BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 06 February, 10, 2008

Filed under: Photography/Picha,Swali kwa Jamii,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:05 AM

 

Picha moja ni sawa na maneno elfu moja. Picha hii ilipigwa mwaka jana na Hassan Mndeme wa Mwananchi huko mkoani Morogoro katika kijiji cha Komtonga kilichopo wilayani Mvomero. Itazame kwa makini picha yenyewe kisha useme unachokiona.Ni ajira kwa watoto,watoto wanacheza,umasikini au nini?Wewe unaona nini?Tuambie. Hii ndio picha yetu ya wiki hii.

Shukrani kwa Charahani kwa picha hii.

Advertisements
 

22 Responses to “PICHA YA WIKI # 06”

 1. Edwin Ndaki Says:

  Pole sana mama pichani pamoja na wanao.

  Naamini ulihaidiwa maisha bora mwaka 2005 wakati wa uchaguzi.

  Najua unabeba mzigo mzito wa matofali ambao sio tu ni hatari kwa mwili na afya yako kwa kuwa huna jinsi utafanyaje.

  Nakutazama kwa jicho la huzuni.Najua kipato kidogo utakachopata hapo.Inakupasa kesho ukachangie nusu ya ilo pato lako ujenzi wa shule na zahanati.Kwa kigezo serikali haina “pesa” na ni “masikini”.

  Nawatazama hao watoto najua hawana tofauti na maisha ya “KAYUMBA”.Najua uwezo wao wa kumaliza shule ni mdogo na mwisho wa siku nao watajiunga kwenye ajira “mbaya” na “hatari” kwa watoto.

  BC…hao watoto sio kwamba wanacheza,haåpo wanavuta muda ili waendeleze libeneke.Naona kuna hizo ngazi ni kwa ajili ya kuweka kwenye kichwa chao na kubeba tofali kichwani pia.

  Pole sana nyie watoto msio na hatia na pia nawambia.

  Ene wei..tutafika tu

 2. Chris Says:

  Vyote ulivyosema yawazekana i.e. ajira kwa watoto, umaskini etc. Ila vyote vinasababishwa na UMASKINI. Huyo mama inawezekana ni watoto wake na hapo inawezekana yu kazini anapiga kibarua au ujenzi wake mwenyewe. Sababu ya UMASKINI watoto inabidi wasaidie hususani huyu mkubwa.

  Hao wengine wadogo tunarudi tena kwenye UMASKINI that kama wangekuwa na njia mbadala wa kucheza kama watoto wengine wangechezea vitu vingine ambavyo mtoto inabidi achezee vimkuzavyo kiakili na si hayo matofali, they’re risked maana waweza umia hapo.

  Na hata huyo mama Maskini matofali aliyobeba ni mengi mno,uwezekano wa kuumwa ni mkubwa, Drs can contribute more on this.

  Tanzania we’ve a long way to go.Wachache wanajitajirisha,wengi ndo hivyo… Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake…wanasema…Ndo maisha bora kwa kila mtanzania hayo.Wezi hao hao jumapili tunao makanisani, Ijumaa Misikitini. Huyu Mungu kama yupo… basi kiama chake ni kikubwa sana.

 3. Gervas Says:

  Hata kama mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe, ila nafikiri pia mila na desturi zetu hasa vijijini zimekisiri. Na maanisha kwamba utakuta mumewe na huyu mama ameenda kunywa pombe,au amelala. mama afanye kazi hiyo afu awahi kumpikia mumewe home na watoto. Maana ukiangalia watoto wana afya safi tu at least wana nguo. Kazi ngumu kama hizi zinapaswa zifanywe na wanaume maana unakuta mumewe anakitambi mama anaonekana mzee kumbe bado kijana. mimi natupia lawama mila zetu hasa vijijini. Wizara ya Jinsia na watoto ndo kazi yake kuplan waondoe vipi mila hizi hata kama ni kucharaza bakora wanaume wenye tabia hizi naunga mkono japo mimi mwanaume.

 4. jamjuah Says:

  picha hii ungempelekea Lowassa, amabaye mpaka leo eti anaitwa mheshimiwa, wala sio mhalifu.
  eti nasikia naye ni mzee wa kanisa.
  jamjuah

 5. Anganile Says:

  Nampa pole mama (pichani). Pia nampa hongera kwani ni mwanamke jasiri, asiyependa kuombaomba, ndo maana kaamua kufanya hicho kibarua. Pia yawezekana ni matofali kwa ajili ya nyumba yake.

  Kinachoniogopesha, itakuwaje kama matofali ma2 au ma3 yadondoke, ni hatari sana kwa wanawe, kwani wapo karibu sana nae. Yote hii ni umaskini, but we should never give up inm life, mama amenipa moyo sana huyo.

 6. Pope Says:

  NAANGALIA MZIGO…,
  NAFIKIRIA MALIPO….,
  NAMUWAZA BABA WA HAO WATOTO AMBAYE ATARUDI NA KUTAKA MAJI YA KUOGA NA CHAKULA…,
  NAWAFIKIRIA HAO WATOTO WENYE UMRI WA KWENDA SHULE…
  NARUDI NAUANGALIA KWA MZIGO WA HUYO MAMA…

  MAJALIWA YA HUYU MAMA NA KESHO YAKE ILIFAA KUPUNGUZWA NA MIKATABA TUNAYOWEKEANA SAINI NJE YA NJIII HII.

  ANAKOTOKA MAMA HUYU NDIKO KWENYE MADINI YA RUBI, MBUGA ZA WANYAMA NA RASILIMALI KEDEKEDE, ANAFAIDIKAJE KAMA MWANANCHI WA KAWAIDA?????????????????/

  KUNA JAMBO LA KUFANYA!!!!

  “TIMIZA WAJIBU WAKO”

 7. Gervas Says:

  Hii ndo reflection ya dhana ya watanzania kula majani iliyotolewa na muheshimiwa Mramba. Msishangae kumuona balali, karamugi, msabaha, zombe, Brother Dito wako kwenye kabinet ijayo au mabalozi nje. Bado dhana ya Good Governance Tanzania ni Taraab tu! hivi hao wanaotuchangia 42% kuongezea budget yetu kila mwaka wakiyasikia haya si watatoa divorce? Hivi African Leaders tukoje? watu waanakuza matumbo tu kwa fedha za wananchi, itafikia kipindi tutawafuata huko huko walikozirundika tuzigawane au vipi Edwin Mkobozi?

 8. mwalimuzawadi Says:

  Mimi napata taswira jinsi huo uzito unavyoweza kuharibu kichwa na mwili wa mzalendo huyu.
  Sidhani kwa suluba hii, huyu mama anaweza kuamini Tanzania hii kuna viongozi wezi wanakula milioni 152 kwa siku. Nadhani itakuwa ngumu kuamini ukatili huu kwa wananchi tena waliowapa kura.
  Mbaya zaidi Lowassa alipita akitangaza tena kwa nyodo eti ‘maisha bora hayatakuja kwa kukaa vibarazani’. Kumbe lowassa na familia yake ndio waliokaa kibarazani wakimtumikisha mama huyu kuwazidishia maisha bora

 9. sponge bob squire pants Says:

  Makofi na vigelegele kwa mwalimuzawadi, umenena!

 10. pangupakavu Says:

  Inasikitisha na kuumiza kupita upeo. Hakuna binaadamu asiyependa raha, hakuna mwanamke asiyependa watoto wake waishi kwa raha amani ni usalama. Unavyomuana hivyo na watoto wake, kama wanacheza au anawafanyisha kazi ni kwa sababu ya shida. Shida iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na uongozi mbaya kinara wao akiwa Raia mwenyewe. Wakati wakitupigia kelele tufanye tuchange hela, rasilimali zetu wanazitumia kutalii na kujineemesha wao familia zao na maswahiba zao. Hawana aibu, hawana huruma na ningewaomba waache kwenda misikitini na makanisani waabudu hizo mali zao wanazotudhulumu. Hata maneno ya kusema hayatoshi. Viongozi ambao wameonyesha kujali wananchi ni Dr slaa, Zitto na kamati ya Dr Mwakyembe. Hawa ndio mashujaa wetu wa kuwapongeza, sio mwizi aliyekubali kosa kwa shingo upande- Lowassa, Karamagi, Msabaha na wengineo wengi tu.

 11. Mama wa Kichagga Says:

  Picha hii inaonyesha hali halisi ya vijiji vyetu na imenikumbusha “MBALI SANA”.

  Watu wanateseka na hawana njia ya kujipatia kipato zaidi ya kufanya kazi ngumu pale inapopatikana.

  Nadhani Watz inatubidi kufumbua macho na kuangalia mbele:

  1. Tumrudie Muumba wetu kwa kuwajali majirani zetu hata kwa kile kidogo tunachokipata.

  2. Wanaome wasiowajibika – wajitahidi kulinda na kuhudumia familia zao ili kumpunguzia mama mzigo mzito katika maisha

  3. Viongozi wetu wawajibike zaidi kwa wananchi badala ya kukaa maofisini na kusubiri kutunda poroja za uchaguzi ujao

  4. Serikali iongeze mipango na mikakati ya maendeleo vijijini

  5. Hebu tukunje sura kidogo tuwajibike ili kutenge Tz ya kesho.

 12. Matty Says:

  Mungu wangu!!!huyu mama anahali ngumu ndo maana anafanya kibarua apate mshiko kama picha inavyoonekana na watoto nao wanamsaidia mama yao nadhani.
  Nikweli kabisa mfano kule Makete wazazi wamekufa na ukimwi na kuwaacha watoto kama hao hawana chakula, hawaendi shule na wanafanya kazi kama hiyo pichani ya kubeba tofali ili wapate hela ya chakula nk. na ukiuliza analipwa sh. ngapi kwa kila tofali moja jibu ni sh.5/-.
  Jamani vijijini unakuta mama na watoto wanafanya vibarua wapate chochote wakati dingi anaenda kilabuni kunywa pombe tu!!!!!nachukia sana hilo yaani mafisadi wanakula na kulala pazuri hawafikirii watu kama hawa!
  Mungu yupo na ipo siku atajibu tu sala zetu!

 13. BongoSamurai Says:

  Mimi ninachokiona kwenye hiyo picha ni matokeo ya ufisadi wa kina Lowassa, Karamagi, Msabaha na wengi ambao BoT na Buzwagi iko mbioni kuwaanika hadharani.

  Natamani sana mafisadi wote wasulubiwe …! Baya hulipwa kwa baya.

  Mungu ibariki Tanzania.

 14. eunice Says:

  Hao watoto wanaonekana wako kazini,labda huyo wa kike ndio anacheza.Sishangai kuona ajira kwa watoto tena ambao hazajafikia kuitwa ma-teenager,tutategemea vipi maisha bora kwa kila mtanzania kupatikana wakati hao tuliowapa dhamana ya kuongoza jahazi ni MARICHIMONDERS.

 15. ngungu Says:

  Huyo wa kike yuko hapo coz hakuna mtu wa kubaki nae nyumbani. na usikute hajala chochote siku nzima. Yaani serikali ya TZ bwana, kama huna utabaki hivyohivyo huna, na kama unacho utaendelea kupewa mpaka mwenyewe useme basi. Serikali hata haiwezi kuwaza kuweka vituo vidogovidogo kwa ajili ya kulea watoto kama hawa wakati mida ambapo wazazi wao wako vibaruani??? Watu wamebakia kula tu kodi za wananchi na wakati kuna sekta zingine wala haziguswi………huu si uungwana kabisa.

 16. mlengwa Says:

  team work

 17. Senyandumi Says:

  Duuh,mama kanikumbusha Msange JKT.Tulipiga tofari za hivo mpaka mgongo ukakubali chini ya Afande Wailer.Sasa kwa sisi ambao tulifanyakazi hiyo kwa kipindi kifupi bado tunakumbuka na maumivu yake,je kwa mama huyu ambae hii ndio shughuli yake mwaka nenda mwaka rudi inakuaje?Serikali inabidi ipambane na mafisadi wote ili kuweza kunusuri watanzania walio wengi haswa vijijini.Aluta mapambano yanendelea.

 18. Abdulrahim Says:

  holla…!
  Duh kwanza natoa pole kwa familia ya John mjema nahisi sasa kila mwanahabari atakuwa na yake ya kula na wazushiwa kitaani nao watazusha amejichinja labda kwa kuwachwa na demu wake au unaweza kusikia anadaiwa namshikaji wake na hana kitu cha kujitetea.Je wa Tz mnaonaje kwa hilo?

 19. tonny Says:

  Hii ndiyo fursa sawa kwa wote!Kalima maharage yamekosa mnunuzi!Kapika pombe auze ataambiwa kaharibu nafaka na asipokuwa mwangalifu ataweza hata kukamatwa kwa kupika pombe isiyokuwa na vipimo vya maabara!Kapeleka mtoto wake shuleni ataambiwa kwanza achangie ujenzi wa choo cha wanafunzi na ununuzi wa madawati!Mumewe kibarua wa kutwa,deiwaka, miaka saba mfululizo bila kuthibitishwa kazini!
  Kalazimika kuuza mwili wake atashutumiwa mzinzi anayehatarisha afya na usalama wa wanakijiji wenziwe!Mbunge wake atamuona tena baada ya miaka mitano atakapo kuja kuomba kura yake lakini kwa sasa hana muda naye na hana thamani kwake!Mkoani kwake yuko Mkuu wa Mkoa lakini kabanwa na majukumu muhimu ‘zaida na nyeti’ ya kitaifa,tatizo la huyo mama ni la kitarafa tu!Wilayani kwake wanasiasa wamejaa kibao lakini wako busy wanajiandaa kwa ‘mkutano mkuu wa chama kitaifa’ utakoweka mikakati ya kuangamiza upinzani!Tatizo la huyo mama ni la kitawi tu,kwa sasa wamekabiliwa na majukumu mazito ya kuandaa vision ya chama itakayo leta maisha bora kwa wote!Hana la kufanya,Mama huyo na wanawe analazimika kwenda kufanya kibarua kinacho udhalilisha ‘Uanamke’!JAMANI TUWAPE HESHIMA WANAYOSTAHILI MAMA ZETU!Bila ya wao sijui dunia ingekuwaje!Wapo watakao sema bila ya Baba je?Sawa lakini Mama anakubeba tumboni miezi tisa.Akiamua kukutosa kabla ya miezi tisa,Baba yako atatambua?Hii ndiyo nadharia ya Ari mpya,Nguvu mpya na Kasi Mpya!

 20. tonny Says:

  Tukio hili limenikumbusha wimbo mmoja wa SOUL KING the late mighty James Brown who passed away only recently,wenye maneno machache lakini yenye hisia kali,’Its a Man’s World.But this World would be NOTHING without a WOMAN!’.aaaaaaaaah,
  ee bwana weeee wimbo mkali sana.God Bless the Woman!

 21. Matty Says:

  Tonny umeongea point moja kali sana kakaangu, mwanamke ni kila kitu sababu miezi 9 tumboni mwake anakulinda mtoto kwa kila unachopenda iwe ndimu,mkaa,udongo nk.jamani tupewe kipaumbele wanawake !!!
  WANAWAKE OYEEEEEE NA JUU JUU ZAIDI!!!

 22. eva moses Says:

  jamani tunahitaji simple things kama wheel barrows ambazo zinaweza kusaidia kubeba matofali hayo……it is not right – kwa mama kubeba hizo tofali kichwani na watoto pia wako karibu…….


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s