BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HOMA IMENIZIDIA February, 22, 2008

Filed under: Burudani,Maisha,Mapenzi,Muziki,Swali kwa Jamii,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Piga picha hii,mwanamke kaolewa,mume wake anampenda na anajitahidi kumtimizia haja zake zote.Anatokea jamaa anamrubuni.Anamwambia jamaa hakufai,jamaa si lolote si chochote.Njoo kwangu nikupe raha za dunia.Kumbuka kurubuni huku huenda na hongo kadha wa kadha.Bia na nyama choma,viwalo kutoka “mamtoni”,usafiri nk.

Mwanamke anaingia mtegoni na kumuacha mume wake kisha anafuatana na “mshikaji”.Baada ya muda mfupi tu jamaa anasema hamtaki tena.Jamaa keshapata alichokitaka kisha analala mbele,anasema Next!!Mwanamke anaanza kujuta,balaa gani hili?

Mambo haya si yanatokea jamani?Nani wa kulaumiwa kwenye situation kama hizi?Mwanamke au mwanamume?Huo ndio ujumbe muhimu kutoka kwa International Orchestra Safari Sound(IOSS) katika wimbo wao Homa Imenizidia.Bonyeza player hapo chini upate burudani.Ijumaa Njema.

Na kwa wale wazee wa kuruka majoka kutoka majuu,pata burudani kutoka kwa Mfalme wa Pop,MJ,katika Wanna Be Startin’ Something.

Advertisements
 

7 Responses to “HOMA IMENIZIDIA”

 1. Pope Says:

  Aaaaaaaaaah wallah wangu yuleee hata kupotea bado yaillah!!

 2. usinijue Says:

  ama kweli ya kale dhahabu,nyimbo ya zamani lakini ujumbe wake valid mpaka kesho wake zetu wadanganywa hovyo nje na kuharibu ndoa wakishtuka ni too late big up bc……ukija huku kwa mj si jui kwanini hii nyimbo nikiisikia i feel like crying or something,nakumbuka utotoni tuki breakdance sidhani kama kuna mtoto shule miaka ya86/87 alikua hatamani kubreak dance jamani ilikua raha…leo naamini utoto mtam…………..ni mawazo yangu

 3. tonny Says:

  Comments mbili tu hadi leo inanipa wasiwasi kwamba wazee wenzangu walokula chumvi nyingi hawajirushi sana katika masuala ya internet.Pengine kutokana na uchomvu wa kimaisha wote tunajua system ilivyotuangusha wasomi wa nchi hii na wote kwa ujumla.Wangapi wenye Laptop majumbani?Wangapi miongoni mwa watu wazima wenye kujua kutumia Kompyuta kwa mawasiliano?Lakini ukweli utabakia kwamba bila ya busara za hawa wazee wetu nchi yetu haiwezi kufanikiwa kwa kiwango kitakacho hitajika.Ooooooooooooops!Off Point.Now back to the point.Nilichotaka kusema ni Kumpongeza kwa dhati kabisa Nyota Lead Vocalist,Outstanding Composer,Distinguished Poet,and one of the greatest musicians of our times ,the most excellent entertainer of his category, put your hands together to BITCHUKA REHANI, aliyeshiriki kuimba na kuunakshi wimbo huo ambao hakika ulitamba wakati wake!Big up Bitchuka na The Unforgettable OSS Safari Soundo ya DSM.

 4. amina Says:

  MI NIMEZALIWA 85 LAKINI NAUJUA HUU WIMBO NA NAUPENDA..KWANINI WANAMUZIKI WETU WA BONGO FLEVA WASIIMBE NYIMBO ZA MAPENZI KWA KUELIMISHA KAMA HIVI,SIYO KUIMBA DEMU WANGU WE UMEUMBIKA,MARA OOH HUKO NYUMA ULIVOFUNGASHIA, MARA TUKIWA KWENYE SITA KWA SITAM MARA CHUCHU ZIMESIMAMA BASI TABU TUPU

 5. Makumbi Says:

  OLD IS GOLD! Thank you bongocelebrirty, kama ni mapishi ningesema mnayo shahada ya uzamili katika mapishi! Yaaani mnavyotuchanganyia mambo! acha!

 6. Kamanzi Says:

  We amina unaonekana unaakili japo mdogo. Just a comment

 7. DUNDA GALDEN Says:

  YA NI DHAHABU KILA KITU KINAKWENDA KWA MPANGILIO GITAA LIMETULIA,DRAMS YAAANI ENZI HIZO NI MAJUTA TUU POLE SANA KAKA KWA HAYO YALIO KUKUTA LAKINI SI WANAWAKE WOTE WANAOFANYA HIVYO WENGI SANA WANA UPEO MKUBWA WA KUBAINI HUYU NDIE YULE SIO COOL BC BIG UP NDANI YA BONGO
  CHAFOSA ALWAYS NEVER DIE


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s