BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PM MSTAAFU JAJI JOSEPH WARIOBA February, 28, 2008

Filed under: Historia,Serikali/Uongozi,Siasa,Tanzania/Zanzibar — bongocelebrity @ 12:06 AM

 

Pichani ni Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania na miongoni mwa wanasheria mahiri ambao Tanzania inajivunia.Pamoja na hayo katika siku za hivi karibuni amekuwa akitoa kauli mbalimbali ambazo kwa kiasi kikubwa zinawachanganya wananchi.Mfano ni kauli yake ya hivi karibuni kuhusiana na suala la kujiuzulu kwa Lowassa na jinsi ambavyo tume ya Mwakyembe “haikumuita” EL ili kumpa nafasi ya kujitetea.

Jaji Warioba alizaliwa tarehe 3 Septemba mwaka 1940 huko wilayani Bunda mkoani Mara. Alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kuanzia tarehe 5 Novemba mwaka 1985 mpaka tarehe 9 Novemba mwaka 1990 alipompisha John Samuel Malecela.Unaweza ukapata zaidi CV yake kwa kubonyeza hapa.

Advertisements
 

17 Responses to “PM MSTAAFU JAJI JOSEPH WARIOBA”

 1. salma Says:

  mwenyekiti unadili gani na amina!?
  picha ya jah kimbute iko wapi??
  irudishe haraka!

 2. Majita Says:

  CV.Alizaliwa bunda akasoma LLB Unv of EA DSM.Bahati nzuri yeye akusoma primary wala secondary.Ni kati ya watu jiniasi sana kwa kuruka madarasa hayo.Hongera kwa CV nzuri.

 3. Said Situ Says:

  Huyu nae fisadi tu. Kwa kuwa enzi zile tulikuwa tunawafungia macho mafisadi haimaanishi yeye ni msafi. Natamani ange save kama PM wakati huu wa JK.

  Ukweli wote tungeujua

 4. Makumbi Says:

  Inasikitisha sana kuona mtu muhimu kama huyu anatoa kauli za kuwachanganya wananchi, Lowasa kama mtanzania yeyote mzalendo angeweza kwenda kutoa maelezo kwa kamati kwa kuwa suala la RICH-MONDULI lilikuwa linagusa maslahi ya taifa. Yeye akiwa kiongozi mkuu wa shughuli za serikali alipaswa kuwa mtu wa kwanza kupata shoku na tatizo la RICH-MONDULI! Inasikitisha sana kuona tume ya Mwakyembe inalaumiwa bila sababu za msingi. Yeye mbona hakumwita Kiula? Ajibu kauli ya Kiula, vinginevyo na yeye ana agenda ya siri, au ni mmojawapo wa wahusika wa EPA? Wamwache Lowasa aamue la kufanya, kama hakutenrewa haki anajua mahali pa kuipata hiyo haki, na Warioba kama mwanasheria analijua hilo!

 5. Kimori Says:

  I despise and look with contempt leaders like Warioba, who are having double standards to others in spelling out paradoxical statements. Hopefully, that’s why his corruption report was dumped under the carpet by Mkapa.

  I think he is missing a point here despite the fact that he served as Attorney General for many years.

 6. kuku wa zebanga Says:

  huyu mzee naona anaaza kuishiwa yakuzungumza, ilipo anza issue ya BOT alitaka kunyamazisha HERO DK SLAA akisema hiyo haikuwa issue yakuishupalia leo tena anatuchanaganya, kama anataka azidi kueshimiwa heri akae kimya,kwanza yeye vile vile alihusishwa na skendo dhahabu na kampuni iliyo kuwa na uhusiano na CCM kwa hiyo anataka kuficha ukweli au vipi.

 7. amina Says:

  hata akiirudisha itakuaje?muache na mipango yake?hata mi imeniuma sana kutoka ile picha

 8. mwalimuzawadi Says:

  Mimi huyu baba simwamini tena tangu nisikie alichokifanya akiwa mwanasheria wa UWT CCM wakati wa kuwatimua wale wanamuziki na kukabidhi jengo kwa tajiri mwekezaji (City Ambassador aka Gogo Hotel). Nakumbuka zali hili lilimbagaisulo Halima Mamuya aliyekuwa katibu mkuu wa UWT. Au anafikiri hatujui hujuma zake?
  Ila kwa Tanzania ni poa…kanyaga twende…

 9. ochumale Says:

  huyu nae anakashfa na kampuni ya dhahabu ya CCM akae kimya tu. kwanza ana kampuni na profesa mahalu aliyeiba hela wakati akiwa balozi italia. birds of the same fether

 10. mkata issue Says:

  Tyson ehee uko wapi?
  Njoo utusaidie tumevamiwa huku!!

 11. Recho Says:

  JIzi hilo jizi hilo mnafiki mkubwa

 12. kino Says:

  mpeni mda, na pia anaweza kujitahidi katika mgogoro wa cuf na ccm, uko zanzibar, kuna viongozi wengine uko ughaibuni pia wapo wanachanganya wananchi, sio warioba tu, kikwete jamani tusaidie.

 13. binto Says:

  sio warioba tu mbona hata huyu salma mke wa kikwete, anachanganya watu vile vile kikwete haoni ilo, afadhali ya warioba ni pamoja na uzee, na huyo salma wake.

 14. mkwanja Says:

  Kauli ya Warioba kwamba tume ya Mwakyembe haikumtendea haki Lowassa kwa kuto mwita mbele ya Kamati yake ili ajitetee, kwa hakika sikutarajia kuisikia ikitoka kwa mtu mwenye sifa za uongozi kama Warioba.Labda aliteleza kuitoa kauli ile au pengine Uzee umeanza kumkamata.Mimi nilifikiri kwamba Tume nzima ya Mwakyembe ilistahili kupongezwa kwa nguvu zote kwa ujasiri na umakini walio udhihirisha katika kufanikisha majukumu waliokabidhiwa na Watanzania wote kwa ujumla kupitia uwakilishi wao Bungeni.History has been written and Time will tell!Call a spade a spade.

 15. amina Says:

  mmhh kumbe naye jizi,sasa anaongea nini?

 16. mkwanja Says:

  Kama kuna jambo ambalo Mzee Warioba anafikiri ataweza kuwasaidia Watanzania ,kama ‘Last Throw’ ,lest should he find himself thrown into the DustBin of Historical Trash, ni kuanza kuibua mjadala wa kitaifa kuhusu Mabadiliko makubwa na ya Kimsingi katika Katiba ya sasa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Iliyopo sasa imepitwa na wakati au kwa lugha ya kistaarabu zaidi imezidiwa mzigo wa kisiasa uliopo nchini hivi sasa.Mamlaka ya Rais lazima yapunguzwe na kusambazwa katika Taasisi nyinginezo za Utawala.Vyeo vya Rais(Head of State) na Waziri Mkuu(Head of Government) lazima vitenganishwe.Waziri Mkuu asiteuliwe na Rais bali atokane na Chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi bungeni.Rais hatahusika na shughuli za kila siku za uendeshaji wa serikali.Waziri Mkuu ndiye atakaye teua Baraza la Mawaziri.Makatibu Wakuu wa wizara ndiyo watako kuwa Manaibu Waziri na ndiyo watakao jibu maswali bungeni kuhusu wizara zao wakisaidiwa na Mawaziri wao.Wakuu wa Mikoa watachaguliwa na Watanzania wanaoishi katika mikoa husika kwa njia ya kura katika uchaguzi mkuu kwa njia ya kidemokrasia.Wabunge hawata ruhusiwa kugombea ubunge zaidi ya vipindi viwili mfululizo.Tume huru ya uchaguzi haitateuliwa na Rais bali itatokana na wawakilishi wa vyama vyote vya siasa vilivyo sajiliwa nchini.Na itakuwa na watumishi wake watakao simamia uchaguzi ulio huru bila ya kuingiliwa na vyombo vya Dola au serikali.Masuala ya kiuchumi yataendeshwa na kusimamiwa kwa karibu zaidi na Mikoa husika katika muundo mpya na taratibu za kisasa zaidi na Wizara kujihusisha na yale tu ambayo yanagusa kitaifa.Nafasi zote nyeti za Uongozi Kitaifa zitathibitishwa na Bunge.Na marekebisho mengine zaidi yenye muelekeo kama huu nilio ugusia kwa kifupi.Na Watanzania wengine nao watachangia mawazo zaidi.Warioba anaweza kuwa chachu katika hili kwa kuwahusisha wanasheria mbalimbali nchini pamoja na watanzania wote kwa ujumla.Tungependa zoezi hilo lianze mara moja ili itakapo pita miaka mitano kuanzia sasa marekebisho hayo katika Katiba yawe yamekamilika.Hata kama uchaguzi mkuu wa 2010 utafanyika bila ya marekebisho hayo kufanyika(bado miaka miwili tu kufikia 2010,NI MUDA MFUPI),basi wakati wowote hata baada ya 2010 marekebisho hayo yakikamilika,Uchaguzi Mkuu mwingine utaitishwa kwa kufuata Katba Mpya iliyo pitishwa!Katiba Mpya lazima ITAKUJA.Kama siyo kesho basi itakuja kesho kutwa.Lakini kuja lazima itakuja.Ni vyema walioko madarakani hivi sasa pamoja na umri wao kuwatupa mkono wakawa wao ndiyo wa kwanza kuyashughulikia mabadiliko hayo ya Katiba Mpya.Wakizembea yakaja fanywa na Vijana watakao fuatia itakuwa BAHATI MBAYA SANA KWAO! Its just a brotherly advice.History has no Mercy! One will be rewarded for what deserves!There will be those who will be swept under the Historical Carpet because they deserved nothing worth of praise! And there will be those who will be glorified by Historical Praise for what they will have done to society!Kwa hiyo Mzee Warioba the choice is yours.Acha kulia machozi ya mamba!

 17. Mary Mkwaya Malamo Says:

  duh!


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s