BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

HAPO VIPI? February, 26, 2008

Filed under: Bongo Flava,Burudani,Muziki — bongocelebrity @ 12:43 PM

 

Alipoanza shughuli za muziki alijulikana kama Nigga Jay.Kisha yakafuata majina kama Jay wa Mtulinga,Mti Mkavu, Mchawi wa Ryhmes,Jay Tunakuzimia,MC Shupavu,Jay Arosto nk.Baada ya hapo majina kama HeavyWeight MC,Professa Jay yakachukua usukani.Hivi sasa mashabiki wake wanamuita Daddy.Wapo wanaomuita Sauti ya Hela.Yawezekana akawa ndio mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya anayetambulika kwa majina mengi kuliko mwingine yeyote.Au?

Mojawapo ya nyimbo zake anazotamba nazo hivi sasa ni huu hapo chini unaokwenda kwa jina la Hapo Vipi?Hii ni mojawapo ya single ambazo zimo kwenye albamu yake inayosubiriwa kwa hamu itakayokwenda kwa jina la Aluta Continua.Tuliwahi kufanya mahojiano na Prof.Jay siku za nyuma.Bonyeza hapa uyasome kama hukuwahi kupata nafasi ya kufanya hivyo hapo kabla.

Advertisements
 

27 Responses to “HAPO VIPI?”

 1. Michelle Says:

  Tatizo la wabongo ni hili, usijiite mwanamziki kwa kufoka, huo sio uimbaji,kila mtu anaweza kufoka kama hivyo. Ngoja nipe ukweli mwanamziki ni ule anaye weza kuondoka mwindoko ya vocals kama R&B au mtu anayeweza kucheza na sauti yake kwa kila namna, mfano wa karibu watu wanao imba Gospel kama Upendo Kilahilo, Flora Mbasha au mtu kama Hayati Lucky Dube hao ndo waimbaji na wanamziki sio tu kufoka basi imekuwa mwananziki, pia TID anajitahidi sana kwa kuwa hufoka na kuimba kabisa tu. Fungukeni macho wabongo. hata hao kina Lady jay dee pamoja na Ray C wanahitaji mazoezi uimbaji wao uko kienyeji sana inabidi wajifunze kutamka maneno kisanii.

 2. Chris Says:

  I do feel dis man. This song is good,n’ I always enjoy listening it.

  BUT

  This is the lamest video of this dude. The video looks cheap..hp u know wat I mean. Hapo ovyo kbs.

 3. anon Says:

  Michelle dada acha hasira
  sikiliza vizuri ujumbe na mipangilio ya ala na sauti za miziki ya prof j ukiona umuhimu uje urekebishe komenti yako,

 4. Jackline Says:

  Big up man song lako limetulia kila ukitoka unakuwa mpya mwanangu

 5. mkata issue Says:

  ‘Hapo vipi, Hapo sawa!! ni sawa na ule wimbo wa
  ‘Nikizipata mtanikoma !!’

  Niliwahi kujiuliza sijui nani atampa ili amkome?
  Kwa kifupi wakati fulani wasanii wa bongo flavor wanatumia muda mwingi kujigamba (kitu ambacho hakivutii wateja wengi) kuliko kutumia usanii kuboresha maisha ya watu kwa kujadili hoja za msingi maishani.

  Ndio maana BC inapo post nyimbo za muziki wa dansi hata za zamani bado zinawakuna watu sana si kwa sababu tu ya upangiliaji wa vyombo bali zaidi ni UJUMBE ULIOKAMILIKA.

  Jay ninakusifu na kuheshimu mchango wako mzuri kupitia kazi ya usanii. Lakini kusema ukweli ni vigumu kwa hadhira kupata mahudhui ya wimbo, ni kweli UMEFOKA ZAIDI KULIKO KUWASILIANA!

 6. amina Says:

  prof jize..aminia baba ake,nakuonaga pale kwenye baa ya kitimoto darajani kijitinyama…jenga shavu

 7. amina Says:

  nawewe michelle,coments zako ni za kweli ila maneno hayo waambie wabana pua,alikiba,z anto,marlow na wengine wanaojifanya wanaimba ukitoa banana zoro lakini siyo hapa kwa prof jize ye hayamuusu kazi yake kufoka na si kuonyesha umahiri wa vocals,elewa mziki umegawanyika anachotakiwa yeye ni kwenda na biti na kiki, na kupanch….sijui umenielewa,na staili yake nzuri tu ya kufoka ndo tunaangali,siyo unakurupuka tu na kuwaka

 8. Kekue Says:

  Nyimbo yako nzuri Prof, lakini to be honest huyu kaka ana kipaji, na kazi zake huwa ni nzuri sana , Nikutakie kila la kheri na afya njema na pia uendelee kutupa mambo au vipi!!!

 9. Ed Says:

  Prof Jay, way back in the days when chuzi wasn’t chuzi, when chemshabongo wasn’t in the media arena. I miss you son, Lakini nafuatilia your game.
  Good job, i like it hasa kuona umekata weight, i hope that photo doesn’t tell lies.
  Keep it up, hope to see you soon.
  Kichwa Mathematics,

 10. tatu Says:

  Upo juu kama kidole cha tatu

  Mie sikupondi wala nini?

  Nyimbo zako zote zinamassage

 11. kijiwe Says:

  MICHELLE
  hivi wewe ni mwanamuziki,prodyuza,au record executive?
  hivi wewe ni mbongo?
  kama ndiyo naomba nikupe somo kidogo by using your own words

  1.”Tatizo la wabongo ni hili, usijiite mwanamziki kwa kufoka, huo sio uimbaji,kila mtu anaweza kufoka kama hivyo. ”

  Mimi sioni kama kuna tatizo sababu muziki ni some kind of an art iwe kuimba au kufoka au hata ku lip sing ,iwe kupiga gitaa au piano au tarumbeta vyote hivyo ni some kind of art na ndiyo maana wanaitwa artists e.g r&b artist,hip hop artist,guitarist,au pianist na wote hao are categorized as artists.
  huyu jamaa Prof Jay ni mwanamuziki sababu he is a hiphop artist na mimi sioni sababu ya kutomuita mwanamuziki unless una sababu nyingine.Infact huu muziki ni poa sana sababu una message nyingi tu halafu mimi binafsi nimeipenda hii video maana heshima ya mwanamke imewekwa katika nafasi yake.mara nyingi hiphop artist wana display dada zetu na vibikini lakini huyu ka mdisplay (dada aliyekuwa anatangaza round za boxing match) akiwa kavaa sketi.

  2.”hata hao kina Lady jay dee pamoja na Ray C wanahitaji mazoezi uimbaji wao uko kienyeji sana inabidi wajifunze kutamka maneno kisanii.”

  Hawa akina dada zetu wanajitahidi sana especially Lady Jay Dee kuinua muziki wa kitanzania.Kwanza mimi nampongeza huyu dada kwa kuanzisha bendi inaonyesha dhahiri anavyouthamini muziki wetu na jinsi anavyopigana kujiendeleza.kumbuka kuwa hata hao akina lucky dube wako(R.I.P) walichukua miaka mingi kufika katika hizo standard zako!
  mimi kama mtanzania na computer programmer naamini katika “keep on trying for better use of what you have done before”
  sasa kama hao wanamuziki wetu wameshajenga msingi then si waachwe waendelee kujinoa ipo siku watakuwa better (according to you)but according to me they are really good artists na i must congratulate them for what they have achieved so far.

  you should be ashamed of your comments about your fellow brothers and sisters unless you can do better than them and if you can then you should consult chama cha muziki wa dansi tanzania uka volunteer kuwafundisha hao wanamuziki .
  stop hatting sister…

  togather tunawakilisha!

 12. kijiwe Says:

  BC please naomba uweke comment yangu

 13. Gervas Says:

  Michelle, acha wivu dadangu, Nakubaliana nawe kiasi flani, ila usijumuishe kuwa mziki lazima uwe kama unavyosema, hii yote ni miziki hata kufoka ni mziki endapo utaendana na tunes, hata style ya john walker mlevi ni mziki. Najua uko kwa hao wazungu na umekuwa influensidi na wao maana wazungu hawapendi miziki ya kufoka. Kumbuka miziki ya kufoka ni ya asili ya waafrika wa kimarekani kama kina Tupac ambao sisi ni binamu zetu na tuna wafeel. Hivi ukoloni utaisha lini kwenye mawazo yetu mpaka tuanze kupenda vya kwetu? nakufuagilia Prof. J keep it up maana unatupa burudani sana sisi wabongo.

 14. amina Says:

  mpasheni huyo shosti michelle amezidi sana

 15. Edwin Ndaki Says:

  MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU BARIKI UKURASA WETU WA MAONI….tutakutana kwenye miziki yetu”ya kale ni dhahabu” keshooo..

  samahani kumbe na wewe amina huwa unatembelea kwa Dani darajani…

  Swali la kizushi….wazalendoo….

  hivi kwa nini wasanii “WALIO WENGI”wa bongo wakishatoa tu album kifuatacho ni kufutuka..kuneneba..kuongezeka uzito wa mwili au kitambi?

 16. amina Says:

  edwin Ndaki kausha..ni mara moja moja pale

 17. amina Says:

  jamani tusimshushue sana michelle isije ikawa ni yule wa destiny’s child?oho,,,kijiwe futa hiyo paragraph yako yakwanza pliz

 18. Dinah Says:

  Prof J alichangia kwa kiasi kikuwa sana kuufanya muziki wa “kusema” ukubalike ktk jamii ya Kibongo alipotoka na Chemsha Bongo.

  Kuanzia “chemsha Bongo” mpaka “ndivyo sivyo” Kijana anapangilia vema maneno yake yenye ujumbe mzuri bila kutumia matusi au madongo.

  Mimi binafsi nitamfananisha na Common kutokana na kuimbwa/tunga nyimbo zao ambazo zinahusu maisha halisi ya mtu/watu wa kawaida.

  Prof J una mchango mkubwa sana ktk Bongo flava na unastahili tuzo pekee ya kuwepo kwako ktk sanaa ya Muziki Tz.

  Ndaki kufutuka kuna sababu nyingi, dalili ya ugonjwa, kuridhika, kurithi, kutofuatalia au pangilia mlo wako, kunywa bila kwa wingi na kila siku, kula nyama nyekundu (hasa kitimoto), kujisahau na kubwa kabisa HATUNA UTAMADUNI WA KUFANYA MAZOEZI bara baada yakumaliza shule za msingi….unakumbuka mchaka-mchaka na yale mazoezi yakuchangamsha mwili kabla ya ukaguzi? 🙂

 19. Jennas Says:

  Nampenda huyu kaka na cjui kwanini mie
  Ila kazi nzuri sidhani kama anakurupuka mie.

  Hivi ule wimbo wako wakuweka viatu kwenye friji unaitwaje tena?
  Hauchoshi ule

 20. Matty Says:

  Mi naona hiki ni kichwa kilichotulia hivyo nakupa 5 Prof.J Michelle kama wewe ni mzalendo lazima umkubali lakini kama wewe ni muzungu so sorry my dear!

 21. Edwin Ndaki Says:

  Jennas..

  kuhusu wimbo wa kuweka viatu kwenye jokofu..au kabati la mbeo unaitwa Nikusaidieje…kamshirikisha Ferouz kutoka kundi la Nunda zone ukipenda Daz Nunda…wazeee wa jahazi…

  Dinah!

  Ni kweli Heavy weight mc anamchango mkubwa lakini kama kumbukumbu zangu zipo njema..nafikiri kwenye mziki wa kizazi kipya wapo walio utoa mbali kipindi bado hata haujawa biashara wakawatengenezea njia wakina J..mafomo Kwanza Unit,Diplomats…mzee wa KIBURI…Sugu.. Ila kubwa ya yote Prof anakipaji.

 22. TEACHER Says:

  HONGERA SAAANA ‘PRO JAY’ NAKUKUMBUKA ULIVYOKUA TANGA JAPO ULIKUA MWIMBAJI NA KUNA WIMBO ULIKUA KWENYE CHATI KIPINDE KILE ILA ILIKUA COOL SI MTU WAMAJISIFA WALA SIO BISHOO NABADO NAKUSIKIA SIFA NZURI ZAKO NA FURAHI SAAANA NIZISILIZA SANA NYIMBO ZAKO NZURI, ULIKUA SIO MTU WA MARINGO OFISINI NAAMBIWA SASA HIVI NI STAAAAAAAAAAAAAR BONGO HONGERA SANA.
  FROM TECHER DENMARK.

 23. amina Says:

  eeh huyu jamaa alikua anafanya kazi buzz tanga enzi hizo haijaitwa tigo..nampata

 24. jomaeli Says:

  big up mkali wa ryhmes

 25. Daniboy Says:

  Twakuskiza hapa kwetu Kenya. Keep it up Proffff. Jize

 26. mzee wa madongo Says:

  kaka J aka profesa….kama utia maguu ukasoma hii mejesesi…..pita kwenye kumbukumbu zako then utuambie michelle ni nani na ulimfanya nini….
  na wewe michelle kama unachuki binafsi usiandike sehemu kama hii namba ya j nii 0713 ……….

 27. Bestman Says:

  big up j!
  waweza kununua mistari from me? check nami nina mistari ya kufa mtu!!! mwaka007@yahoo.com


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s