BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 08 February, 24, 2008

Filed under: Photography/Picha,Sanaa/Maonyesho,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:10 AM

 

Upigaji picha ni sanaa.Sanaa inayoongea bila kutumia maneno.Ili ubobee kwenye upigaji picha,sharti uwe mvumilivu na uwe na ‘jicho”.Yaani uweze kuona mandhari na kwa haraka sana uweze kufanya tathmini ufanye nini au upige picha kinamna gani ili uweze kupata picha nzuri.

Maelezo hayo kidogo ndio unayoweza kuyaona ukitizama picha hii iliyopigwa na Muhidin Issa Michuzi katika fukwe zetu za Zanzibar.Hii ndio picha yetu ya wiki hii.

Picha kwa hisani yake Issa Michuzi.

Advertisements
 

14 Responses to “PICHA YA WIKI # 08”

 1. tanzanitefc Says:

  saidia watanzania wenzangu kuingia site hii kusapoti timu ya tanzanite fc ya atlanta, ambao wanacheza ligi hapa atlanta ga.site yao hii
  http://www.tanzanitefc.com/
  http://www.wabongofc.blogspot.com

 2. Said Situ Says:

  Ah wapi hamna lolote. Nyie marafiki kwaiyo kusifiana na Michuzi muhimu. Mara nyingi tu Michuzi kaboronga lakini uweki hizo picha.

 3. ma'reen Says:

  Wewe Said una matatizo binafsi…kabla ya kusema wenzako wanaboronga jitafakari wewe binafsi kwanza.Naomba utambue uwepo wa herufi “h” katika alfabeti za lugha ya kiswahili…kwa hiyo siku nyingine utakapokua unakurupuka ku-criticize wenzako kumbuka kuandika “kwa hiyo” na sio “kwaiyo”, “huweki” na sio “uweki”…EBO!

  Baada ya kusema hayo naomba utueleze katika picha hiyo ya michuzi ni mapungufu gani uliyoyaona kuliko kusema tu kuwa huwa anaboronga…msooooooonyo!

 4. amina Says:

  ma’reen usinichekeshe…tunaweza kuonana jioni nikakulipia hata kinywaji?bora ulivompasha huyo shosti saidi nani vile ?heheheheh

 5. ma'reen Says:

  Hahahaha…poa amina tutaonana usihofu.

 6. Said Situ Says:

  Huyo ambaye haoni mapungufu kwenye hiyo picha, inabidi akamuone daktari wa macho. Na huyo anyeitwa amina ambae anatetea pumba nataka nimuulize kilichopigwa picha hapo juu ni kitu gani?
  Msimtukuze misupu hana lolote ambalo mimi na wewe tukishika camera ya kisasa tutashindwa kufanya.

 7. amina Says:

  bwana we saidi huwezi kuelewa tunajua sisi wenye upeo na kuelewa..we umeona giza tu…kwa mimi ambae nafanya kazi ktk sekta ya utalii najua ukali wa hii picha tena hata akiuza kwa wazungu atakula hela nyingi..labda kwa kifupi nikutafsirie hii picha imepigwa ktk moja ya fukwe za znz, ni mawio yani jua linazama, na kuna watalii wawili wanawake wanapita pembezoni mwa bahari,acha kukurupuka na kuponda vitu,unajulia wapi mabo haya

 8. ma'reen Says:

  Masikini Said pole sana,maoni yako yanatosha kutoa taswira ya wewe ni mtu wa aina gani…sikiliza kwa makini!Dhamira ya yeyote aliyepiga picha hiyo si kuonesha sura na mavazi ya mpigwa picha…picha hiyo imepigwa kuonesha mazingira ya Zanzibar ufukweni katika machweo ya jua, and this has been perfectly reflected.Naona mwenzetu picha nzuri unadhani ni ya mtu aliyepiga nne studio akionesha dole juu akisema cheers.Pole sana kaka yangu siku nyingine usidandie gari kwa mbele bora uulize uelezwe…watakucheka waaaaatu! Sisi tumeisifia picha hii na kutoa sababu…Hebu na wewe tueleze kasoro unazoziona!

 9. amina Says:

  mi sihitaji kumuona daktaei ila wewe unahitaji uwekewe jicho la tatu kuona vizuri au una jicho moja?ehh saidi

 10. Said Situ Says:

  Basi yaishe ndugu zangu nimeelewa (Nimeelimika) mnachokisema. Mimi niliangalia picha kwa haraka nikaona hamna kitu hapo. Yaani hakuna Meli, watu weusi na hawaonekani na kuhusu kupiga picha jua sidhani kama kuna mtu atashindwa kulipiga picha jua, ndio maana nikatoa hiyo comment maana jua hali move na liko everywhere everyday. Sasa nilishangaa kuona mtu anasifiwa kupiga picha jua.
  Au mnataka na mimi nielekeze Camera juu nipige picha jua nimtumie BC aiweke hapa? Na je mtanisifu kama Mlivyomsifu misupu?

 11. Karim Says:

  Said
  Nadhani kama utakumbuka vizuri,BC walipoanzisha zoezi hili la ‘picha ya wiki” walitamka wazi kabisa kwamba mtu yeyote anaruhusiwa kuwatumia picha.Walitoa hata na maelezo ya size ya picha.Kwa hiyo nadhani ukiwatumia wataiweka tu.Jaribu tuone.

 12. mie Says:

  Mh! uswahili mtupu hapa! nina wasiwasi na haya majina ma’reen na amina anaweza kuwa mtu mmoja. Tabia inaonesha zinafanana hata uandikaji!

 13. Chris Says:

  Said ulivyokubali kushindwa nimekuelewa sana…maana umejua ulipokosea baada ya kuelimishwa na Ma’reen na Amina.Ila pumba ulizotoa kwenye hiyo comment ya mwisho nimeshindwa kupata jibu how to rank you…. JUA HALI-MOVE? Tofautisha kupiga picha jua na kupiga picha mazingira ya kuonyesha machweo ya jua.

 14. amina Says:

  we mie..kama we mzungu unafata nini hapa?siungie kwenye blog za wazungu wenzio?nawewe na huyo saidi ni mtu mmoja hamna lolote


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s