BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PRESIDENT BUSH ARRIVES IN TANZANIA February, 16, 2008

 

Rais wa Marekani,George Bush amewasili nchini Tanzania katika ziara yake ya kikazi na ya mwisho barani Afrika kabla hajaachia madaraka.

Nchini Tanzania,kama inavyoonekana pichani,alilakiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete.Makamu wa Rais,Dr.Mohamed Shein,baraza zima la mawaziri,viongozi mbalimbali wa kiserikali na wananchi wengi wakazi wa jijini Dar-es-salaam na mikoa ya jirani walijitokeza kumlaki Rais Bush.Rais huyo wa Marekani amewasili Tanzania akitokea nchini Benin,Afrika ya Magharibi na ataondoka jumanne kuelekea Rwanda kuendelea na ziara yake hiyo barani Afrika.Bush ameongozana na mkewe Laura Bush na Waziri wake wa mambo ya kigeni,Condoleeza Rice.

Nini maoni yako kuhusiana na ziara ya Rais Bush barani Afrika na hususani nchini kwetu Tanzania?Nini mchango wa Marekani kwa nchi zinazoendelea ikiwemo yetu ya Tanzania?

 

Rais Bush akiwa ameongozana na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.
Advertisements
 

26 Responses to “PRESIDENT BUSH ARRIVES IN TANZANIA”

 1. any Says:

  Kikwete is nervous/not at easy! sijui anawaza ataulizwa ufisadi kulikoni? na baraza lake ikawa ikawaje? Maskini, nadhani kaandaa desa!

 2. Gervas Says:

  Mimi hata nafikiri wawekezaji wote Tanzania wangekuwa wamarekani yaani tungefaidika si ki uchumi tu bali hata good pay kwa waajiliwa, upande wa elimu wangewekeza, watanzania wengi wakasoma kule. Maana sisi wenyewe mmeona hatuwezi Richmond inakuwa Richmonduli..ufisadi tu. Sasa tukijifanya jeuri ya kuandamana tutakula jeuri yetu na mafisadi wetu. kwani ubaya wa Bush unaweza ulinganishe na mafisadi wanaokula fedha za watanzania na kusababisha hali mbaya ya wa tz?, umeme juu, huduma za elimu, afya mbovu, mbona watu hawaandamani? Au Janjaweed(waarabu)wanaoendelea kuua waafrica wenzetu, Darful. Mi naomba tufumbe vidomodomo hivi ili bush afanye mambo, maana si ajabu amesikia au ameambiwa kuwa Tanzania has Potential and condusive environment for investment, maana bado Tanzania tupo kati ya nchi maskini duniani. nawasilisha

 3. danieli Says:

  Suits matching Xactly: guess they did it deliberately, uh?

  On a more serious note, what’s the real purpose of the mission? our “oil”? Joking, joking.

 4. Angelina Says:

  Karibu Tanzania Joji, lakini Hili la kufunga mitaa kibao kwa ajili ya ‘easy flow of traffic ‘silipatii picha, hiyo mitaa hata siku za kawaida inakuwa kimbembe, leo ndo ifungwe kabisa My Gosh sijui itakuwaje, nawaonea huruma sana makapuku kama mimi ambao tunategemea daladala kama usafiri wetu mkuu, watatembea kwa mguu mpaka waseme ndio……Joji fanya urudi kwako….soon.

 5. Gervas Says:

  Hey, Daniel! to see how special this visitation to Jk is, He had to watch Kichaka the way he had dressed while boarding his Airforce one in UsA and did the match so as to surprise him. You know what? have u forgotten the huge reservour of Uranium discovered recently at Bahi-Dodoma? and the Colbat somewhere Ngara, just relate that with terrorism. whom do u think can be a good investor on that? Malaria is just a justification…indeed i support him.

 6. Mbarikiwa Says:

  Du! Gervas,
  Kimsingi ninakubaliana nawe baadhi ya mambo, lakini ukiwachunguza sana Wamarekani kuna kitu fulani wanachofuatilia hapa wakisha pata baadae watatuacha hewani. Mfano mzuri wa waliokuwa wakibebwa na Wamarekani hatimaye wakaachwa hewani ni: Savimbi (Angola), Mobutu Seseseko Kuku wa Zabanga (Zaire) na hata Robert Mugabe (Zimbabwe). Hawa Mabeberu ukiwaona wanakuja kwetu kuna ‘dili’ fulani wanafuatilia. Tuombe Mungu uzima kama hatutalala wote utaona kwa macho yako mwenyewe.
  Urafiki wa kweli ni uliokuwa kati ya Tanzania na China, wakati ule wachina hawakuwa na hiana (sijui sasa); tungeendeleza urafiki wetu na china na kuacha kuwa popo (kutofungamana) sasa tungekuwa mbali sana. Hata Umeme tungekuwa na vinu vya nyuklia.
  Watanzania vyote tunavyo isipokuwa ‘teknologia’. Mungu atusaidie.

 7. steve nyagonde Says:

  ok karibu bongo ila achana na uhuni wa security base hapa hiki ni kisiwa cha amani !! Kama umeleta hizo dola milion 700 sie tutakula tu mafisadi kibao mshikaji!! kuna jamaa najua anatamani mwakyembe angetoa report yake mwezi ujao ili mradi tu achote vijisent hivyo na afanye shaken hand with youu!! Allah ujackia wanaita the home land of peace zanzibar and kilimanjaro uctuambie sera za kigaidi sawa we mbabe!! kama vipi waambie wakulete UDSM tutalk critique issue wright men tukupe changamoto ukasimulie america wright!! karibu saana bongo!! hii ndiyo bongo newyork chamtoto!!!

 8. Chris Says:

  Mimi nafikiri BC toeni mada mahsusi ili tuchangie kuhusu hata Mke wa Raisi (mama Kikwete) kuvaa nguo eti yenye picha ya George kichaka.

  Nakuwa na mtazamo tofauti kabisa kuhusu hilo vazi lenye picha.Naona kama amejishusha kupita. Sijui wengine mnaonaje hii jamani. Hata kama ni umaskini duuuuh…

 9. Gervas Says:

  Mbarikiwa! nakubaliana na wewe kabisa unavosema, Mimi binafsi naamini ujamaa ndo mode pekee inayoweza kuleta usawa na maendeleo kwa kila mwanachi. lakini ujamaa ndo unazikwa duniani hivo urusi, China. Ubepari ndo uliopo hauna mjadala labda km unataka kuwa km Chavez na Castro. Nikuulize swali Tanzania tulipenda wenyewe kuukalibisha Utandawazi? au tulilazimishwa!. Hatuna uwezo wa kuwakataa hawa jamaa lasivo tutageuka Zimbabwe, Cuba nk, cha msingi ni kuwa makini tu hasa kwa viongozi wetu. Nchi za Asia kusini Km Malaysia, Thailand wametoka sababu ya kushirikiana na hawa wakubwa. Tusiogope, lasivo uhuni wa kuanzisha kampuni uchwara hata ya mkobani kama richmond afu kwa kutumia influence utakuwa muwekezaji, ndo yanayotokea saizi Bongo!

 10. Dinah Says:

  Tanzani tumejitia aibu na niwa zi kuwa tunababaikia Wamalekani, kufunga barabara ndio sio jambo la busara (kusimamisha shughuli za watu za kimaisha kwa ajili ya kamtu kamoja tu), vilevile kuremba jiji (kupoteza hela) kwa jaili ya siku mbili sijui 3 tu sio jambo la muhimu na ni kupoteza senti za mlipa Kodi.

  Kichaka alitakiwa kulikuta jiji namitaa yake kama ambavyo iko kila siku ili yeye na wenzake akina EU wajue kuwa wanatuibia sana Afrika kwa manufaa yao alafu wanajifanya kutupa misaada ya billions amabyo haifikii walichokiiba na wanachoendelea kujipatia kutoka Afrika na Tz ikiwemo.

  Mama Kikwe kuvalia khanga ya huyo Kichaka ni kujidhalilisha, ulitakiwa kuvaa ya Kikwe au yeyote yenye ujumbe wa kuwaambia US au kichaka mwenyewe kuwa Warudishe mapesa yaliyowekwa kwenye acc za wale ma-balali oops Mafisadi since 1995 mapaka jana.

  Kwa kifupi sijafurahishwa na ziara ya Kichaka bongo, maandalishi yaliojaa ubabaikaji a.k.a kujigonga a.k.a kujipendekeza a.k.a uoga.

  Alafu na ninyi waislamu mliojifanya kuandamaana kuhusiana na vita dhidi ya Ugaidi acheni kutuharibia Taifa letu, kama mnahasira sana na vita yake dhidi ya Osama si mngemfuata huko-huko US…..acheni kujipendekeza indirect šŸ™‚

 11. Mbarikiwa Says:

  Gervas,
  Tanzania tulilazimishwa kuukaribisha utandawazi. Na hii ilitokea baada ya vita varidi kuisha Duniani, pamoja na kusambaratika kwa USSR. Sisi Watanzania tulikuwa Popo (tulikuwa na siasa zisizofungamana na upande wowote = Non-Aligned-Movement). Na hapo ndipo tulipoanza kubaki hewani maana ile siasa yetu ya ki-popo ilikuwa haina tena maana hivyo ilibidi bila kulazimishwa moja kwa moja tuegemee kwenye Ubepari. Huko kwenye ubepari ambako kunaongozwa na Marekani walitupa masharti ambayo kwa namna moja au nyingine ndio UTANDAWAZI.
  Kuhusu hawa wanaoandamana eti kupinga ziara ya Bush, mie sielewi, inawezekana kuna mkono wa Mwarabu; Maana Sijawasikia, au Kuwaona Waislamu na/au Wanaharakati wameandamana kwenda Ubalozi wa Sudan kupinga kuuwawa kwa ‘Weusi’ wenzetu kule Darfur. Au Waislam wa Darfur sio Waislam halisi maana hawana asili ya Kiarabu ??? Kwa kweli sielewi na sielewi kabisa. Sijasikia nchi yoyote ya Kiarabu ikilaani kitendo cha Waislam wa Kiarabu waliopo kaskazini mwa Sudan kuwaua Waislam wa Kiafrika waliopo Darfur. Jamani hapa kuna haki ??? au tuandamane tu kumpinga Bush kuwa ni Muuaji; Je Waarabu wa Sudan si ni Wauaji zaidi ???

  Watanzania, tusiendeshwe na ‘wenye pesa’ kwa kusingizia Imani.
  Mungu atusaidie.

 12. eva moses Says:

  karibuni bongo land

 13. Misifa Says:

  Safari ya Bushi ina mshindo mkubwa!tusicheke wala tusilie!chochote kinaweza kutokea na wala hatuwezi kuokoka!
  Wakatabahu
  Sifa!

 14. ISMA KABENGO Says:

  KILA LA KHERI BUSH,ASANTE KWA DOLA MILLION 700,WALIOANDAMANA AIBU KWENU HAMUONI KALETA NEEMA BARABARA ZA TUNDURU.MTWARA ,SONGEA KUWEKEWA RAMI NANI ANGELITOA FEDHA??????????? TUNGEISIKIA MPAKA 200 KILA LA KHERI WEWE NDIYE RAFIKI WA KWELI

 15. Mama wa Kichagga Says:

  Mi naona kila kitu ni kheri tuu.

  Mji umekuwa msafi hadi raha! Basi tuendeleze huu usafi kwani ni jambo jema.

  Hongera JK kusaini mkataba wa Changamoto ya Milenia.

 16. Matty Says:

  Mi mwenyewe sijaelewa vizuri vitenge wamevaa sare kwa ajili ya mgeni tu na wametumia Tshs. kadhaa za walipa kodi (mweeeee au kwa kuwa ataacha something in our account??ambazo nazenyewe zitaishia juu kwa juu) kuvidraft hapo ndo huwa nachoka, maana mawaziri na wake wa vigogo wa serikali wote wamevalia hiyo sare, si wangevaa nguo zao za kawaida tu!nway karibu at our lovely home!

 17. kijiwe Says:

  Gervas,Mbarikiwa,Dinah
  Nawafeel sana kwa vision zenu.
  Its true there is nooo way and I mean no way kichaka,mchele na wengine wote wakaja bongo for 4 days?
  yaani tusidanganyane kabisa hawawezi kufanya hivyo kama hakuna faida kna kitu kipo related to this lazima hata siku moja republican hawezi kuja kutembelea africa eti kusaidia malaria ukimwi hamna chochote hiyo ni pazia tuu.
  kwanza huyo kichaka alishasemaga during midahalo kabla ya kuwa rais kuwa Africa will be his last priority sasa kulikoni?
  mi nilisemaga huyu vasco da gama hana dili its just another version ya beni mtaona
  nawasilisha

 18. bisekoson Says:

  mhh! ujio huu wa Bush si wa Amani haya ni manyunyu tu ya utandawazi mvua yenyewe bado na tusidhani hayo mamilioni ya madola yanatolewa kwa roho nyeupe kuna gharama zake kubwa ambazo watanzania wengi tutakuja kuumia sana na tutazilipa kwa njia nyengine na kwa hali hiyo tusitegemee hata siku moja kukua kwa uchumi wa Tanzania hata siku moja hakuna bepari ambaye yuko tayari kumnufaisha masikini hata siku moja hizo ni salaam zangu kwa watanzania wenye upeo wa kufikiri.

 19. mmy Says:

  karibu bongo ahsante kwa mshiko. lakini usije kutugeuka baadaye kama umefuata vitu vingine unatuzuga kwa mshiko wako wa madolla na ushindweeeeeeeeeeee. we need peace

 20. tonny Says:

  Nimemsoma Rais Bush katika hotuba zake alizozitoa hapa DSM na jinsi alivyokuwa mnyenyekevu na mwenye bashasha na utu wa hali ya juu akisalimiana na kila mtu bila kuonesha maringo,dharau na kiburi ambacho kwa kiongozi wa nchi yenye nguvu ulimwenguni kama Marekani angeshawishika kuidhihirisha ili watanzania wanyonge wazidi kusinyaa na kuhofia kuwepo kwake nikaridhika kwamba Rais Bush yeye binafsi kama binadamu siyo yule ‘Shetani’ ambaye siasa za Marekani zinataka sisi Watanzania tuamini.Nimekubali kwamba kuwa Rais au Kiongozi wa Taifa kubwa na lenye nguvu ulimwenguni kote kama Marekani Rais wa nchi hulazimika kutii na kutekeleza matakwa na sera za Makampuni Makubwa ‘Conglomerates’ yenye himaya ulimwenguni kote na kukabiliana na taifa lolote litakalo onekana kuwa tishio kwa usalama na uchumi wa taif ala Marekani.Rais hujikuta akilazimika kutekeleza hata mambo ambayo pengine yeye mwenyewe binafsi asingekubali yatekelezwe iwapo angekuwa na uamuzi wa mwisho.Nimpongeze Rias Kikwete kwa dhati kwa ushindi huo mkubwa wa kidiplomasia.Akiwa Mwenyekiti wa sasa wa AU umoja wa nchi huru za Afrika naamini atakuwa ameitumia fursa hiyo ya kukutana na Rais Bush kujenga uwezo mkubwa zaidi wa kukabiliana na migogoro ya Afrika iliyopo sasa na itakayo kuja huko mbeleni.Tujitahidi adui wa rafiki yetu awe rafiki yetu ili tujenge uwezo wa kuweza kuwasuluhisha kwa manufa a yetu sote.Rais Kikwete hakuna kurudi nyuma katika hili.Ufisadi upigwe vita na utokomezwe,Demokrasia iimarishwe zaidi nchini!

 21. Baba Koku Says:

  out of 700 mio usd… 53 mio will be for administrating it? I will administer it for free! Hivi, hizi pesa n mkopo au sadaka?

 22. Ed (USA) Says:

  Pamoja na kutambua kuwa kila mtu ana mdomo wa kusema anachopenda, nimegundua wengi wetu humu tunatumia usanii wa ze comedy tukiweka pembeni uungwana na uzalendo katika kulitakia mema taifa letu changa. Tukiwa makini katika kauli zetu tutawashawishi wengi kupitia humu na kuchota mawazo ya kuelimisha jamii yetu hasa huko nyumbani.

  Ukiwa muungwana na mzalendo lazima utatambua na kupongeza juhudi binafsi za kiongozi wetu Kikwete kufanikiwa kumleta Bush na ujumbe wake nchini Tanzania. Jamaa wamesign $ milioni 700 kusaidia masuala nyeti huko nyumbani. Nasikitika ninaposoma watu wanaokosa uzalendo wanavyobeza ujio na usaidizi huu wakati hatuna hata uhakika ni kiasi gani wanasaidia kuinua uchumi zaidi ya kupayuka wakitumia usanii kufurahisha nafsi zao.

  Pamoja na kuwepo mifano mibaya kihistoria kwa taifa la marekani kama kumsaidia bwana Savimbi na wengineo. Ebu tuwe positive tukisuport mwelekeo mzuri wa rais Kikwete japokuwa kibinadamu upo udhaifu kwa watendaji wanaomsaidia.

  Jamani tukosoe inapobidi kwa kusudi la kuelimisha na sio kupayuka tukiwakimbiza waungwana kupitia humu kupata point za msingi katika kuijenga Tanzania.

 23. anonymous Says:

  usituletee ze huko USA umepewa makaratasi ya kuishi basi unaona kila kitu sawa tu.
  wadau tunaungana kupinga mapepo ya USA na wengine mnaoishi huko USA tunawaombea huyo pepo awafunue.

 24. trii Says:

  jamani huku kusign bila ya wa tz kujulishwa kilicho ndani ya makaratasi hayaaaaa,vizazi vitakuja kilipia miaka ijayo HAKUNA KITU CHA BURE HAPA DUNIANI.hata wazazi wetu tunapokuwa wadogo wanajitahidi kutupa elimu bora ili baadae wakizeeka tujisaidie+kuwasaidia.

 25. tonny Says:

  Nakubaliana kabisa na Ed(USA) hapo juu kwamba wapo wachangiaji wengine wanao itumia vibaya fursa hii ya kupashana habari,kubadilishana mawazo na pia kusalimiana na kujifariji kwa kutakiana heri na kupongezana.Lakini tusisahau vilevile kwamba hili ni kama darasa ambalo huwakutanisha watanzania wa rika zote popote pale walipo ulimwenguni na kuyajadili masuala yatakayo kuwa na maslahi kwa taifa letu.Hatukatai utani au uzecomedy unaweza ukawemo ndani yake ili kuchangamsha baraza ,lakini hilo lisipitilize kiasi cha kuwafanya wasomaji wa kutoka nchi zingine za bara la Afrika na ulimwenguni kwa ujumla wakatuona kumbe sisi watanzania ni majitu ‘hopeless’kweli kweli.Mimi huwa inanipa faraja sana ninapo soma hoja au dodosa zilizotolewa hususan na vijana wetu wa kitanzania halafu ukazikuta dodosa au hoja zile zimejaa busara na umakini wa hoja kweli kweli.Una pata imani kwamba nchi yetu ya Tanzania sasa imeanza ukurasa mpya.Tusirudi kule tulikotoka.Tusiutumie muda mwingi zaidi uliopo sasa kusonononeka na kunun’gunika kuhusu yale yote yaliyopita,yatatunyima muda wa kutosha kuweza kushughulikia matatizo yanayo tukabili sasa na yatakayo tukabili hapo baadaye.Ni kweli tusirudie makosa ya huko nyuma.Atakaye rudia tena makosa yaleyale apumzishwe, kazi imemshinda na usukani ashike mwengine.Safari inaendelea.Tuitumie fursa hii pekee kutoa mawazo yatakayo wajenga watanzania popote pale walipo.Hata wale waliopo Ughaibuni watakapo soma kinacho andikwa na wakafarijika kwamba sasa nchi yetu kweli kuna mabadiliko watanzania wanapiga hatua kimaendeleo tutakuwa tumitimiza wajibu wetu.Linapo fanyika jambo la kitaifa ambalo litastahili kupongezwa basi watanzania wote tushikamane na kuwa na sauti moja.Patakapo stahili kulaumiwa au kukosolewa basi ni haki pakosolewe.Lakini Unafiki hapana siyo jadi ya watanzania.Hilo litatuongezea sana heshima ulimwenguni.Katika ujio huu wa Rais Bush,tayari Watanzania wameuthibitishia ulimwengu kwamba Watanzania ni wakarimu na wapenda amani.Hatuchaguliwi maadui zetu na marafiki zetu.Lakini tungependa kuiona dunia hii ikiwa na amani zaidi kuliko ilivo sasa.Kwa kuja Tanzania Rais Bush atakuwa amethibitisha kwa macho yake mwenyewe ni mambo gani ambayo bara la Afrika litatarajia kutoka kwa taifa la Marekani.Tusisahau kwamba watanzania tunakabiliwa na ‘African Agenda’.Bara letu la Afrika liondokane na Aibu hii iliyopo sasa hadi likapuuzwa kama vile halina watu wanaoishi ndani yake.Watanzania tunacho kibarua hicho.Tukishikamana pamoja TUTAWEZA.YES WE CAN!

 26. binti-mzuri Says:

  SASA HUYO MAMA KIKWETE NA HIYO KANGA YA TANZANIA NA MAREKANI..HIVI YEYE AKIENDA HUKO,NA YEYE ATAVALIWA!?


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s