BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

NERVOUS CONDITIONS KUTOKA KWA NAKAAYA February, 25, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Wanawake na Watoto — bongocelebrity @ 12:10 AM

 

Kila kukicha vipaji vipya vya wasanii au wanamuziki nchini Tanzania vinazidi kujitokeza.Mojawapo ya vipaji hivyo ni kutoka kwa binti aitwaye Nakaaya(pichani). Ingawa sio muda mrefu sana tangu alipojitokeza rasmi kwenye anga za muziki nchini Tanzania,tayari ameanza kujitengenezea jina na nafasi maalumu katika fani.

Isitoshe anaelekea kuwa mwanamuziki anayeelewa jinsi gani,yeye kama msanii,anapaswa kuhakikisha kwamba jasho lake halipotei bure.Kwake yeye,muziki sio tu burudani bali pia biashara ambayo inahitaji kila aina ya jitihada za kibiashara.

Hivi karibuni amefyatua albamu yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Nervous Conditions.Ipo mitaani hivi sasa ikiwa imesheheni nyimbo kali ikiwemo hit single yake Mr.Politician inayotamba hivi sasa kupitia vituo mbalimbali vya televisheni na radio.

Kwanini ameeiita albamu yake Nervous Conditions?Tuna maana gani tunaposema Nakaaya ni msanii ambaye amedhamiria kuhakikisha jasho lake halipotei bure?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;

BC: Nakaaya,karibu ndani ya BC,hongera kwa kufanikiwa kumaliza albamu yako ya kwanza. Labda kwa kifupi tu na kwa faida ya wasomaji wetu ambao hawajapata fursa ya kutembelea tovuti yako na kujua mengi kuhusu wewe,unaweza kutuambia juu ya historia ya maisha yako kwa ufupi tu?

NAKAAYA: Mimi ni msanii wa kiafrica, nilikulia Kenya na muziki nimeufanya tangia utotoni, nimeuchukulia kwa makini kuanzia mwaka 2006 na mpaka sasa unazidi kunifurahisha.Nimemaliza album yangu ya kwanza baada ya mwaka mzima studio na ninaamini ni muziki wa tofauti na tulichokizoea.

BC: Nini kilikusukuma hasa kuingia kwenye fani ya muziki?Je unao ndugu au jamaa zako wa karibu ambao ni wanamuziki pia?

NAKAAYA: Ndio, mama na baba ni wanamuziki wazuri tu, na kilichonisukuma ni maisha. Muziki kwangu mimi ni kama tiba, na sehemu yangu ya kujieleza na ya kufurahisha nafsi yangu…

BC: Mbali na kutengeneza pesa na kufanya kazi aipendayo na kutumia kipaji chake,mwanamuziki huwa anaweza kuwa na malengo mengine kabla ya kufyatua albamu. Nini hasa malengo yako katika albamu hii ya kwanza? Na kwa upande wa maudhui au ujumbe katika albamu nzima,ni upi?

NAKAAYA: Malengo kwa kweli ni mengi, hasa hasa ni kuibadilisha sura ya muziki wa bongo, ili ulimwengu ujue kwamba Tanzania au Africa inaweza, pia ninalenga kuwa ‘the next Miriam Makeba’!!!! ujumbe sio mmoja kwenye album. kama maisha yalivyo, album yangu ina message tofauti tofauti… Nawashauri wapenzi wa muziki wainunue kwani nina uhakika watapata vitu tofauti 😉

 

BC: Kumekuwepo na hisia kwamba muziki wa siku hizi hauna ujumbe kama ilivyokuwa katika miziki ya hapo zamani kidogo.Unasemaje kuhusu hilo?

NAKAAYA: Ni kweli kwa kiasi fulani, lakini ninaamini kwamba wa kwangu una ujumbe na mimi ni mwanamuziki wa sasa hivi, it’s a musical revolution!

BC: Kwanini umeiita albamu yako Nervous Conditions?Ina nyimbo ngapi?

NAKAAYA: Ina nyimbo 11.Nimeiita Nervous Conditions kwa sababu, mimi nikiwa msichana wa kiafrika, ni vitu vingi sana ninategemewa nifanye, tangia kuzaliwa, kwa mfano, jinsi ya kuongea, nini cha kusema, nini nivae, kwa kifupi, jamii ina tupresha sana wanawake hivyo muda wote tuna ‘nervous conditions’.

BC: Umewashirikisha wasanii gani katika albamu yako na imetengenezwa katika studio gani?

NAKAAYA: Nimewashirikisha wasanii wawili tu, M1 of Dead Prez, na Lufu. Album ilirekodiwa 41 records, Dar–es- salaam.

BC: Wakati tunaanda mahojiano haya umetudokeza kwamba wewe mwenyewe ndio unasimamia shughuli nzima ya usambazaji wa albamu hii.Kwanini umeamua kufanya hivyo?Pia unaweza kutuambia mpaka hivi sasa,wapenzi wa muziki wanaweza kuipata wapi albamu hii?

NAKAAYA: Nimeamua kufanya hivyo kwa sababu nime invest muda na pesa kwenye project hii, na haina maana kwangu mimi kumtumia distributor, ambaye ni mmoja tu hapa Tanzania na ambaye kila msanii anamlalamika, sio maendeleo mazuri. Kama tunataka muziki wa bongo uendelee na ulipe, sisi kama wasanii lazima tun’gate msumari na tufanye wenyewe hadi siku tutakapompata distributor mwenye haki na faida kwetu sisi.

Wanaweza kuipata au kuinunua kupitia Shear Illusions- Millennium Towers na Mlimani City, Rose Garden na pale Nakiete Pharmacy. Pia wanaweza kuinunua online kupitia www.cdbaby.com.Wakiingia pale wanaweza kusearch tu jina ‘Nakaaya” wataipata.

 

Cover la Nervous Conditions

BC: Wimbo wako wa Mr.Politician ni hit single yako.Kwanini uliamua kuandika au kuimba wimbo wenye maudhui ya namna hii?Je siasa za nchi ni jambo ambalo unalifuatilia kwa karibu?Nini mtizamo wako kwa ujumla kuhusiana na siasa za Tanzania?

NAKAAYA: Mtazamo wangu kwa ujumla na siasa yetu ni mtazamo ambao ninao kwa Africa nzima, na nadhani nyimbo yangu inaueleza huo mtazamo kwa kituo. Ndio, nafuatilia siasa ya dunia nzima kwa karibu..

BC: Katika baadhi ya nyimbo,ukiwemo huo wa Mr.Politician,umechanganya kiingereza na Kiswahili.Ni kwanini umeamua kufanya hivyo?

NAKAAYA: Kwa sababu nina kitu cha kusema, na ninataka dunia nzima inielewe, mimi kuwa mtanzania haina maana lazima niimbe kiswahili, mtu wa Nigeria ambaye amechoshwa na siasa za kwao atanielewaje? Kiingereza ni lugha ambayo inaeleweka zaidi ya kiswahili, na pia nilipenda kuwa adventurous…

BC: Ingawa hujaanza shughuli za muziki muda mrefu sana uliopita,tayari umeonyesha kuwa msanii ambaye ana malengo makubwa.Ungepewa nafasi ya kuwashukuru watu wasiozidi kumi ambao mpaka hivi sasa wamechangia mafanikio yako ungewashukuru kina nani?Kwanini?

NAKAAYA: Yaani ni watu wengi mno na kwa kiasi kikubwa sana siwezi kuwataja mmoja mmoja, na ninawashukuru sana.

BC: Tukiachana na mambo ya albamu yako,ni wanamuziki gani ndani na nje ya Tanzania ambao hujafanya nao kazi ambao ungependa sana siku moja kushirikiana nao kwa njia moja au nyingine?

NAKAAYA: Ningependa kufanya kazi na K’naaan, Sizzla (ambao tunafanya makubaliano ya album ya pili) Miriam Makeba, Ms Dynamite…..mmmh wengi mno! Tuombe heri!

BC: Vijana wengi huwa wanapenda kupata ushauri wa kimaisha na kimahusiano kutoka kwa vijana wenzao kama wewe.Ungependa kuwapa ushauri gani vijana wenzako kuhusiana na suala zima la maisha na mahusiano kwa ujumla?Wewe mwenyewe umeshaolewa,una mchumba au..?

NAKAAYA: Ndio,nina mchumba, na ningependa kuwaambia vijana wenzangu, wawe jasiri na wasikate tama.Maisha ni kizungu zungu na huwa yanabadilika usipotegemea, kama moyo wako unataka kitu, kifuate na ukipiganie usiogope, na usikate tamaa.

BC: Nini mipango yako ya baadaye kisanii?

NAKAAYA: To be better and better, and the best there ever was in Tanzania and in Africa.

BC: Kila la kheri Nakaaya.Tunakutakia mafanikio mema katika shughuli zako.

NAKAAYA: Asante sana. peace

Advertisements
 

70 Responses to “NERVOUS CONDITIONS KUTOKA KWA NAKAAYA”

 1. amina Says:

  kwani lazima utie na kiingereza unaboa bwana..usista duu usio na maana….na unatoa albamu wakati nyimbo zako nyingine hujatuonjesha?hii moja sawa nzuri ila unatakiwa uzoeleke kwanza kabla hujatoa albamu…he nyimbo moja albamu..

 2. Joyce Says:

  To be honest nampa hongera sana mwana dada kama kipaji kweli anacho hata mimi nimemkubali sana keep it up my sister!!!

 3. Edwin Ndaki Says:

  Nakaaya safi kwa hatua uliyofikia.

  Kikubwa ambacho wasanii wa kibongo inabidi kufanya ni kama ulivyo amua kutomlamba miguu huyo MDOSI ..msambazaji wa kazi za wasanii.

  Najua wapo wasanii wachache ambao wanaonyesha kwa vitendo kuwa wanapinga wizi wa huyo mdosi.

  Pongezi kwa Ngwair,Mr II sugu na wengine woote wenye misimamo mikali kutokubali kulamba miguu ya mdosi.

  Ila ka USHAURI tu Nakaaya.

  Jinsi maelezo yako ulivyoyatoa hiyo album inakuwa ngumu kwa watu walio nje ya dar wasiotumia mitandao kuipata.Hivyo mbali ya hizo sehemu ulizotaja ambazo zote zipo Dms.Ni vema angalia jinsi gani ifike na huko Monduli,Mwanza n.k

  Najua wengine wanaweza kununua kwa kutumia mtandao ingawa kwa hapa bongo ni wachache wanaweza kutumia hiyo hudumu.

  Nakutakia kila la kheri,unaweza..endelea

  Peace an love Nakaaya

 4. Pope Says:

  Hongera dada unajitahidi,
  jiyo Colabo na akina makeba uifanye kweli sio uandike tu tuone una malengo!!

  Maana Q-Chilla aliwahi kusema kwenye interview kuwa yeye anajilinganisha na akina The Game!!

 5. Mama wa Kichagga Says:

  Nakaaya,

  Kazi nzuri sana. Nakuweka kwenye kundi la wanawake wanamapinduzi!

  Usikilize moyo wako utashinda.

  “Go confidently in the direction of your dreams! LIVE THE LIFE you have imagined!”

  Kila la kheri.

 6. mchangiji Says:

  Huo wimbo ulio kwenye youtube ndio wa kwanza kwangu kuusikia kutoka kwa huyo dada.Nampongeza kwa JITIHADA ZAKE za kutaka kuwa msanii bora.Mnaopongeza mafanikio,msisahau kumpa changamoto ya yeye kuangalia nini kina-miss kwake kama msanii.Mie nimepongeza jitihada tu

 7. Dinah Says:

  Kazi nzuri, mahojiano bomba ila kwa mujibu wa ganda la CD ni wazi kuwa umewalenga wanaojua kiingilishi kimauzo nikiwa na maana kimataifa kwa vile msikilizaji mkuu, mshiriki wa matamasha na shows na mnunuzi ni yule mbongo wa kawaida ambae ktk hali halisi kiingilishi ni lugha ya 2 na haitilii maanani.

  Ukitaka mafanikio ya haraka ni vema kuanza na pale ulipo ili sio tu ili wakuzoee bali kwa kufanya hivyo kutasadia wao kukutangaza (kuzungumzia kazi na kipaji chako) kama wanavyokuona kwenye shows zako nakukusikiliza Radioni.

  Angalia wasanii wenzako wa muziki wenye mafaniko hapo nyumbani akina Jay Dee, Ntuyabaliwe, Twanga pepeta, Deo mwanambilimbi waliegemea zaidi mahali walipo kabla hawajaanza kujirusha “kiingereza”.

  Vilevile pigania kazi zako zipigwe radioni the more zinapigwa the better mana’ke ili msikilizaji anunue kazi yako inabidi asikilize kazi hiyo….toa singles chache kwa nyakati tofauti kabla ya kuachia Album nzima….epuka kutoa nusu ya nyimbo zako kama single kwani kufanya hivyo kutafanya watu wasinunue kwa vile wameshazisikia karibu zote.

  Umauzi uliochukua wa kusimamia usambazaji ni mzuri, ila kutokana na ugumu wa shughuli yenyewe hasa wakati wa ku-promote the ablum (tour) utahitaji msaidizi au msimamizi amabe sio wewe….zingatia hilo.

  Kila la kheri na mafanikio mema ktk shughuli zako.

 8. Subby Says:

  Sasa jamani mnamshauri aimbe kiswahili kama hakipandi je? Msinicheke, hawa watoto wetu siku hizi wanapelekwa kusoma International school au English Academia tangu yuko Chekechea na akirudi nyumbani mzazi unakazana na hiyo broken Inglish yako ili mtoto aongee inglish nyumbani na shuleni. Na hata huko nyumbani anakuja kipindi cha likizo, na shule kumeandikwa speak english only. Hebu niambieni akishakuwa mkubwa ataweza kweli kuongea kiswahili fasaha? Au kutunga mashairi ya kiswahili ili aimbe?

  Hapo Nakaaya si wa kulaumiwa kwa sababu hata kwenye vijiwe vyake inglish ndiyo lugha yake ya mawasiliano na ndio iko comfortable kwake kuwasiliana na watu. Ukimhamisha kwenye kiswahili pengine atachemsha.

  Nakaaya hiyo ni changamoto prove me wrong! Imba kiswahili tuone kama kweli unakijua!

 9. anon Says:

  huyu demu sijui huwa anaimba nini? mi naona anang’ang’aniza umaarufu
  mtu atakae ni-convince anionyeshe kazi zake kabla Nancy hajawa maarufu, anionyeshe prove kuwa kaanza kuimba way before Nancy hajaingia kwenye umiss mkishindwa basi jibu ni “kaingia kwenye fani kutafuta umaarufu” sio mbaya ila you can easily tell from her songs
  If trying to follow “fake it till you make it”, still have a long way for that na kama wengine walivyosema put focus to home market
  usis-ta-do wa kuongea english sio biggy nowadays

 10. Pope Says:

  Subby ndugu yangu!!!
  Kuna wasiojua Kiswahili na wameimba kiswahili!! Kuna wajapan wameimba Kiswahili na hata Wachina Pia, umeshasikia Interview za Josse Chameleon wa Uganda hajui kiswahili lakini umeona anavyoimba vizuri Kiswahili? hata Michael Jackson aliimba kiswahili sembuse Nakaaya jamani!!

 11. amina Says:

  mmbana comment zangu nyingine poa tu

 12. Dinah Says:

  Naomba kuweka sawa kidogo….ilipotumia maneno “kiingilishi” na “uingereza” nilimaanisha Kimataifa. 🙂

 13. Matty Says:

  Kwanza nampongeza wimbo mzuri kwa upande wangu mimi, haijalishi language aliyotumia iwe mix na kiswanglish poa tu!hizo bongo fleva za kiswahili kila siku, hebu nakaaya tupe na singo moja ya kimasai kabisa tuburudike!
  Nakuunga mkono Subby hapo juu, wengine wamesoma International school kwa hiyo bora tuwaache wafanye kile roho inapenda!

 14. asaki Says:

  JACKLINE (KLYN) ANAMAFANIKIO GANI KUUZA SURA MAGAZETINI? AU? HATA KUIMBA HAJUI BASI HIVYOHIVYO TU JINA BASI. JD BWANA YUKO FULL HANA MPINZANI

 15. Chris Says:

  The gal flies.

  Nyie mnaosema kiinglish nawashangaa sana. Mzee Tuku week kadhaa alikua huko Bongo,humu ndani watu kibao mlimkubali.Japo si nyimbo zake zote mnazielewa zaidi ya mirindimo tu.

  Kila mtu ana asprirations zake,she has to fulfil them in a way she deems is best. Na international lgs zina nafasi yake katika kufanikisha hilo,japo si always,maana hata Akon anakubali kazi za AY-japo AY hajawahi imba kiinglish,maybe km sijawahi isikia hiyo nyimbo.Tena uzuri yeye baadhi ya nyimbo kaimba Kiswahili.

  Tumpe support tu mdada,japo its good pia kutoa challenges km hizo,think she will harmonise those challenges.

  Keep on flying Babe…. Head up…

 16. Anna Says:

  Nyie wote mnaoandika eti aimbe kiswahili au aungee kiswahili ni washamba. lugha yeyote inaweza kutumika kuimba na hata kuongea ni utashi wa mtu.
  Kama mnamjudge basi angalieni kazi zake sio kukaa na kuangalia ooh lugha sijui nini?
  Kinachotakiwa ujumbe ufike.

 17. mtz Says:

  Mie ninaishi Marekani kwa miaka kumi sasa. Chukua Mkenya au Msauzi yoyote hanifikii kiingereza, bt bado naongea Kiswahili fasaha. Huyo dada bishoo tu.

 18. Michelle Says:

  Heeeeeeeeeeeeeee we dada umechanganyikiwa nini? Miriam Makeba hakuwa anaimba nyimba za aina hiyo, jifunze kutumia sauti yako kwa kuimba zaidi ya hapo fanya nyimbo zinazoweza kukuonyesha uwezo wako wa sauti, Jaribu vitu kama R&B jamaniiiiiiii mpaka mnachosha aaah.

 19. amina Says:

  mtz nakuunga mkono,hao wanaomtetea wao ndo washamba na wanashabikia vitu wasivyovijua….huyu ni sista duu tukubaliane ila hatukatai kama anaimba vizuri..mnamshushua nani hapa,bendera wafuata upepo

 20. LOUISA Says:

  WIVU SINA ILA ROHO INAUMA (WABONGO WANATABU SANA) NAKAAYA NYANYUA NDINGA KILA MTU ANAPENDA KWA MTAZAMO WAKO MIMI NIMEKUFAGILIA SANA NA ENDELEA WALE MAIMUNA HAKUNA MTU ALIWANYIMA KWENDA SHULE WAKATI SISI TUNAHAMKA ASUBUHI KWENDA SHULE TENA BURE ULIPI ADA A NORMAL GOVERMENT SCHOOL WAO WALIKUWA WANAKULA MAANDAZI NA CHAI ZA ILIKI NDIO SHIDA HIYO .NAKILA MTU ATAUCHUKUA MZIGO WAKE MWENYEEEEE

 21. Ed Says:

  “To be better and better, and the best there ever was in Tanzania and in Africa”

  Here we go again, another celebs. I think i need reality check concern so called Tanzania celeb.

  I have nothing against that quoted statement above, however it sound more political incorrect.
  Other than that, i don’t know nothing about this young lady, but she sound smart and energetic

 22. amina Says:

  HALAFU MWANANGU UNABANA SOMETIMES EHH UFISADI HUO

 23. tatu Says:

  Hivi nyie mnalalama nini hebu muacheni NAKAAYA wa watu aimbe anavyopenda hata akiimba kilugha ni kivyake tu. kwani hamjui siku hizi kiswanglish ndio lugha ya TZ nyie vipi wenyewe tu hapa mnatoa micomment yenu kishwanglishi sasa kwa nini hamtumii kiswahili kitupu?

  Inamaana NAKAAYA ndio wakwanza kuimba kiswahili na kithungu????

  NAKAAYA WAACHE WENYE MIDOMO WAANDIKE ILA MIE NASEMA HIVI MR. POLITICIAN YAKO INABAMBA KINOMAAAAAAAAAAAAA

  BIG UP SAAAAAAANAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

 24. Goodluck Says:

  I am going to write this response in English because I dont think we have a word in Swahili for HATER, which clearly, many of you are. But it’s cool. Folks hate on Mary J and Whitney too… I just hope Nakaaya continues to do her thing. It doesn’t matter what K-Lynn or Jay D do, they are their own people and should do their thing, and you all should let Nakaaya do hers. Its funny to see people on here hating on English, but you are the same people who support foreign, English speaking artists more than you support Tanzanians. Who gets more airplay, J Moe or 50 cent? Whens the last time any of you bought a Swa movie from a hawker on the street? And if you are critical of English because you want to support Tanzanian culture, why aren’t you all just as critical of all the wigs and weaves we see on this site, Michuzi, all the papers… I mean come on… since when is straight hair Tanzanian? (Please don’t bring up Richa, that’s a whole different story…and a sad one at that).

  Why don’t we celebrate the fact that she spoke up, in English and Swahili, about issues that we should all care about, while the Bunge sat by and let us get robbed… over and over and over… and then pretended they were doing us a favor when they finally did their jobs and spoke up. They still haven’t cancelled the Richmond contract (now there is a piece of work in English you should be hating on), nor has Lowassa been punished… and I doubt he will be. He still has his cushy job as a minister and will still get a lifelong retirement package for his two years as Prime Thief.

  Where were all the voices of dissent at the way our President bent over for Bush… in English… Why is Tanzania the only country that offered such uncritical praise to a man widely seen as one of the worst Presidents in American history? Is that less important than whether or not Nakaaya mixes English and Swa on her album? Let’s get our priorities straight… Please.

 25. Jennas Says:

  Amina me najua kuna kitu unatype ila wanakubania kuweka hadharani embu ngoja na mimi niangalie kama hii itawekwa hapo.

  Alafu ndo niandike nyingine.

 26. Said Situ Says:

  We jennas mkwara wako wa kutanguliza hiyo sentensi umefanya kazi. Kwa mantiki hii kuanzia leo nikitaka kuandika kitu cha utatanishi natanguliza sentensi yako ya mwisho.

 27. Said Situ Says:

  Hivi huyu nakaaya na nansi sumari wakoje? ni mama yake mdogo au? Naona anafanana na nansi hasa kwa hiyo hair style.

 28. KOBY Says:

  We Amina
  Embu soma jinsi Goodluck alivyo fafanua..Big up Nakaaya kwa kuongeza huwezi jua malengo ya mtu kwanza biashara si ndani pekee watu wanaangalia ,masoko ya nje ya nchi may be in euro,us etc.cha muhimu ni kutarget ur dreams mtu haishi au kufanya kazi kama unavyo taka ila anafanya kadri malengo yake ya mbeleni..si mara oohh sister du ..oohh kaimba.. ki english..sasa huo usister du ukowapi hapo sasa? huwezi kumbadilisha mtu aonekane mchafuchafu au kama unavyo taka nawakati si style ya maisha yake..naheshimu ndoto za mtu mwache afanye anacho dhani ni bora kwake na maisha yake…umeambiwa hiyo Project aliiandaa mwaka mzima hivyo lazima uelewe hakukurupuka..labda ungekuwa mstaarabu unge muuliza nini malengo yako kimataifa?..lakini zaidi ya hapo unaweza ukaona ana kitu cha kimataifa..halafu wabongo wachache wakisha ona kunamabadiliko kidogo tuu oohh..hajui!!!!!.BIG UP NAKAAYA LOVE U GURL.

 29. kkiwango Says:

  Jamani mi sio,mchangiaji wa hii site ila leo imenibidi niseme machache na mie!
  Huyu binti kwa kweli anajitahidi, nilikuwa sijapata kuzisikia nyimbo zake, hii ni ya kwanza, anajitahidi mno kwa viwango vyetu vya Tz. Kwa wale mnaomnanga eti aimbe kiswahili, hiyo ni stage ya baadae, huyu bado ni msanii mchanga anatafuta soko na ameangalia mbali zaidi katika soko la kimataifa, believe me!! kama mtu hafahamu kiswahili na hajawahi kumsikia ni ngumu kununua CD yake ila kama atajitahidi kwa albamu hii apate soko hata la nje na mamfahamu basi albamu zinazofuata hata akiiimba kindengereko watanunua tu sababu wanamfahamu tayari.
  Ningeomba badala ya kumnanga tumpe moyo hivyo ndivyo tutaendelea, wasanii wa bongo wanaoimba kiswahili wako wapi na lugha yao??? Keep it up girl!!
  Kwenye radio zetu top ten charts ni kina Beyonce na wenzie, je wameimba kiswahili? Mbona tunataka kumtumia binti wa watu ndio afanye kazi ya BASATA wakati shirika lipo na malengo yake yanajulikana?
  Mangapi yanafanywa na watanzania na yanatukuza uzungu?
  Anyway!!
  Nakaaya you go gal, am your No1 fan.
  By the way kama ukisoma maoni haya drop some lines, kkiwango@hotmail.com, nina jambo la kuongea na wewe!!!

 30. Chris Says:

  Kkiwango kumbe mkware/bazazi tu…

 31. mtz Says:

  Jamani mlioko bongo acheni ushamba, BIG UP sio kiingereza sahihi. Pulizi.

 32. mtz Says:

  Amina pole sana. Bongo wamezoea kusifiwa na ubishoo. Comment yako kuhusu kutambua market ni muhimu sana. Ukiimba kwa lugha ya kwenu ndo unathaminiwa. Watu hawajui kwamba soma shule yoyote Africa ukienda Uingereza, Canada au Marekani wanakuona hujui Kiingereza na hawakuelewi ukiongea. Tembeeni muone, halafu mtakithamini Kiswahili na Nyerere wake

 33. amina Says:

  we koby,sisomi na utanifanya nini?unajua maana ya comments?kila mtu anamshauri vile anavyoona,atakachoamua kufata afate!we kama nani unaniambia mi hivyo au huyo gudluck ni nani?mnababaikia vitu vidogovidogo

 34. amina Says:

  jennas mwanangu huyu bc amekatakata coment yangu ya kwanza ndo mana namnyamba na n yingine hajatoa kabisa..tumfungie nini blog tuseme huu ni mtandao wa kigaidi?unaliongeleaje hilo mkuu

 35. zawad haji Says:

  Nakaaya anatisha me namfagalia sana,Napenda anavyoimba kwa hisia na hata sauti yake ananimaliza kabasaaaa! kuhusu kuchanganya lugha mboni poa tu jamani hata yule asiyjua kiswahili atajua huu wimbo unamaisha nini.Na huyo anaeuliza nancy na Nakaaya eti mtu na mama ake mdogo, kwani hajui kuwa hao ni mtu dada ake au anazuga tu, hata magazeti yanaandika.

 36. amina Says:

  FREEDOM OF SPEECH NDO TUNAIANGALIA HAPA..MSITAKE TUWAFATISHE MNACHOPENDA NYIE ALA

 37. amina Says:

  WE KOBY,KWANI MI NIMEMWAMBIA USISTA DUU NI USAFI NA ANATAKIWA KUWA MCHAFU?USISTA DUU UNA MAMBO MENGI HATA ACTUALLY,INFACT,ATLEAST,UNLESS OTHERWISE KTK KILA SENTENSI NI USISTA DUU AMBAO MI NDO NIMEMAANISHA, KWANZA NINI MAANA YA COMMENTS NIKUULIZE?WE MSHAURI UNAVYOTAKA NAMIMI NAMSHAURI NINAVYOTAKA USIINGIE KWENYE ANGA ZANGU NITAKUSAMBARATISHA…HAPA TUNAMSHAURI NAKAAYA SIYO KUMSHAURI AMINA….UNAMSHUSHUA NANI HAPA

 38. Matty Says:

  Amina usiwe na chuki mtu wangu kwani kuimba kiswanglish inakuwa nini wangapi hawajatumia kiswahili na isitoshe watu wanakubali kazi zao.
  Mfano Saida Karoli alianza na kihaya mix na kiswahili (chambua kama karanga, wanchekecha nkebinyobwa) na sasa anaingiza sokoni album yenye nyimbo za kiswahili na kihindi kama kuchi kuchi hotaeeee nakupenda kama gahawa n.k
  Watu wanaangalia masoko zaidi si kuimba kiswahili tu!!!sasa sisi tunaomkubali Nakaaya na wewe nani mshamba???imba na wewe kimakonde tusikie te te te !!!!nakutania.

 39. Michael Says:

  Kuna mmoja wetu mtoa comment naona amekosa kazi. Embu mumuignore, muacheni aandike anachotaka hata kama anakosea. Naanza kuona kwa nini BC anahitaji ku moderate comments la sivyo maoni ya mabwege yatajazana humu.
  BC embu chuja zaidi maana kama mtu hana kazi ya kufanya baki ya kubisha na kupinga kila anachokiona akalime kijijini kwao huko kwa wajinga wenzie.

 40. KOBY Says:

  Amina,mimi sina la zaidi nilikuwa najaribu kukuweka sawa tuu kimtazamo..ok nimekuelewa.
  mtz.nashukuru kwa maoni yako pia..nitatafuta kiingereza sahii…

 41. QG Says:

  i thinx hyo albamu umepewa utoe bure !!!! lol bt Hongera

 42. amina Says:

  matty mi sina chuki huu ni mtazamo wangu tu……hata lady jay dee namafanikio yote haya kuna watu hawamkubali si ndio…..na lazima tuziheshimu comments za kila mtu mi sijampinga mtu humu ila nimempinga nakaaya ila nashangaa watu mmekaza amina amina

 43. amina Says:

  BC hapa weka unachokiona we kinakupendeza kwenye macho yako isipokua matusi tu…anaeona kunaubwege humu yeye ndo asiingie humu,akafunugue mitandao ya werevu huko….atuache sisi wajinga humu,bc hongera unaelewa nini maana ya comments ndo mana unaziweka ingekua ujinga usingeweka!hata mungu pia mabaniani wanampinga ndomana wanaabudu masanamu

 44. james Says:

  jamani tusimbanie huyo dada mwenyewe kasema ame invest hela na muda katika ku iandaa albam yake labda hela nyingine zilienda British Council kwa ajili ya kuwapata wataalam wa lugha,all i can say is big up to you Nakaaya my be you will open a new page of Tanzania music

 45. Matty Says:

  Nimekupata Amina!!!!

 46. caroline Says:

  wewe amina usiwe na mdomo sana wewe yako iko wapi? tuone ili tukosowe? au unaongea tu. na wewe ni wale wale una lolote wewe amina

 47. mhondo Says:

  kaza buti sister ,personally i real salute you,keep on but mind you that the game z hot,so what you have z just to be more creative.dont mind on what the say any way

 48. mkwanja Says:

  Nakaaya nakupongeza sana, uko bomba! Waweza kujaribu hata modelling sometime yaweza lipa mtu wangu!Ukiweza katika tungo zako pia jaribu lugha mbalimbali za kimataifa kama vile spanish, french, lingala, kichina nk. utkuwa umewafikia wapenzi wako ulimwenguni kote.Hujui muziki wako utatangulia kukubalika zaidi wapi na wakati gani.JUST KEEP ON KEEPING ON. And give them people what them people want.Give them Real Raw Stuff, dig me babe! Acha waendelee ku EXHALE tu pumzi zitawaishia! Looking forward to your yet another BLOCKBUSTER! Wanga watakoma mwaka huu mshikaji wangu!

 49. jomaeli Says:

  wengine humu ni bendera wafuata upepo, hata hicho kiingereza hamuelewi lakini sababu flani kasifia basi…..nanyonyi mnasifia,mziki mnauelewa au mashabiki tu?acheni kuropoka

 50. any Says:

  dadangu punguza menu, ukizidisha apa utakuwa mkubwa sana, na apo mbado katoto. ni mtazamo tu.

 51. deiz Says:

  yani we any unaonekana una sura mbaya sana

 52. any Says:

  Wee deiz u wanna talk to me, bring it on, and we will start from there.
  Yeah, sura ninayo mbaya wee yako nzuri unauza bei gani?

 53. deiz Says:

  nimefurahi sana any, nitafute nikupe bei on hdhfefbheeufgvh.net

 54. any Says:

  i am done shopping, why dont u focus ur business kwenye sehemu zenye market. Sikujua hadi leo watu mnaringia sura. Sura zinaletaje maendeleo if i may ask u?

 55. changa la macho Says:

  Hey Yoo,deiz & any,stop that silly nonsense!Hakuna anayepanga azaliwe vipi.Utajikuta umezaliwa tu vyovyote vilivyo ni mapenzi ya Mungu.Besides,’BEAUTY IS IN THE EYE OF THE BEHOLDER’,alituasa Shakespeare,genious mmoja wa lugha ya Kiingereza.Uzuri u machoni mwa mtazamaji.Aliyependa, Chongo huita Kengeza.Wewe ukisema ni Mwanamke gani,Mwenzio anasema atampata lini.Halafu,jamani uzuri hauliwi.Kosa sura upate bahati.Fikiria dunia hii binadamu wooooooooooooote wangekuwa weupe.Dunia hii ingechukiza kiasi gani?Vivyo hivyo,fikiria dunia hii watu wote wangekuwa weusi.Dunia ingechosha kiasi gani?Haya fikiria nyingine,duniani hapa watu wote wangekuwa wanafanana kwa kila kitu kuanzia sura hadi unyayoni.Dunia ingependeza kweli?Mwenyezi Mungu alikuwa na siri yake kutuumba Binadamu tukiwa na maumbile tofauti.INAPENDEZA SANA!Kosa Sura Upate Akili!Lakini uwe na sura lakini akili huna ni Balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,mdogo wangu.Ushauri tu.

 56. deiz Says:

  Asante sana kaka changa la macho kwa ushauri wa busara, nitazingatia uliyoyasema, god bless u

  peace

 57. mtz Says:

  wewe deiz una ‘lucky of education’!! Degree za Marekani sio mchezo

 58. mamii Says:

  Wote mnaompondea Nakaaya either mna wivu au hamuelewi nini hasa malengo yake… mmoja wenu amesema hata wazungu, wajapani wanaimba kiswahili, je mnafikiri ni kwa nini… jamani naomba niwapeleke shule na nimpongeze Nakaaya kwa kuwa na targets za kimataifa.. mnafikiri yeye aliimba ili waswahili tuu ndio wasikilize?? ameweka vionjo vya kiiengereza na kiswahili ili aongeze idadi ya fans!! hii ni hatua kuelekea muziki wa kimataifa… Tumechoka bongo fleva!!!!!!!!

 59. ze bebi Says:

  nakaaya uko juu,na unaweza kuimba ucpyme!! but watch ur dress code mtu wangu…hapo katikati hujatulia wala niini….ficha tumbo hizoooo, naona zimepaki.si lazma kuziacha tumbo hizo wazi,jama….unazo kama tatu hiviiii…ila nakupenda

 60. maryciana Says:

  hiyo picha ya pili,mbona katoka kaa jini?

 61. maryciana Says:

  hahaha MATTY NUMBER 38, WEWE NI MUHAYA NINI??? hahaa

 62. maryciana Says:

  amina comment yako ya 1 ina utata kidogo… mbona marekani au nchi nyingine yoyote watu wanatoa mwimbo mmoja then ndio albamu,anakupa kionjea,ili kama umekolezwa uinunue albamu,sasa ulitaka atoe nyimbo zote?wats the point of the albumt hen…. JAMANIII EEEEEHHH

 63. maryciana Says:

  JUST A CONTRADICTION POINT!!!!!

  KISWAHILI CHENU KIMEWAPELEKA WAPI TANZANIA???LETS BE FRANK PEOPLE, ENGLISH NI LUGHA YA KIMATAIFA,,ITS ABOUT TIME TUANZE KUKIPRATICE MMEKAZANIAGA KISWAHILI,NDIO MAANA MTAFIA NA UMASIKINI WENU..SASA HIVI MIMI NI MDANISH!

 64. Gebo Arajiga Says:

  Nakuaminia dada kwa mabo yako kaza uzi

 65. ok unajitahidi, nakumbuka ulivyotolewa tusker fame nilisikitika kwani unatoa single za kijaluo nzuri,mimi nikiwa mdau mzuri wa kijaluo nimetokea kule kwakina obama kisumu, ebu toa single nyingine ya kijaluo basi hongera

 66. nashipai Says:

  jamani nyie wote mlio toa comment nazikubali ila sio ustaarabu kuanza kutupiana maneno,hp mnataka kumsaidia huyo dada kufanikisha kazi yake,kwa wanao mponda poleni kwani mwenzenu anasonga mbele nyie mmbakia kung’aa macho mtaani,fanyeni kazi zenu nzuri tuzione.hongera sana ma lv sister

 67. Mary Mkwaya Malamo Says:

  sister uko juu….! kinoma ile mbaya.
  keep it up baby

 68. watubwana Says:

  hahahahahaha……..watu bwana,
  siri ya mtungi aijuaye ngata.
  hahahaahahaha…….. watu bwana,
  hongera mama.jitahidi kuimba lugha yoyote unayoiweza na unayoona utaweza uza kokote duniani,muziki sio tanzania tu,kila sehemu.

 69. chapombe Says:

  jamani ataakiimba kuzungu si muziki mnausikia tu,mbona saida kaloli kaimba kihaya,we unafikiri watu wa mtwara hawanengui nyimbo zake.sema kwa mimi ile picha fulani pale juu duh,midomo miekunduu,sijui kaipakaza rangi ya nyumba!

 70. PUZZO Says:

  Kwa people wasio-know ku-knock ng’eng’e ndo inawaboa sana!! km mnaboleka na artists wana-mix language c lzm u-read au u-listen interview zao! Infact Ni freedom of speech usichopenda ww c lzm na mm nicpende…..Xchuz ccsta AMINA ka nimekuboa na mm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s