio sulibiswa kwa niaba….LOWASA na wenzako msikubali watajeni wenzenu maana nina imani hamjala peke yenu….SEMENI MSIOGOPE ili tujue mafisadi wote then tuanze upyaaa TANZANIA yetu
  TATIZO NI SYSTEM WAJAMENI…….MIMI NAONA WOTE WALE WALE.HATA KAMA NI MSAFI AKISHAKUWA KWENYE SYSTEM ANAFANANA NAO
  Anayejijua hana dhambi/hana ufisadi ndani yake achukue jiwe na kuanza kumpiga FISADI
  Ni maoni yangu tu wajameni

 52. nice kz Says:

  Siwezi kupoteza muda kwa kumpongeza Ndg. Lowasa kujiuzulu hiyo ilikuwa wajibu wala haikuwa ombi. Hivi ufisadi alioufanya kwa kutesa watanzania tunaishi maisha ya shida, umeme ni nishati muhimu sana katika ukuaji wa nchi.

  Leo tukitaka kumchambua lowasa na mafisadi wenzake na imani kila mtanzania aliyemzalendo na nchi yake angejitolea kwa hali yoyote ile kuhakikisha lowasa na mafisadi wenzake wananyongwa na mali zao zinaingizwa kwenye nchi ili kurekebisha maisha ya watanzania tulionyonywa kwa muda kwa kuogopana.

  Sasa imefika mwisho wa uvumilivu hatutakubali tuone watu wanajilimbikizia pesa kwa kujenga mahekalu wakati watoto wa kitanzania wanakaa chini mashuleni, huduma za afya ni shida kwa mtanzania wa kawaida. Tusipochukua hatua kwa ufisaidi wa richmond, BoT,TICTS na mikataba ya madini kweli hata hiyo misaada ya kina Bush itakuwa nothing ni bora ingepelekwa Darfur kuliko kuja kunenepesha mafisadi. Lowasa na mafisaidi wenzake wanatakiwa hata bungeni wasikanyage tunaomba wananchi wa majimbo yao wachukue hatua ya kuwatema kwenye uchaguzi ujao.

  Kwanza ninaimani mungu anasikia sala za waja wake si dhani kama wanamuda wa kuvuta hii puzi wasipotubu na kurejesha mali ya watanzania, ili wawe huru na hii dhambi la kujilimbikizia. Lowasa ulidhani utakufa au mitoto yako itaishi milele kwanza mungu atakupa mapigo ya ayubu ni hafadhali.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s