BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

RUSHWA NI ADUI WA HAKI-THE NGOMA AFRICA BAND February, 8, 2008

Filed under: Burudani,Mawazo/Tafakuri,Muziki,Swali kwa Jamii,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:06 AM

Kwa kila mtanzania,iwe anajitambulisha kama mzalendo au asiye mzalendo,matukio ya wiki hii nchini Tanzania yanatia simanzi,tena sana.Inakuwaje watu fulani fulani,wachache tu,wamuumize kila mtu kwa sababu ya uroho wa kujilimbikizia mali usio na kifani?Hivi kuna raha gani kuwa na mabilioni ya pesa halafu ukitoka tu getini kwako unakutana na ombaomba? Kuna raha gani ya maisha kutoka getini kwako kisha ukakumbana na barabara zilizojaa mashimo na mavumbi eti kisa umekula rushwa na hivyo kuzuia mradi mzima wa utengenezwaji wa barabara? Kuna raha gani kulala huku jenereta likiunguruma usiku kucha(kwako,tena kwa sababu unaweza kulinunua hilo jenereta) huku karibuni nchi nzima ikiwa kizani kwa ukosefu wa umeme eti kwa sababu wewe umeamua kuneemesha mfuko wako kwa njia isiyo halali?Kuna raha gani….?

Kama tulivyodokeza kidogo juma hili,swali sasa sio tena tunaelekea wapi bali tumefikaje hapa? Sasa leo kwa sababu ni Ijumaa na piga ua,jadi lazima iendelee,burudani ya mziki ipo pale pale.Lakini leo tuna ujumbe mahsusi kabisa.Ni kutoka kwao The Ngoma Afrika Band(pichani),bendi ya watanzania chini ya uongozi wa Ras Ebby Makunja na yenye makao yake makuu kule Oldenburg,Germany.Wao wanasema Rushwa Ni Adui wa Haki.Pengine hapa ndipo tunapoweza kuanzia katika kujibu swali Tumefikaje Hapa?

BC inaanda mahojiano rasmi na The Ngoma Africa Band.Yatawajieni yatakapokamilika.Ila kwa sasa pata burudani ya wimbo wao huu wenye ujumbe murua hususani katika mazingira tuliyonayo hivi sasa.Bonyeza tu player hapo chini.Ijumaa Njema.

Lakini subiri kidogo,yaani zilipendwa leo hamna BC?Haiwezekani,wasikilize Western Jazz Band wakisema Sasa Tutacheza Cha Cha Cha.

Advertisements
 

5 Responses to “RUSHWA NI ADUI WA HAKI-THE NGOMA AFRICA BAND”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Bc..yaani unafikiri hata nina nguvu ya kucheza leo.

  Yaani bado hiyo report ya Richmond imenimaliza nguvu kabisa jinsi Tanzania yangu inavyotafunwa na wachache.

  Ene wei,tutafika tu.

 2. LOON Says:

  Ehee kwa viongozi wa Tanzania kutochukua Rushwa ndio si Haki sijui siku wakihapishwa wanaona maandishi yote yanasema nilazima uwe mbadilifu

 3. Deo Says:

  Eh! inaelekea wanamziki hao wanaijua wazi nchi yao?
  maana wimbo wao huo nimeusikiliza kwa makini,wanajua
  nini?wanachokiimba!na wakina nani?wanao warushia mipasho hiyo!tena kali ya mwaka
  Big up BC

 4. mti mkavau Says:

  Wajama wetu hawa! wanajulikana kwa tabia zao hizo
  hawaweki mambo moyoni,wao kisa kidogo tayari wimbo!
  umaarufu wao unataokana na vitendo vyao hivyo vya kukemea na kukosoa

 5. DUNDA GALDEN Says:

  HAYA MAMBO HAYO KAKA JK TUMIA NEEMA YA CHAMA CHAKO KUMBOLESHA MLALA HOI WAANGALIE SANA WANAOKUSAIDIA KWENYE GULUDUM LA SERIKALI WENGINE MAILI YAO NI YA KIFISADI,NA KULE CHUO IWEJE CHETI KIFATWE NYUMBA YA WAGENI MMHH ATIMA IMEFIKA LAKINI JAMAA ALIFARIKI YAAAN HUYO MUHUSIKA MPENDA RUSHWA YA NGONO WALIO BAKI AKILI KICHWANI
  CHAFOSA CHAI GODA


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s