BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

WAKUU WA DAR February, 20, 2008

Filed under: Afrika Mashariki,Historia,Mahusiano/Jamii,Serikali/Uongozi,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:04 AM

 

Jiji la Dar-es-salaam lina historia ndefu sana.Tangu enzi hizo likiitwa Mzizima mpaka wajanja walipolibatiza jina maarufu la “Bongo” ingawa baadaye “Bongo” imekuja kuwa sio tu jiji la Dar-es-salaam bali Tanzania nzima.

Katika historia mbalimbali za jiji la Dar,mojawapo ni kuwa na wakuu wake wa mkoa ambao huwa na machachari na mbwembwe za aina yake.Nani anaweza kusahau kwamba kuna wakati jiji la Dar-es-salaam lilikuwa linajulikana kama “Jiji la Makamba” kutokana na uongozi wa Mheshimiwa Yusuf Makamba?

Historia ya Dar bado inaendelea kuandikwa.Kila kukicha Dar inazizima na mambo mapya.Kila siku kuna geni jijini Dar.Kila siku maelfu ya wananchi wanatoka mikoani na kuhamia jijini Dar kwani inasemekana Dar ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi.Haishangazi kwamba mpaka hivi leo,kuhamia Dodoma kwa serikali kumebakia kuwa sera isiyotekelezeka.

Hivi sasa jiji la Dar-es-salaam lipo chini ya uongozi wa Mheshimiwa Abbas Kandoro.Hivi sasa anapumua baada ya jiji lake/letu kufikwa na ugeni mzito wa George W.Bush.Historia yake ndio hivyo inaandikwa.

Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Dar,Abbas Kandoro(kushoto) na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo kabla ya Kandoro,Mheshimiwa Yusuf Makamba.Makamba hivi sasa ndiye Katibu Mkuu wa CCM taifa.

Advertisements
 

5 Responses to “WAKUU WA DAR”

 1. Albert Says:

  Ni vizuri kuwa historia bado inajiandika lakini Ndugu zangu wengi tunaomba Tuwe tunaandikiwa pia Historia ya miaka ya nyuma ya Nchi hii vipi maisha na makazi ya watu yalivyo kuwa kabla na baada ya wakoloni kuingia na kutoka hatuandikwi wala hatuoni hali ilivyokuwa kama vile majengo kivazi vipi watu maisha yayo walikuwa wanaishi (utamaduni wa wakati ule mpaka kufikia hivi sasa )tunasoma historia za nchi majirani na tunaona lakini zetu hatuzioni Tunanaomba tuelimishwe na historia ya jiji hili au nchi hii kwa ujumla ili isijeikatoweka tukabakiwa na Historia mpya tu

 2. Makumbi Says:

  Makamba alikuwa mzushi! alikuwa ananikera sana haswa pale alipokuwa anawasimamisha viongozi wenzake mbele za wananchi na kuwatolea maneno ya kejeli! Kandoro bwana! hana utani wala mzaha na kiongozi yoyote, anawaheshimu walioko chini yake na ndiyo maana hakuna anayeleta mzaha kwenye maagizo yake! Makamba alizidisha mzaha kwenye kazi!
  j K, alishamjua kuwa ni mtaalamu wa propoganda ndiyo maana akampeleka akapambane na wanapropaganda wenzie akina Seif!

 3. Pope Says:

  Makumbi naungana na wewe moja kwa moja, Makamba alikuwa anapenda sana Media Coverage na anazidisha sifa akiona Camera ya TV, Kandoro mserikali hasa anachapa kazi na hana mas’hara hata kidogo kwenye kazi. Acha msambaa akapambane na mpemba wana kunywa chai na seating allowances kila siku hakuna cha muafaka wala nini.

 4. amina Says:

  ndiyo makamba maneno mengi…bora akapambane na wenzie huko…

 5. Ald Says:

  Suti zao nimezikubali!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s