BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MSIKILIZE RAIS JK AKITANGAZA BARAZA JIPYA February, 12, 2008

Filed under: Breaking News,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 3:05 PM

Leo hii,kutokea makao makuu ya nchi,Dodoma,Rais Kikwete ametangaza Baraza Jipya la Mawaziri. Mabadiliko kadhaa yamefanyika ikiwemo kupunguza kidogo ukubwa wa baraza la mawaziri na pia kuunganisha wizara mbalimbali na mabadiliko mengine mengine ya kiutendaji.Lakini mabadiliko haya yanamaanisha nini kwako wewe ukiwa kama mtanzania,ndani na nje ya nchi?

Msikilize Rais,Kikwete,kwa sauti yake mwenyewe, akitangaza baraza hili jipya la mawaziri na pia kufafanua mambo kadha wa kadha kuhusu muelekeo wa serikali kiutendaji.Msikilize kwa kubonyeza hapa. Kwa orodha kamili ya Mawaziri na Manaibu Waziri wao bonyeza hapa.

Upatikanaji wa hotuba hii mtandaoni umewezeshwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya BC,Jiachie,na EastAfricanTube.

Advertisements
 

16 Responses to “MSIKILIZE RAIS JK AKITANGAZA BARAZA JIPYA”

 1. Mr. Upendo Furaha Amani Says:

  Hongereni sana B.C. kwa kutuwezesha kusikiliza Baraza Jipya la Mawaziri na kuona Majina ya Mawaziri wetu. Ninakupongezeni sana kwa kazi kubwa mnayoifanya.

  Kuhusu Baraza Jipya la Mawaziri, Ninampongeza Rais pamoja na wasaidizi wake wa karibu (Makamu wa Rais, na Waziri Mkuu) kwa kupunguza mzigo mzito uliokuwepo mabegani kwa walipa kodi kwa kupunguza Baraza la Mawaziri.

  Tuipende Tanzania, Nchi Tuliozaliwa

 2. Dinah Says:

  Hongera Kikwe kwa kupunguza wingi wa mawaziri…..Hao wengine nitawapongeza nikiona utendaji wao wa kazi kwa sasa nawatakia kila la kheri ktk nyadhifa zao mpya. INATIA MOYO a.k.a MTUMAINI.

 3. Boss Says:

  He he h Dinah na wewe kumbe wajuwa siasa lol! Nlizani wajuwa yale mambo yako tu…( kublenda).

 4. Mama wa Kichagga Says:

  Kura yangu kwa Mh. JK sikuitoa bore! Na 2010 ataipata bila mjadala wala mkutano!

  Hongera sana Kiongozi wetu na fanya kazi kwa bidii hivyo hivyo. Pia nakupongeza kwa kufanyakazi na vyombo vya habari maana namna hii umma wa Watz wote ndani na nje ya nchi wanafikiwa na habari moto moto moja kwa moja toka jikoni.

  Usije ukatulia anza mchakamchaka maisha yetu hasa vijijini ni mabaya sana!

  1. Rudisha Nyumba zote za serikali mikononi mwa serikali kila aliyejinyakulia nyumba kiujanja ujanja atoe maelezo na wawajibishwe maana huo ni ufisadi mkubwa.

  2. Usisahau kutumia sheria kwa watuhumiwa (Mafisadi na wengine).

  3. Hebu fanya kama suprise fulani hivi uwakusanye hao waheshimiwa wako kila mmoja aje na maiwaifu/husband/partener to be wake mujumuike kwa brainstorm vile! Usije ukawa unafanya kazi na wababaishaji flani vile. Ni hayo tuu Mh.

 5. chachu Says:

  JK ametupa moyo wananchi wake,maana kuna sura nyingine zilichosha.amepunguza mrundiikano wa mawaziri na wizara zilizokua na msingi,hii italeta uwajibikano zaidi na ufanisi wa kazi.nadhani mawaziri wapya sasa watakua kidogo na uwoga na kujifikiria mara mbili mbili kabla ya kufanya ufisadi.
  Hongera sana mh rais,una support ya wananchi wako.

 6. aluta Says:

  BIG UP MH RAIS KWA MABADILIKO MAKUBWA ULIYOFANYA MAANA YANAHITAJI MOYO,LAKINI UMEKUBALIANA NA WANANCHI YAKO KWAMBA TULICHOSHWA NA UBABE WA VIONGOZI WETU NA UFISADI WA WAZI ULIOKUA UNAFANYWA KIHOLELA.
  IMANI YANGU IMERUDI KWAKO.

 7. ThaBoss Says:

  Watanzania kweli mnachekesha na ni rahisi sana kusifia vitu ambavyo hata hamjaviingiza akilini na kuvifanyia uchambuzi yakinifu. Mimi nadhani hili ni tatizo la ujinga na uoga wa hali ya juu uliowatawala Watanzania. Siwezi kumsifia Kikwete kwa sababu hakuna mabadiliko ya kweli aliyoyafanya. Watu aliowarudisha kwenye hili Baraza la Mawaziri jipya ni wale wale ambao walishindwa kufanya kazi zao katika Baraza lililopita. Hivi mnategemea kutakuwa na mabadiliko yeyote katika hili Baraza la Mawaziri. Kweli nyinyi ni WADANGANYIKA.

  Baraza la Mawaziri la Kikwete bado ni kubwa sana ukilinganisha na ufanisi wake. Gharama za kuliendesha hili Baraza ni za juu sana. Kikwete alitakiwa alipunguze lile Baraza na kuwa na watu 30 au chini ya hapo. Hakuna proven Research yeyote inayoonyesha ukubwa wa Baraza la Mawaziri inaashiria ufanisi katika utendaji. Hapa amechemsha sana Ndugu Rais.

  Sidhani kabisa Kikwete ana ubavu wa kuwachukulia hatua MAFISADI nchini Tanzania, tukianzia na rafiki yake mkubwa Lowassa. Baraza la Mawaziri halikuvunjwa na JK bali lilivunjika kikatiba baada wa Waziri Mkuu Kujiuzulu. Kwa hiyo Lowassa sasa hivi anaheshimika kama Waziri Mkuu Mstaafu pamoja na uchafu wake wote alioufanya. Hivi ni lini hawa Viongozi majambazi watawajibishwa na kuchukuliwa hatua za kisheria?? Kikwete alichotakiwa kufanya ni kumfukuza Lowassa na wenzake wote na si vinginevyo.

  Kwa Maoni yangu Kikwete amechemsha na baraza lake la Mawaziri ni bovu kama lile la zamani.

 8. chau Says:

  HONGERA SANA JK.BARAZA LINATIA MATUMAINI YA MAISHA BORA.ILA HAO ULIOWAACHA UWAACHE FOR GOOD SIO TENA UWAANZISHIE TAASISI NA VIJIIDARA UWACHOMEKEZE HUKO, UTAHARIBU.

 9. Edwin Ndaki Says:

  Nikiwa kama mwanaharakati wa maendeleo ya tz kwa upande mmoja nakupongeza ingawa kwa upande wa pili nakupa changamoto.

  Binafsi kwanza naomba utuambie HATMA ya Lowassa na wengine woote waliohusika kwenye hiyo RICH-MONDULI(richmond).Maana kujiuzuru pekee hatoshi.

  Kwenye upande wa pongezi.binafsi haijalishi KIGUNGE aliomba kupumzika au JK aliamua kupigia chini.Binafsi ndio kitu pekee ninachofurahia.Huyo mzee kwanza alichelewa sana kupumzika.Maana naona alikuwa tayari kapumzika miaka kibao sema alikuwa tu ameng’ang’ania madarakani na kufanya propaganda tu.

  Sasa JK kama wapambe wako watakufikishia salaama zangu chonde chonde mafisadi usiwapatie vitengo vingine mfano balozi zetu ,utakuwa uanzidi kusambaza ugonjwa.

  Mwisho mh rais tupo pamoja.Usiwe nguvu ya soda.Acha kuwachekea “nyani” ccm mtavuna “mabua”2010.

  Sio muda wa kuuza sura..weka ndita pita tupoJAH!!

  Amani na upendo.

  Ene wei,naamini tufika tu.

 10. tonny Says:

  Kutoka wizara 29 hadi 26!Gani tumepunguza?Bado kuna wizara kama 8 hivi zingeweza kuunganishwa na kubakia 4.Na hivyo kuzifanya wizara zote zibakie kuwa 22 tu na siyo 26.Tungeokoa mabilioni mangapi ambayo yangeweza kutumika kusomesha vijana wetu wengi zaidi vyuo vikuu au hata kuboresha zaidi huduma za afya ya msingi,maji na nishati vijijini?Bado kuna mawaziri kama wanne ambao hawakustahili kabisa kuwemo katika baraza jipya la mawaziri tokana na sababu mbalimbali iwe za kashfa,ukongwe,au udhaifu wa kiutendaji.Kuna mawaziri wengine kama watano ambao hawakustahili kabisa kupewa wizara walizokabidhiwa kutokana na udhaifu wa kiutendaji waliodhihirisha katika miaka miwili iliyopita na ingefaa wappangiwe wizara nyingine watakazo ziweza zaidi!Ni juu yake kuwatambua hao ni kina nani.Mdharau mwiba guu huota tende!Ukiacha hayo mapungufu mawili,nimpongeze Rais Kikwete kwa kuweza kwa kiasi kikubwa kusikiliza kilio cha watanzania.Amejitahidi lakini bado haitoshi,tunahitaji mabadiliko zaidi.Nimpongeze kwa kuwapumzisha ‘Wazee’,ambao hakika walijisahau.Tunawakaribisha ‘kijiweni’ waje waonje machungu ya sera walizo zitengeneza na kuzitetea wao wenyewe kwa miaka 30 waone zinavyo fanya kazi!Tuondokane na dhana ya kuteua baraza la mawaziri ili kukidhi ‘convenience ya kutawala tu’,badala ya kuwa wakweli katika dhamira yetu ya kumkomboa mtanzania na mifumo yote dhalimu ya utawala tuliyo irithi toka kwa wakoloni!Mimi nina imani Rais Kikwete bado anao uwezo wa kutusikiliza na yeye mwenyewe kusoma alama za nyakati badala ya kutuletea ‘cosmetic changes na political romanticism!’ ili kutuliza hasira za watanzania nyakati hizi zilizogubikwa na utitiri wa kashfa .

 11. noah gondwe Says:

  NICE WORK OUR PRESIDENT SOME HOW IT IS GOOD.

 12. zawad haji Says:

  Hongera mh. umepunguza idadi ya mawaziri ni sawa lakini mkuu unaonaje ingekuwa chini ya hapo mi kwa mtazamo naona ingekuwa imetulia.Na kitu kingine waungwana mnaonaje uteuzi wa Getruda kuwa mbunge, sio siri mwenzenu imeniboa ile mbaya ,Hembu tujiulize hivi sasa anavyotaka kuwa muumini wa kawaida na sio mchungaji tena inakupa picha gani? mi naona mh. Rais anayo haja ya kuchagua kiongozi asiye na majukumu mengi kwa jamii.

 13. amina Says:

  Tha boss nakuunga mkono kabisa hakuna mabadiliko hapo wezi wapo pale pale

 14. Misifa Says:

  Nampongeza Rais Kikwete kwa kutokuwa na pupa.Haya mambo ya uoza wa mawaziri wake yalianza mwanzo wa awamu yake.Watu wakalalamika wengine wakamshusha chati toka 95% hadi 42% kuwa hawezi kazi.Yeye akawa kimya.Lakini Raisi wetu anaamimi kuwa ya mbayana hayamfichi mtu..iko siku yatamuumbuwa tu!Ndio hayo ya Richmond!yambayana.Leo nasikia kuwa waliomshusha chati wamempandisha tena hadi 95% tena!Nionavyo mimi uongozi ni hekima!Kama alivyo Rais wetu mpendwa Jakaya Mrisho Kikwete.Baba Kikwete ”sala mosala nzambe akosalisa yo”(fanya kazi na mungu atakusaidia)
  Wakatabahu,
  Sifa

 15. nice kz Says:

  Hongera rais kwa mabadiliko uliyofanya katika baraza la mawaziri, kwa kuondoa mafisadi japo kuna ambao wamebaki sasa sijui ulitumia vigezo gani kuwabakiza.

  Tunaomba kama kweli umedhamiria kuondoa ufisaidi tunaomba mhe.Chenge nae aachie ngazi, ndg Hosea wa TAKUKURU na wengine wote waliohusika kwa namna yoyote kwa uzembe au makusudi waachie ngazi.

  Na pili kuonyesha Tanzania Utawala bora tunaomba Mhe. Rais wahusika wote wa ufisaidi mali zao zitaifishwe na ziingizwe kwenye bajeti ya mwaka 2008/09 kwa kuangalia kuongeza nguvu kwenye sekta nyeti mf. kilimo cha umwagiliaji,afya,miundo mbinu,viwanda na usalama wa raia.

  Mwisho kabisa tunakuombea Mungu akupe afya njema katika kutumikia taifa la wanyonge wenye kupenda amani.

 16. Kiapo Says:

  KIAPO KIPYA CHA MAWAZIRI:-
  MIMI JOHN LAGER MAGUFULI, NAAHIDI KUTORICHMOND NCHI YANGU NA KWAMBA NITAMWAKYEMBE MTU YEYOTE ATAYEIBALALI NCHI YANGU.
  NITAJIEPUSHA NA UNGOYAYI, UKARAMAGI, AU USABAHA WA AINA YEYOTE NA KWAMBA WAKATI WOTE NITAWALINDA WOTE WANAOISLAA, AU KUIZITO NA KUIKILANGO NCHI YETU.
  EWE MWENYEZI MUNGU NIBARIKI.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s