BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

BI.KIDUDE NDANI YA DAR IJUMAA HII February, 27, 2008

Filed under: Burudani,Muziki,Sanaa/Maonyesho,Taarab,Watu na Matukio — bongocelebrity @ 2:56 PM

 

WASANII maarufu wa muziki wa taarab nchini, Bi Kidude(pichani) na Shakila Said ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza katika tamasha la mwaka mmoja la kundi la muziki huo la Jahazi Modern Taarab litakalofanyika Ijumaa jijini Dar es Salaam.Kwa undani zaidi wa habari hii bonyeza hapa. Hii ni fursa nzuri kwa wapenzi wa muziki wa taarab na pia Bi.Kidude na Shakila Said kwenda kuwaona.

Advertisements
 

15 Responses to “BI.KIDUDE NDANI YA DAR IJUMAA HII”

 1. Makumbi Says:

  Inafurahisha sana kumwona mama yetu huyu yuko bomba bado na anaweza kupamba jukwaani. Lakini bado najiuliza, je, ana kitu gani cha kujivunia (kama gari nzuri,au nyumba nzuri) aliyoipata kama mafanikio ya kuwa katika sanaa ya muziki wa taarabu? kwa kweli wasanii wetu wanahitaji kulindwa zaidi kuhusu maslahi yao! Mbona kila siku tanzania kunaibuka viundi vya kupambana na masuala ya ukimwi, maslahi ya wenyenyumban.k. Sina uhakika kama kuna hata NGO moja iliyojitoa muhanga kushughulika na maslahi ya wasanii wetu! Kama ipo, good!

 2. amina Says:

  makumbi..siku moja channel ten walionesha kwake panasikitisha kwa kweli ni gofu labda pawe pamependezeshwa saivi…..mi nashindwa hata kuelewa,ila huyu bibi anakatika bwana

 3. Jennas Says:

  Me nimependa rangi ya bi kidude jamani
  Hivi wale wanaotumia chemical mwamuonana mama yenu na kuzurura kote nchi nyingi ila hakupenda kutumia chemical hata moja ama yeye akuwa na pesa????

  Sijatoka nje ya mada najieleza tu nilivyochukulia hii pic

  Karibu mama wa shoka tunakusubiri sisi wanao

  Na akija naongea nae achambe wanaojichubua(hahaha)

 4. Matty Says:

  Ni sawa anakipaji lakini mimi kwa mtizamo wangu nilifikiri apumzike kutokana na umri kwenda mbele maana anatumia nguvu nyingi kuimba (kujikakamua).
  Makumbi kwenye suala la mafanikio sizani nishawahi kugongana nae maeneo ya raha leo Zenj hajavaa hata kandambili nikajiuliza anadumisha mila au??jibu nilikosa au kwa kuwa ashazeeka watu wanamfisadi hela anazolipwa baada ya kuperform??

 5. Gervas Says:

  napenda lips zake jamaaniii!!! vere nachuro

 6. any Says:

  kapunguze sigara kameshazeeka kabibi ka watu! kansa uzeeni mbaya sana.

 7. Pastor Petro Says:

  Maskini, kila akipata kitu wajanja wanamwibia. Ni illiterate. aliibiwa pesa za kigeni kiasi kikubwa alivyotoka kwenye ziara Ulaya wakati fulani. Waliomwimbia watu waliojiita wajukuu zake. Bi Kidude hana mtoto! Sasa alishindwa kusema exact amount ya pesa hivyo no case. Watu wana mwexlpoit huyo bibi!

 8. amina Says:

  Gervas…we haya

 9. Shuu Says:

  Bi Kidude sasa umezeeka rudi kwa muumba wako usije ukaangukia jukwaani bure sasa ni wakati wao kina mzee Yusuph kutumbuiza

 10. Kekue Says:

  Apumzike sasa aangalie watoto na wajukuu wanafanya nini kama ni ushauri wakachukue kwake, mana unaweza anguka jukwaani bibi!!

 11. Emmanuel-kingsstudio Says:

  Sio siri kwa uimbaji ni mahiri,na ukitaka ushauri kwake kweli utanufaika.Lakini kubwa ni lilelile,amejikakwamua vipi kimaisha.Kweli kwa umri wake sidhani kama anaimbia raha tena zaidi ya kujikimu kimaisha.Kwa ubora na umaarufu wake kwa umri huo alitakiwa awe anakula alichojichumia.Lakini masikini bado anachuma juani na hakuna dalili ya kulia kivulini zaidi ya hao wanaomtumia kujinufaisha.Kweli maisha kizunguzungu.Hili ni tatizo sugu kwa wasanii wetu hata fani ikiisha inabakia tu mimi enzi zangu…..lakini

 12. mkwanja Says:

  Bibi Kidude hivi sasa amefikia umaarufu wa kuwa kielelezo cha utamaduni wa wana Zanzibari ulimwenguni kote!Bila ya shaka yoyote ana hadhi sawasawa kabisa na Balozi wetu yoyote katika fani ya Utamaduni katika majukwaa ya kimataifa.Kupitia usanii wake ameitangaza sana Zanzibar ulimwenguni kote, ameiletea sifa tele Tanzania nzima kwa jumla katika matukio mbalimbali.Wakati sasa umefika kwa Serikali ya Zanzibar kuthamini mchango wake kwa kumjengea nyumba ya kisasa na yenye hadhi ya Msanii wa Kimataifa kama walivyo wasanii wenzie wenye umri kama wa kwake kwengineko ulimwenguni.Siyo kumjengea nyumba tu ya kisasa bali vilevile apewe malipo ya kila mwezi kama pensheni kutokana na umri wake kuwa mkubwa.Tusisubiri msiba utukute Watanzania tuka anza ujinga wetu wa kumtolea misifa kemkem ya kijinga isyo na maana.Mwenyezi Mungu apishilie mbali yasitupate!Watanzania tunafuatilia kwa karibu ili kujua serikali italichukuliaje sual hili.

 13. Saidi Situ Says:

  Duh huyu mama mtumzima kusikia bado anakatika na kuimba vizuri ni ajabu. Jamani watoaji pension mko wapi? Mama yetu huyu hatakiwi awe jukwaani kwa umri huu.

  Bi kidude ningekuwa mimi ndio wewe kazi ya mziki ningeacha. Kwa sasa unatakiwa uwe umepumzika nyumbani labda unaamka na kutengeneza garden na kusali swala zako tano basi.

 14. jamy Says:

  Kwa kweli bi Kidude umezeeka sana ni muda wa kupumzika sasa na kuonja raha ya uzeeni, Achana na mambo ya mziki bibi huoni kama umechoka?

 15. DUNDA GALDEN Says:

  NILKUTANA NAE PALE KISIWANI KWENYE MAONYESHO YA NCHI ZA MAJAAZI YEYE ALIKUBALI SANAA ZETU ZA SCULPTURE LAKINI JIONI YA SIKU HIYO NDANI YA NGOME KONGWE WOTE TULISALIM AMRI NI MSANII MZURI SANA
  Na CHAFOSA CHAI GODA NEVER DIE


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s