BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

DOWN THE MEMORY LANE March, 5, 2008

Filed under: African Pride,In Memory/Kumbukumbu,Michezo,Watanzania Kimataifa — bongocelebrity @ 12:10 AM

 

Mtanzania Hasheem Thabeet(pichani katikati) hivi sasa anazidi kutamba na kujiimarisha katika kuwa mmojawapo kati ya wanamichezo wazaliwa wa Afrika waliopo nchini Marekani ambao wanafanya vizuri katika anga za michezo nchini humo.Hasheem anasoma katika Chuo Kikuu Cha Connecticut akichezea timu yao maarufu ya mpira wa kikapu(basketball) ijulikanayo kama Connecticut Huskies.

Hata hivyo Hasheem ametoka mbali kama ambavyo unaweza kuona katika picha hiyo hapo juu.Hapo bado alikuwa jijini Dar akiwa na wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mandojo na Domokaya.BC inamtakia Hasheem kila la kheri katika jitihada zake.Unaweza kutembelea tovuti ya Hasheem kwa kubonyeza hapa.

Advertisements
 

16 Responses to “DOWN THE MEMORY LANE”

 1. mstari mbele Says:

  jamani hiyo ni timu ya kikapu ya chuoni kwake,na si kama watu wengine wanavyosema ya kua anachezea ligi ya kikapu NBA, ila yote kwa yote big up sana bwana hashimu.

 2. jomaeli Says:

  mhhh hii kitu ndefu jamani

 3. Kekue Says:

  Mmmh!!! Lakini urefu wake umempatia umaarufu mkubwa na hiyo sijui ndo mpira wa kikapu ndo usiseme tena, atafika mbali, da!! Lakini ni mrefu, alikuwa anapataga shida kichizi kwenye hizi dala dala zetu kuna siku nilimbamba akiwa anapanda daladala. Hongera kaka na kila la kheri.

 4. Chris Says:

  Hv jamani huyu mshikaji ndo time fulani alisomaga Makongo,alikua anaishi Sinza ( I suppose). Time hizo alikuaga gumzo kwa kupata shida kwenye vipanya/daladala cuz of urefu… Head up dude…

 5. yese Says:

  mhhh mkaka kaenda hewani haswa…

 6. Dinah Says:

  Kitu ndefu yaani imeenda hewani Mkaratusi (ni mti sio tusi) Akipiga kanzu nyeupe huyu akakatika barabarani mida ya jioni anadundika kibongo-bongo unaweza ukasikiwa watu wakisema “kwa jina la yesu shetani toka” wakidhani ni jini hahahahahha….

  Hashim Thabiti kila la kheri ktk kuutumia urefu wako vilivyo.

 7. solange Says:

  mstari mbele ni kweli jamaa anachezea kikapu NBA

 8. Said Situ Says:

  Hivi binadamu wa kawaida huacha kurefuka akiwa na umri gani? Mi naona kuna uwezekano kuwa huyo dogo bado anarefuka.

  Ongeza bidii ndugu yangu utafika mbali.

 9. Chris Says:

  Mshikaji kwao wanamuita Andunje…

 10. Dinah Says:

  Saidi Situ; Ukifikisha miaka 20 (wengine wanaamini 18yrs) binadamu wa kawaida unaacha kukua/kurefuka na badala yake unanenepa nakukomaa lakini kimo kinabaki palepale.

  Naomba kuuliza, mtu akiwa mfupi sana (zaidi ya mbilikimo) inaaminika kuwa ni ulemavu kama sio kuwekwa kwenye kundi la walemavu sasa je, ukiwa mrefu kama huyu jamaa inakuwaje?

 11. amina Says:

  chris ndo huyu alikua anasoma makongo ndiyo, naanaishi sinza mi nilimbamba sinza makaburini ndo kilikua kijiwe chake pale kwa wauza mitumba sasa hivi pamevunjwa pale kituoni,sasa hata mi nimemkumbuka huyu dogo alikua anapata shida kwenye daladala

 12. Reg Miserere Says:

  Wengine wanasema mtu huacha kurefuka akiwa na umri kati ya 21.

  Dinah ndio ulemavu huo huo. ila usinikoti………

 13. Gervas Says:

  Dinah, unamaanisha urefu gani? au sijakuelewa..,

 14. Matty Says:

  Gervas usiandike el (l) tena akija Said Situ hapa atakuja na kifimbo cheza chake….vinginevyo huyu dogo ni mrefu sana wajameni mweeeeeee!

 15. Dinah Says:

  Gervas namaanisha urefu wa kimo, urefu wa kwenda juu kama Hashimu 😉

 16. Chris Says:

  Thanx amina…. Inamaana Saidi Situ mmembatiza ukifimbo cheza humu…. Hahahahahahaaaaaa. Tutaona how he’ll react… Huo urefu….. hhhhhhhmmmmmmmmm………. ngoja wenye vinywa watajibu…


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s