BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MH.MIZENGO PINDA NDIYE WAZIRI MKUU MPYA. February, 8, 2008

Filed under: Breaking News,Serikali/Uongozi,Siasa — bongocelebrity @ 11:48 AM

Rais Jakaya Kikwete amemteua Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uteuzi huo tayari umethibitishwa na Bunge kwa kura 279 za ndio katika jumla ya kura 283 zilizopigwa.Kura 2 zilisema hapana na kura 1 iliharibika.

Kabla ya uteuzi huu wa leo,Mheshimiwa Mizengo Pinda,ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mpanda Mashariki,alikuwa ni Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Mizengo Pinda ambaye kitaaluma ni mwanasheria(alipata degree yake ya sheria kutoka Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam mwaka 1974),alizaliwa tarehe 12 August 1948.Habari ambazo hazijathibitishwa rasmi zinasema Mpinda anatarajiwa kuapishwa kesho jumamosi huko Dodoma.

Wakati huo huo,baraza jipya la mawaziri linatarajiwa kutangazwa jumatatu ijayo.

Advertisements
 

36 Responses to “MH.MIZENGO PINDA NDIYE WAZIRI MKUU MPYA.”

 1. Mama wa Kichagga Says:

  Hongera sana Mh. Pinda.

  Unayo changamoto kubwa mbele yako ya kuurizisha umma wa Watanzania na kuponya majeraha ya ufisadi. Ukweli ndio utakao kuweka huru daima.

  Karibu kwenye pima Joto

 2. Obwatasyo Says:

  1. Hongera

  2. Kama wewe si pinda pinda bali Peter Pinda kama wewe si mizengwe bali Mizengo, basi tumia dhamana na mamlaka yako kuhakikisha kuwa wote waliohusika na ufisadi BOT, Richmond, Buzwagi n.k ukianzia na 6 (maana ndiye mzuia hoja za kuwaumbua wahalifu) na Lowasa na Balali na wengine wote wanakamatwa mara moja na kufilisiwa mbele ya sheria.

 3. Khamis MwiliMkubwa Says:

  Naomba niseme wazi kwamba nimesikitishwa na huu uteuzi.Mimi nilitegemea JK angemchagua mtu kutoka nje kabisa ya baraza lake la mawaziri alilolivunja kuwa Waziri Mkuu.Kwanini nasema hivyo?Huyu Pinda anatokea ofisi ya Waziri Mkuu…huyo huyo Lowassa!!Yaaani hii ndio kusema kule kule kwenye kisima cha ufisadi.JK anataka kutuambia kwamba huyu jamaa yeye alikuwa hajui kabisa chochote kinachoendelea huko kwenye ofisi ya waziri mkuu japo fununu?Haingii akilini.Ni wamoja hawa.Na jinsi Lowassa alivyoushadadia leo uteuzi wa huyu bwana utajua kabisa kwanini anafanya hivyo.

  Halafu jinsi haya mambo yalivyokwenda faster faster yananifanya nigune…ni kama vile yalishapangwa kabisa..JK..are you serious for real?Hivi lini sura mpya zitaanza kuingia serikalini?

 4. Alfonso Says:

  Mzee JK hapo nakupa BIG FIVE! mimi binafsi namfahamu Pinda, ni mchapa kazi na wala sio mroho, labda aanze leo. Lowasa alijitahidi sana kumfunika Pinda kwa kuogopa kuwa uchapa kazi wa PINDA ungempunguzi (LOWASA) umaarufu, lakini mungu sio Ngoyayi, mzee JK aalikuwa anaona. Sasa mzee JK achana na marafiki! ukicheka na nyani utavuna mabua! Angalia uadilifu wa mtu na wala sio urafiki. Mzee Pinda naamini utatutibu majeraha, sio ajabu tukapata umeme kwa bei ya kuridhisha, na hao mafisadi warudishe pesa zetu ili TANESCO wakanunue vifaa tufungiwe umeme! Jamani, umaskini huu mpka lini? Tutatoana macho ! Tumechoka! siku kipenga kinalia mtashangaa uwanja utakavyojaa! mwenye jiwe, nondo, kiberiti, hata wagonjwa mahututi siku hiyo watatoroka wodini kwa kuamua kufia uwanja wa mapambano kuliko hospitalini kwenye mashuka machafu yanayomwongezea mgonjwa maradhi mara dufu!

 5. kijiwe Says:

  Khamisi nakubaliana nawe kabisa. Nilishasema before kuwa Tanzania imeingiliwa na free masons. Na sijawahi kusikia free masons wana give up kirahisi ndiyo maana hata nguvu za giza hazija give up mpaka tulipo sekunde hii.
  There is no way and I mean NO way huyu pinda is clean sababu alikuwa katika Line up.
  I really really dont get this nonsense sababu umeona wapi suspects wakawekwa katika list ya witnessess?
  Mimi ningeona kuna unafuu kama JK angeteua mtu neutral kabisaa.
  Kwa kifupi huyu Pinda kama angekuwa nyooka angeanzisha moto kule kule kwao Sumbawanga maana kuna zinga la dili limepigwa kule.Kama mnamjua mbunge wa Kwela Mh Mzindakaya huyu mzee ana kiwanda cha kusindika nyama tena ni kiwanda cha kisasa kinachosimamiwa na meneja expatriate kutoka Zimbabwe huyu meneja Mzindakaya alikuja kumchomoa Botswana Meat Commission ambako alikuwa analipwa hela kali tuu.Nasema hivi sababu game lote alilocheza huyu mzee nililiona kwa macho yangu sababu meneja alikuwa anakaa mtaa wa pili.
  Sasa basi kama huyu Pinda ni nyooka angeanzisha moto bungeni kuuliza kwamba huyu mzee kapata wapi hicho kisu cha kuwa na kiwanda kama hicho?(does BOT ring the bell?)Na aliyekifungua rasmi ni Richmonduli.
  Tusidangannyane kabisa hapa kuna walakini mkubwa sana I am even starting to lose my faith of JK sababu kama ana mean real business to Tanzanians kwa nini anaanza ma game?
  Huku si kulindana libe jamani?
  I said this before and I am going to say this again THIS IS JUST ANOTHER VERSION OF MCHANGA WA MACHO tena huu ni extended remix….
  sasa hivi tunaelekea lala salama nyie endeeleni kusifia msiyoyajua
  mimi simo

 6. Shabby Says:

  Mhh uteuzi wa Mpinda hauna lolote jipyaaa.Kwa sababu ameshakaa ikulu miaka karibu 20, so ni miongoni mwao, hana jipyaa.Usitegemee atamwajibisha mtu kama ANABEN, EL kwa lolote lile.Anyway, hii ina safisha njia ya Opposition to ikulu 2010

 7. any Says:

  kwanza alianza kwa kumpongeza Lowassa, shame on him, unampongeza mtu alieondolewa kwa skendo ya wizi. i hate recycling! hadi lini? ndo tz tambarare, after 10 yrs watu tutalia kilio kibaya sana. hata huduma muhimu kama maji na umeme inakuwa dili! ari mpya na kasi mpya iko wapi sasa! JK shame on you too, why dont you pick new face, sio wale wale. Tumechoka. hatukawii kusikia Lowasa nae kachaguliwakuwa waziri wa sehemu sehemu, a kafisadie na huko tena. phew. tired!

 8. ibrahim Says:

  inakera sana.mbona sura ndo zile zile kila kukicha?hio cabinet mpya utawasikia tena kila Meghji,nk.Huyu kikwete vipi lakini?

 9. Kimori Says:

  Yes, kazi ipo…no comment so far!

 10. Mr. Upendo Furaha Amani Says:

  Mie ninaungana na Watanzania wote wenye kuipenda nchi yao kwa kumpongeza Mh. Mizengo Kayanza Peter Pinda kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Mungu amlinde, ampe afya na mema mengi, wala asimuache yule muovu shetani na maajenti wake wampe matamanio ya rushwa. Amen.
  Tuipende Tanzania, nchi tuliyozaliwa.

 11. Peter M Says:

  Tatizo ni chama chenu, chetu, au chao, ambacho kimelewa kwa staili fulani kwa miaka yote hii. ni system ambayo yenyewe haisafiki hata kwa kutumia acid, labda wasafi wajitofautishe na wachafu kama Nyerere wakati fulani alivyodhani. As long as system haijasafika (na inahitaji mtu mwenye uadilifu, umakini na roho ngumu kidogo kuisafisha ile), si rahisi kupata aliye 100% kutoka humo. Na sijui kama katiba inamruhusu muheshimiwa kuchukua mtu nje ya chama chao. Lakini watanzania walipenda sana falsafa ya kuleana au kulindana hata kama mtu anafanya kosa la kuua au kuiba; hayo madhambi yataendelea kuligharimu taifa. Lakini Mpeni muda Mheshimiwa, nadhani anatupeleka kuzuri.

 12. kijiwe Says:

  Mr. Upendo Furaha Amani
  please punguza kumchanga mungu na mambo ya kifisadi

 13. kijiwe Says:

  Mr. Upendo Furaha Amani
  please punguza kumchanganya mungu na mambo ya kifisadi

 14. any Says:

  na jumatatu mawaziri watakaokuwepo ni kichekesho! mawaziri 60 na manaibu ndani, hadi mawaziri hawajui kazi zao. JK unagawa posts kwa kujaribu kumridhisha kila swaiba yako, itakupeleka pabaya. mpe mtu kazi anaeweza kazi na kuwe na kitengo, usi create vitengo ili kuwapa shoga zako posts, please, usirudie uliyofanya wakati umeunda baraza la mawaziri for the first time, ilikuwa “kichekesho, and please usituchekeshe tena this time”.

 15. Mama wa Kichagga Says:

  UJUMBE MAALUM KWA PINDA MIZENGO

  Mh.unaendaga nyumbani? na kama jibu ni ndiyo unatumiaga njia gain ya usafiri? Yaani Sumbawanga/Rukwa ni soo la kimataifa kwa umaskini wa kupindukia licha ya kuwa kati ya mikoa inayozalisha chakula kwa wingi TZ. Vijijini hakuna huduma za jamii labda makao makuu ya wilaya tu yaliyo zaidi ya km 100!

  Nakuomba chonde chonde ktk nafasi hii ya sasa, (baada ya kubonyea ulipokuwa serikali za mitaa) uende Laela ukiwa unaelekea S’wanga ingia kushoto nyoosha moja kwa moja km 90 utakutana na kijiji CHA “MITITI”.

  Yaani kwenda kituo cha basi ni km 90 na kama ni mgonjwa basi wanaume wanabanjuka na mgonjwa mzega mzega umbali huo hadi Laela wasubirie usafiri mwingine wa kubahatisha km nyingine 30 (S’wanga Mjini)!

  TAFADHALI SANA WAOKOE WAKINA MAMA, WATOTO, WAZEE NA WAGONJWA WA KIJIJI HIKI. CHUKUA HATUA ZA KIPEKEE KUHAKIKISHA PMO-RALG WANAWAFIKIA WANANCHI WA KIJIJI HIKI NA VIJIJI VINGINE VYENYE MATESO YANAYOFANANA NA HIKI KIJIJI (Mifano michache ni Katumba, Isubangala, Kanazi-Mang’o nk).

  KAMA HUNA UCHUNGU NA MAHITAJI MUHIMU YA KIJAMII NYUMBANI KWAKO NAMNA HII NITAKUWA NA WASIWASI KAMA KWELI UTAWEZA KUTUPELEKA MAHALI TUNAPOPATAKA.

 16. ola Says:

  Jamani haya mambo yanavyoendeshwa,inatia wasiwasi.uchaguzi wa mizengo pinda ni mchanga wa macho,ni sura zilezile miaka nenda rudi.
  tuna uhakika gani kwamba hawa watu hawakupanga before this scandal happened?na JK huyohuyo anasema nguvu mpya,ari mpya,please!!!!
  watanzania sio watoto,au mpaka tugeuke kenya ndo wajue kwamba tumechoka na ujinga?

 17. Pope Says:

  MwiliMkubwa naomba nikutoe wasiwasi, kwa wale mabingwa wa Siasa za Bongo wanamjua Bwana Pinda kwanza huyu alitajwa sana katika watu ambao wangechukua Form mwaka 2005, Pili jamaa yuko safi sana waliofanya naye kazi wanajua namaanisha nini, hana harufu ya Rushwa kama anakula basi atakuwa anaanawa uzuri kiasi hata kiharufu hukisikii inamaana atakuwa anadokoa hahaha. tofauti na mafisadi ambao hula kwa pupa, na hula sana na akitoka midomo yote mpaka kwenye nguo ananuka shombo.

 18. Kaka K Says:

  Mh.Pinda , hongera sana ila unapashwa kufahamu kuwa watanzania wa jana sio wa leo so please do your job seriously though tunajua kuwa your system is a Babylon. Kuna wizara nyeti zinatakiwa kukabidhiwa kwa watu wenye vigezo (shule + uzoefu wa kuridhisha) kwenye suala husika, acheni ancheni ancheni urafiki kenye masilahi ya nchi! Wewe na JK mmebeba mstakabari wa nchi in the next 10 years. Mwisho, hakuna kitu mtaweza kufanya kuendelea kuuongopea uma pale mtanzania atakapo choka nahisi itakuwa zaidi ya yale yaliyowakuta jirani zetu japo siombi iwe hivyo japo ndo taswira mnayojenga.

  Kaka K

 19. jewel Says:

  Hongera pinda !!!!!!!!!! na hizo kura mbili za hapana ni za lowasa na karamagi iliyoharibika nahisi ni ya msabaha

 20. amina Says:

  yaleyale wezi wenzao tu hao

 21. man himself Says:

  kwa kweli dalili zinaonyesha kwamba mambo yataendelea kutokea kutokana na huyo aliye mchagua naye alikuwamo kwenye cabinet iliyo vunjwa..je ina maana yeye alikuwa hajui chochote?kama raia tu wa kawaida ana fununu na hayo mambo je yeye aliye na mtu huyo mhusika ktk ofisi moja hajui?
  Mi nafikiri makosa bado yapo ktk katiba yetu ambayo inaleta hali ya kulindana..kama kweli tunahitaji mabadiliko sasa umefika wakati wa kuwa na serikali ya mseto maana uzembe ukitoke itakuwa rahisi kuumbuana..Bado cc wa chini tutaendelea kuumia,

 22. george Kahangwa Says:

  Naungana na wanaosema kuwa tatizo kubwa linaloikabili nchi yetu ni system iliyopo. Well, wanaweza kuendelea kuteuana wale wale kadri watakavyo, letu sisi watanzania ni kuendelea kushikiria msimamo ule ule, tumeichoka system na mwisho wao 2010.
  Ama kuhusu katiba, hairuhusu waziri mkuu kuteuliwa kutoka chama kingine tofauti na kilicho na wabunge wengi zaidi Bungeni(kwa sasa ni CCM) laiti watanzania hali tukijua hilo tuamue ni wabunge wa aina gani tutawachagua kuanzia 2010. Vile vile kwa sababu hiyo, tuendelee kuona mantiki ya madai ya katiba mpya. Kwa sasa system iliyopo inaendelea kupuuza uwepo wa watu wenye uwezo mkubwa sana wa kushika kwa uadilifu nyadhifa za uwaziri, eti kwa sababu wako nje ya chama tawala. Huo mfumo unastahili kuzikwa ifikapo 2010.
  Kwa Mhe. Pinda, pole sana maana kazi uliyopewa ni nzito tena katika kipindi cha majaribu makubwa, angalia mwenzio kanyolewa (japo upande tu) kama hutaki kutia maji fanya watanzania tunachokitaka. Vinginevyo tazama wembe una makali usije ukakupitia.

 23. Mr. Upendo Furaha Amani Says:

  Kijiwe,
  Kumbuka kuwa hata Mafisadi ni Watoto wa Mungu. Pia kumbuka hakuna binadamu aliyezaliwa akiwa fisadi, bali ufisadi ni “acquired character”. Tukumbuke kuwa ukimnyoshea mwenzako kidole kuwa mkosaji na vingine vitatu vinakuambia kuwa wewe ni mkosaji mara tatu, na kidole gumba kinasema kuwa Mungu ni shahidi yetu. Tujihadhari sana kuhukumu ili nasi tusijehukumiwa.
  Nawasilisha.

 24. Gervas Says:

  Ndugu yangu Kijiwe, pamoja na wale woote mnaosema angechagua sura mpya kabisa, naomba niwasihi kuwa heri ya zimwi likujualo, maana nikukumbushe jinsi Ben alivyomchagua Sumaye, watu walifurahi wakijua hakuwa anajulikana maana alimchomoa hukoo! ..sura mpya, lakini si uliona kilichofanyika? mi nawashauri mpeni muda muuone maana kwa sasa si wabunge pekee yao bali hata wananchi tumeshaamka!!

 25. Gervas Says:

  Halafu unapokuwa waziri sio kwamba kila issue unaruhusiwa kuingilia, Pinda alikuwa tawala za mikoa, sasa sioni usiano wake na issue ya mzindakaya. Hivo hata cabinet yote sio mbovu, kuna wazuri tu kila mmoja anatawala wizara yake. Hata hivo mambo mengi yanakuwa ni uamuzi wa cabinet kama kabinet ukimjumlisha presida.. wakulaumiwa hasa ni Takukuru ambao wanapaswa wapambane sio kupamba, na wachunguze maeneo korofi sio yanayonuka tu bali kunukia nukia nukia rushwa. Kama wewe ni mtu mwema ukiona mkubwa anaweka ubavu basi jiuzuru.

 26. Matty Says:

  Wote ndo hao hao tu!!!!mabest friend zake na ndo maana wanachota chao mapema wakijua hatawaadabisha!
  Sasaivi utasikia Lowasa kawa balozi wa ……checkslovakia sijua malaysia!!!!au atapewa uwaziri sector nyingine we ngoja tuone na MUNGU ATASIKIA KILIO CHA WANYONGE IPO SIKU LETS PRAY!

 27. YA Says:

  Hongera bwana P. Pinda. Muombe mwenyenzi mungu akusaidie na kazi yako itafanikiwa. Hata angechaguliwa nani mngelalamika tu nendeni na nyie mkasome mapate madegree ili wawa chague nyie muongoze basi kazi hamliziki hii ni kwawale mnao sema pinda hafani mnamtakananiiiiiiiiiiiii.

  hee tukubari tu

 28. noah gondwe Says:

  man himself jamaa alikuwa kwenye sekta ya TAMISEMI( tawala za mitaa na serikali za mikoa) hivyo kujua nini kilichomo ni minor sana ebu blog hapo kwa the greaty man ucheki hiyo ripoti n then uniambie? ulimpata jana zitto in the house?

 29. Peter M Says:

  Ndugu zangu, someni kwanza nadharia 30 za ufisadi ili muelewe ukubwa wa shida na uzito wake kutafuta mikakati inayofaa. Inahitajika umakini mkubwa kupambana na ufisadi, maana baadhi ya wale wanaojifanya wapiga vita watakuwemo wachache wasaliti kwa sababu ya ubinafsi.

  NADHARIA THELATHINI KUHUSU UFISADI:
  UNAVYOJITENGENEZA, KUJILINDA, NA NAMNA YA KUPAMBANA NAO.

  Nadharia hii imeandikwa baada ya kutafakari matukio mbali mbali duniani yaliyotokea katika vipindi mbalimbali vya historia. Nadharia hii inajaribu kuchambua ufisadi pamoja na adhari zake na namna ya kupambana nao. Mwandishi alipoandika nadharia hii hakusoma kitabu au kazi ya mtu yeyote; wala hakuandika kwa mtiririko maalumu; bali alijaribu kutafakari na kuyaandika mawazo yake kama yalivyojitokeza ili kuchokoza mjadala, utafiti, au mchango zaidi kutoka kwa watu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wasomi, wataalamu wa sayansi ya jamii, na wahanga wa ufisadi. Lakini pamoja na kwamba nadharia hii ni ya awali, naamini inaweza kuwasaidia wana jamii kuufahamu kidogo ufisadi ulivyo na kufikiria namna ya kujipanga kupambana nao. Kwa watafiti na wasomi, itakuwa ni nafasi nzuri ya kuchambua zaidi, kutafiti na kuelimisha jamii zaidi juu ya adui huyu mkubwa wa mwanadamu.

  1. Ufisadi ni aina fulani ya tabia inayojitengeneza ndani ya moyo wa mtu mwenye asili ya uchoyo na ubinafsi.
  2. Ufisadi huanza kidogo kidogo katika maisha ya watu, hasa wale wanaopenda daima kuweka maslahi yao binafsi mbele zaidi kuliko ya wengine.
  3. Kama haupigwi vita mapema katika jamii, ufisadi unakua na kujieneneza; na kasi ya kukua kwake inaongezeka kama kuna watu wanaoshabikia ‘mafanikio’ yanayotokana na ufisadi huo.
  4. Ufisadi ulioachiliwa (ama kwa sababu ya hofu, kuoneana aibu, au vinginevyo) hujiimarisha kwa kujitengenezea mtandao wake mwenyewe.
  5. Mtandao wa ufisadi usipovunjwa mapema hukomaa na kutengeneza tabaka la mafisadi katika jamii, ambao hutafuta namna ya kuhalalisha ‘matunda’ ya ufisadi wao.
  6. Mojawapo ya njia inayotumika kuhalalisha matunda ya ufisadi ni kusaidia katika jamii, kutoa michango katika jamii au vyama, kuwekeza katika biashara, kusaidia wanasiasa kushinda uchaguzi, au kuingia serikalini; na ikibidi husaidia mafisadi wenzao kuingia kwenye siasa au shughuli nyingine muhimu.
  7. Wakati wote, tabaka la mafisadi huteteana kwa siri, lakini wakishajiona wamekomaa hukosa aibu hivyo huteteana kwa wazi. Na kwa hiyo fisadi mmoja hawezi kumwadhibu fisadi mwingine isipokuwa wamekosana katika mambo au maslahi yao
  8. Ufisadi uliojitengenezea tabaka huwa ni ngome ngumu kuivunja, kwani unatafuta mbinu zote kujilinda, kujitanua, na kujihalalisha.
  9. Ufisadi uliokomaa hauna huruma, aibu, wala staha. Na unakuwa mkali kwa wale wanaojaribu kuupiga vita.
  10. Mbinu kubwa ya ufisadi ni kusema uongo, kutumia vitisho, au kutumia nguvu yoyote ilioyokaribu nao (ya kipesa, kicheo, kichawi, kisilaha, kisiasa, kijeshi, kikabila, n.k.).
  11. Mbinu ya uongo ikishindwa, vitisho vinatumiwa, vitisho vikishindwa nguvu hutumika kutetea maslahi yao.
  12. Ufisadi ukipigiwa sana kelele na wananchi, unajipaka chokaa nyeupe kwa nje na kujifanya unaongoka, na hivyo kuwahadaa wananchi; kwa namna hiyo ufisadi hautenganishwi na unafiki.
  13. Unafiki wa mafisadi una mbinu tatu. Mbinu ya kwanza ni ya kujisafisha kwa juu juu pasipo toba la kweli. Hilo lisiposaidia, mbinu ya pili hutumika ambayo ni kuwachafua watu wengine waliosafi ili kuiaminisha jamii kuwa kila mmoja ni fisadi hivyo wasifuatwefuatwe. Hilo lisipofaa, mbinu ya nyingine hutumika ambayo ni ya kuwachafua baadhi ya mafisadi wenzao wachache, na hasa waliobainika, ili watolewe kafara na wengine wapate kupona. Mbinu zote zikishindikana, mafisadi wanaweza kudhuru watu ili kujitetea.
  14. Mtandao wa ufisadi unaweza ukawa wa sehemu moja kijiografia; au ukasambaa nchi nzima, na hata kuchukua sura ya kimataifa. Na unapovuka mipaka kuingia nchi nyingine, unatumia hila ya kuhadaa na kuwalainisha watu mashuhuri wa nchi au sehemu husika.
  15. Kama jamii ya wapenda HAKI na KWELI isipojizatiti na kupambana na ufisadi, na ukiachiwa utawale jamii kama unavyopenda, matokeo katika jamii yanakuwa ni mabaya sana. Jamii inakuwa mtumwa wa ufisadi, na mafisadi wanakuwa kama wafalme wa kudumu.
  16. Ufisadi unajidhihirisha katika sura mbalimbali kama vile rushwa kubwa na ndogo, ukandamizaji wa wanyonge, unyonyaji, kikundi kimoja kunyanyasa kingine, ubabe wa kiuchumi au kisiasa, biashara haramu (kama vile ya utumwa, madawa ya kulevya, bidhaa feki, biashara ya magendo, n.k.), uporaji wa mali na haki za wengine, demokrasia bandia, utawala mbovu, udikiteta, ajira mbaya kama vile ya watoto, n.k.
  17. Baadhi ya matokeo mabaya ya ufisadi ni kuongezeka unyonge na umasikini; kuporomoka maadili; chuki za kitabaka, kisiasa, kikabila, au kivikundi; vita vya wenyewe kwa wenyewe; mauaji ya kikabila, kikoo, au kisiasa; kukosa kuaminiana katika jamii, ukoloni wa sura mbali mbali, maisha ya wasiwasi, n.k.
  18. Kwa mantiki hiyo, ufisadi sio kitu cha kuchekea kabisa (hata kama unafanywa na ndugu wa kuzaliwa). Ni janga, aibu, na hatari kwa jamii au nchi yeyote ile. Pia ni ugonjwa mbaya unaoua kabisa maadili ya jamii, kwa maana vizazi vipya vinakosa mifano mizuri ya kuiga; pia vinakosa maongozi sahihi, licha ya kukosa haki zao za msingi na msaada wa kweli.
  19. Lakini jamii pia lazima ifahamu kuwa ufisadi uliokomaa hauwezi kujiondoa wenyewe, maana unajikita kama ufalme mdogo ndani ya jamii. Ili kupambana nao, umoja wa wananchi, nguvu, busara, na maarifa yanahitajika.
  20. Ufisadi hauwezi kupigwa vita na mafisadi, bali utapigwa vita na watu walio safi, wapenda maendeleo, haki, na kweli. Mwenye madoa ya kifisadi akipigana na mafisadi ataumbuliwa; ndio maana si rahisi kwa asiyesafi kupambana na mafisadi.
  21. Vita ya kupambana na ufisadi inatoka ndani ya moyo wa dhati wa mpenda haki, amani, na maendeleo ya watu; inahitaji uvumilivu, ni vita ya muda wote, haitafuti mafanikio binafsi.
  22. Vita ya kupambana na ufisadi inahitaji viongozi safi, wenye maono safi, wenye uadilifu, wanaoweze kuelezea umma malengo yao na kuhamasisha haki na kweli, na wanaoonyesha mfano wa kweli kupitia maisha yao wenyewe.
  23. Vita ya kupambana na ufisadi sio lele mama, ina hitaji kujitolea kwa hali ya juu. Lakini matunda yake ni mazuri, yanaleta faraja kwenye jamii, na yanadumu kwa muda mrefu.
  24. Kila mwana jamii aukemee ufisadi wakati wote na mahali popote anapouona, pasipo kujali kama ungemletea yeye faida fulani.
  25. Viongozi wa taasisi zote za jamii, serikali, kidini, na kitaaluma wapige vita ufisadi wa namna zote, na wahamasishe watu wao kuupiga vita ufisadi. Wanapofanya hivyo wajisafishe kwanza ili wawe mfano kwa wananchi wao wenyewe.
  26. Vyombo vya habari vina nafasi kubwa kusaidia wananchi katika vita hii, kwa kuendelea kufichua vitendo vya ufisadi, kuandika taarifa kwa busara, na kuhamasisha haki, kweli, na uadilifu katika jamii.
  27. Inawezekana kupambana na kuushinda ufisadi, unyonge, na umasikini kama wanajamii wakimaanisha na wakikusudia kujiletea maendeleo ya haki na kweli.
  28. Ikumbukwe kuwa ufisadi hauwezi kujiondoa wenyewe; wala malalamiko tu na kusimanga mafisadi haviwezi kuuondoa ufisadi. Wala ushabiki tu wa juu juu hauwezi kuuondoa ufisadi. Kinachohitajika ni juhudi na nguvu za dhati na za pamoja kati ya wananchi na viongozi wao, pamoja na taasisi za dini na zile zinazotetea haki za watu.
  29. Kwa kuwa ufisadi unatumia mwanya wowote na hasa udhaifu fulani katika jamii, ni vema kuhakikisha kuwa maeneo yote ya kijamii yanaboreshwa (kama vile sheria za nchi na serikali za mitaa, kanuni na taratibu za taasisi, utendaji wa vyombo vya kusimamia haki na sheria, utawala bora, utendaji wa vyombo vya habari, demokrasia na ushirikishwaji umma, maadili ya viongozi, n.k.)
  30. Ili kusaidia vizazi vijavyo, elimu na itolewe kuanzia ngazi ya shule za msingi. Elimu hiyo ilenge kuwasaidia vijana kuwa waadilifu, kuuchukia na kupambana na ufisadi. Kama vile tunavyopambana kulinda mazingira yetu, ni lazima kupambana pia kulinda jamii zetu na utu wetu. Mazingira ni muhimu, lakini ni kweli pia kuwa utu wetu ni muhimu zaidi. Maana utu wetu ukiharibiwa, na jamii ikiharibiwa na ufisadi, je mazingira hayo yatamsaidia nani?

  Imeandikwa na mtanzania – mwanafunzi wa uongozi, Marekani.

 30. Kekue Says:

  Mi sioni cha kushangaza hapo, yani ni yale yale!! kama aliweza kumteua naibu wa Balali kuchukua nafasi ya Balali atashindwaje kumteua huyu aliyekuwa anafanya kazi na Lowasa kuchukua nafasi ya Lowasa??? Mi nishachoka bwana.

 31. kijiwe Says:

  TO GERVAS
  habari yako mdau Gervas.Kwanza kabisa naomba kukutaarifu kuwa Sumaye hakuwa mtu from nowhere,alikuwa swahiba wa Mkapa tangu miaka ya 90(1993 in particular) walikuwa wanapata wote kinywaji pale TEXCO bar/club in Upanga sea view kwa hiyo hiyo mimi nakukatalia kuhusu Sumaye alivutwa from nowhere.
  Pili hata kama huoni kuna uhusiano gani kati ya Mzindakaya na Pinda hiyo ni opinion yako na mimi nilimtaja huyo Mzindakaya in particular because to be clean you have to start by cleaning yourself halafu you clean your house halafu by all means clean your sorroundings because what lieas next to you might affect you or your people or whateva..
  Anyway nasema hivyo sababu kama tupo mkoa mmoja na wewe najua kabisa unafanya ufisadi wa namna moja au nyingine na nikikaa kimya si ina maana to some degree nausupport huo ufisadi?
  Its not my problem I know but it is to my highest degree of concen because this is the roots of evil are grown na kama hu deal na vitu vinavyomhusu jirani yako then utadeal vipi na vitu vinavyohusu taifa zima?
  Anyway kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe maana wengine mna take it personal wakati humu ndani tuna share ideas tu na kufumbuana macho when possible na siyo KUTUPIANA MICHANGA YA MACHO
  nawasilisha

 32. kijiwe Says:

  TO GERVAS
  habari yako mdau Gervas.Kwanza kabisa naomba kukutaarifu kuwa Sumaye hakuwa mtu from nowhere,alikuwa swahiba wa Mkapa tangu miaka ya 90(1993 in particular) walikuwa wanapata wote kinywaji pale TEXCO bar/club in Upanga sea view kwa hiyo mimi nakukatalia kuhusu Sumaye alivutwa from nowhere.
  Pili hata kama huoni kuna uhusiano gani kati ya Mzindakaya na Pinda hiyo ni opinion yako na mimi nilimtaja huyo Mzindakaya in particular because to be clean you have to start by cleaning yourself halafu you clean your house halafu by all means clean your surroundings because what lies next to you might affect you or your people or whateva..
  Anyway nasema hivyo sababu kama tupo mkoa mmoja kama wabunge(wote pinda na mzindakaya) na najua kabisa unafanya ufisadi wa namna moja au nyingine na nikikaa kimya si ina maana to some degree nausupport huo ufisadi?
  Its not my problem I know but it is to my highest degree of concen because this is the roots of evil are grown na kama hu deal na vitu vinavyomhusu jirani yako then utadeal vipi na vitu vinavyohusu taifa zima?
  Anyway kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe maana wengine mna take it personal wakati humu ndani tuna share ideas tu na kufumbuana macho when possible na siyo KUTUPIANA MICHANGA YA MACHO
  nawasilisha

 33. zawad haji Says:

  Waziri huyu wa sasa ni lazima atafanya kazi vizuri kwa sababu mh.Rais hana urafiki mbele ya kazi na siamini hata yeye mwenyewe atakubali kupata aibu kama aliyoipata Lowasa, so,lazima atakuwa makini.Huwezi jua kama uteuzi wa Rais kama uko sahihi ama la! kwani yeye ni binadam sio malaika .

 34. ngungu Says:

  Mi sielewi hi system ya tanzania jamani. Kuna watu wana-graduate mashuleni kila kukicha na shahada za juu za political science. lakini wanaishia kufanya kazi Tigo , vodacom nk. Hivi humo serikalini hakunaga ku-staafu?? Ili na wengine waingie na sera mpya? tatizo sera ni hizohizo na hakuna changamoto yoyote maana watu ni haohao tuuuuu. Wakubadilisha sana sana, utaona wanaweka wafanya biashara maarufu ambao hawana ujizi wowote na mambo ya siasa, au wanaweka watoto wao uli kuendeleza libeneke. Mi nimeshachoka na hii serikali. Makaratasi na plastiki ngio huwa kuna recyceling na si uongoze unaohusisha wanadamu. Yaani kwakweli tuwa wawazi na wa kweli, SERIKALI YA TZ IMEOZAAAAAA

 35. kijiwe Says:

  ngungu big up!

 36. MR VITA Says:

  JK WHAT ARE U DOING? NO ONE EXPECTED TO SEE YOU DOING NYERERE TYPE, COME ON MEN, REMEMBER U WANTED TO BE A PRESIDENT WHEN U WAS UNDER 50 CLAIMING THAT YOUNG STARS COULD BRING EXCELLENT IDEAS AND NYERERE THE BABA WA TAIFA AS OTHER PEOPLE BELIEVE WHICH IS UNACCEPTABLE FOR ME, U MISSED IT, THEN WHY ARE DOING THE SAME MISTAKES WHY THIS OLD MAN OF 60 YEARS OLD
  ? UR PRIME MINISTER? WHAT NEW IDEAS DO U EXPECT FROM HIM? BE CAREFUL OTHER WISE U WILL FIND YOURSELF 10 YRS WITH NOTHING NEW, GOD BLESS AMERICA GOD BLESS TANZANIA


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s