BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MILLENIUM CHALLENGE COMPACT February, 18, 2008

Filed under: Developing News,Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 12:10 AM

 

Rais George W.Bush wa Marekani(kushoto) na Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania wakitiliana saini kwenye mkataba/mapatano ya Millenium Challenge ikulu jijini Dar-es-salaam jana.Katika mapatano hayo Marekani itatoa msaada wa dola za kimarekani milioni 698 ($698m) kwa ajili ya kuimarisha mapambano dhidi ya umasikini,magonjwa ya malaria na ukimwi na pia uboreshwaji wa miundombinu.Unaweza kusoma zaidi kuhusu mkataba/makubaliano haya kwa kubonyeza hapa

 

Rais Kikwete na mgeni wake Rais Bush wa Marekani wakiwapungia viongozi na wananchi mbalimbali wakati alipowasili Ikulu jijini Dar-es-salaam mapema jana.Zulia jekundu,kwa heshima ya mgeni,lilikuwa limetandikwa.
Advertisements
 

9 Responses to “MILLENIUM CHALLENGE COMPACT”

 1. kijiwe Says:

  Gervas,Mbarikiwa,Dinah
  Nawafeel sana kwa vision zenu.
  Its true there is nooo way and I mean no way kichaka,mchele na wengine wote wakaja bongo for 4 days?
  yaani tusidanganyane kabisa hawawezi kufanya hivyo kama hakuna faida kuna kitu kipo related to this trip lazima hata siku moja republican president hawezi kuja kutembelea africa eti kusaidia malaria ukimwi hamna chochote hiyo ni pazia tuu.
  kwanza huyo kichaka alishasemaga during midahalo kabla ya kuwa rais kuwa Africa will be his last priority sasa kulikoni?
  mi nilisemaga huyu vasco da gama hana dili yeye anachekelea anajua exactly what the 411 he is just another version ya beni mtaona
  nawasilisha

 2. Gervas Says:

  Hapa Bush anafikiria kwamba watanzania wote wananyuka suti namna hii, yaani km wamarekani weusi tu. Nafikiri hata Amana yenyewe waliwaficha wagonjwa wengine, maana ninavyoifahamu amana!!! sasa Bush anaondoka na picha tofauti kabisa na aliyofikiria. Mimi nafikiri wangempeleka Manzese uwanja wa Fisi ili aone jinsi gani chochoro zinazosababishwa na mpango mbaya wa nyumba unavyozalisha mbu wa malaria.
  Pili hizo fueza utasikia zimewekwa kwenye MKUKUTA, MKURABITA, sijui nini, basi tu justification za ulaji. watu wanaenda eti semina ya Mkurabita Kempiski!!! mmm!,

  Edwin Ndaki, tutafika kweli?

 3. Edwin Ndaki Says:

  Mmh!yaani huu upendo kwa Tanzania wa ghafla ghafla hivi?
  Nitabaki kwenye kile ninachoamini kwamba hapo zinapigwa sahihi kama walizopigishwa machifu kuuza raslimali zetu enzi hizo.

  Amerika wanajua kuwa hayo madola wanayomwaga ni “Chambo” tu ila lengo kubwa wapate samaki mnono.

  Tunaambiwa kuna agenda iliyojificha ya kijeshi pamoja nishati.

  Leo mnaka kuwa ni issue ya mbu tu ..muda utatwambia siku zikifika.

  Ene wei ..naaamini tutafika tu

 4. Kimori Says:

  Nimejaribu kupekua katika historia lakini sehemu iliyonieleza kuwa kuna raisi yeyote wa Marekani ambaye ameishafanya ziara ya kiserikali ya siku nne nchi yoyote duniani hata katika zile nchi ambazo ni washirika wake wakubwa.

  Napenda sana kuamnini kuwa hakuna ajenda ya siri inayoendelea ila naona dhamira yangu inaniambia kuwa kuna kitu kinaendelea nyuma ya pazia.

  Hebu tusubiri tu tutaona kama tukijaaliwa kuwa hai, lakini ni mapema mno kufurahia ziara hii pamoja na ukarimu wetu wa kuwafurahia wageni wanapokuja kututembelea nyumbani kwetu.

 5. amina Says:

  yani amekuja bush kila kitu cha kuact,,,red carpet na hawa wengine pembeni wameazimisha masuti tehetehe

 6. tonny Says:

  Jamani Watanzania wenzangu ujumbe wa Rais Bush kwa Watanzania wote ni huu hapa:No Corrupt Government;Good Governance & Trully Democratic Institutions;Market Economics full stop.Serikali isijihusishe na Ufisadi wa aina yoyote;Serikali ifuate misingi yote ya Kidemokrasia na Utawala wa Haki na Sheria;Uchumi wa Soko na Kipau Mbele kwa Sekta Binafsi.Kwa mwendo huu CCM isiogope itashinda chaguzi nyingi zijazo.Kama ni Demokrasia basi Taasisi zote muhimu ili kufanikisha Utawala Bora katika misingi ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa lazima ziwepo.Pawepo na MABORESHO YA KATIBA .Pawepo na Tume huru ya Uchaguzi.Pawepo na Wagombea Binafsi japo hadi ngazi fulani kwa majaribio ya kwanza.Hili likifanyika Tutaichagua CCM kwa kipindi cha miaka KUMI mingine ijayo.Ikiwa Ufasadi utapigwa vita vitakatifu hadi utokomee kabisa basi tutaichagua tena CCM kwa kipindi kingine cha nyongeza cha MIAKA KUMI MINGINE.that makes it twenty years from 2010.Na ikiwa sera zitakazo fanikisha Uchumi wa Soko na Sekta Binafsi zitakuwepo na kufanya kazi na MATUNDA YAKE KWA KILA MTANZANIA YAKAONEKANA,basi CCM itajihakikishia miaka mingine 10 madarakani.HIYO NI JUMLA YA MIAKA 30 MADARAKANI.Kama yote hayo aliyoagiza Rais Bush yatatekelezwa basi CCM itajihakikishia kuwa madarakani kwa kipindi kijacho cha miaka isiyopungua 30.Hapa tunazungumzia mwaka 2040 labda Chama kimojawapo cha Upinzani kitaweza kushinda uchaguzi na kuunda serikali.Kwa hiyo CCM isiogope lolote.Njia nyeupe iwapo tu hayo yatatekelezwa.TRANSPARENCY kiwe ndicho kigezo cha utekelezaji.Hakuna siri katika masuala yanayo husu maslahi ya watanzania.Kila kitu kiwekwe wazi hatua kwa hatua.CCM ITASHINDA.Kinyume na hapo itakuwa taabu!Tanzania should set the example to the rest of Africa in the Democratic Reforms and Liberal Market Economics.We will all stand united for the cause.Kikwete is our INSPIRATION AND RAY OF HOPE.GOD BLESS YOU ALL.

 7. Baba Koku Says:

  Vipi tena, hawa ndio wametuachia pesa na wameondoka na Jamboforums yetu?.. Kichaka kaacha balaa hapa…

 8. Stranger Says:

  Mnaibiwa nyie wenyewe hamjijui…mtanikumbuka,
  Stranger.

 9. amina Says:

  we stranger tukukumbuke kwa lipi..acha kujishaua


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s