BONGO CELEBRITY

All You Wanted To Know But Didn’t Know How and Where

INSPEKTA MSTAAFU March, 11, 2008

Filed under: In Memory/Kumbukumbu,Serikali/Uongozi — bongocelebrity @ 10:35 AM
Mmojawapo kati ya wakuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania ambao wataendelea kukumbukwa kwa muda mrefu ni Inspekta Jenerali mstaafu, Alhaj Omari Mahita(pichani). Wewe unakumbuka tukio gani kutoka enzi za uongozi wake?
Advertisements
 

42 Responses to “INSPEKTA MSTAAFU”

 1. Mbarikiwa Says:

  BC,
  Mie ninakumbuka liposema:
  Kama hao (CUF) ni Ngangari, basi sisi (Polisi) ni Ngunguri

 2. Kisaka Says:

  Namkumbuka alipoposhabikia siasa huku akijuwa kuwa ni mtumishi wa serikali pale aliposema kama C.U.F ni ngangari yeye ni ngunguri

 3. simba Says:

  TUKIO NINALO KUMBUKA LA MUHESHIMIWA MAHITA,KWANZA LA KUUWA WATU MSIKITI WA MWEMBECHAI,PILI KWA KUMKINGIA KIFUA ABDLLLAH ZOMBE ,BAADA YA KUUWA AKAMPELEKA KUWA RPC RUKWA ,MH RAIS KIKWETE AKABADILI MAAMUZI HAYO ,HIVYO NDIVYO VISA VYA MTANI WANGU (MIMI MNYAMWEZI) AMBAVYO NAVIKUMBUKA

 4. Pot Says:

  weeeee!!!! wachaaa!! hilo ndio sura ra kiporisi!!!

 5. Edwin Ndaki Says:

  Namkumbuka jinsi alivyoonyesha visu vya kupikia jikoni na kusema zana za ugaidi za CUF.

  Pili hospitali yake ya binasfi kulindwa na FFU.
  Ni hayo tu.

  Pia alikuwa anachanganya sana kazi yake na siasa

 6. KC" Europe Says:

  Nampongeza kwa mda wote aliotumikia Jeshi la polisi then mimi binafsi nilipenda utawala wake i mean jeshi linataka nidhamu na command.
  Walifanya kazi kwa ushirikiano mzuri na Kamanda Tibaigana kwa kweli walijipanga vizuri hasa katika kipindi cha uchaguzi na mivutano ya hapa na pale na wapinzani vyama vya siasa na wafuasi wa vyama hivyo.
  Nakumbuka moja ya speech zake na watu wa media alisema “wanataka kuchezea jeshi la polisi na kulichafua hatutakubali hata kidogo wanasema wenyewe ngangali basi na sisi ngunguli….

 7. Mswahilina Says:

  KC Europe.
  Andika “Ngangari” na sio “Ngangali”
  Andikia “Ngunguri” na sio “Ngunguli”

  Penda Lugha yako ya Kiswahili.

 8. Makumbi Says:

  Namkumbuka alivyokuwa na usongo na viongozi wa vyama vya upinzani! du, utadhani alikuwa na uhasama wa kuchukuliana mali!

 9. msafwa Says:

  Nakumbuka alipokuwa na kesi ya kutembea na house girl wake ila ikafunikwa mpaka alipostaafu na pia amekwepa kwenda mahakamani

 10. Albert Says:

  Atakumbukwa kwa mauwaji yahalaiki na kauli zake za zidi ya wale wasiokuwa na hatia na pia msisahau huyu ni miongoni mwa mafisadi wa mali zauma na alikuwa na mali za wizi ambazo ziliwahi kutajwa tajwa lakini kwa kuwa Nduli mkapa alikuwa anakula nae hakuna aliyeweza kusemchukulia hatuwa zozote Tukumbuke kuwa ipo siku yatadhihirika kama mtowa maoni number 6alivyompa sifa ambazo hastahiki kwani wakati wake polisi na ujambazi vilikuwa nikama kitu kimoja na ndio matokeo yake amejilimbikizia mali za wizi

 11. Dinah Says:

  Kuna tofauti kati ya sura ya kipolisi na ile ya kiburi au roho mbaya au ya husda!

  Mimi nakumbuka kujieleza kwake ambako kulikuwa kukinifanya nihojo Elimu yake au uwelewa wake wa mambo. Pia namkumbuka huyu bwana alipokuja na ile NGUNGULI bila kusahai sakata la kukana mtoto wake.

  Ingekuwa wasomi wale wenye chama cha wasomi Tz ( ubaguzi tu eti chama cha wasomi hahaha) wanakubali kujiunga na jeshi la Polisi sidhani kama huyu Mzee angefikia hapo 🙂

  Naomba kuuliza hivi Kozi ya criminoloji na forensiki inapatikana wapi hapa nyumbani? Nataka kujiunga na Polisi wandugu.

 12. Edwin Ndaki Says:

  Nilisahau..mahita naamini hata yeye mwenyewe binafsihawezi sahau jinsi wabunge walivyomjia juu kuhusu kitendo cha yeye “kuingilia kile kinachoitwa shughuli za bunge” ,
  pale alipotoa maelezo kupitia vyombo vya habari kuwa..wabunge inabidi wawaongezee maafande chapaa maana mshahara wa chini ni sawa na posho ya siku moja ya mbunge.(nukuu isiyo rasmi)

  Ilikuwa alimanusra AJILOWASA

 13. Mpita njia Says:

  Nakumbuka alivyokuwa anatumiwa na ccm kuwakandamiza wapinzani, akafikia kuonyesha visu kuwa ni vya CUF akijua sio kweli.

  Pia hospitali yake kulindwa na FFU ni ufisadi wa wazi aliokuwa anaufanya, maana hospitali yake ilikuwa ni private estate

 14. Saidi Situ Says:

  Namkumbuka kwa kununua kiwanja na kujenga msikiti Morogoro. Msikiti wa mahita unaitwa. Mungu ambariki na amsamehe dhambi zake zote.

  http://mjengwa.blogspot.com/2007/05/maarufu-msikiti-wa-mahita.html

 15. Mswahilina Says:

  Wabongo wenzangu,
  Ni NGANGARI na NGUNGURI sio NGANGALI na NGUNGULI kama wengi mnavyo andika, tafadhali, Ngangali sio sawa na Ngangari, pia Ngunguli sio sawa na Ngunguri.
  Tafadhali tuipende lugha yetu ya Kiswahili.

 16. Dullah Says:

  Asante Mswalihina kwa kuweza kuwarekebisha wachafuzi wa lugha! Unanikumbusha mbali saanaa kwa mzee kifimbo cheza wa gazeti la sani. Keep it up!!

  Nakumnbuka Mahita aliwahi kusema Gari zote zenye TIN-TED ni za majambazi, wakamatwe akisahauu wengi wao walikuwa mawaziri Palikuwa patamm

 17. Majita Says:

  Namkumbuka kwa mambo mengi.
  1:kumkana mtoto wake aitwae Rashid Mahita aliyemaliza depo mwaka 1999 baada ya mtoto huyo kufanya so fulani hivi huko mikoani.
  2:Namkumbuka alivyomtwisha staff Officer wake kamanda Dau bonge la zingo kule lindi wakati yeye ni RPC huko lilompelekea Dau kupelekwa mshauri wa mgambo.Anyway alimnyanyua baadae alivyoupata u-aijipiii.
  3:Nakumbuka uimara wake uliompelekea kuogopwa sana na maarapisii wake hadi kumpelekea ritani ya mbuzi,ng’ombe na mchele kila mwisho wa mwezi kwa kujaza kometi.
  4:Nakumbuka alivyokuwa anamuogopa yule mama arapisii wa Tanga enzi hizo,siju fatma sijui nani,sijui chakla.
  5:Nakumbuka alivyomkung’uta Mrema mabomu kule Moshi.
  6:Nakumbuka alivyowatumia madaktari wa Polisi kufanya kazi kwenye hospital yake kule Gmboto bila malipo kwa kuwatishia tu kuwapiga malindo.
  7:NAKUMBUKA MEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEENGI ila zaidi ni alivyokata anka baada ya kula muziki wa kumuaga arapisii Shekiondo pale morogoro aliyekuwa anaamia idara ya madawa ofisi ya waziri mkuu.Kwi kwi kwi

 18. amina Says:

  mi nalikumbuka hili liliwaambia matrafiki dereva mkorofi mchapeni viboko…lilikua na mambo ya ajabu kwa kweli na sura yake imekaa kiroho mbaya

 19. chau Says:

  mi nakumbuka liliwaambia matrafiki, madereva wa daladala wanaovunja sheria za barabarani wawapige viboko…..

 20. Gervas Says:

  Mswahirina, jifunze kutumia nukta na koma…sio kuzimwaga tu upendavyo kabla na baada ya neno “tafuazari”…afu sio Kiswahili ni Kiswahiri. Mie simo!

 21. Matty Says:

  Nakumbuka alimkataa mtoto aliyemzaa nje ya ndoa!hii mtu inasura ya ukali sana ila nadhani ndo nzuri kwa jeshi la polisi.
  Dinah unataka kusoma hiyo kozi uje uwe nani vile??? te te te !!!!!!!

 22. Mariam Says:

  Namkumbuka kwa tabia yake ya kukunja sura kama anataka kutapika

 23. sikubaliani Says:

  mie sisemi kitu maana hiyo sura tu naogopa

 24. Freddy Macha Says:

  Nakubaliana kabisa na Mswahilina.
  Hili ni suala muhimu sana la lugha yetu.
  Watanzania wengi (akiwepo rafikiangu Masudi wa London) hatujui kutofautisha kati ya RA na LI; LA na LU. Ndiyo maana wengine tunasema LUNINGA (tv) badala ya RUNINGA; DALISALAMA badala ya DARISALAMA, UGARI badala ya UGALI, LAFIKI badala ya RAFIKI, nk.
  Ubaya (na kinachotisha zaidi) ni kuwa wengi tunaandika au kusema kwa makosa bila hata kujua. Wanaokumbusha kama Mswahilina ni wachache sana.

 25. Pot Says:

  Mie namkumbuka wakati akiwa RPC Kilimanjaro ..na wakati huo .Aliyekuwa naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani….. Meku…. AGUSTINO MREMA, bosi wake enzi hizo , alijiunga na upinzani alikwenda kufanya mkutano wa siasa Moshi ,ambao uliongozwa na maandamano bila kibali huku yeye MREMA akiongoza maandamano hayo, …. ”YEYE AKIWA KAMA RIKAMANDA RA GESHI RETU RA PORISI”….Hakusita kuwatwanga MABOMU YA MACHOZI ,yaliyopelekea Mrema kuugua macho, kwa muda mrefu, na RPC huyo kujitapa ,…”kama ulikuwa bosi wangu ni zamani sio sasa”, kitendo hicho kilimpa ujasiri mkubwa ndani ya CCM na kupandishwa cheo kuwa INSPECTOR GENERAL OF POLICE (IGP)

 26. kijiwe Says:

  Huyu ni Lil Fisadi

 27. amina Says:

  pot umenichekesha kumbe huyu jamaa anhistoria ya utemi hahahhah

 28. Dinah Says:

  Mswalihina sio kwamba hatukipendi kiswahili, ingekuw ahivyo basi tusinge kitumia kufikisha maelezo yetu bc, nadhani hii inatokana na kujisahau kutokana na kutokukitumia Kiswahili mara kwa mara.

  BTT: Ikiwa alilalama kuwa Mishahara ya Polisi ni Posho ya Wabunge ya siku, kwamba mishahara ni mdogo ukilinganisha na kazi za Polisi…….atueleze alipata wapi Pesa za kujenga Hospitali yake na Msikiti wakatia likuwa Polisi tu?

  🙂

 29. Chris Says:

  Kwanini BC mmebania message yangu????????????

 30. NYAKATAKULE UNYILISYA ECHALO Says:

  Tofauti yake kubwa na gavana mngátuka Eliot Spitzer ni kuwa skandali ya Afande mfawidhi iliminywa kinamna na ikaisha kihasara hasara wakati ya Mh. mbeba rungu la torati wa New York imeongeza pato la Taifa kwa uuzaji mzuri wa T-shirt na hata vipodozi vyenye chata ya namba kenda!

 31. amina Says:

  hawa wanabana sana wana u-ccm sana, chris we mwombe mungu tu

 32. Edwin Ndaki Says:

  Kaka Fredy Macha nimefurahi kuona maoni yako kuhusu matumizi ya lugha ya kiswahili.

  Najua wewe ni mwandishi garacha ninayekukubali.

  Ila kuuliza sio ujinga natumaini utanisaidia kwa hili.

  Nakunukuu wewe mwenyewe…”DALISALAMA badala ya DARISALAMA”

  Nimeshindwa kukuelewa,hapo unaongelea jiji la Dar es salaam? au unaongelea sehemu ya juu ya nyumba ipo salama, yaani Darini?

  Natumaini utatumia utanipatia majibu ya maswali yangu hayo.

  Wasalaam

 33. amina Says:

  au chris nawewe ulitukana humu ndomana wanabana? mhhh

 34. Dotto Says:

  Huyu jamaa alikuwa mbabe vilevile alikuwa hawajali polisi wake kwani walikuwa wanavaa uniform zimechakaa na kupauka tofauti na sasahivi kidogo wanaonekana kuvutia na rushwa kwa mapolisi ilizidi sana mtu ukifika tu polisi ujue lazima utachomolewa mara uambiwe gari halina mafuta kwenda kumkamata mhalifu mara sijanywa chai

 35. Chris Says:

  Amina sijui kama nimetukana, naamini hawa BC ndo wanaeza sema kama nimetukana au nimegusa walipokua hawataki.

  Ilikua ni msg nzuri sana kuhusu nimkuavyo huyu Mahita. sasa BC wameifisadisha juu kwa juu…

 36. Kalaghe GMh Says:

  Yule jamaa ana sifa zote za u-afande! Ingekuwa si umri kusonga mbele, tungeandamana aendelee angalau kuwa mkuu wa kule wanakopikiwa maafande!! Teh teh teh…..

 37. amina Says:

  chris basi hii bc itakua ya serikali hii ukiongea ukweli sana hawataki ehhh….

 38. Chris Says:

  Amina nafikiri siyo ya serikali,nafikiri ni ya mafisadi walio serikalini….

 39. amina Says:

  Chris hehehehe….hebu tuma nyingine tuone!nawewe usiandike vitu vya ndani sana vya kiserikali

 40. fukara Says:

  Nitamkumbuka kwa zuri moja tu.Pale walipokutana kwenye kikao cha iterpool juu ya mikakati ya kuzuia dawa za kulevya alisema yafuatayo
  nanukuu”watu wakishafanya biashara hii haramu na kupata fedha,fedha ile wanakuja kuiTAKASA kwa njia ya uwekezaji”mwisho wa kunukuu.Naalimaanisha wapo waheshimiwa ktk jamii ambao ni mfano huu.Hilo namweshi.
  Lakini mengine aliboronga kwani shule ni ndogo

 41. mie Says:

  hivi we ndaki umeoa au

 42. Said Says:

  namkumbuka alipokuwa na kashfa ya kuzaa na house girl wake!na kumkana mtoo,halafu hile bendi ya vichaa wanao kaa
  ujerumani the ngoma nani?ni hii walimtungi wimbo wa BABA ASHIBAE kapteni wa mapenzi! wanavyodai baadhi ya washabiki


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s