BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

PICHA YA WIKI # 10 March, 9, 2008

Filed under: Photography/Picha,Weekend Special — bongocelebrity @ 12:05 AM
Advertisements
 

33 Responses to “PICHA YA WIKI # 10”

 1. Senyandumi Says:

  Huyu jamaa alikua disco ama harusini.Nadhani itakua ni Amana hapo,maana Msondo ndio wanacheza vifua wazi!

 2. Gervas Says:

  Eheee Bc utakuta hiyo ndo breakfast, tukirudia ile topic yetu ya juzi, mtoto kamrithi babake kipaji cha kugida..teh, teh, unaona jinsi kanavyoi enjoy larger mpaka kamekunja vidole na usikute hiyo ni ya nne. afu kakienda chekechea inabidi wakarushe madarasa hadi la tano maana IQ yake iko juu sana. Happy children’s day

 3. Edwin Ndaki Says:

  Asalaleeee!!!

  Mtumeeeeee…..

  Kama hili tukio sio tamthiliya ya kutengeneza kwamba dogo kaa hivi nikupige picha basi hali inatisha,

  Ukishangaa ya Musa,utayaona ya Firauni..unaweza kukuta huyo sio mtoto labda ana umri kama wa kaka Gervas,sema yeye tofauti na yule Thabit anayerufuka kwa kwenda juu,huyo anarefuka kwa kwenda chini.

  Kama ni andunje basi naona bora wamuongezee round nyingine.

  BC..mbona hamjatuampia chanzo cha picha hiyo..au ndio mambo ya “duka la picha”Photoshop…tee tee aaa aaa kumbe na mimi kiingilishi nipo juu.

  Inaonekana sikuwa kuwa “swahili speaker”

  jpili njema..tukutane mwalufote

 4. Mswahilina Says:

  Haya, ndio walisema baadhi ya wadau kwa binti wa Mubaraka Mwaruka Mwishehe kwamba: Mrithishe mtoto wako kazi yako. Yaani kama wewe ni Mlevi, mrithishe na Mtoto ulevi.

 5. Pope Says:

  Nilipoambiwa kua uyaone nikajua niyaone Maghorofa kumbe ndio haya!!
  Wallah hii chiboko!!

 6. hellen Says:

  duuuu,aka katoto katakuwa kachaga au kahehe simnajua asubuhi ulanzi badala ya chai,kweli haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania kakijana kanakula maisha na moja baridi.

 7. Gervas Says:

  Teh, teh.. Edwin!! hivi ni wewe?? Basi umenikumbusha mbaaali sana ndugu yangu, Miaka 12 hivi iliyopita. Yaani tukishatoka mwalufote tunapitia kwa mama Abel kugonga “the Ulanzi” afu ndo Bwenini afu ndo ukikutana na Mwl Paralyzer au Kabika gizani unazuga unatembea kama kilema ili asinkunotisi..teh, teh. Bc, nashukuru Blog yako mbali na kutoa maoni pia ni nafuasi ya kukutana na tuliopotezana miaka mingi… Uko kona gani ya Ulimwengu huu wa Jua Edwini?? a.k.a…..

 8. Chris Says:

  A.k.a ze lager… Daah dingi hayupo na ashukuriwe kwa kuleta hz lager….Fasta ngoja nitandike mitungi….

  Na hiyo chupa ni gea tu maana dogo anagida gongo hapo…

 9. Makumbi Says:

  Ndugu yangu Ndaki sio kwamba tu hali inatisha, bali ni kiama!Watasingizia eti ni dawa ya kuzuia surua! Ingekuwa dawa kweli, hapa sauzi usingekuwepo ugonjwa wa surua. Kinachoniogopesha zaidi ni hatima ya huyu mtoto! Hata kama ni anducje basi angepewa kwenye kijiko cha chai! ukizingatia S I Units za walevi, yaani alcoholic % per height, hiyo chupa sio size yake, mzunguko wa kilevi ndani ya mwili wake utakuwa wa speed ya ajabu! Kweli bongo imeisha , baba kampa hadi kofia yake! mmmmhhhhn

 10. Mwana wa mkulima Says:

  Safi sana dogo dumisha mila..urithi wetu huo….

 11. Gene Says:

  Mtoto wa Masele Chapombe anayeigiza Mizegwe ITV

 12. sikubaliani Says:

  hehehe alafu hii picha imepigwa tu na sio kweli dogo anaginda ukitaka kuangalia vizuri hebu ona dogo yupo juu kakalia cret la bia vimiguu vyaning’inia hiyo ni gelesha tu dingi wake yuko pembeni.

 13. Matty Says:

  Ehhhhheee hii sasa kali!dogo kaona kila siku dingi anakunywa peke yake ngoja na yeye leo aonyeshe kipaji chake!!!!!!halafu anakunywa huku anasikilizia radha halisi ya kil akiwa amefumba ze eyez.
  Ni kweli ndo yale tuliyosema kwa binti wa Mwinshehe unaweza rithi talent ya mzazi..na dogo hapa karithi kabisa maana umri huo hata shule hajaanza akianza shule ndo kabisa atakuwa chapombe.
  Kule kwetu nanihhhhiii lazima dogo asubuhi apate ulanzi mtogwa na kiporo cha ugali na kumbikumbi!!!!!!bongo tambarare!Gervas upo hapo??

 14. Kekue Says:

  Kwa raha zake

 15. Dogo Says:

  Kama baba kama mwana au kama mama kama mwana, lazima mzazi wake mmoja awe cha pombe

 16. Dogo Says:

  Kama mi ni kaka yake, wallah sina mdogo

 17. Portland Says:

  Jamani hiyo ni Tongwa si unajua kule uswahili , tongwa huwakwa kwenye chupa za soda , sasa ni new staili kwenye chupa za bia kama mnazi

 18. solange Says:

  jamani nimeshangaa mpaka basi mhhh..haka katoto kama ni bar kalienda kenyewe kakaagiza kaakanze kugida? au?

 19. Mama wa Kichagga Says:

  Sijapenda, hii haijakaa vizuri kabisa!

  Huyu mtoto na wengine walio kwenye mazingira kama haya wanatengenezewa future ya namna gani? Akianza kuwa mlevi darasa la nne akafukuzwa shule mzazi/jamii italaumu?

  Mi naona huyu mzazi aliyemwacha mtoto hivi hadi wakamfotografia namna hii akiwa sijui ni baa au wapi jamani achukuliwe hatua za kisheria/ustawi wa jamii ili kuokoa maisha ya mtoto huyu.

  BC mnaweza kunidokozea hapo ni wapi?

 20. Gervas Says:

  Mama wa Kichagga, mbona shwari tu, kumwonjesha kidogo, kwanza kama anakusumbua atalala, si ni chakula tu? miye nilianza mdogo na mambo yangu shwari tu saizi ni suppliier mzuri tu wa “hizi wisiki za asili kata nzima najulikana” ubaya huanzia pale unapojifanya eti umedata kwa pombe. Matty, hayo maisha ndo nimeyapitia afu shwari tu nategemea mwanangu nae adumishe mila

 21. Longolongo Says:

  Hivi Mama wa Kichagga, unaishi Tanzania au nchi gani vile … ? Hivi uwewahi kwenda kwenye mabaa ya miji ya vijijini ukaona watoto wanavyorandaranda huko? Inawezekana wewe huishi Tanzania.

 22. Liz Baraka Says:

  Jamani siku zote maji hufuata mkondo wake.

 23. vianne Says:

  Wow!Yan hii hali sasa inatisha kwan kijana ana tisha hata kama kurithi kwa baba basi ni mapema sana,
  hali mbaya basi.

 24. KIOKOTE Says:

  Hiyo geresha tu hakuna lolote

 25. Heavyweight Says:

  Damn…huyu dogo msikute anakunywa mafuta ya taa jamani…Bc…tueleze kama dogo bado yuko hai au alipata kasheshe gani baada ya hiyo stunt…LOL.

 26. mzee wa madongo Says:

  eee hapa ni msasani…mambo ya kawaida haya…..

 27. msdon Says:

  jamani haya mambo yapo tena haswa iringa,kutokana na hali ngumu ya maisha watoto asubui wanapikiwa uji uliochanganywa na ulanzi,yani ulanzi(pombe) inatumika kama sukari hapo,maana wanywaji wanasema ulanzi unasukari sana,hivyo ilikuepusha gharama za manunuzi ya sukari mtoto anakunywa huo uji mchanganyiko na ulanzi then analewa,
  usishangae tu hiyo huko iringa maeneo wanapogema ulanzi utakuta nyoka amekunywa ulanzi amelewa tu wala haondoki,thts Tanzania

 28. Daw Says:

  Duh hii kali… lkn maji hufata mkondo kama hajarithi kwa Baba yake basi ni kwa mamaye…. Si mchezo

 29. Albert Says:

  Jamani hako katoto kanaonekana ni ‘kapampula’ Lakini hata baba yake atakuwa ni wa dizaini hiyo manake micrate kibao ya bia maskani

 30. sweetoh Says:

  picha haina hadhi ya “picha ya wiki” ni udhalilishaji wa watoto ambao ndio taifa la kesho, tunapaswa tukemee vikali!
  tukiifurahia itafanya watu kutafuta itakayowashangaza zaidi,
  kuna siku watatuma picha chafu za watoto, sifikirii kama tutapenda ifike huko! picha inaonyesha mpigaji ameipanga na siyo ya kushtukizia.
  BC WAJIBIKENI.

 31. kilao1 Says:

  Ni kweli mtoto wa paka ni paka, hawezi kuwa kicheche, japo ni tafsida tu. Jongo jipya halikosi kunata, hata ukioga rangi itabaki. Huyu anaonyesha nikiasi gani karine hizi nitofauti na zama zile. Me nasema na nitasema Tabia Mbaya ya mtoto husababishwa na wazazi wa mtoto na tabia mbaya si kunywa pombe tu kwani wenye uelewa hawata potoka.

  Inatupasa tuache kuwa tunajibu hovyo mbele ya watoto sisi ni wazazi pia maana watu wanafikilia tabia mbaya ni kutumia unga pekee wanaweza hoji mboa baba yake hatumii si hivyo.
  Baba au mama huwa wanamwita mtoto wao wewe kuku tena kuku afadhali yani wengine “wewe Irene” mtoto “ehee” mama au baba nyokooo” ” mse.. wewe njoo hapa ” mku… wewe nk
  Ok sisemi tusiwakehee wakataze ila kimaadili tu
  Kipanya1

 32. ss Says:

  haloooo…yaaaarabii taubahh.. dogo ajinoma tuu


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s