BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

MSAFIRI KAKIRI-JUWATA JAZZ BAND February, 29, 2008

Filed under: Burudani,In Memory/Kumbukumbu,Weekend Special,Zilipendwa — bongocelebrity @ 12:05 AM

Ijumaa nyingine imewadia.Mwezi wa pili ndio unakatika hivyo.Naona kama vile mwaka huu unaenda kwa kasi sana.Wewe unaonaje? Pamoja na hayo sisi wanadamu hatutakiwi kwenda kwa haraka sana kwani mwenda pole huwa hajikwai,au sio?

 

Kwa ujumla ujumbe huo ndio uliomo kwenye burudani yetu ya leo.Leo tunalo jina kubwa katika muziki wa dansi nchini Tanzania.Juwata Jazz Band.Wimbo unaitwa Msafiri Kakiri ukiwa ni utunzi wake Marehemu TX Moshi William(jina halisi Shaaban Ally Mhoja Kishiwa) ambaye alitutoka mwezi Machi 2006.Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

 

Ukisikiliza wimbo huu utakiri jambo moja muhimu sana.Utunzi wa nyimbo enzi zile ulikuwa sio lelemama.Ilikuwa ni lazima wimbo uwe na ujumbe mzito na unaoeleweka.Burudani ilikuwa inakwenda sambamba na kuelimishana haswa.Nadhani wanamuziki wa leo wanaweza kujifunza mengi kwa japo tu kusikiliza tungo za wakongwe kama TX Moshi na wengineo wengi.Asikudanganye mtu,nyimbo zenye ujumbe wa maana na unaoeleweka bado na zitaendelea kuwa na nafasi sana katika mioyo ya wapenzi wa muziki.Kwa hiyo,wanamuziki wa leo au wa kizazi kipya,jitahidini basi,au sio?

 

Katika wimbo huu,gitaa la solo lilipigwa na Abdi Ridhiwani(Totoo) Rhythm na Pishuu,bass guitar na Issa Ramadhani huku saxophones zikiwa chini ya usimamizi wa Mnenge,Abdi Mketema na Hagai Kauzeni.Mnaojua zaidi mtarekebisha kama kuna makosa.Kama kawaida,bonyeza player hapo chini upate burudani.Ijumaa Njema

Advertisements
 

9 Responses to “MSAFIRI KAKIRI-JUWATA JAZZ BAND”

 1. majuto Kitobo Says:

  Asikudanganye mtu…muziki wa TZ ndo huu hapa. Hizi kele za kitoto ama Bongo Flava ni ujinga mtupu tu. Sijawahi kusikia wimbo wowote wa Flava wenye maana, zote ni masuala ya pipipi tu na ujinga wa kuchukuliana mademu, Hii yote kwa sababu kila mtu aliyeshindwa maisha Bongo anataka aimbe Flava matokeo yake ndo hivi…ujinga wa kujifananisha na kina black americans na kuimba porojo. BC leteni raha kamili tuwekeeni nyimbo zetu za asili.

 2. Emmanuel-kingsstudio Says:

  Hongera sana BC.
  Hayo ni mambo ya kiutuuzima.Sanaa ya muziki ina raha yake.Hapo umetuwekea miongoni mwa sauti adimu za dhahabu zenye maadili yasiyo kifani,ambayo ubora wake hautakoma…

 3. jomaeli Says:

  majuto kitobo nakukubali..kweli bc huu ndo mziki

 4. Saidi Situ Says:

  Yeyote anyeupenda huu mziki lazima ni mtu mzima. Yaani umri umeenda na nyimbo hii inamkumbusha mbali sana. Ni haki kupenda huu mziki na sio bongo flava maana ni kitu ulichozoea.

  Vijana wa siku hizi tunaokuwa na bongo flava mziki kama huu lazima tuone mbaya. Kwa maoni yangu kitakachokufanya huu mziki uupendi kuliko mavituz ya Alikiba na wengineyo ni umri.

  Kama unaupenda huu mziki kwa dhati basi jijue kuwa umo miongoni mwa watu wazima.

 5. Fred Says:

  jina la wimbo ni msafiri kakiri au kafiri!

 6. Kamanzi Says:

  Jina la wimbo ni MSAFIRI KAKIRI sio KAFIRI. Yaani amekiri kuwa mwenda pole ajikwai upo hapo Fred?

 7. DUNDA GALDEN Says:

  NITAIWEKA BC KUWA HOME PAGE KILA NIKIWA NA FIKRA KUH MYUMBANI NAWEZA KUSOMA NA KUBURUDIKA HASWA KWA UJUMBE NA MAWAZO YA WANA WA BC HATA VIBAO VIKALI KAMA HIKI MSAFIRI KAKIRI TOKA NYUMBANI BONGO MPAKA HAPA AUSTRALIA DARWIN NDUGU ZANGU YOTE MAISHA LAZIMA TUKILI REMEMBER HOME IS HOME
  CHAFOSA CHAI GODA NEVER DIE

 8. Napingana na mawazo ya said situ kuwa muziki kama huu ni wawatu ambao umri umesha kwenda, sio kweli kabisa, muhimu hapa ni kujua maana ya kuwa mwanamuziki. mwanamuziki anatakiwa kuelimisha jamii, kuburudisha na kuonya sasa mambo hayo sio suala la umri na suala la ujuzi. vijana wengi wa sasa awajui muziki wanakimbila uko katika namna ya kuganga njaa.
  wanaona raha kuonekana katika luninga tu. awana vipaji vya muziki, na ndio maana tungo zao hazidumu. hakuna wimbo unaoweza kukaa kwenye chati kwa miaka 5 kwa kuwa tungo azilengi jamii na tungo nyingi zinalenga watu wachache tu, si ajabu kuwa na wimbo unaotaja majina ya marafiki wa mtunzi tu.

 9. Sally Says:

  Oooh gosh……This song is one of those can’t get enough of when playing, goes straight to to “the” heart.


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s